ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (41) سورة: فاطر
۞ إِنَّ ٱللَّهَ يُمۡسِكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ أَن تَزُولَاۚ وَلَئِن زَالَتَآ إِنۡ أَمۡسَكَهُمَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنۢ بَعۡدِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ كَانَ حَلِيمًا غَفُورٗا
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuilia mbingu na ardhi zisiondoke. Na zikiondoka hapana yeyote wa kuzizuia isipo kuwa Yeye. Hakika Yeye ni Mpole Mwenye kusamehe.
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye zuia mpango wa mbingu na ardhi usivurugike, na ndiye anaye zihifadhi mbingu na ardhi zisiondoke. Na lau akizijaalia kuondoka hapana wa kuweza kuzihifadhi hizo isipo kuwa Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Hakika Yeye ni Mpole, hafanyi papara kuwaadhibu wakhalifu. Yeye ni Msamehevu wa madhambi ya wenye kurejea kwake wakatubu. Aya hii tukufu inathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la peke yake ndiye Muumba mbingu na ardhi. Yeye ndiye Mwenye kuzishika zisiondoke. Kwani hivi vitu viliomo mbinguni vya karibu na mbali vinavyo onekana katika qubba la mbingu vimeshikamana kwa mujibu wa mpango maalumu wa namna ya pekee alio uumba Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Kutukuka. Na Yeye ndiye aliye viwekea mvutano usio katika kwa kupita zama na vizazi, na ndiye anaye vihifadhi visikosee mizani yao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala ndiye Mwenye uweza huu, wala hapana mwenginewe.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (41) سورة: فاطر
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق