ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (71) سورة: يونس
۞ وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ نُوحٍ إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ إِن كَانَ كَبُرَ عَلَيۡكُم مَّقَامِي وَتَذۡكِيرِي بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَعَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡتُ فَأَجۡمِعُوٓاْ أَمۡرَكُمۡ وَشُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُنۡ أَمۡرُكُمۡ عَلَيۡكُمۡ غُمَّةٗ ثُمَّ ٱقۡضُوٓاْ إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ
Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu!Ikiwa kukaa kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu.Kisha nihukumuni, wala msinipe muhula.
Yanayo kupata kutoka kwa watu wako, yaliwapata Manabii walio kutangulia. Basi wasomee hawa watu, Ewe Mtume, aliyo kuteremshia Mola wako Mlezi katika Qur'ani kisa cha Nuhu, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alipo iona chuki na uadui wa watu wake kwa ujumbe wake, aliwaambia: Enyi watu wangu! Ikiwa kuwa pamoja nanyi kwa ajili ya kufikisha ujumbe kumekuwa ni shida juu yenu, basi mimi ni mwenye kuendelea na wito wangu, na ni mwenye kushikilia hapo hapo, na ni mwenye kumtegemea Mwenyezi Mungu katika hili jambo langu. Basi nyinyi na washirika wenu jifungeni madhubuti katika shauri yenu, wala msiufiche uadui wenu kwangu kabisa, wala msinipe muhula wowote kwa maovu mnayo nipangia kunitendea, kama kweli mnaweza kuniletea madhara. Kwani Mola wangu Mlezi ananilinda.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (71) سورة: يونس
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق