prev

Al-Mulk

next

1 : 67

تَبَٰرَكَ ٱلَّذِي بِيَدِهِ ٱلۡمُلۡكُ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Zimekithiri kheri za Allah Mtukufu na wema Wake kwa viumbe Vyake, Ambaye mkononi Mwake upo ufalme wa duniani na Akhera na mamlaka ya viwili hivyo, Anapitisha amri Yake na uamuzi Wake kwenye mamlaka Yake hayo, na Yeye kwa kila jambo ni Muweza. Faida inayopatikana katika aya hii ni kuwa inathibitisha sifa ya mkono kwa Allah Mtukufu Aliyetakasika na kutukuka, kwa namna inavyonasibiana na utukufu Wake. info
التفاسير: |

2 : 67

ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡمَوۡتَ وَٱلۡحَيَوٰةَ لِيَبۡلُوَكُمۡ أَيُّكُمۡ أَحۡسَنُ عَمَلٗاۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡغَفُورُ

Aliyeumba mauti na uhai ili awatahini nyinyi, (enyi watu), na kujua ni yupi miongoni mwenu aliye mwema wa matendo na utakasaji wa nia? Na Yeye Ndiye Mshindi Ambaye hakuna chochote kinachomshinda, Ndiye Mwingi wa msamaha kwa anayetubia miongoni mwa waja Wake. Katika aya hii pana kuhimiza kufanya utiifu na makemeo ya kutenda maasia. info
التفاسير: |

3 : 67

ٱلَّذِي خَلَقَ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ طِبَاقٗاۖ مَّا تَرَىٰ فِي خَلۡقِ ٱلرَّحۡمَٰنِ مِن تَفَٰوُتٖۖ فَٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ هَلۡ تَرَىٰ مِن فُطُورٖ

Aliyeumba mbingu saba zilizopangika, baadhi yake juu ya nyingine, huoni katika uumbaji wa Allah Mtukufu (Mwingi wa rehema), ewe mwenye kuangalia, tofauti yoyote, basi rudia tena kuangalia mbinguni: je unaona mpasuko wowote au nyufa? info
التفاسير: |

4 : 67

ثُمَّ ٱرۡجِعِ ٱلۡبَصَرَ كَرَّتَيۡنِ يَنقَلِبۡ إِلَيۡكَ ٱلۡبَصَرُ خَاسِئٗا وَهُوَ حَسِيرٞ

Kisha rudia kuangalia tena, mara kwa mara, yatakurudia hayo macho yakiwa manyonge na dhalili, hayataona upungufu wowote, na yatapatwa na usumbufu na uchovu. info
التفاسير: |

5 : 67

وَلَقَدۡ زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِمَصَٰبِيحَ وَجَعَلۡنَٰهَا رُجُومٗا لِّلشَّيَٰطِينِۖ وَأَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابَ ٱلسَّعِيرِ

Na hakika tumeupamba uwingu wa karibu unaoonekana na macho kwa nyota kubwa zenye kung’ara, na tumezifanya nyota hizo ni vimondo vyenye kuwachoma wenye kusikiliza kwa kuiba miongoni mwa mashetani, na tumewaandalia huko Akhera adhabu ya Moto wenye kuwaka, watakua ni wenye kuadhibika kwa joto lake. info
التفاسير: |

6 : 67

وَلِلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمَصِيرُ

Na wenye kumkanusha Mola wao watapata adhabu ya moto wa Jahanamu, na ubaya zaidi wa mahali pa mtu kurejea ni huo moto wa Jahanamu! info
التفاسير: |

7 : 67

إِذَآ أُلۡقُواْ فِيهَا سَمِعُواْ لَهَا شَهِيقٗا وَهِيَ تَفُورُ

Waingizwapo hao wakanushaji ndani ya moto wa Jahanamu, watausikia ukitoa sauti kali yenye kutisha, huku ukichemka machemko makali sana. info
التفاسير: |

8 : 67

تَكَادُ تَمَيَّزُ مِنَ ٱلۡغَيۡظِۖ كُلَّمَآ أُلۡقِيَ فِيهَا فَوۡجٞ سَأَلَهُمۡ خَزَنَتُهَآ أَلَمۡ يَأۡتِكُمۡ نَذِيرٞ

Unakaribia huo moto wa Jahanamu kupasuka kwa ukali wa hasira ulizonazo juu ya wakanushaji. Kila linapotiwa humo kundi la watu, wale wawakilishi wa kusimamia mambo ya huo moto wa Jahanamu wanawauliza kwa njia ya kuwalaumu na kuwakaripia: Je kwani hakuwajia, huko duniani, mjumbe wa kuwatahadharisha na adhabu hii ambayo nyinyi mmo ndani yake? info
التفاسير: |

9 : 67

قَالُواْ بَلَىٰ قَدۡ جَآءَنَا نَذِيرٞ فَكَذَّبۡنَا وَقُلۡنَا مَا نَزَّلَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٍ إِنۡ أَنتُمۡ إِلَّا فِي ضَلَٰلٖ كَبِيرٖ

Watawajibu kwa kusema, Ndio! Tumejiwa na Mjumbe anayetoka kwa Allah Mtukufu, akatuonya na tukamkanusha na tukasema kuhusu miujiza aliyokuja nayo: Allah Mtukufu hakumteremshia binadamu kitu chochote. nyinyi si kingine, (enyi Mitume), isipokuwa mmeenda mbali na haki. info
التفاسير: |

10 : 67

وَقَالُواْ لَوۡ كُنَّا نَسۡمَعُ أَوۡ نَعۡقِلُ مَا كُنَّا فِيٓ أَصۡحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ

Na watasema kwa kukubali makosa, «Lau tungekua tunasikia usikivu wa mwenye kutafuta haki, au tunafikiria juu ya yale tunayoitiwa kwayo, tusingekua kati ya watu wa Motoni». info
التفاسير: |

11 : 67

فَٱعۡتَرَفُواْ بِذَنۢبِهِمۡ فَسُحۡقٗا لِّأَصۡحَٰبِ ٱلسَّعِيرِ

Hivyo basi wakakubali kukanusha kwao na kukufuru kwao kulikowafanya wastahili adhabu ya Moto. Basi kuwa mbali na rehema za Allah Mtukufu ni kwa watu wa Motoni! info
التفاسير: |

12 : 67

إِنَّ ٱلَّذِينَ يَخۡشَوۡنَ رَبَّهُم بِٱلۡغَيۡبِ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَأَجۡرٞ كَبِيرٞ

Hakika wale wanaomuogopa Mola wao, wakamuabudu hali wako mbali na macho ya watu, na wanaiogopa adhabu ya Akhera kabla hawajaiona, watapata msamaha wa dhambi zao kutoka kwa Allah Mtukufu na malipo mema makubwa ambayo ni Pepo. info
التفاسير: |
prev

Al-Mulk

next
:
0:00 0:00