ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس * - فهرس التراجم

ترجمة معاني سورة: الرحمن   آية:

سورة الرحمن - Surat Ar-Rahman

ٱلرَّحۡمَٰنُ
mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema
التفاسير العربية:
عَلَّمَ ٱلۡقُرۡءَانَ
Amemfundisha binadamu Qur’ani kwa kurahisisha kuisoma, kuihifadhi na kuelewa maana yake.
التفاسير العربية:
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ
Amemuumba binadamu,
التفاسير العربية:
عَلَّمَهُ ٱلۡبَيَانَ
Amemfundisha ufasaha wa kujieleza ili kumtenganisha na wengine.
التفاسير العربية:
ٱلشَّمۡسُ وَٱلۡقَمَرُ بِحُسۡبَانٖ
Jua na mwezi zinatembea kwa kufuatana, moja baada ya nyingine, kwa hesabu madhubuti isiyotafautiana wala kugongana.
التفاسير العربية:
وَٱلنَّجۡمُ وَٱلشَّجَرُ يَسۡجُدَانِ
Na nyota iliyo mbinguni na miti ya ardhini, vinamjua Mola wao, vinamsujudia na vinanyosha shingo zao kufuata vile ambavyo vimepangiwa vifuate vya maslahi ya waja Wake na manufaa yao.
التفاسير العربية:
وَٱلسَّمَآءَ رَفَعَهَا وَوَضَعَ ٱلۡمِيزَانَ
Na mbingu Ameiinua na kuifanya iwe juu ya ardhi, Na Ameweka kwenye ardhi uadilifu Aliouamrisha na kuulazimisha kwa waja Wake.
التفاسير العربية:
أَلَّا تَطۡغَوۡاْ فِي ٱلۡمِيزَانِ
Ili msipite mipaka na msimfanyie hiyana mnayempimia.
التفاسير العربية:
وَأَقِيمُواْ ٱلۡوَزۡنَ بِٱلۡقِسۡطِ وَلَا تُخۡسِرُواْ ٱلۡمِيزَانَ
Na simamisheni upimaji kwa usawa na msipunguze mizani mnapowapimia watu.
التفاسير العربية:
وَٱلۡأَرۡضَ وَضَعَهَا لِلۡأَنَامِ
Na ardhi Ameiweka na Ameitayarisha, ili viumbe vitulie juu yake.
التفاسير العربية:
فِيهَا فَٰكِهَةٞ وَٱلنَّخۡلُ ذَاتُ ٱلۡأَكۡمَامِ
Humo mna matunda na mitende yenye makarara ya matunda. Na humo kuna nafaka zenye maganda, vikiwa ni chakula chenu na wanyama wenu.
التفاسير العربية:
وَٱلۡحَبُّ ذُو ٱلۡعَصۡفِ وَٱلرَّيۡحَانُ
Na humo mna kila mmea wenye harufu nzuri.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Bas ni neema gani za Mola wenu, za kidini na za kidunia, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha? Na ni jawabu nzuri ilioje ya majini alipowasomea wao Nabii, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, sura hii, kila akipita kwenye aya hii walikuwa wakisema, «Hakuna chochote miongoni mwa neema zako, ewe Mola wetu, tunachokanusha. Sifa njema zote ni zako.» Na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa mja anapoelezewa neema za Mwenyezi Mungu na mema Yake akubali na amshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema hizo.
التفاسير العربية:
خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِن صَلۡصَٰلٖ كَٱلۡفَخَّارِ
Amemuumba baba wa wanadamu, naye ni Ādam, kwa udongo mkavu kama vyungu.
التفاسير العربية:
وَخَلَقَ ٱلۡجَآنَّ مِن مَّارِجٖ مِّن نَّارٖ
Na Amemuumba Iblisi, naye ni katika majini, kwa mroromo wa moto uliochanganyika.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقَيۡنِ وَرَبُّ ٱلۡمَغۡرِبَيۡنِ
Mola wa pande mbili za Mashariki ya jua, katika kusi na kaskazi, na Mola wa pande mbili za Magharibi ya jua, katika kusi na kaskazi, kwani vyote viko chini ya uendeshaji Wake na ulezi Wake..
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
مَرَجَ ٱلۡبَحۡرَيۡنِ يَلۡتَقِيَانِ
Mwenyezi Mungu Ameyachanganya maji ya bahari mbili, tamu na chumvi, yanakutana, baina yake kuna kizuizi,
التفاسير العربية:
بَيۡنَهُمَا بَرۡزَخٞ لَّا يَبۡغِيَانِ
mojawapo haiingii sehemu ya nyingine na kuiondoa sifa yake, bali ya tamu inasalia kuwa tamu na ya chumvi inasalia kuwa chumvi pamoja na kukutana kwake.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
يَخۡرُجُ مِنۡهُمَا ٱللُّؤۡلُؤُ وَٱلۡمَرۡجَانُ
Inatoka kwenye bahari mbili hizo, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, lulu na marjani.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
وَلَهُ ٱلۡجَوَارِ ٱلۡمُنشَـَٔاتُ فِي ٱلۡبَحۡرِ كَٱلۡأَعۡلَٰمِ
Ni Yake Yeye, Aliyetakasika na kutukuka, mamlaka ya kuyaendesha majahazi makubwa yanayotembea baharini kwa manufaa ya watu, yenye kusimamisha juu milongoti yake na matanga yake kama vile majabali.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu mnazikanusha?
التفاسير العربية:
كُلُّ مَنۡ عَلَيۡهَا فَانٖ
Kila aliye juu ya uso wa ardhi miongoni mwa viumbe ni mwenye kuangamia,
التفاسير العربية:
وَيَبۡقَىٰ وَجۡهُ رَبِّكَ ذُو ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ
na utasalia uso wa Mola wako Mwenye utukufu, ubora, kheri nyingi na upaji. Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya uso kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inavyonasibiana na Yeye, kutakasika ni Kwake, bila kufananisha wala kueleza namna ulivyo.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
يَسۡـَٔلُهُۥ مَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ كُلَّ يَوۡمٍ هُوَ فِي شَأۡنٖ
Wanamuomba Yeye walioko mbinguni na ardhini haja zao. Hakuna yoyote anayejitosheleza kutomhitajia Yeye, kutakasika ni Kwake. Kila siku Yeye Yuko kwenye jambo: Anatukuza na Anatweza, Anatoa na Anazuia.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
سَنَفۡرُغُ لَكُمۡ أَيُّهَ ٱلثَّقَلَانِ
Nitawatengea kipindi cha kuwahesabu na kuwalipa kwa matendo yenu mliyoyafanya, enyi vizito viwili:-majini na binadamu-, tuwatese watu wa maasia na tuwape malipo mema watu wa utiifu.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
يَٰمَعۡشَرَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ إِنِ ٱسۡتَطَعۡتُمۡ أَن تَنفُذُواْ مِنۡ أَقۡطَارِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ فَٱنفُذُواْۚ لَا تَنفُذُونَ إِلَّا بِسُلۡطَٰنٖ
Enyi mkusanyiko wa majini na binadamu! Mkiweza kuihepa amri ya Mwenyezi Mungu na uamuzi Wake kwa kukimbia kwenye pambe za mbingu na ardhi basi fanyeni, na hamuwezi kufanya hivyo isipokuwa kwa nguvu na hoja na amri inayotoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka. (Na vipi mtaweza kufanya hivyo na hali nyinyi hamzimilikii nafsi zenu manufaa yoyote wala madhara?).
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
يُرۡسَلُ عَلَيۡكُمَا شُوَاظٞ مِّن نَّارٖ وَنُحَاسٞ فَلَا تَنتَصِرَانِ
Mtatumiwa mroromo wa moto na shaba iliyoyayushwa, mmiminiwe juu ya vichwa vyenu msiweze kusaidiana.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazukanusha?
التفاسير العربية:
فَإِذَا ٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ وَرۡدَةٗ كَٱلدِّهَانِ
Na pindi mbingu itakapopasuka na kuachana Siku ya Kiyama, ikawa nyekundu kama rangi ya waridi na kama mafuta yaliyochemshwa na risasi iliyoyayushwa, kutokana na mambo magumu na vituko vya Siku ya Kiyama.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
فَيَوۡمَئِذٖ لَّا يُسۡـَٔلُ عَن ذَنۢبِهِۦٓ إِنسٞ وَلَا جَآنّٞ
Katika Siku hiyo Malaika hawatawauliza wale wahalifu, miongoni mwa binadamu na majini, kuhusu dhambi zao.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
يُعۡرَفُ ٱلۡمُجۡرِمُونَ بِسِيمَٰهُمۡ فَيُؤۡخَذُ بِٱلنَّوَٰصِي وَٱلۡأَقۡدَامِ
Malaika watawajua wahalifu kwa alama zao, hapo wawashike kwenye paa za vichwa vyao na nyayo zao wawarushe Motoni.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
هَٰذِهِۦ جَهَنَّمُ ٱلَّتِي يُكَذِّبُ بِهَا ٱلۡمُجۡرِمُونَ
Wataambiwa hao wahalifu kwa njia ya kulaumiwa na kudhalilishwa, «Huu ndio moto wa Jahanamu ambao wahalifu duniani walikuwa wakiukanusha:
التفاسير العربية:
يَطُوفُونَ بَيۡنَهَا وَبَيۡنَ حَمِيمٍ ءَانٖ
mara wanaadhibiwa kwenye Jaḥīm, na mara nyingine wananyweshwa Hāmīm, nacho ni kinywaji kilichofikia upeo wa ukali wa moto, kinakata tumbo na sehemu za ndani ya mbavu.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu mnazikanusha?
التفاسير العربية:
وَلِمَنۡ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِۦ جَنَّتَانِ
Na anayemcha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa waja Wake binadamu na majini, akaogopa kusimama kwake mbele Yake, akamtii na akaacha kumuasi atakuwa na mabustani mawili ya Pepo.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
ذَوَاتَآ أَفۡنَانٖ
Mabustani mawili hayo ya Pepo yana matawi yaliyostawi kwa matunda ya kila aina.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
فِيهِمَا عَيۡنَانِ تَجۡرِيَانِ
Katika Pepo mbili hizo kuna chemchemi mbili za maji zinazopita katikati yake.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
فِيهِمَا مِن كُلِّ فَٰكِهَةٖ زَوۡجَانِ
Katika mabustani hayo mawili ya Pepo kuna sampuli mbili za kila aina ya matunda.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ فُرُشِۭ بَطَآئِنُهَا مِنۡ إِسۡتَبۡرَقٖۚ وَجَنَى ٱلۡجَنَّتَيۡنِ دَانٖ
Na wale wanaoogopa kusimama mbele ya Mola Wao watakuwa na mabustani mawili ya Pepo, ambayo ndani yake watastarehe, hali ya kutegemea juu ya matandiko yaliyojazwa dibaji nzito. Na matunda ya mabustani mawili hayo ya pepo yako karibu nao.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mtazikanusha?
التفاسير العربية:
فِيهِنَّ قَٰصِرَٰتُ ٱلطَّرۡفِ لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
Katika matandiko hayo wapo wake macho yao yanawatazama waume zao tu, hawawatazami wengineo, wamefungamana na wao. Hakuna aliyewaingilia, kabla ya hao waume zao, binadamu yoyote wala jini.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadanu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
كَأَنَّهُنَّ ٱلۡيَاقُوتُ وَٱلۡمَرۡجَانُ
Kama kwamba hawa wake wa kihurulaini ni yakuti na marijani katika sifa zao na uzuri wao.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa najini na binadamu , mnazikanusha?
التفاسير العربية:
هَلۡ جَزَآءُ ٱلۡإِحۡسَٰنِ إِلَّا ٱلۡإِحۡسَٰنُ
Je atakuwa na malipo yoyote, huyu aliyekuwa mwema wa matendo duniani, isipokuwa ni afanyiwe wema kwa kupewa Pepo huko Akhera?
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
وَمِن دُونِهِمَا جَنَّتَانِ
Na chini ya mabustani ya Pepo mawili yaliyotangulia kuna mabustani ya Pepo mawili mengine.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
مُدۡهَآمَّتَانِ
Mabustani haya mawili ni rangi ya kijani. Ujani wake umeiva sana mapaka umeingia kwenye weusi.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
فِيهِمَا عَيۡنَانِ نَضَّاخَتَانِ
Ndani ya mabustani mawili hayo ya Peponi kuna chemchemi mbili zenye kububujika maji daima bila kukatika.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
فِيهِمَا فَٰكِهَةٞ وَنَخۡلٞ وَرُمَّانٞ
Kwenye mabustani hayo mawili kuna aina za matunda, mitende na mikomamanga.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
فِيهِنَّ خَيۡرَٰتٌ حِسَانٞ
Ndani ya mabustani haya manne ya Pepo kuna wake walio wema wa tabia na wazuri wa nyuso.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
حُورٞ مَّقۡصُورَٰتٞ فِي ٱلۡخِيَامِ
Mahurulaini wakunjufu wa macho, waliositiriwa na kuhifadhiwa mahemani.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
لَمۡ يَطۡمِثۡهُنَّ إِنسٞ قَبۡلَهُمۡ وَلَا جَآنّٞ
Hawajaingiliwa Mahurulaini hawa na binadamu yoyote wala jini kabla ya waume zao.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
مُتَّكِـِٔينَ عَلَىٰ رَفۡرَفٍ خُضۡرٖ وَعَبۡقَرِيٍّ حِسَانٖ
Hali ya kuwa wametegemea kwenye mito yenye mifuko rangi ya kijani na matandiko mazuri.
التفاسير العربية:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ
Basi ni neema gani za Mola wenu, enyi mkusanyiko wa majini na binadamu, mnazikanusha?
التفاسير العربية:
تَبَٰرَكَ ٱسۡمُ رَبِّكَ ذِي ٱلۡجَلَٰلِ وَٱلۡإِكۡرَامِ
Zimekithiri mno baraka za Jina la Mola wako, na kheri Zake zimekuwa nyingi, Mwenye haiba kubwa, utukufu wenye kukamilika na takrima kwa wenye kumtegemea Yeye.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: الرحمن
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

إغلاق