prev

At-Taghabun

next

1 : 64

يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ لَهُ ٱلۡمُلۡكُ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Vinamtakasa Allah Mtukufu na sifa zisizonasibiana naye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini. Ni Wake Yeye Allah Mtukufu, kutakasika na kila upungufu ni Kwake, uendeshaji mambo usio na kizuizi katika kila kitu. Na Yeye Ndiye Mwenye sifa njema zilizo nzuri. Na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. info
التفاسير: |

2 : 64

هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُمۡ فَمِنكُمۡ كَافِرٞ وَمِنكُم مُّؤۡمِنٞۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٌ

Allah Mtukufu Ndiye Aliyewafanya nyinyi mpatikane kutoka kwenye hali ya kutokuwako, kati yenu kuna wenye kuukanusha uungu Wake na baadhi yenu kuna wenye kuuamini na kufuata Sheria Zake kivitendo. Na Yeye, (kutakasika na kila sifa za upungufu ni Kwake), ni Mwenye kuviona vitendo vyenu, hakuna chochote chenye kufichika Kwake, na Atawalipa kwavyo . info
التفاسير: |

3 : 64

خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّ وَصَوَّرَكُمۡ فَأَحۡسَنَ صُوَرَكُمۡۖ وَإِلَيۡهِ ٱلۡمَصِيرُ

Ameumba mbingu na ardhi kwa hekima kubwa, na Akawaumba nyinyi katika sura nzuri, na Kwake ndio marejeo Siku ya Kiyama, Amlipe kila mtu kwa matendo yake. info
التفاسير: |

4 : 64

يَعۡلَمُ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَيَعۡلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا تُعۡلِنُونَۚ وَٱللَّهُ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ

Anajua, kutakasika na kutukuka ni Kwake, kila kilichoko mbinguni na ardhini, na Anakijua mnachokificha, (enyi watu), na mnachokidhihirisha. Na Allah Mtukufu ni Mjuzi wa yale yanayodhamiriwa na vifua na kufichwa na nafsi info
التفاسير: |

5 : 64

أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَبَؤُاْ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَبۡلُ فَذَاقُواْ وَبَالَ أَمۡرِهِمۡ وَلَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ

Je haikuwajia, (enyi washirikina), habari ya wale waliokufuru miongoni mwa watu waliopita kabla yenu, ulipowafikia mwisho mbaya wa ukafiri wao na uovu wa vitendo vyao hapa ulimwenguni, na kuwa kesho Akhera watakuwa na adhabu kali iumizayo? info
التفاسير: |

6 : 64

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُۥ كَانَت تَّأۡتِيهِمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٞ يَهۡدُونَنَا فَكَفَرُواْ وَتَوَلَّواْۖ وَّٱسۡتَغۡنَى ٱللَّهُۚ وَٱللَّهُ غَنِيٌّ حَمِيدٞ

Hayo yaliyowapata duniani na yatakayowapata kesho Akhera ni kwamba wao walikuwa wakijiliwa na Mitume wa Allah Mtukufu na alama za wazi na miujiza iliyodhihiri, walikuwa wakisema, «Je binadamu kama sisi wanatuongoza? Hapo wakamkufuru Allah Mtukufu, wakaukanusha ujumbe wa Mitume Wake na wakaipa mgongo haki wasiikubali. Na Allah Mtukufu Hana haja na kuamini kwao wala kuabudu kwao. Na Allah Mtukufu ni Tajiri, Ana utajiri uliotimia usio na mpaka, ni Mwenye kusifiwa kwa maneno Yake, matendo Yake, na sifa Zake, Hawajali wao wala haumdhuru Yeye upotevu wao chochote». info
التفاسير: |

7 : 64

زَعَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَن لَّن يُبۡعَثُواْۚ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتُبۡعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلۡتُمۡۚ وَذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٞ

Walidai wale waliomkanusha Allah Mtukufu kwamba wao hawatatolewa kwenye makaburi yao baada ya kufa. Waambie, (ewe Mtume), «Ndio. Naapa kwa Mola wangu! Mtatolewa makaburini mwenu mkiwa hai, kisha mtapewa habari ya yale mliyoyafanya duniani. Na hilo kwa Allah Mtukufu ni sahali na rahisi». info
التفاسير: |

8 : 64

فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلنُّورِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلۡنَاۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ

Basi muaminini Allah Mtukufu na Mtume Wake, (enyi washirikina), na mjiongoze kwa Qur’ani Aliyomteremshia Mtume Wake. Na Allah Mtukufu kwa mnayoyafanya ni Mtambuzi, hakuna kinachofichika kwake cha matendo yenu na maneno yenu, na Yeye ni Mwenye kuwalipa kwa hayo Siku ya Kiyama. info
التفاسير: |

9 : 64

يَوۡمَ يَجۡمَعُكُمۡ لِيَوۡمِ ٱلۡجَمۡعِۖ ذَٰلِكَ يَوۡمُ ٱلتَّغَابُنِۗ وَمَن يُؤۡمِنۢ بِٱللَّهِ وَيَعۡمَلۡ صَٰلِحٗا يُكَفِّرۡ عَنۡهُ سَيِّـَٔاتِهِۦ وَيُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Ikumbukeni Siku ya Mkusanyo ambayo Allah Mtukufu Atawakusanya wa mwanzo na wa mwisho. Siku hiyo ambayo ina mpunjano na mtengano kati ya viumbe: Waumini wawapunje makafiri na wenye kuasi, na wao hao (makafiri na waasi) iwadhihirikie wazi kuwa wao ndio waliopata hasara. Basi wenye Imani wataingia Peponi kwa rehema za Allah Mtukufu, na wenye ukafiri wataingia Motoni kwa uadilifu Wake. Na mwenye kumuamini Allah Mtukufu na akafanya matendo ya utiifu Kwake, Atamfutia dhambi zake na Amtie kwenye mabustani ya Pepo ambayo chini ya majumba yake ya fahari inapita mito ya maji, hali ya kukaa milele humo. Kukaa milele huko Peponi ndiko kufaulu kukubwa ambako hakuna kufaulu kushinda huko. info
التفاسير: |
prev

At-Taghabun

next
:
0:00 0:00