9 : 62

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوۡمِ ٱلۡجُمُعَةِ فَٱسۡعَوۡاْ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَذَرُواْ ٱلۡبَيۡعَۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkazifuata Sheria Zake kivitendo! Pindi mwadhini atakapoita kwa ajili ya Swala Siku ya Ijumaa, nendeni upesi msikilize hutuba na mtekeleze Swala, na muache uuzaji na pia ununuaji na kila kinachowashughulisha na hiyo Swala. Hilo mliloamrishwa ni bora kwenu kutokana na yaliyo humo ya kusamehewa dhambi zenu na kupatiwa malipo mema kutoka kwa Allah Mtukufu. Basi iwapo mnayajua manufaa ya nafsi zenu, fanyeni hilo. Kwenye aya hii kuna dalili kua kuhudhuria Swala ya Ijumaa na kusikiliza hutuba ni lazima. info
التفاسير: |
prev

Al-Jumu'ah

next
:
0:00 0:00