ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (165) سورة: الأنعام
وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَكُمۡ خَلَٰٓئِفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٖ دَرَجَٰتٖ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِي مَآ ءَاتَىٰكُمۡۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمُۢ
Naye ndiye aliye kufanyeni makhalifa wa duniani, na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa, ili akujaribuni kwa hayo aliyo kupeni. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwepesi wa kuadhibu, na hakika Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Na Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyeni makhalifa (walio chukua pahala pa) kaumu zilizo tangulia katika kuamirisha ulimwengu. Naye amewanyanyua baadhi yenu kuliko wengine kwa daraja nyingi katika mambo yanayo onekana na yasiyo onekana kwa vile kukupeni njia za kuyafikilia, ili apate kukujaribuni, kukufanyieni mtihani, katika hizo neema alizo kupeni, vipi mtazishukuru, na katika sharia alizo kupeni mtazitumia vipi. Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwepesi wa kuwaadhibu wakhalifu, kwani hakika adhabu yake itakuja tu bila ya shaka, na kila lijalo lipo karibu. Na Yeye ni mwenye maghfira makubwa kwa makosa ya wenye kutubu na wakatengenea, na Mkunjufu wa rehema kwao.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (165) سورة: الأنعام
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق