prev

Al-Haqqah

next

1 : 69

ٱلۡحَآقَّةُ

Kwa hakika kiama ni chenye kutokea, ndani yake itatimia ahadi ya Allah Mtukufu na onyo Lake. info
التفاسير: |

2 : 69

مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Kiyama chenyewe ni zipi sifa zake na hali zake? info
التفاسير: |

3 : 69

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحَآقَّةُ

Na kitu gani kilichokujulisha wewe, (ewe Mtume), na kukueleza uhakika wa Kiyama? na kikakupa picha ya janga lake na shida zake? info
التفاسير: |

4 : 69

كَذَّبَتۡ ثَمُودُ وَعَادُۢ بِٱلۡقَارِعَةِ

Thamûd, nao ni watu wa Ṣãliḥ, na ‘Ãd, nao ni watu wa Hûd, walikikanusha Kiyama ambacho kinagonga nyoyo kwa vitisho na janga lake. info
التفاسير: |

5 : 69

فَأَمَّا ثَمُودُ فَأُهۡلِكُواْ بِٱلطَّاغِيَةِ

Ama hao Thamûd waliangamizwa kwa ukelele mkubwa uliopita kiasi ukali wake. info
التفاسير: |

6 : 69

وَأَمَّا عَادٞ فَأُهۡلِكُواْ بِرِيحٖ صَرۡصَرٍ عَاتِيَةٖ

Na ama ‘Ãd waliangamizwa kwa upepo wa baridi unaovuma kwa nguvu. info
التفاسير: |

7 : 69

سَخَّرَهَا عَلَيۡهِمۡ سَبۡعَ لَيَالٖ وَثَمَٰنِيَةَ أَيَّامٍ حُسُومٗاۖ فَتَرَى ٱلۡقَوۡمَ فِيهَا صَرۡعَىٰ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٍ خَاوِيَةٖ

Allah Mtukufu Aliwasaliti nao masiku saba na michana minane yenye kufuatana, isiyokatika wala kusimama. Utawaona watu katika masiku hayo na michana hiyo wamekufa, kana kwamba ni vigogo vya mitende iliyo mibovu iliyolika ndani. info
التفاسير: |

8 : 69

فَهَلۡ تَرَىٰ لَهُم مِّنۢ بَاقِيَةٖ

Basi hivi utamuona mtu yoyote miongoni mwao mwenye kusalia bila kuangamia? info
التفاسير: |
prev

Al-Haqqah

next
:
0:00 0:00