ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (39) سورة: الأنعام
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا صُمّٞ وَبُكۡمٞ فِي ٱلظُّلُمَٰتِۗ مَن يَشَإِ ٱللَّهُ يُضۡلِلۡهُ وَمَن يَشَأۡ يَجۡعَلۡهُ عَلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na walio kanusha Ishara zetu ni viziwi na mabubu waliomo gizani. Mwenyezi Mungu humwachia kupotea amtakaye, na humweka katika Njia iliyo nyooka amtakaye.
Na ambao hawakuzisadiki dalili zetu zinazo onyesha uwezo wetu na ukweli wa Utume wako, basi hao hawakunafiika na hisiya zao kuwawezesha kuitambua Haki. Kwa hivyo wakawa wanababaika katika upotovu wa ushirikina na inda, kama anavyo babaika kiziwi-bubu katika giza la usiku, hawezi kuepuka kuangamia. Lau kuwa watu hawa wameelekea kheri Mwenyezi Mungu angeli wawezesha wamfikie, kwani Yeye Subhanahu akitaka kumpoteza mtu kwa ufisadi wake alio ukusudia, basi humwachilia mbali na shani yake; na akitaka kumwongoa mtu kwa kuwa makusudio yake ni sawa, basi humsahilishia njia ya Imani iliyo wazi na iliyo nyooka.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (39) سورة: الأنعام
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق