ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (91) سورة: الأنعام
وَمَا قَدَرُواْ ٱللَّهَ حَقَّ قَدۡرِهِۦٓ إِذۡ قَالُواْ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ بَشَرٖ مِّن شَيۡءٖۗ قُلۡ مَنۡ أَنزَلَ ٱلۡكِتَٰبَ ٱلَّذِي جَآءَ بِهِۦ مُوسَىٰ نُورٗا وَهُدٗى لِّلنَّاسِۖ تَجۡعَلُونَهُۥ قَرَاطِيسَ تُبۡدُونَهَا وَتُخۡفُونَ كَثِيرٗاۖ وَعُلِّمۡتُم مَّا لَمۡ تَعۡلَمُوٓاْ أَنتُمۡ وَلَآ ءَابَآؤُكُمۡۖ قُلِ ٱللَّهُۖ ثُمَّ ذَرۡهُمۡ فِي خَوۡضِهِمۡ يَلۡعَبُونَ
Na hawakumkadiria Mwenyezi Mungu kwa haki ya kadri yake, walipo sema: Mwenyezi Mungu hakumteremshia mwanaadamu chochote. Sema: Nani aliyo teremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, chenye nuru na uwongofu kwa watu, mlicho kifanya kurasa kurasa mkizionyesha, na mengi mkiyaficha. Na mkafunzwa mlio kuwa hamyajui nyinyi wala baba zenu? Sema: Mwenyezi Mungu. Kisha waache wacheze katika porojo lao.
Na hawa makafiri hawakumkadiria Mwenyezi Mungu na rehema yake na hikima yake kwa anavyo stahiki, walipo kanya kuteremshwa ujumbe wake kwa binaadamu yeyote! Ewe Nabii! Waambie washirikina na wanao waunga mkono katika hayo miongoni mwa Mayahudi: Nani aliye kiteremsha Kitabu alicho kuja nacho Musa, ambacho kina nuru iliyo zagaa, na uwongofu wa kuongozea? Nyinyi Mayahudi mnakifanya hicho kuwa ni maandiko yaliyo gawiwa mafungu mbali mbali. Yanayo kubaliana na mapendo yenu mnayaonyesha, na mengi mnayaficha yale yanayo kupelekeeni kuiamini na kuisadiki Qur'ani. Na kutokana na Kitabu hicho mmejifunza mambo ambayo nyinyi na baba zenu hamkuwa mkiyajua!! Na ewe Nabii! Jawabu wape wewe kwa kuwaambia: Mwenyezi Mungu ndiye aliye iteremsha Taurati. Kisha waache wakiendelea katika upotovu, wakicheza kama watoto wadogo.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (91) سورة: الأنعام
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق