ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: الأحزاب   آية:

سورة الأحزاب - Surat Al-Ahzab

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ ٱتَّقِ ٱللَّهَ وَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Ewe Nabii! Mche Mwenyezi Mungu wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
Ewe Nabii endelea hivyo hivyo, kama ulivyo, kumcha Mwenyezi Mungu, wala usiyakubali mawazo ya makafiri na wanaafiki. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa kuvijua, ni Mwenye hikima katika kauli yake na vitendo vyake.
التفاسير العربية:
وَٱتَّبِعۡ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا
Na fuata uliyo funuliwa kwa wahyi kutokana na Mola wako Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari ya mnayo yatenda.
Na fuata wahyi unao teremka juu yako kutokana na Mola wako Mlezi. Hakika Mwenyezi Mungu anaye kufunulia kwa wahyi anazo khabari hata za mambo madogo madogo unayo yatenda wewe, na wanayo yatenda makafiri na wanaafiki.
التفاسير العربية:
وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا
Na mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni wa kutegemewa.
Na wewe mwachilie mambo yako yote Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kabisa kuwa ni mtegemewa wa kila jambo.
التفاسير العربية:
مَّا جَعَلَ ٱللَّهُ لِرَجُلٖ مِّن قَلۡبَيۡنِ فِي جَوۡفِهِۦۚ وَمَا جَعَلَ أَزۡوَٰجَكُمُ ٱلَّٰٓـِٔي تُظَٰهِرُونَ مِنۡهُنَّ أُمَّهَٰتِكُمۡۚ وَمَا جَعَلَ أَدۡعِيَآءَكُمۡ أَبۡنَآءَكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ قَوۡلُكُم بِأَفۡوَٰهِكُمۡۖ وَٱللَّهُ يَقُولُ ٱلۡحَقَّ وَهُوَ يَهۡدِي ٱلسَّبِيلَ
Mwenyezi Mungu hakumwekea mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake. Wala hakuwafanya wake zenu - ambao mnawalinganisha migongo yao na migongo ya mama zenu - kuwa ni mama zenu. Wala hakuwafanya watoto wenu wa kupanga kuwa ni wana wenu khasa. Hayo ni maneno ya vinywa vyenu tu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye sema kweli, naye ndiye anaye ongoa Njia.
Mwenyezi Mungu hakumjaalia mtu yeyote kuwa ana nyoyo mbili ndani ya mwili wake; wala hakumfanya mke wa yeyote katika nyinyi kuwa ni mama yake, pale anapo sema ati: Wewe kwangu mimi kama mgongo wa mama yangu! Wala hakuwafanya watoto mnao wapanga kuwa ni wenenu, kuwa hakika ni wana wenu kwa nasaba. Hayo ya kuwafanya watoto wa kupanga kuwa ni wenenu, ni kauli inayo toka kwenye vinywa vyenu, wala hayana ukweli. Hapana hukumu yoyote inayo tokana na hayo. Na Mwenyezi Mungu anasema jambo lilio thibiti la hakika. Na anakuongozeni mlifikie. Na Yeye peke yake Subhanahu ndiye anaye ongoa watu kwenye Njia iliyo sawa.
التفاسير العربية:
ٱدۡعُوهُمۡ لِأٓبَآئِهِمۡ هُوَ أَقۡسَطُ عِندَ ٱللَّهِۚ فَإِن لَّمۡ تَعۡلَمُوٓاْ ءَابَآءَهُمۡ فَإِخۡوَٰنُكُمۡ فِي ٱلدِّينِ وَمَوَٰلِيكُمۡۚ وَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٞ فِيمَآ أَخۡطَأۡتُم بِهِۦ وَلَٰكِن مَّا تَعَمَّدَتۡ قُلُوبُكُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا
Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Na ikiwa hamwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika Dini, na rafiki zenu. Wala si lawama juu yenu kwa mlivyo kosea. Lakini ipo lawama katika yale ziliyo fanya nyoyo zenu kwa makusudi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Wanasibishieni hawa watoto kwa baba zao khasa. Hayo ndiyo ya uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu. Ikiwa hamwajui baba zao walio nasibiana nao khasa, basi hao ni ndugu zenu katika Dini na rafiki zenu wa kuwanusuru. Wala nyinyi hamna dhambi ikiwa mmewanasibisha na watu wasio kuwa baba zao kwa kukosea. Lakini inakuwa dhambi kwa mlio kusudia kwa nyoyo zenu baada ya kwisha jua yaliyo. Na Mwenyezi Mungu anakusameheni kwa kukosea kwenu, na anaikubali toba yenu kwa makosa mliyo kusudia.
التفاسير العربية:
ٱلنَّبِيُّ أَوۡلَىٰ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ مِنۡ أَنفُسِهِمۡۖ وَأَزۡوَٰجُهُۥٓ أُمَّهَٰتُهُمۡۗ وَأُوْلُواْ ٱلۡأَرۡحَامِ بَعۡضُهُمۡ أَوۡلَىٰ بِبَعۡضٖ فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ إِلَّآ أَن تَفۡعَلُوٓاْ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِكُم مَّعۡرُوفٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا
Nabii ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Na wake zake ni mama zao. Na jamaa ni karibu wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuliko Waumini wengine na Wahamiaji. Ila muwe mnawafanyia wema marafiki zenu. Haya yamekwisha andikwa Kitabuni.
Nabii Muhammad ni mwenye kustahiki zaidi urafiki kwa Waumini, na ana huruma zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao. Basi yawapasa wao wampende na wamt'ii. Na wake zake ni Mama zao kwa kuwatukuza na kuwahishimu, na kuwa ni haramu juu yao kuwaoa baada yake. Na jamaa walio khusiana ni karibu zaidi kuliko Waumini wenginewe na Wahajiri, walio hama Makka, kwa kurithiana wao kwa wao kama ilivyo wajibika katika Qur'ani. Lakini inafaa kumfanyia wema mlio fanya urafiki naye katika Dini asiye kuwa jamaa yenu, kwa kuwapa wema na mapenzi au hata kumuandikia mali katika wasia. Hayo ya kurithiana jamaa walio khusiana yamethibiti katika Kitabu cha Qur'ani wala hayawezi kubadilishwa.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ أَخَذۡنَا مِنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ مِيثَٰقَهُمۡ وَمِنكَ وَمِن نُّوحٖ وَإِبۡرَٰهِيمَ وَمُوسَىٰ وَعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَۖ وَأَخَذۡنَا مِنۡهُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا
Na tulipo chukua ahadi kwa Manabii na kwako wewe, na Nuhu na Ibrahim na Isa mwana wa Mariamu, na tulichukua kwao ahadi ngumu!
Na kumbusha pale tulipo fanya agano na Manabii wote walio tangulia kuwa watafikisha ujumbe na wito kulingania Dini iliyo sawa, na wewe, na Nuhu, na Ibrahim, na Musa, na Isa bin Maryamu; na tukachukua kwao agano lenye shani kubwa.
التفاسير العربية:
لِّيَسۡـَٔلَ ٱلصَّٰدِقِينَ عَن صِدۡقِهِمۡۚ وَأَعَدَّ لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابًا أَلِيمٗا
Ili (Mwenyezi Mungu) awaulize wakweli juu ya ukweli wao. Na amewaandalia makafiri adhabu chungu.
Ili Mwenyezi Mungu awaulize Manabii Siku ya Kiyama juu ya waliyo waambia kaumu zao. Na Yeye amewaandalia wenye kuwakataa Mitume adhabu yenye kutia uchungu.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَةَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ جَآءَتۡكُمۡ جُنُودٞ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا وَجُنُودٗا لَّمۡ تَرَوۡهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرًا
Enyi mlio amini! Zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu. Pale yalipo kufikilieni majeshi, nasi tukayapelekea upepo, na majeshi msiyo yaona. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
Enyi mlio amini zikumbukeni neema na fadhila za Mwenyezi Mungu zilio juu yenu, pale yalipo kujieni makundi katika Siku ya Handaki. Tukawapelekea upepo mkali wa kimbunga ubaridi, na Malaika ambao nyinyi hamwaoni. Kikawaingia kiwewe katika nyoyo zao. Na Mwenyezi Mungu alikuwa Mwenye kuviona vitendo vyenu, na ukweli wa niya zenu. Basi akaingia kukulindeni.
التفاسير العربية:
إِذۡ جَآءُوكُم مِّن فَوۡقِكُمۡ وَمِنۡ أَسۡفَلَ مِنكُمۡ وَإِذۡ زَاغَتِ ٱلۡأَبۡصَٰرُ وَبَلَغَتِ ٱلۡقُلُوبُ ٱلۡحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِٱللَّهِ ٱلظُّنُونَا۠
Walipo kujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipo kodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali.
Walipo kujieni kutoka upande wa juu ya bonde, na kutoka chini, na macho yakakodoka, na nyoyo zikapanda mpaka kwenye koo, kwa kufazaika na kubabaika. Na nyinyi katika wakati ule wa shida kubwa kila namna ya dhana zilikujieni juu ya ahadi ya Mwenyezi Mungu. Si makusudio ya maneno haya kuwa maadui walikuja kutoka kila upande. Tukiangalia ufafanuzi wa tukio hili inadhihirika kuwa makusudio ni kuwa walio kuja kutoka upande wa juu ya Waislamu, ni kabila ya Ghat'fan na walio wafuata katika wakaazi wa Najdi, kwani wao walikuja pande za juu ya Bara Arabu upande wa mashariki. Na inatudhihirikia kuwa walio kuja upande wa chini ya Waumini ni Makureshi, kwa sababu wao walikuja kutoka upande wa chini ya Bara Arabu upande wa magharibi.
التفاسير العربية:
هُنَالِكَ ٱبۡتُلِيَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ وَزُلۡزِلُواْ زِلۡزَالٗا شَدِيدٗا
Hapo ndipo Waumini walipo jaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali.
Katika wakati ule Waumini walifanyiwa mtihani juu ya kusubiri kwao juu ya Imani. Wakatikisika kwa khofu kwa mtikiso mkubwa.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ يَقُولُ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ مَّا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ إِلَّا غُرُورٗا
Na walipo sema wanaafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao: Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakutuahidi ila udanganyifu tu.
Na kumbuka shaka iliyo waingia wanaafiki na wagonjwa wa nyoyo walipo sema: Ahadi aliyo tupa Mwenyezi Mungu na Mtume ni ahadi ya uwongo, imekusudiwa kutudanganya tu.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ قَالَت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ يَٰٓأَهۡلَ يَثۡرِبَ لَا مُقَامَ لَكُمۡ فَٱرۡجِعُواْۚ وَيَسۡتَـٔۡذِنُ فَرِيقٞ مِّنۡهُمُ ٱلنَّبِيَّ يَقُولُونَ إِنَّ بُيُوتَنَا عَوۡرَةٞ وَمَا هِيَ بِعَوۡرَةٍۖ إِن يُرِيدُونَ إِلَّا فِرَارٗا
Na kundi moja katika miongoni mwao lilipo sema: Enyi watu wa Yathrib! Hapana kukaa nyinyi! Rudini. Na kundi jingine miongoni mwao likaomba ruhusa kwa Mtume kwa kusema: Hakika nyumba zetu ni tupu. Wala hazikuwa tupu; hawakutaka ila kukimbia tu.
Na kumbuka walipo sema kikundi cha wanaafiki na ambao wanao rega rega: Enyi watu wa (Yathrib, yaani) Madina! Hapana maana kubakia hapa nyinyi katika vita hivi vya kushindwa. Rudini mwende makwenu. Na kundi jingine kati yao walimtaka ruhusa Mtume warejee Madina, na wakasema: Hakika nyumba zetu hazina ulinzi. Hatuna budi kurejea tukazilinde. Wala nyumba zao hazikuwa khatarini kabisa kama walivyo sema. Hawakutaka ila kukimbia vita tu, kwa udhuru wa uwongo.
التفاسير العربية:
وَلَوۡ دُخِلَتۡ عَلَيۡهِم مِّنۡ أَقۡطَارِهَا ثُمَّ سُئِلُواْ ٱلۡفِتۡنَةَ لَأٓتَوۡهَا وَمَا تَلَبَّثُواْ بِهَآ إِلَّا يَسِيرٗا
Na lau kuwa wangeli ingiliwa kwa pande zote, kisha wakatakiwa kufanya khiana, wangeli fanya, na wasingeli sita ila kidogo tu.
Lau kuwa makundi ya majeshi ya maadui wangeli waingilia Madina kwa kila upande, na wakawataka watangaze kuwa wameuwacha Uislamu na wawapige vita Waislamu bila ya shaka wangeli wakubalia yale waliyo takiwa, na wala wasingeli sita ila muda mfupi tu.
التفاسير العربية:
وَلَقَدۡ كَانُواْ عَٰهَدُواْ ٱللَّهَ مِن قَبۡلُ لَا يُوَلُّونَ ٱلۡأَدۡبَٰرَۚ وَكَانَ عَهۡدُ ٱللَّهِ مَسۡـُٔولٗا
Na hakika walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kwamba hawatageuza migongo yao. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa.
Na hakika hawa wenye kukimbia kutoka midani ya vita walikwisha muahidi Mwenyezi Mungu kabla yake kuwa watasimama imara katika vita pamoja na Mtume, na wala hawatakimbia. Na ahadi ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuulizwa kwa yule mwenye kuitoa, na yampasa aitimize.
التفاسير العربية:
قُل لَّن يَنفَعَكُمُ ٱلۡفِرَارُ إِن فَرَرۡتُم مِّنَ ٱلۡمَوۡتِ أَوِ ٱلۡقَتۡلِ وَإِذٗا لَّا تُمَتَّعُونَ إِلَّا قَلِيلٗا
Sema: Kukimbia hakukufaeni kitu ikiwa mnakimbia mauti au kuuwawa, na hata hivyo hamtastareheshwa ila kidogo tu.
Waambie: Kukimbia hakukufaeni kitu ikiwa ndio mnayakimbia mauti au kuuwawa, maadamu ajali yenu imekwisha fika. Na ikiwa haijafika, basi hamtobaki mkistarehe katika dunia ila kwa muda wa umri wenu, nao ni mchache.
التفاسير العربية:
قُلۡ مَن ذَا ٱلَّذِي يَعۡصِمُكُم مِّنَ ٱللَّهِ إِنۡ أَرَادَ بِكُمۡ سُوٓءًا أَوۡ أَرَادَ بِكُمۡ رَحۡمَةٗۚ وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Sema: Ni nani wa kukulindeni na Mwenyezi Mungu pindi akikutakieni uovu, au akikutakieni rehema? Wala hawatapata mlinzi wala msaidizi isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
Waambie hawa wanao babaika: Nani atakaye kulindeni na Mwenyezi Mungu akitaka kukuleteeni shari, au atakaye kuzuieni msipate kheri, akitaka Yeye kukurehemuni? Wala hawatapata badala ya Mwenyezi Mungu yeyote wa kuwalinda au kuwaokoa.
التفاسير العربية:
۞ قَدۡ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ ٱلۡمُعَوِّقِينَ مِنكُمۡ وَٱلۡقَآئِلِينَ لِإِخۡوَٰنِهِمۡ هَلُمَّ إِلَيۡنَاۖ وَلَا يَأۡتُونَ ٱلۡبَأۡسَ إِلَّا قَلِيلًا
Kwa hakika Mwenyezi Mungu anawajua hao wanao zuilia, na wanao waambia ndugu zao: Njooni kwetu! Wala hawaingii vitani ila kidogo tu.
Hakika Mwenyezi Mungu anawajua wanao zuilia miongoni mwenu, na wanao waambia ndugu zao: Unganeni nasi! Wala hawaingii katika vita vinapo shitadi ila kidogo tu.
التفاسير العربية:
أَشِحَّةً عَلَيۡكُمۡۖ فَإِذَا جَآءَ ٱلۡخَوۡفُ رَأَيۡتَهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ تَدُورُ أَعۡيُنُهُمۡ كَٱلَّذِي يُغۡشَىٰ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡمَوۡتِۖ فَإِذَا ذَهَبَ ٱلۡخَوۡفُ سَلَقُوكُم بِأَلۡسِنَةٍ حِدَادٍ أَشِحَّةً عَلَى ٱلۡخَيۡرِۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَمۡ يُؤۡمِنُواْ فَأَحۡبَطَ ٱللَّهُ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٗا
Wana choyo juu yenu. Ikifika khofu utawaona wanakutazama na macho yao yanazunguka, kama yule ambaye aliye zimia kwa kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanakuudhini kwa ndimi kali, nao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini, basi Mwenyezi Mungu amevibat'ilisha vitendo vyao. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Wana pupa juu yenu kwa kuonekana dhaahiri inapo kuwa hapana khofu. Na ikija khofu ya adui au ya Mtume s.a.w. utawaona wanakuangalia na macho yao yanawazunguka hawajitambui, kama hali ya mwenye kuzimia wakati wa sumbuko la kukaribia mauti. Na khofu ikiondoka wanapita mpaka kukutukaneni na kukushutumuni kwa ndimi za kukata. Hao ni mabakhili kwa kila la kheri. Hao hawakuamini kwa nyoyo zao, ijapo kuwa wametangaza kuwa ni Waislamu. Basi Mwenyezi Mungu amezibat'ilisha a'mali zao kwa ukafiri wao walio dhamiria. Na kubat'ilisha huko ni jambo jepesi kwa Mwenyezi Mungu. Aya hii tukufu inaashiria ukweli wa kisayansi ambao ulikuwa haukujuulikana namna yake wakati wa kuteremka Qur'ani Tukufu. Ukweli huo ni kuwa jicho wakati wa kukurubia mauti au wakati wa khofu huzunguka. Na katika sababu za hayo ni kuwa kwa shida ya khofu utambuzi hutoweka, ikawa mtu hajitambui. Vituo vya navo zisio tambua katika ubongo hupoteza mizani yake, basi huwa huyo mwenye khofu kama mfano wa mwenye kuzimia kwa kukaribia kufa, jicho lake huzunguka na mboni ya jicho hupanuka, na hubaki katika hali ya kukodoa macho mpaka kufa.
التفاسير العربية:
يَحۡسَبُونَ ٱلۡأَحۡزَابَ لَمۡ يَذۡهَبُواْۖ وَإِن يَأۡتِ ٱلۡأَحۡزَابُ يَوَدُّواْ لَوۡ أَنَّهُم بَادُونَ فِي ٱلۡأَعۡرَابِ يَسۡـَٔلُونَ عَنۡ أَنۢبَآئِكُمۡۖ وَلَوۡ كَانُواْ فِيكُم مَّا قَٰتَلُوٓاْ إِلَّا قَلِيلٗا
Wanafikiri yale makundi ya maadui hayajaondoka. Na yakija hayo makundi watatamani laiti wao wako majangwani pamoja na mabedui, wakiuliza khabari zenu. Na lau wakiwa pamoja nanyi hawapigani ila kidogo tu.
Wanadhani hawa wanaafiki kwamba majeshi ya makafiri yaliyo ungana bado yapo mahali pao wanaizinga Madina. Na hayo makundi ya maadui yakirejea tena, watatamani hao woga laiti wangeli kuwa wanaishi pamoja na mabedui huko majangwani wakidondoa khabari zenu. Na lau wakibaki kwenye kambi zao, na wasikimbie, na majeshi mawili yakapambana, basi hata hivyo wasinge pigana pamoja nanyi ila kidogo tu, kama kujionyesha na watajwe kuwa nao walikuwamo.
التفاسير العربية:
لَّقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِي رَسُولِ ٱللَّهِ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَ وَذَكَرَ ٱللَّهَ كَثِيرٗا
Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa anaye mtaraji Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na akamkumbuka Mwenyezi Mungu sana.
Hakika nyinyi mna kiigizo kizuri kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu, na neema za Siku ya Mwisho, na akamkumbuka na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa wingi katika khofu na kutumai, na katika shida, na katika neema.
التفاسير العربية:
وَلَمَّا رَءَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلۡأَحۡزَابَ قَالُواْ هَٰذَا مَا وَعَدَنَا ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥ وَصَدَقَ ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥۚ وَمَا زَادَهُمۡ إِلَّآ إِيمَٰنٗا وَتَسۡلِيمٗا
Na Waumini walipo yaona makundi, walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Na hayo hayakuwazidisha ila Imani na ut'iifu.
Na Waumini walipo yaona makundi ya washirikina walisema: Haya ndiyo aliyo tuahidi Mwenyezi Mungu na Mtume wake zamani. Kwani walituahidi tutapata shida, na kisha tutapata ushindi. Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamesema kweli. Taabu hizi basi, hazikuwazidishia ila nguvu za kumuamini Mwenyezi Mungu, na uzuri wa kuinyenyekea kwao hukumu yake.
التفاسير العربية:
مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ رِجَالٞ صَدَقُواْ مَا عَٰهَدُواْ ٱللَّهَ عَلَيۡهِۖ فَمِنۡهُم مَّن قَضَىٰ نَحۡبَهُۥ وَمِنۡهُم مَّن يَنتَظِرُۖ وَمَا بَدَّلُواْ تَبۡدِيلٗا
Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.
Miongoni mwa hawa Waumini wapo watu walio muahidi Mwenyezi Mungu kuwa watasimama imara na Mtume katika vita. Nao wakatimiza ahadi yao. Miongoni mwao wapo walio pata utukufu wa kufa mashahidi, na wengine wamebakia wahai wakingojea nao kupata utukufu huo. Wala hawakuigeuza ahadi ya Mwenyezi Mungu waliyo jikatia juu ya nafsi yao, wala hawakugeuza chochote katika hayo.
التفاسير العربية:
لِّيَجۡزِيَ ٱللَّهُ ٱلصَّٰدِقِينَ بِصِدۡقِهِمۡ وَيُعَذِّبَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ إِن شَآءَ أَوۡ يَتُوبَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Ili Mwenyezi Mungu awalipe wakweli kwa sababu ya ukweli wao, na awaadhibu wanaafiki pindi akitaka, au apokee toba yao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ili Mwenyezi Mungu apate kuwalipa Waumini walio wakweli kwa sababu ya ukweli wao katika Imani yao na kutimiza kwao ahadi waliyo itoa. Na awaadhibu wanaafiki - pindi akitaka - au amwezeshe aliye elekea, kufikia toba. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe kwa kukubali toba, Mwenye kurehemu kwa kusamehe maasi.
التفاسير العربية:
وَرَدَّ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِغَيۡظِهِمۡ لَمۡ يَنَالُواْ خَيۡرٗاۚ وَكَفَى ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱلۡقِتَالَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ قَوِيًّا عَزِيزٗا
Na Mwenyezi Mungu aliwarudisha nyuma makafiri juu ya ghadhabu yao; hawakupata kheri yoyote. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na uweza.
Mwenyezi Mungu akawarudisha nyuma makafiri walio jiunga makundi kumpiga Mtume na nyoyo zao zimejaa chuki. Hawakupata kheri yoyote kwa ushindi wala ngawira. Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini wasipate mashaka, kwa kuwapatiliza wale makafiri kwa upepo na Malaika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza wa kutimiliza alitakalo, ni Mwenye nguvu hapana wa kumshinda.
التفاسير العربية:
وَأَنزَلَ ٱلَّذِينَ ظَٰهَرُوهُم مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ مِن صَيَاصِيهِمۡ وَقَذَفَ فِي قُلُوبِهِمُ ٱلرُّعۡبَ فَرِيقٗا تَقۡتُلُونَ وَتَأۡسِرُونَ فَرِيقٗا
Na akawateremsha wale walio wasaidia (maadui) katika Watu wa Kitabu kutoka katika ngome zao; na akatia khofu katika nyoyo zao. Baadhi yao mkawa mnawauwa, na wengine mnawateka.
Na Mwenyezi Mungu aliwateremsha walio wasaidia makundi ya maadui katika Watu wa Kitabu, nao ni Mayahudi wa Bani Quraidha, kutokana na ngome zao walipo kuwa wakijilinda ndani yake. Na akaingiza katika nyoyo zao kitisho. Wengine mkawa mnawawauwa, nao ni wanaume, na wengine mnawachukua mateka, nao ni wanawake na watoto.
التفاسير العربية:
وَأَوۡرَثَكُمۡ أَرۡضَهُمۡ وَدِيَٰرَهُمۡ وَأَمۡوَٰلَهُمۡ وَأَرۡضٗا لَّمۡ تَطَـُٔوهَاۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٗا
Na akakurithisheni ardhi zao na nyumba zao na mali zao, na ardhi msiyo pata kuikanyaga. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
Na akakurithisheni ardhi zao, na nyumba zao, na mali zao, na ardhi ambazo nyayo zenu hazijapata kuzikanyaga kabla yake. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Muweza wa kutimiza kila alitakalo.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّأَزۡوَٰجِكَ إِن كُنتُنَّ تُرِدۡنَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا وَزِينَتَهَا فَتَعَالَيۡنَ أُمَتِّعۡكُنَّ وَأُسَرِّحۡكُنَّ سَرَاحٗا جَمِيلٗا
Ewe Nabii! Waambie wake zako: Ikiwa mnataka maisha ya dunia na pambo lake, basi njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni mwachano mzuri.
Ewe Nabii! Waambie wake zako kwa kuwanasihi: Ikiwa mnataka maisha ya duniani na starehe zake, basi jongeeni nitakupeni cha kupunguza upweke wa talaka, itakuwa ni tunza yenu. Na nitakupeni talaka isiyo na uovu ndani yake.
التفاسير العربية:
وَإِن كُنتُنَّ تُرِدۡنَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَٱلدَّارَ ٱلۡأٓخِرَةَ فَإِنَّ ٱللَّهَ أَعَدَّ لِلۡمُحۡسِنَٰتِ مِنكُنَّ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Na ikiwa mnamtaka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema, miongoni mwenu, malipo makubwa.
Na ikiwa mnakhiari mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na neema za nyumba ya Akhera, na mnaridhi maisha magumu mlio nayo hivi sasa, basi hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia mfano wenu nyinyi miongoni mwa wanawake walio wema kwa vitendo vyao, ujira ambao haukadiriki.
التفاسير العربية:
يَٰنِسَآءَ ٱلنَّبِيِّ مَن يَأۡتِ مِنكُنَّ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖ يُضَٰعَفۡ لَهَا ٱلۡعَذَابُ ضِعۡفَيۡنِۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٗا
Enyi wake wa Nabii! Atakaye fanya uchafu dhaahiri miongoni mwenu, atazidishiwa adhabu mara mbili. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Enyi wake wa Nabii! Miongoni mwenu mwenye kufanya makosa yaliyo dhaahiri ubaya wake, basi juu ya adhabu yake zinaongezwa adhabu mbili, ili iwe adhabu tatu kwa kulinganisha na mwenziwe. Na kuongeza huko kwa Mwenyezi Mungu ni kwepesi.
التفاسير العربية:
۞ وَمَن يَقۡنُتۡ مِنكُنَّ لِلَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا نُّؤۡتِهَآ أَجۡرَهَا مَرَّتَيۡنِ وَأَعۡتَدۡنَا لَهَا رِزۡقٗا كَرِيمٗا
NA MIONGONI mwenu atakeye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, tutampa malipo yake mara mbili, na tutamwandalia riziki ya ukarimu.
Na katika nyinyi mwenye kudumu juu ya kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akatenda mema, Mwenyezi Mungu atampa ujira mara mbili. Na tumemuandalia kwa Akhera riziki ya kipimo kizuri.
التفاسير العربية:
يَٰنِسَآءَ ٱلنَّبِيِّ لَسۡتُنَّ كَأَحَدٖ مِّنَ ٱلنِّسَآءِ إِنِ ٱتَّقَيۡتُنَّۚ فَلَا تَخۡضَعۡنَ بِٱلۡقَوۡلِ فَيَطۡمَعَ ٱلَّذِي فِي قَلۡبِهِۦ مَرَضٞ وَقُلۡنَ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا
Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema.
Enyi wake wa Mtume! Nyinyi si kama wanawake wengine kwa fadhila na utukufu. Kama mnataka uchamngu, basi msizungumze kwa maneno ya kuregeza sauti, hata ambaye ana uharibifu katika moyo wake akaingia tamaa. Kusema kwenu kuwe kama kawaida sio kujitia.
التفاسير العربية:
وَقَرۡنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجۡنَ تَبَرُّجَ ٱلۡجَٰهِلِيَّةِ ٱلۡأُولَىٰۖ وَأَقِمۡنَ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتِينَ ٱلزَّكَوٰةَ وَأَطِعۡنَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُذۡهِبَ عَنكُمُ ٱلرِّجۡسَ أَهۡلَ ٱلۡبَيۡتِ وَيُطَهِّرَكُمۡ تَطۡهِيرٗا
Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani. Na shikeni Swala, na toeni Zaka, na mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu, enyi Watu wa Nyumba ya Mtume, na kukusafisheni baarabara.
Na kaeni nyumbani kwenu, wala msitoke ila kwa haja. Wala msidhihirishe uzuri wenu na mapambo yenu kwa wanaume pale mnapo toka, kama walivyo kuwa wakifanya watu wa ujahili wa zamani. Na timizeni Swala kwa ukamilifu, na toeni Zaka, na fuateni amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hakika Mwenyezi Mungu anataka, kwa yote anayo kuamrisheni na kukukatazeni, mpate utukufu na hishima, ili muondokewe na madhambi na maasia, enyi Ahli Baiti Nnabii, Watu wa Nyumba ya Nabii, na akusafisheni kwa usafi usio kuwa na shaka.
التفاسير العربية:
وَٱذۡكُرۡنَ مَا يُتۡلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ وَٱلۡحِكۡمَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ لَطِيفًا خَبِيرًا
Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye khabari.
Na hifadhini yanayo somwa katika nyumba zenu ya Qur'ani aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu, na hikima zilio sawa za Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua mambo yalio zama ndani kabisa na ya hakika yake. Basi tahadharini na kwenda kinyume naye na kumuasi Mtume wake.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱلۡمُسۡلِمِينَ وَٱلۡمُسۡلِمَٰتِ وَٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ وَٱلۡقَٰنِتِينَ وَٱلۡقَٰنِتَٰتِ وَٱلصَّٰدِقِينَ وَٱلصَّٰدِقَٰتِ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَٱلصَّٰبِرَٰتِ وَٱلۡخَٰشِعِينَ وَٱلۡخَٰشِعَٰتِ وَٱلۡمُتَصَدِّقِينَ وَٱلۡمُتَصَدِّقَٰتِ وَٱلصَّٰٓئِمِينَ وَٱلصَّٰٓئِمَٰتِ وَٱلۡحَٰفِظِينَ فُرُوجَهُمۡ وَٱلۡحَٰفِظَٰتِ وَٱلذَّٰكِرِينَ ٱللَّهَ كَثِيرٗا وَٱلذَّٰكِرَٰتِ أَعَدَّ ٱللَّهُ لَهُم مَّغۡفِرَةٗ وَأَجۡرًا عَظِيمٗا
Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa.
Hakika wenye kut'ii miongoni mwa wanaume na wanawake, na wenye kumsadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wanaume na wanawake, na wenye kusimama kwa ut'iifu wanaume na wanawake, na walio wa kweli katika kauli zao na vitendo vyao katika wanaume na wanawake, na wenye kusubiri katika kubeba mashaka kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wanaume na wanawake, na wanyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu wanaume na wanawake, na wenye kuzihifadhi tupu zao kwa yasiyo kuwa halali wanaume na wanawake, na wenye kumdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi katika nyoyo zao na ndimi zao wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia kuwasamehe madhambi yao, na kuwalipa malipo makubwa kwa vitendo vyao.
التفاسير العربية:
وَمَا كَانَ لِمُؤۡمِنٖ وَلَا مُؤۡمِنَةٍ إِذَا قَضَى ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَمۡرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ ٱلۡخِيَرَةُ مِنۡ أَمۡرِهِمۡۗ وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلٗا مُّبِينٗا
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.
Haimjuzii Muumini, mwanamume au mwanamke, kuwa na khiari katika jambo lolote baada ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake wakisha lihukumia. Na mwenye kwenda kinyume na alivyo hukumu Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi amejitenga mbali na njia iliyo sawa kwa umbali ulio dhaahiri.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ تَقُولُ لِلَّذِيٓ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَأَنۡعَمۡتَ عَلَيۡهِ أَمۡسِكۡ عَلَيۡكَ زَوۡجَكَ وَٱتَّقِ ٱللَّهَ وَتُخۡفِي فِي نَفۡسِكَ مَا ٱللَّهُ مُبۡدِيهِ وَتَخۡشَى ٱلنَّاسَ وَٱللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخۡشَىٰهُۖ فَلَمَّا قَضَىٰ زَيۡدٞ مِّنۡهَا وَطَرٗا زَوَّجۡنَٰكَهَا لِكَيۡ لَا يَكُونَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ حَرَجٞ فِيٓ أَزۡوَٰجِ أَدۡعِيَآئِهِمۡ إِذَا قَضَوۡاْ مِنۡهُنَّ وَطَرٗاۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولٗا
Na ulipo mwambia yule Mwenyezi Mungu aliye mneemesha, nawe ukamneemesha: Shikamana na mkeo, na mche Mwenyezi Mungu. Na ukaficha nafsini mwako aliyo taka Mwenyezi Mungu kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki zaidi kumchelea. Basi Zaid alipo kwisha haja naye tulikuoza wewe, ili isiwe taabu kwa Waumini kuwaoa wake wa watoto wao wa kupanga watapo kuwa wamekwisha timiza nao shuruti za t'alaka. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutekelezwa.
Na kumbuka pale ulipo mwambia Zaid bin Haritha, ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha kwa kumwongoa kwenye Uislamu, na wewe ukamneemesha kwa kumlea na kumkomboa utumwani: Shikamana na mkeo, Zainab binti Jahsh, na umche Mwenyezi Mungu, na vumilia kukaa naye. Na wewe ulikuwa unaficha nafsini mwako ambayo Mwenyezi Mungu atakuja yadhihirisha, yaani kuwa yeye atampa t'alaka na wewe utakuja muwoa. Nawe ukakhofu watu wasije kukulaumu. Na Mwenyezi Mungu ndiye anaye stahiki umkhofu, ijapo kuwa hayo ni mashaka juu yako. Basi Zaid alipo kwisha haja naye, na akampa t'alaka kujiondolea dhiki ya kuishi naye, tukakuoza wewe, ili iwe ni chanzo cha kuvunja ada iliyo mbovu. Baada ya hayo hapana ubaya tena kwa Waislamu kuwaoa walio kuwa wake za walio kuwa wamewapanga utoto, baada ya kwisha wat'aliki. Na amri ya Mwenyezi Mungu aitakayo ni lazima iwe bila ya pingamizi.
التفاسير العربية:
مَّا كَانَ عَلَى ٱلنَّبِيِّ مِنۡ حَرَجٖ فِيمَا فَرَضَ ٱللَّهُ لَهُۥۖ سُنَّةَ ٱللَّهِ فِي ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلُۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ قَدَرٗا مَّقۡدُورًا
Hapana ubaya kwa Nabii kufanya aliyo mhalalishia Mwenyezi Mungu. Huo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu kwa walio pita zamani. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kudura iliyo kwisha kadiriwa.
Nabii hana makosa kutenda kitendo alicho muamrisha Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ameweka mwendo huo kwa Manabii walio tangulia, kuwa wasipige marfuku alicho wahalalishia na akawakunjulia. Na amri ya Mwenyezi Mungu ni kupitisha alicho pitisha, na hukumu iliyo thibiti.
التفاسير العربية:
ٱلَّذِينَ يُبَلِّغُونَ رِسَٰلَٰتِ ٱللَّهِ وَيَخۡشَوۡنَهُۥ وَلَا يَخۡشَوۡنَ أَحَدًا إِلَّا ٱللَّهَۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبٗا
(Hao wa zamani) walio kuwa wakifikisha risala za Mwenyezi Mungu na wanamwogopa Yeye, na wala hawamwogopi yeyote isipo kuwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye atoshaye kuhisabu.
Manabii hao ndio walio wafikishia watu ujumbe wa Mwenyezi Mungu kama tulivyo wateremshia. Nao wanamkhofu Yeye, wala hawamkhofu yeyote asiye kuwa Yeye. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Yeye ndiye Muangalizi Mwenye kuhisabu.
التفاسير العربية:
مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَآ أَحَدٖ مِّن رِّجَالِكُمۡ وَلَٰكِن رَّسُولَ ٱللَّهِ وَخَاتَمَ ٱلنَّبِيِّـۧنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا
Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu hata iwe ni haramu kwake kumwoa mt'alaka wake. Lakini yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na ni Mwenye kukhitimisha Manabii wote. Juu yake ni kufikilisha ujumbe kama alivyo muamrisha Mola wake Mlezi, bila ya kumchelea yeyote. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuvizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ ذِكۡرٗا كَثِيرٗا
Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru.
Enyi ambao mmeamini! Msifuni Mwenyezi Mungu kwa namna mbali mbali za sifa, na mfanye hayo kwa wingi. Na mtakaseni na kila kisicho kuwa laiki naye mwanzo wa mchana na mwisho wake.
التفاسير العربية:
وَسَبِّحُوهُ بُكۡرَةٗ وَأَصِيلًا
Na mtakaseni asubuhi na jioni.
Enyi ambao mmeamini! Msifuni Mwenyezi Mungu kwa namna mbali mbali za sifa, na mfanye hayo kwa wingi. Na mtakaseni na kila kisicho kuwa laiki naye mwanzo wa mchana na mwisho wake.
التفاسير العربية:
هُوَ ٱلَّذِي يُصَلِّي عَلَيۡكُمۡ وَمَلَٰٓئِكَتُهُۥ لِيُخۡرِجَكُم مِّنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِۚ وَكَانَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ رَحِيمٗا
Yeye na Malaika wake ndio wanakurehemuni ili kukutoeni gizani mwende kwenye nuru. Naye ni Mwenye kuwarehemu Waumini.
Na Yeye ndiye aliye kuahidini kukupeni rehema yake na upole wake. Na Malaika wake wanakuombeeni maghfira na uwongofu, ili Mwenyezi Mungu akutoeni kwenye giza la ukafiri na upotovu, mwendee kwenye nuru na ut'iifu. Na Mwenyezi Mungu hakika ni Mkuu wa kuwarehemu Waumini.
التفاسير العربية:
تَحِيَّتُهُمۡ يَوۡمَ يَلۡقَوۡنَهُۥ سَلَٰمٞۚ وَأَعَدَّ لَهُمۡ أَجۡرٗا كَرِيمٗا
Maamkiano yao siku ya kukutana naye yatakuwa: Salama! Na amewaandalia malipo ya ukarimu.
Maamkio yao siku watakapo kutana naye ni: Amani na Salama kwao. Na amewatengezea kwa vitendo vyao ujira wa ukarimu utakao waonyesha fadhila zake.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ شَٰهِدٗا وَمُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا
Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji,
Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma kwa watu wote uwapelekee ujumbe wa Uislamu. Ushuhudie Haki, na uwabashirie Waumini kwamba watapata kheri na thawabu, na uwaonye makafiri kuwa watapata mwisho muovu.
التفاسير العربية:
وَدَاعِيًا إِلَى ٱللَّهِ بِإِذۡنِهِۦ وَسِرَاجٗا مُّنِيرٗا
Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru.
Na umetumwa uwe ni mwenye kuwaita viumbe vyote vimwendee Mwenyezi Mungu kwa amri yake. Na uwe ni taa ya uwongofu kuwaongoa kwa nuru yake waliopo katika kiza cha shaka.
التفاسير العربية:
وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ بِأَنَّ لَهُم مِّنَ ٱللَّهِ فَضۡلٗا كَبِيرٗا
Na wabashirie Waumini ya kwamba wana fadhila kubwa inayo toka kwa Mwenyezi Mungu.
Na wabashirie Waumini kwamba watapata kheri kubwa ya kuzidi katika dunia na Akhera.
التفاسير العربية:
وَلَا تُطِعِ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَدَعۡ أَذَىٰهُمۡ وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا
Wala usiwat'ii makafiri na wanaafiki, na usijali udhia wao. Nawe mtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mtegemewa.
Na wala usiwafuate makafiri na wanaafiki, wala usijishughulishe na maudhi yao. Na mfanye Mwenyezi Mungu ndiye Wakili wako wa kumtegemea kukulinda na madhara yao na shari zao. Na Mwenyezi Mungu anakutosha kabisa kuwa ndiye Mtegemewa wa kukukifia na kukukinaisha.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نَكَحۡتُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ طَلَّقۡتُمُوهُنَّ مِن قَبۡلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمۡ عَلَيۡهِنَّ مِنۡ عِدَّةٖ تَعۡتَدُّونَهَاۖ فَمَتِّعُوهُنَّ وَسَرِّحُوهُنَّ سَرَاحٗا جَمِيلٗا
nyi mlio amini! Mkiwaoa wanawake, Waumini, kisha mkawapa t'alaka kabla ya kuwagusa, basi hamna eda juu yao mtakayo ihisabu. Basi wapeni cha kuwaliwaza, na muwawache kwa kuwachana kwa wema.
Enyi mlio amini! Mkifunga ndoa na wanawake Waumini, kisha mkawat'aliki kabla ya hamjawaingilia, basi haiwalazimu eda wao mkawa mnaihisabu. Basi wapeni kitu katika mali kwa kuwapoza. Na mwatoe majumbani kwenu bila ya kuwaletea madhara yoyote.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ إِنَّآ أَحۡلَلۡنَا لَكَ أَزۡوَٰجَكَ ٱلَّٰتِيٓ ءَاتَيۡتَ أُجُورَهُنَّ وَمَا مَلَكَتۡ يَمِينُكَ مِمَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ وَبَنَاتِ عَمِّكَ وَبَنَاتِ عَمَّٰتِكَ وَبَنَاتِ خَالِكَ وَبَنَاتِ خَٰلَٰتِكَ ٱلَّٰتِي هَاجَرۡنَ مَعَكَ وَٱمۡرَأَةٗ مُّؤۡمِنَةً إِن وَهَبَتۡ نَفۡسَهَا لِلنَّبِيِّ إِنۡ أَرَادَ ٱلنَّبِيُّ أَن يَسۡتَنكِحَهَا خَالِصَةٗ لَّكَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۗ قَدۡ عَلِمۡنَا مَا فَرَضۡنَا عَلَيۡهِمۡ فِيٓ أَزۡوَٰجِهِمۡ وَمَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُمۡ لِكَيۡلَا يَكُونَ عَلَيۡكَ حَرَجٞۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Ewe Nabii! Tumekuhalalishia wake zako ulio wapa mahari yao, na ulio wamiliki kwa mkono wako wa kulia katika alio kupa Mwenyezi Mungu, na mabinti ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada za mama yako walio hama pamoja nawe; na mwanamke Muumini akijitoa mwenyewe kwa Nabii, kama mwenyewe Nabii akitaka kumwoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Sisi tunajua tuliyo wafaridhia wao katika wake zao na wanawake ilio wamiliki mikono yao ya kulia. Ili isiwe dhiki kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekuhalalishia wake zako ulio wapa mahari. Na tumekuhalishia wajakazi ulio wamiliki mkono wako wa kulia, katika alio kuneemeshea Mwenyezi Mungu. Na tumekuhalalishia kuwaoa mabinti ami zako, na mabinti wa shangazi zako, na mabinti wa wajomba zako, na mabinti wa dada, yaani ndugu wa kike, wa mama yako, walio hama nawe. Na tumekuhalalishia mwanamke Muumini akijitolea nafsi yake bila ya mahari, nawe ikawa unataka kumwoa na umempenda. Kujitolea huku ni kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine. Kwao haifai hivyo. Tunajua hukumu tulizo wafaridhia Waumini kwa wake zao na wajakazi wao, na tuliyo kuruhusu wewe, si wao, ili isiwe dhiki juu yako kwa tuliyo kuhukumia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe madhambi ya waja wake, Mwenye kuwarehemu kwa ukunjufu.
التفاسير العربية:
۞ تُرۡجِي مَن تَشَآءُ مِنۡهُنَّ وَتُـٔۡوِيٓ إِلَيۡكَ مَن تَشَآءُۖ وَمَنِ ٱبۡتَغَيۡتَ مِمَّنۡ عَزَلۡتَ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكَۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن تَقَرَّ أَعۡيُنُهُنَّ وَلَا يَحۡزَنَّ وَيَرۡضَيۡنَ بِمَآ ءَاتَيۡتَهُنَّ كُلُّهُنَّۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ مَا فِي قُلُوبِكُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَلِيمٗا
Unaweza kuakhirisha zamu kwa umtakaye katika wao, na umsogeze umtakaye. Na kama ukimtaka yule uliye mtenga, basi si vibaya kwako. Kufanya hivi kutapelekea yaburudike macho yao, wala wasihuzunike, na wawe radhi juu ya kile unacho wapa wao wote. Na Mwenyezi Mungu anajua yaliyomo nyoyoni mwenu, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
Unaweza kumuakhirisha umtakaye katika kugawa zamu, na ukamjongeza umtakaye. Na kumtaka uliye muakhirisha zamu yake hapana lawama juu yako. Hivyo kuachiliwa utakavyo wewe yakaribia zaidi kupelekea furaha yao na baada ya kuwahuzunikia, na wao wote wawe radhi kwa ulio wapa. Na Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo ndani ya nyoyo zenu, ya kuudhika au kuridhika kwa aliyo kufanyieni sharia. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua yaliomo vifuani, Mpole hafanyi papara kuadhibu.
التفاسير العربية:
لَّا يَحِلُّ لَكَ ٱلنِّسَآءُ مِنۢ بَعۡدُ وَلَآ أَن تَبَدَّلَ بِهِنَّ مِنۡ أَزۡوَٰجٖ وَلَوۡ أَعۡجَبَكَ حُسۡنُهُنَّ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ يَمِينُكَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ رَّقِيبٗا
Baada ya hawa hawakuhalalikii wewe wanawake wengine, wala kuwabadilisha kwa wake wengine ingawa uzuri wao ukikupendeza; isipo kuwa yule uliye mmiliki kwa mkono wako wa kulia. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu.
Hawakuhalalikii wanawake wengine baada ya hawa, wala kuwapa t'alaka kwa ajili ya kuwabadilisha kwa wengine uwatakao, hata wakikupendeza kwa uzuri wao. Lakini Mwenyezi Mungu amekuhalalishia wajakazi ulio wamiliki kwa mkono wako. Na Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu, na anakihifadhi.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَدۡخُلُواْ بُيُوتَ ٱلنَّبِيِّ إِلَّآ أَن يُؤۡذَنَ لَكُمۡ إِلَىٰ طَعَامٍ غَيۡرَ نَٰظِرِينَ إِنَىٰهُ وَلَٰكِنۡ إِذَا دُعِيتُمۡ فَٱدۡخُلُواْ فَإِذَا طَعِمۡتُمۡ فَٱنتَشِرُواْ وَلَا مُسۡتَـٔۡنِسِينَ لِحَدِيثٍۚ إِنَّ ذَٰلِكُمۡ كَانَ يُؤۡذِي ٱلنَّبِيَّ فَيَسۡتَحۡيِۦ مِنكُمۡۖ وَٱللَّهُ لَا يَسۡتَحۡيِۦ مِنَ ٱلۡحَقِّۚ وَإِذَا سَأَلۡتُمُوهُنَّ مَتَٰعٗا فَسۡـَٔلُوهُنَّ مِن وَرَآءِ حِجَابٖۚ ذَٰلِكُمۡ أَطۡهَرُ لِقُلُوبِكُمۡ وَقُلُوبِهِنَّۚ وَمَا كَانَ لَكُمۡ أَن تُؤۡذُواْ رَسُولَ ٱللَّهِ وَلَآ أَن تَنكِحُوٓاْ أَزۡوَٰجَهُۥ مِنۢ بَعۡدِهِۦٓ أَبَدًاۚ إِنَّ ذَٰلِكُمۡ كَانَ عِندَ ٱللَّهِ عَظِيمًا
Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila mpewe ruhusa kwenda kula, sio kungojea kiwive. Lakini mtakapo itwa basi ingieni, na mkisha kula tawanyikeni, wala msiweke mazungumzo. Hakika hayo yanamuudhi Nabii naye anakustahini, lakini Mwenyezi Mungu hastahi kwa jambo la haki. Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao. Wala haikufalieni kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake kabisa. Hakika jambo hilo ni kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.
Enyi mlio amini! Msiingie nyumba za Nabii ila kwa idhini yake kwa ajili ya kwenda kula chakula, bila ya kwenda kungoja wakati mpaka kitapo kuwa tayari. Lakini Mtume akikuiteni, basi ingieni. Na mkisha kula ondokeni. Wala msikae baada yake mkijizoeza mazungumzo nyinyi kwa nyinyi. Kwani hakika kuingia bila ya idhini yake, na kukaa muda mrefu baada ya kwisha kula, kunamuudhi Nabii, naye anakustahini hawezi kukutakeni mtoke. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu hana la kumzuia asiitangaze haki kama wanavyo zuilikana viumbe. Na mtakapo wauliza wake za Nabii s.a.w. haja yoyote, basi waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ni usafi bora kwa nyoyo zenu na nyoyo zao zisiingiwe na uchochezi wa Shetani. Na haikufaliini nyinyi kumuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala kuwaoa wake zake baada yake milele, kwa sababu ya hishima yake na yao. Hakika jambo hilo ni dhambi kubwa kwa Mwenyezi Mungu. Yanarejea maelezo ya ki-ilimu juu ya Aya mbili 58, na 59 za Surat An-nur, katika yaliyo khusu adabu za kuzuru.
التفاسير العربية:
إِن تُبۡدُواْ شَيۡـًٔا أَوۡ تُخۡفُوهُ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا
Mkidhihirisha chochote kile, au mkikificha, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
Mkidhihirisha walau kidogo katika mambo yanayo muudhi, au mkikificha katika vifua vyenu, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kila kitu.
التفاسير العربية:
لَّا جُنَاحَ عَلَيۡهِنَّ فِيٓ ءَابَآئِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآئِهِنَّ وَلَآ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ إِخۡوَٰنِهِنَّ وَلَآ أَبۡنَآءِ أَخَوَٰتِهِنَّ وَلَا نِسَآئِهِنَّ وَلَا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُهُنَّۗ وَٱتَّقِينَ ٱللَّهَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا
Hapana ubaya kwao (wake za Mtume) kuonana na baba zao, wala watoto wao, wala ndugu zao, wala watoto wa ndugu zao wanaume, wala watoto wa ndugu zao wanawake, wala wanawake wenzao, wala wale iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Na enyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.
Hapana dhambi kwa wakeze Nabii wakitojificha kwa baba zao, au watoto wao, au ndugu zao, au watoto wa ndugu zao wa kiume, au watoto wa ndugu zao wa kike, au wanawake Waumini wenginewe, au watumwa walio wamiliki, kwa sababu ya shida ya kuwahitajia kwa matumishi. Nanyi wanawake, mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo aliyo kuamrisheni, wala msipindukie mipaka yake. Kwani Yeye hakika anajua kila kitu, hapana kilicho fichikana kwake.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِيِّۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ صَلُّواْ عَلَيۡهِ وَسَلِّمُواْ تَسۡلِيمًا
Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.
Hakika Mwenyezi Mungu anamrehemu Nabii wake na yu radhi naye. Na Malaika wanamwombea yeye. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُ فِي ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِ وَأَعَدَّ لَهُمۡ عَذَابٗا مُّهِينٗا
Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehi.
Hakika wanao muudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kuwapinga na kuchochea watu wawakatae, Mwenyezi Mungu amewafukuza kwenye rehema yake duniani na Akhera; na amewaandalia adhabu itayo wavunja kiburi chao.
التفاسير العربية:
وَٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ بِغَيۡرِ مَا ٱكۡتَسَبُواْ فَقَدِ ٱحۡتَمَلُواْ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا
Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasina wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri.
Na wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake kwa maneno au vitendo, bila ya wao kufanya makosa yoyote, hao basi wamebeba migongoni mwao mzigo wa ule uwongo wao, na inakuwa wametenda dhambi iliyo dhaahiri ubaya wake.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّبِيُّ قُل لِّأَزۡوَٰجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَآءِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ يُدۡنِينَ عَلَيۡهِنَّ مِن جَلَٰبِيبِهِنَّۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَن يُعۡرَفۡنَ فَلَا يُؤۡذَيۡنَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake wa Waumini, wateremshe nguo zao juu ya miili yao. Na wakivaa namna hii ni afadhali na wanaelekea zaidi kujuulikana na kwa hivyo wasipate kuudhiwa. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kumrehemu mwenye kuacha madhambi yake.
التفاسير العربية:
۞ لَّئِن لَّمۡ يَنتَهِ ٱلۡمُنَٰفِقُونَ وَٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِم مَّرَضٞ وَٱلۡمُرۡجِفُونَ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لَنُغۡرِيَنَّكَ بِهِمۡ ثُمَّ لَا يُجَاوِرُونَكَ فِيهَآ إِلَّا قَلِيلٗا
Kama wanaafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu.
Ninaapa! Ikiwa hawataacha hao wanaafiki, na wenye maradhi katika nyoyo zao, na wanao eneza khabari za uwongo katika Madina, hapana shaka nitakusalitisha juu yao, kisha hawatabakia kuwa karibu yako ila kwa muda mchache tu.
التفاسير العربية:
مَّلۡعُونِينَۖ أَيۡنَمَا ثُقِفُوٓاْ أُخِذُواْ وَقُتِّلُواْ تَقۡتِيلٗا
Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa.
Hao wanastahiki laana na kufukuzwa. Kila watapo patikana wakamatwe na wauliwe moja kwa moja.
التفاسير العربية:
سُنَّةَ ٱللَّهِ فِي ٱلَّذِينَ خَلَوۡاْ مِن قَبۡلُۖ وَلَن تَجِدَ لِسُنَّةِ ٱللَّهِ تَبۡدِيلٗا
Hii ni ada ya Mwenyezi Mungu iliyo kuwa kwa wale walio pita zamani. Wala hutapata mabadiliko katika ada ya Mwenyezi Mungu.
Mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu tangu zamani, kwa walio kuwa wakiwafanyia unaafiki Manabii na Mitume, na wakiasi, ni kuwa huuwawa kila wanapo kutikana. Wala mwendo wa Mwenyezi Mungu haugeuki.
التفاسير العربية:
يَسۡـَٔلُكَ ٱلنَّاسُ عَنِ ٱلسَّاعَةِۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِۚ وَمَا يُدۡرِيكَ لَعَلَّ ٱلسَّاعَةَ تَكُونُ قَرِيبًا
Watu wanakuuliza khabari ya Saa (ya Kiyama). Sema: Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu. Na nini kitakujuvya? Pengine hiyo Saa iko karibu.
Watu wanakuuliza lini itasimama Saa ya Kiyama. Waambie hao: Hakika ujuzi wa wakati wake uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Na nini kitakujuvya? Pengine wakati wa kusimama Saa ya kiyama upo karibu.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱللَّهَ لَعَنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ وَأَعَدَّ لَهُمۡ سَعِيرًا
Hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na amewaandalia Moto unao waka kwa nguvu.
Hakika Mwenyezi Mungu amewafukuza makafiri kwenye rehema yake, na amewatengenezea Moto mkali mno.
التفاسير العربية:
خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ لَّا يَجِدُونَ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Watadumu humo milele. Hawampati mlinzi wala wa kuwanusuru.
Hawatatoka humo kabisa. Hawatampata wa kuchukua dhamana ya kuwahami, wala wa kuwatetea.
التفاسير العربية:
يَوۡمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمۡ فِي ٱلنَّارِ يَقُولُونَ يَٰلَيۡتَنَآ أَطَعۡنَا ٱللَّهَ وَأَطَعۡنَا ٱلرَّسُولَا۠
Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume!
Siku zitakapo geuka nyuso zao Motoni kutoka hali hii kwendea hali hiyo, wakisema kwa majuto: Laiti kuwa sisi tulimt'ii Mwenyezi Mungu na tungeli mt'ii Mtume!
التفاسير العربية:
وَقَالُواْ رَبَّنَآ إِنَّآ أَطَعۡنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَآءَنَا فَأَضَلُّونَا ٱلسَّبِيلَا۠
Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.
Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwafuata maraisi wetu, na wakubwa wetu katika kukukataa Wewe na Mtume wako. Na wao ndio wakatutenganisha mbali na Njia Iliyo Nyooka.
التفاسير العربية:
رَبَّنَآ ءَاتِهِمۡ ضِعۡفَيۡنِ مِنَ ٱلۡعَذَابِ وَٱلۡعَنۡهُمۡ لَعۡنٗا كَبِيرٗا
Mola wetu Mlezi! Wape wao adhabu mara mbili, na uwalaani laana kubwa.
Mola wetu Mlezi! Wajaalie adhabu yao iwe mardufu, na uwafukuze kwenye rehema yako kabisa kwa kadri ya madhambi yao na makosa yao.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَكُونُواْ كَٱلَّذِينَ ءَاذَوۡاْ مُوسَىٰ فَبَرَّأَهُ ٱللَّهُ مِمَّا قَالُواْۚ وَكَانَ عِندَ ٱللَّهِ وَجِيهٗا
Enyi mlio amini! Msiwe kama wale walio mtaabisha Musa, lakini Mwenyezi Mungu akamtakasa na waliyo yasema, naye alikuwa mwenye hishima mbele ya Mwenyezi Mungu.
Enyi mlio amini! Msimuudhi Nabii kwa namna yoyote ya udhia, kama wale walio muudhi Musa katika kaumu yake. Na Mwenyezi Mungu akamtoa makosani na akamsafisha na hayo waliyo mzulia. Na Musa mbele ya Mwenyezi Mungu alikuwa ni bwana mwenye hadhi.
التفاسير العربية:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَقُولُواْ قَوۡلٗا سَدِيدٗا
Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawasawa.
Enyi mlio amini! Iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu mkimuasi, na semeni maneno yalio simama sawa yasio kwenda upogo.
التفاسير العربية:
يُصۡلِحۡ لَكُمۡ أَعۡمَٰلَكُمۡ وَيَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡۗ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدۡ فَازَ فَوۡزًا عَظِيمًا
Apate kukutengenezeeni vitendo vyenu na akusameheni madhambi yenu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, bila ya shaka amefanikiwa mafanikio makubwa.
Apate kukuwezesheni kutenda mema, na azifute dhambi zenu. Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi huyo amepata kufuzu kukubwa kwa kuepuka adhabu, na kupata thawabu.
التفاسير العربية:
إِنَّا عَرَضۡنَا ٱلۡأَمَانَةَ عَلَى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَٱلۡجِبَالِ فَأَبَيۡنَ أَن يَحۡمِلۡنَهَا وَأَشۡفَقۡنَ مِنۡهَا وَحَمَلَهَا ٱلۡإِنسَٰنُۖ إِنَّهُۥ كَانَ ظَلُومٗا جَهُولٗا
Kwa hakika Sisi tulikadimisha amana kwa mbingu na ardhi na milima; na vyote hivyo vikakataa kuichukua na vikaogopa. Lakini mwanaadamu akaichukua. Hakika yeye amekuwa dhaalimu mjinga.
Sisi kwa hakika tulizitaka mbingu na ardhi na milima zichukue dhamana, nazo zikakataa kuichukua, na wakaiogopa. Lakini mwanaadamu aliichukua. Hakika yeye amekuwa ni mkubwa wa kujidhulumu nafsi yake kwa kutojua jukumu la kuchukua huko.
التفاسير العربية:
لِّيُعَذِّبَ ٱللَّهُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡمُنَٰفِقَٰتِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ وَٱلۡمُشۡرِكَٰتِ وَيَتُوبَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمَۢا
Kwa hivyo Mwenyezi Mungu anawaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na anawapokelea toba Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Ili Mwenyezi Mungu awaadhibu wanaafiki wanaume, na wanaafiki wanawake, na washirikina wanaume, na washirikina wanawake; na Mwenyezi Mungu apate kukubali toba za Waumini wanaume, na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwingi wa rehema.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: الأحزاب
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق