Prijevod značenja časnog Kur'ana - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: Sura el-A'araf   Ajet:

Surat Al-A'raf

الٓمٓصٓ
«Alif, Lām, Mīm, Ṣād.» Yametangulia maneno kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah.
Tefsiri na arapskom jeziku:
كِتَٰبٌ أُنزِلَ إِلَيۡكَ فَلَا يَكُن فِي صَدۡرِكَ حَرَجٞ مِّنۡهُ لِتُنذِرَ بِهِۦ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Hii Qur’ani ni Kitabu kitukufu, Mwenyezi Mungu Amekiteremsha kwako, ewe Mtume. Basi pasiwe na shaka katika kifua chako kwamaba imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Na usiwe na wasiwasi katika kuifikisha kwa watu na kuwaonya nayo. Tumeiteremsha kwako ili uwatishe nayo makafiri na uwakumbushe Waumini.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱتَّبِعُواْ مَآ أُنزِلَ إِلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ وَلَا تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۗ قَلِيلٗا مَّا تَذَكَّرُونَ
Yafuateni, enyi watu, hayo yaliyoteremshwa kutoka kwa Mola wenu miongoni mwa Qur’ani na Sunnah(mafundisho ya Mtume) kwa kufuata maamrisho na kuepuka makatazo Na wala msiwafuate wategemewa badala ya Mwenyezi Mungu, kama mashetani na wasomi wa Kiyahudi na watawa wa Kinaswara. Hakika nyinyi ni mara chache mnapowaidhika na kuzingatia na mkarudi kwenye haki.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَكَم مِّن قَرۡيَةٍ أَهۡلَكۡنَٰهَا فَجَآءَهَا بَأۡسُنَا بَيَٰتًا أَوۡ هُمۡ قَآئِلُونَ
Na miji mingi tuliwaangamiza watu wake kwa sababu ya kwenda kinyume kwao na Mitume wetu na kuwakanusha. Hilo likawaletea utwevu wa duniani uliounganishwa na unyonge wa Akhera. Basi adhabu yetu iliwajia, wakati mwingine wakiwa wamelala usiku, na wakati mwingine wakiwa wamelala mchana. Mwenyezi Mungu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuwa ni nyakati za utulivu na mapumziko. Hivyo basi, kuja kwa adhabu kwenye nyakati mbili hizi kunababaisha zaidi na adhabu yenyewe huwa ni kali zaidi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَمَا كَانَ دَعۡوَىٰهُمۡ إِذۡ جَآءَهُم بَأۡسُنَآ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ إِنَّا كُنَّا ظَٰلِمِينَ
Basi hawakuwa na neno la kunena ilipoteremka adhabu isipokuwa ni kukubali kwao kwamba walifanya madhambi na walikosea na kwamaba wao wanastahili kupata adhabu iliyowashukia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلَّذِينَ أُرۡسِلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَنَسۡـَٔلَنَّ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Basi tutawauliza, tena tutawauliza, wale watu waliopelekewa Mitume, «Mliwajibu vipi Mitume wetu?» Na tutawauliza, tene tutawauliza, wale Mitume kuhusu kuufikisha kwao ujumbe wa Mola wao na namna walivyojibiwa na wale watu waliotumwa kwao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيۡهِم بِعِلۡمٖۖ وَمَا كُنَّا غَآئِبِينَ
Tutawaelezea, tena tutawaelezea, viumbe wote yale waliyoyatenda, kutokana na ujuzi wetu wa vitendo vyao ulimwenguni katika yale tuliyowaamrisha na tuliyowakataza. Na wala hatukwa mbali na wao katika hali yoyote ile.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلۡوَزۡنُ يَوۡمَئِذٍ ٱلۡحَقُّۚ فَمَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Na kuvipima vitendo vya watu Siku ya Kiyama kutakuwa ni kwa mizani ya kikweli, kwa usawa na uhaki ambao hauna maonevu. Basi yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nzito, kwa wingi wa mema yake, hao ndio watakaofaulu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ فَأُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُم بِمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَظۡلِمُونَ
Na yoyote yule ambaye mizani za vitendo vyake zitakuwa nyepesi, kwa wingi wa maovu yake, hao ndio waliopoteza bahati yao ya kupata radhi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa sababu ya kukiuka kwao mipaka kwa kuzikanusha aya za Mwenyezi Mungu , Aliyetukuka, na kukosa kuzifuata.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ مَكَّنَّٰكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَجَعَلۡنَا لَكُمۡ فِيهَا مَعَٰيِشَۗ قَلِيلٗا مَّا تَشۡكُرُونَ
Kwa hakika tumewapa utulivu, enyi watu, katika ardhi, na tumewaekea humo vitu mtakavyovitumia katika maisha yenu miongoni mwa vyakula na vinywaji; na pamoja na hayo, shukrani zenu juu ya neema za Mola wenu ni chache.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ خَلَقۡنَٰكُمۡ ثُمَّ صَوَّرۡنَٰكُمۡ ثُمَّ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ لَمۡ يَكُن مِّنَ ٱلسَّٰجِدِينَ
Na kwa hakika, tumwaneemesha nyinyi kwa kumuumba chanzo chenu - naye ni baba yenu Ādam- kutokana na kutokuwako kamwe, kisha tukamtia sura ya umbo lake lililo bora kuliko lile la viumbe wengi. Kisha tuliwaamuru Malaika wetu, amani iwashukie, wamsujudie kwa ajili ya kumtukuza na kumuheshimu na kuonyesha ubora wa Ādam. Nao wakamsujudia wote, isipokuwa Iblisi, ambaye alikuwa pamoja na wao, hakuwa ni miongoni mwa wenye kumsujudia Ādam kwa kumuhusudu kwa heshima hii kubwa aliyopewa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسۡجُدَ إِذۡ أَمَرۡتُكَۖ قَالَ أَنَا۠ خَيۡرٞ مِّنۡهُ خَلَقۡتَنِي مِن نَّارٖ وَخَلَقۡتَهُۥ مِن طِينٖ
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akasema hali ya kumkemea Iblisi kwa kuacha kwake kumsujudia Ādam, «Ni lipi lililokuzuia usisujudu nilipokuamuru?» Iblisi akasema, «Mimi ni bora kuliko yeye, kwa kuwa mimi nimeumbwa kwa moto na yeye ameumbwa kwa udongo.» Akaona kuwa moto ni bora kuliko udongo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ فَٱهۡبِطۡ مِنۡهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَٱخۡرُجۡ إِنَّكَ مِنَ ٱلصَّٰغِرِينَ
Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Iblisi, «Shuka kutoka Peponi, kwani haifai kwako kufanya ujeuri humo; toka Peponi, kwani wewe ni miongoni mwa wanyonge waliyo watwevu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ أَنظِرۡنِيٓ إِلَىٰ يَوۡمِ يُبۡعَثُونَ
Iblisi akasema kumwambia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, alipokata tamaa na rehema Yake, «Nipe muda mpaka Siku ya watu kufufuliwa, ili nipate kumpoteza ninayeweza kumpoteza kati ya wanadamu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ إِنَّكَ مِنَ ٱلۡمُنظَرِينَ
Akasema Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, «Wewe ni miongoni mwa wale niliowaandikia kucheleweshwa kipindi chao cha kufa mpaka Mvivio wa Kwanza katika Parapanda pindi viumbe wote watakapokufa.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِي لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٰطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ
Iblisi akasema, Mwenyezi Mungu Amlaani, «Kwa sababu ya kuwa wewe umenipoteza, nitafanya bidii katika kuwapoteza binadamu wawe kando ya njia yako iliyolingana sawa na nitawazuia wao wasiuuandame Uislamu ambao wanasibiana na umbile lao ulilowaumbia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ثُمَّ لَأٓتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِيهِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَيۡمَٰنِهِمۡ وَعَن شَمَآئِلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَٰكِرِينَ
«Kisha nitawajia kutoka pande zote na pambizo niwazuie wasiifuate haki, niwapambie batili, niwafanye wavutike na dunia na niwatie shaka kuhusu Akhera. Na hutawapata wengi wa wanadamu ni wenye kukushukuru wewe kwa neema zako.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱخۡرُجۡ مِنۡهَا مَذۡءُومٗا مَّدۡحُورٗاۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ لَأَمۡلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمۡ أَجۡمَعِينَ
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akasema, kumwambia Iblisi, «Toka Peponi ukiwa umechukiwa na umefukuzwa. Nitaujaza Moto wa Jahanamu kwa kukuingiza wewe humo na binadamu wote watakaokufuata.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَيَٰٓـَٔادَمُ ٱسۡكُنۡ أَنتَ وَزَوۡجُكَ ٱلۡجَنَّةَ فَكُلَا مِنۡ حَيۡثُ شِئۡتُمَا وَلَا تَقۡرَبَا هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
«Na ewe Ādam, keti wewe pamoja na mke wako Ḥawwā’ Peponi na kuleni matunda yaliyo humo popote mnapotaka na wala msile matunda ya mti huu (Aliwatajia mti huo), mkifanya hilo mtakuwa ni madhalumu wenye kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَوَسۡوَسَ لَهُمَا ٱلشَّيۡطَٰنُ لِيُبۡدِيَ لَهُمَا مَا وُۥرِيَ عَنۡهُمَا مِن سَوۡءَٰتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَىٰكُمَا رَبُّكُمَا عَنۡ هَٰذِهِ ٱلشَّجَرَةِ إِلَّآ أَن تَكُونَا مَلَكَيۡنِ أَوۡ تَكُونَا مِنَ ٱلۡخَٰلِدِينَ
Hapo Shetani aliwashawishi Ādam na Ḥawwā’ ili awatokomeze kwenye kumuasi Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kula matunda ya mti ule ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza kuula, ili mwisho wao uwe ni kufunukwa na tupu zao zilizokuwa zimesitiriwa. Na akawaambia, katika kujaribu kwake kuwafanyia vitimbi, «Hakika Mola wenu Amewakataza kula matunda ya mti huu ili msipate kuwa Malaika na ili msipate kuwa ni miongoni mwa wenye kuishi milele.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَاسَمَهُمَآ إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ ٱلنَّٰصِحِينَ
Na Shetani Aliwaapia Ādam na Ḥawwā’ kwa Mwenyezi Mungu kwamba yeye ni miongoni mwa wale wanaowapa nasaha kwa kuwashauri kula kutoka mti ule, huku yeye ni mrongo katika hilo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَدَلَّىٰهُمَا بِغُرُورٖۚ فَلَمَّا ذَاقَا ٱلشَّجَرَةَ بَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۖ وَنَادَىٰهُمَا رَبُّهُمَآ أَلَمۡ أَنۡهَكُمَا عَن تِلۡكُمَا ٱلشَّجَرَةِ وَأَقُل لَّكُمَآ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ لَكُمَا عَدُوّٞ مُّبِينٞ
Hapo yeye aliwatia wao ujasiri na akawadanganya wakala kutoka mti huo ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza wasiukaribie. Walipokula kutoka mti huo, ziliwafunuka tupu zao na kikaondoka kile ambacho Mwenyezi Mungu Aliwasitiri nacho kabla ya wao kufanya uhalifu huo, wakawa wanayaambatisha majani ya miti ya Peponi kwenye tupu zao. Hapo Mola wao, Aliyetukuka na kuwa juu, Aliwaita, «Kwani sikuwakataza kula kutoka mti ule na nikawaambia kwamba Shetani, kwenu nyinyi, ni adui ambaye uadui wake uko waziwazi?» Katika aya hii kuna ushahidi kwamba kukaa uchi ni kati ya mambo makubwa na kwamba hilo ni jambo lililokowa lachukiza na linaloendelea kuchukiza katika tabia, na ni ovu kwenye akili za watu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمۡنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمۡ تَغۡفِرۡ لَنَا وَتَرۡحَمۡنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Ādam na Ḥawwā’ walisema, «Ewe Mola wetu, tumejidhulumu nafsi zetu kwa kula kutoka kwenye mti ule. Na iwapo hutatusamehe na kuturehemu, tutakuwa ni miongoni mwa waliopoteza bahati zao katiku ulimengu wao na Akhera yao.» Maneno haya ndiyo yale aliyoyapokea Ādam kutoka kwa Mola wake akayatumia katika kumuomba, ndipo Mola wake Akaikubali toba yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ
Akasema, Aliyetukuka, kumwambia Ādam, Ḥawwā’ na Iblisi, «Shukeni kutoka mbinguni muende ardhini, baadhi yenu mkiwa ni maadui ya wengine. Huko mtakuwa na mahala pa nyinyi kutulia na pa kujiliwaza mpaka muda wenu ukome.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ فِيهَا تَحۡيَوۡنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنۡهَا تُخۡرَجُونَ
Mwenyezi Mngu, Aliyetukuka, Akasema kumwambia Ādam, Ḥawwā’ na kizazi chao, «Huko ardhini mtaishi, yaani mtapitisha siku za uhai wenu duniani, na huko kitakuwa kifo chenu, na kutoka huko Mola wenu atawatoa na awakusanye mkiwa hai Siku ya Ufufuzi.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ قَدۡ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمۡ لِبَاسٗا يُوَٰرِي سَوۡءَٰتِكُمۡ وَرِيشٗاۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقۡوَىٰ ذَٰلِكَ خَيۡرٞۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Enyi wanadamu, tumewaekea vazi lenyi kusitiri tupu zenu, nalo ni vazi la lazima, na vazi la pambo na kujirembesha, nalo ni vazi la kujikamilisha na kujifurahisha. Na vazi la uchaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo, ndilo vazi bora kwa aliyeamini. Hayo Ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha nayo miongoni mwa alama za uola wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, upweke Wake, wema Wake na rehema Zake kwa waja Wake, ili mpate kuzikumbuka neema hizi na mumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٰتِهِمَآۚ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Enyi wanadamu! Asiwadanganye Shetani akawapambia maasia, kama alivyowapambia wazazi wenu, Ādam na Ḥawwā’, akawatoa Peponi kwa sababu hiyo, akawavua vazi lao ambalo Mwenyezi Mungu Aliwasitiri nalo ili tupu zao zifunuke. Shetani na kizazi chake na viumbe wa jinsi yake wanawaona nyinyi, na nyinyi hamuwaoni, basi jichungeni nao. Hakika sisi tumewafanya Mashetani ni wategemewa wa makafiri ambao hawampwekeshi Mwenyezi Mungu wala hawawaamini Mitume Wake wala hawautumii muongozo Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةٗ قَالُواْ وَجَدۡنَا عَلَيۡهَآ ءَابَآءَنَا وَٱللَّهُ أَمَرَنَا بِهَاۗ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na makafiri wanapofanya tendo ovu, wanajitetea kwa kusema kwamba hilo ni miongoni mwa yale waliyoyapokea kutoka kwa baba zao na kwamba hilo ni katika yale Aliyoyaamrisha Mwenyzi Mungu. Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Hawaamrishi waja Wake vitendo vichafu na viovu. Je, mnasema, kumsingizia Mwenyezi Mungu msiyoyajua, urongo na uzushi?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mola wangu Ameniamrisha usawa, na Amewaamrisha nyinyi mumtakasie ibada katika kila sehemu za ibada, hasa katika misikiti, na mumuombe Yeye hali ya kumtakasia utiifu na ibada, na muamini kufufuliwa baada ya kufa. Na kama Alivyowaleta kutoka kuwa hamkuwako,Yeye ni Muweza kuwarudishia uhai mara nyingine.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلضَّلَٰلَةُۚ إِنَّهُمُ ٱتَّخَذُواْ ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُم مُّهۡتَدُونَ
Mwenyezi Mungu Amewafanya waja wake makundi mawili: kundi moja Amelielekeza kwenye uongofu, kwenye njia iliyolingana; na kundi lingine limelazimika kupotea njia iliyolingana, kwani wao wamewafanya Mashetani ni wategemewa wao badala ya Mwenyezi Mungu, waliwasikiliza Mashetani kwa ujinga wao na kudhania kwao kuwa wao wamefuata njia ya uongofu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ خُذُواْ زِينَتَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَكُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Enyi wanadamu! Kuweni, kila mnapotekeleza Swala, katika hali ya pambo linalokubalika kisheria la nguo zinazofinika tupu zenu na muwe katika hali ya usafi, utohara na mfano wake. Na kuleni na kunyweni katika vizuri Alivyowapa Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka ya wastani, kwani Mwenyezi Mungu Hawapendi wakiukaji wenye kupitsha kiasi katika vyakula na vinywaji na mengineyo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ مَنۡ حَرَّمَ زِينَةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِيٓ أَخۡرَجَ لِعِبَادِهِۦ وَٱلطَّيِّبَٰتِ مِنَ ٱلرِّزۡقِۚ قُلۡ هِيَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا خَالِصَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ
Sema, ewe Mtume, uwaambie hao wajinga miongoni mwa washirikina, «Ni nani aliyewaharamishia vazi zuri ambalo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amelifanya kuwa ni pambo kwenu? Na ni nani Aiyewaharamishia kujistarehesha kwa chakula kizuri cha halali kilichoruzukiwa na Mwenyezi Mungu?» Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, «Kwa hakika vile alivyoviruhusu Mwenyezi mungu, miongoni mwa mavazi na vitu vizuri miongoni mwa vyakula na vinywaji, ni haki kwa walioamini pamoja na wengineo katika maisha ya ulimwenguni, na ni haki kwa walioamini peke yao Siku ya Kiyama. Maelezo kama hayo ni mafundisho ambayo Mwenyezi Mungu Anayaelezea kwa watu wenye kuyajua mambo wanayoelezwa na kuyaelewa wanayofafanuliwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliyetuka, vitu vyingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia urongo,» kama madai ya kwamba Mwenyezi Mungu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٞۖ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمۡ لَا يَسۡتَأۡخِرُونَ سَاعَةٗ وَلَا يَسۡتَقۡدِمُونَ
Kila kikundi kilichojikusanya kumkanusha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na kuwakanusha Mitume Wake, amani iwashukie, kina wakati wa kushukiwa na mateso. Huo wakati, Aliouweka Mwenyezi Mungu wa kuwaangamiza, hawatakawia nao, japokuwa kwa muda mfupi, wala hawataungulia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ إِمَّا يَأۡتِيَنَّكُمۡ رُسُلٞ مِّنكُمۡ يَقُصُّونَ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِي فَمَنِ ٱتَّقَىٰ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Enyi wanadamu! Pindi watakapokuja kwenu Mitume wangu, miongoni mwa watu wenu, wakiwasomea aya za Kitabu changu na kuwafahamisha hoja juu ya ukweli wa yale waliyokuja nayo, basi watiini, kwani mwenye kujikinga na hasira zangu na akayatengeneza matendo yake, hao hawatakuwa na hofu na mateso ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama wala hawatahuzunika juu yale yaliyowapita miongoni mwa hadhi za duniani.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na makafiri ambao wamezikanusha hoja za kumpwekesha Mwenyezi Mungu na wakaacha kuzifuata kwa kujiona bora, hao ni watu wa Motoni wenye kukaa milele humo, hawatatoka humo kabisa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ يَنَالُهُمۡ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوۡنَهُمۡ قَالُوٓاْ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ
Hakuna yoyote aliye na udhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, urongo au akazikanusha aya Zake zilizoteremshwa, hao itawafikia sehemu yao ya adhabu waliyoandikiwa katika Al-Lawh( Al-Mhfūd) (Ubao uliohifadhiwa) mpaka atakapowajia Malaika wa mauti pamoja na wasaidizi wake kuzichukua roho zao, watawaambia, «Wako wapi wale mliokuwa mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, kati ya washirika, wategemewa na masanamu, waje wawaokoe na janga lililowafika?» Watasema, «Wametutoroka.» Wakati huo watakiri makosa kwamba wao duniani walikuwa ni wenye kuupinga na kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱدۡخُلُواْ فِيٓ أُمَمٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِكُم مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ فِي ٱلنَّارِۖ كُلَّمَا دَخَلَتۡ أُمَّةٞ لَّعَنَتۡ أُخۡتَهَاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا ٱدَّارَكُواْ فِيهَا جَمِيعٗا قَالَتۡ أُخۡرَىٰهُمۡ لِأُولَىٰهُمۡ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ أَضَلُّونَا فَـَٔاتِهِمۡ عَذَابٗا ضِعۡفٗا مِّنَ ٱلنَّارِۖ قَالَ لِكُلّٖ ضِعۡفٞ وَلَٰكِن لَّا تَعۡلَمُونَ
Hapo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Atasema kuwaambia washirikina hawa wazushi, «Ingieni Motoni mkiwa pamoja na makundi ya walio mfano wenu katika ukafiri, waliotangulia kabla yenu, kati ya majini na wanadamu. Kila kundi la mila mimoja likiingia Motoni litalaani watu wa kundi lingine linalofanana nalo, waliokuwa ni sababu ya kupotea kwake kwa kuwafuata. Mpaka watakapokutana ndani ya Moto wote pamoja: wa mwanzo, miongoni mwa wafuasi wa mila za kikafiri, na wa mwisho miongoni mwao; hapo watasema wa mwisho, waliokuwa ni watu wa kuandama ulimwenguni, kuwaambia viongozi wao, «Mola wetu, hawa ndio waliotupoteza wakatupotosha na haki, basi wape adhabu nyongeza ya Moto.» Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Atasema, «Kila mmoja atapata nyongeza.» Yaani, kila mmoja kati yenu na wao atapata adhabu nyongeza ya Moto, «lakini nyinyi wafuasi hamuijui ile sehemu ya adhabu na machungu ambayo kila kundi miongoni mwenu ataipata.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَالَتۡ أُولَىٰهُمۡ لِأُخۡرَىٰهُمۡ فَمَا كَانَ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلٖ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ
Hapo watasema wale waliofuatwa miongoni mwa viongozi na wengineo kuwaambia wafuasi wao, «Sisi na nyinyi tuko sawa katika uharibifu na upotevu na katika kufanya vitendo ambavyo ndio sababu ya kupata adhabu, kwa hivyo, nyinyi hamuna ubora juu yetu.» Mwenyezi Mungu Atawaambia wao wote, «Basi ionjeni adhabu,» yaani adhabu ya Jahanamu «kwa makosa mliyoyatenda.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمۡ أَبۡوَٰبُ ٱلسَّمَآءِ وَلَا يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ ٱلۡجَمَلُ فِي سَمِّ ٱلۡخِيَاطِۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Hakika wale makafiri ambao hawakuzikubali hoja zetu na aya zetu zinazojulisha upweke wetu na ambao hawakuzitumia sheria zetu kwa kiburi na majivuno, vitendo vyao maishani, na pia roho zao wakati wa kufa, havitafunguliwa milango ya mbingu. Na haiwezekani kwa makafiri hawa kuingia Peponi isipokuwa iwapo ngamia ataingia kwenye tundu ya sindano; na hilo ni muhali. Na mfano wa malipo haya tutawalipa wale ambao uovu wao umezidi na kukiuka kwao mipaka kumepindukia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٞ وَمِن فَوۡقِهِمۡ غَوَاشٖۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّٰلِمِينَ
Makafiri hawa ni wenye kukalishwa milele Motoni. Watapata humo kwenye Moto wa Jahanamu tandiko chini yao, na juu yao kutakuwa na mifiniko inayowafinika. Na mfano wa mateso haya mabaya Atawatesa nayo Mwenyezi Mungu wale madhalimu ambao wamekiuka mipaka Yake, wakamkanusha na wakamuasi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na wakafanya vitendo vyema kwa kiasi cha uwezo wao, kwani Mwenyezi Mungu Hamlazimishi mtu matendo isipokuwa yale ayawezayo, hao ni watu wa Peponi, wao humo ni wenye kukaa milele, hawatoki humo kabisa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلّٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَقَالُواْ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي هَدَىٰنَا لِهَٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهۡتَدِيَ لَوۡلَآ أَنۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُۖ لَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّۖ وَنُودُوٓاْ أَن تِلۡكُمُ ٱلۡجَنَّةُ أُورِثۡتُمُوهَا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ataziondoa chuki na mafundo ndani ya vifua vya watu wa Peponi. Na miongoni mwa kukamilika neema zao ni kwamba mito ya maji itakuwa ikipita chini yao. Na watasema watu wa Peponi pindi watakapoingia humo, «Shukrani ni za Mwenyezi Mungu Aliyetuafikia kufanya vitendo vyema ambavyo vimetupatia starehe hizi ambazo tuko nazo. Na hatukuwa tuna uwezo wa kuifuata njia iliyolingana sawa kama si Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kutuongoza kufuata njia hii na kutuwezesha kukita juu yake. Mitume wa Mola wetu wametuletea habari za ukweli za ahadi njema kwa wenye kumtii na za kuwaonya wenye kumuasi. Na wataitwa kwa kupongezwa na kukirimiwa waambiwe, «Hiyo ndiyo pepo Mwenyezi Mungu Aliyowapa ni urathi kwa rehema Zake na kwa mliyoyatanguliza ya Imani na matendo mema.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِ أَصۡحَٰبَ ٱلنَّارِ أَن قَدۡ وَجَدۡنَا مَا وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقّٗا فَهَلۡ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمۡ حَقّٗاۖ قَالُواْ نَعَمۡۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنُۢ بَيۡنَهُمۡ أَن لَّعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ
Watu wa Peponi, baada ya kuingia humo, watawaita watu wa Motoni wawaambie, «Sisi tumeshapata kuwa ni kweli tuliyoahidiwa na Mola wetu, kupitia ndimi za Mitume Wake, kuhusu kuwalipa wanaomtii. Je, nyinyi mumeyapata mliyoahidiwa na Mola wenu, kupitia ndimi za Mitume Wake, kuwa ni kweli kuhusu kuwaadhibu wanaomuasi?» Hapo watu wa Motoni watawajibu watu wa Peponi wakiwaambia, «Ndio, kwa kweli tumeyapata yale Aliyotuahidi Mola wetu kuwa ni kweli.» Hapo Atatangaza mwenye kutangaza, akiwa kati baina ya watu wa Peponi na watu wa Motoni akisema, «Laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie watu madhalimu» ambao walikiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wakamkanusha Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱلَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجٗا وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ كَٰفِرُونَ
Makifiri hawa ndio wale waliokuwa wakiipuuza njia ya Mwenyezi Mungu iliyolingana sawa, na wakiwazuia watu wasiifuate, na wakitaka kwamba njia ya kuifuata iwe kombo ili kusiwe na yoyote wa kuielewa; na wao, kuhusu Akhera na mambo yake, ni wenye kukanusha.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَبَيۡنَهُمَا حِجَابٞۚ وَعَلَى ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٞ يَعۡرِفُونَ كُلَّۢا بِسِيمَىٰهُمۡۚ وَنَادَوۡاْ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ أَن سَلَٰمٌ عَلَيۡكُمۡۚ لَمۡ يَدۡخُلُوهَا وَهُمۡ يَطۡمَعُونَ
Na baina ya watu wa Peponi na watu Motoni patakuwa na kizuizi kikubwa kinaitwa Al-A’rāf. Na juu ya kizuizi hiki kutakuwa na wanaume wanaowajuwa watu wa Peponi na watu wa Motoni kwa alama zao kama weupe wa nyuso za watu wa Peponi na weusi wa nyuso za watu wa Motoni. Wanaume hawa ni watu ambao vitendo vyao vizuri na viovu viko sawasawa, na wao wana matumaini ya kupata rehema ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Wanaume hao wa hapo Al-A’rāf watawaita watu wa Peponi kwa maamkuzi wakiwaambia, «Salamun 'alaykum»(Amani iwe juu yenu.) Watu hawa wa Al-A’rāf bado hawajaingia Peponi, na wao wana matumaini ya kuingia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَإِذَا صُرِفَتۡ أَبۡصَٰرُهُمۡ تِلۡقَآءَ أَصۡحَٰبِ ٱلنَّارِ قَالُواْ رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Na yatakapogeuzwa macho ya watu wa Al-A’rāf upande wa watu wa Motoni watasema, «Ewe Mola wetu, usitufanye kuwa pamoja na watu madhalimu» kwa ya ushirikina wao na ukafiri wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَعۡرَافِ رِجَالٗا يَعۡرِفُونَهُم بِسِيمَىٰهُمۡ قَالُواْ مَآ أَغۡنَىٰ عَنكُمۡ جَمۡعُكُمۡ وَمَا كُنتُمۡ تَسۡتَكۡبِرُونَ
Na watu walioko Al-A’rāf watawaita wanaume, miongoni mwa viongozi wa makafiri waliomo motoni, wanaowajua kwa alama zao fulani zinazowatenganisha wawaambie, «Hayakuwafaa chochote mali mliokuwa mkiyakusanya ulimwenguni wala watu; pia hakikuwafaa kiburi chenu kilichowafanya nyinyi msimuamini Mwenyezi Mungu na msiikubali haki.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَهَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ أَقۡسَمۡتُمۡ لَا يَنَالُهُمُ ٱللَّهُ بِرَحۡمَةٍۚ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ لَا خَوۡفٌ عَلَيۡكُمۡ وَلَآ أَنتُمۡ تَحۡزَنُونَ
Je madhaifu na mafukara hawa, kati ya watu wa Peponi, ndio wale mlioapa huko duniani kwamba Mwenyezi Mungu Hatawakusanya Siku ya Kiyama Awatie kwenye rehema na Hatawaingiza Peponi? Ingieni Peponi, enyi watu wa Al- A'rāf, hakika mumesamehewa; hamna tene kicho cha kupata adhabu ya Mwenyezi Mungu, wala hamtahuzunika juu ya hadhi za duniani zilizowapita.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَنَادَىٰٓ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِ أَصۡحَٰبَ ٱلۡجَنَّةِ أَنۡ أَفِيضُواْ عَلَيۡنَا مِنَ ٱلۡمَآءِ أَوۡ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُۚ قَالُوٓاْ إِنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَهُمَا عَلَى ٱلۡكَٰفِرِينَ
Watu wa Motoni wataomba msaada kwa watu wa Peponi wawamiminie maji au chakula Mwenyezi Mungu Alichowaruzuku. Na wao watawajibu kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameviharamisha vinywaji na vyakula kwa walioukanusha upweke Wake na wakawafanya Mitume Wake kuwa ni warongo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَهُمۡ لَهۡوٗا وَلَعِبٗا وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ فَٱلۡيَوۡمَ نَنسَىٰهُمۡ كَمَا نَسُواْ لِقَآءَ يَوۡمِهِمۡ هَٰذَا وَمَا كَانُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَجۡحَدُونَ
Wale ambao Mwenyezi mungu, Aliyetukuka, Atawanyima starehe za Akhera ni wale ambao waliifanya Dini, ambayo Mwenyezi Mungu Amewaamuru kuifuata, kuwa ni pumbao, na yakawadanganya wao maisha ya ulimwenguni, wakashughulishwa na mapambo yake wasifanye matendo ya kuwafaa Akhera, hao Atawasahau Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Siku ya Kiyama, na Atawaacha ndani ya adhabu iumizayo, kama walivyoyaacha matendo ya kuwafaa kwa kukutana na Siku yao hii, na kwa kuwa wao walikuwa wakizikanusha dalili za Mwenyezi Mungu na hoja Zake pamoja na kujua kwao kuwa ni za ukweli.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ جِئۡنَٰهُم بِكِتَٰبٖ فَصَّلۡنَٰهُ عَلَىٰ عِلۡمٍ هُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Hakika tumewaletea makafiri Qur’ani tuliyokuteremshia wewe, ewe Mtume, tuliyoibainisha, inayokusanya elimu kubwa, yenye kuongoza, kutoa kwenye upotevu, kupeleka kwenye njia ya usawa, hali ya kuwa ni rehema kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na kuzitumia sheria Zake. Amewahusu wenye kuamini kwa kuwataja, bila ya wengine, ni kwamba wao ndio wenye kunufaika nayo
Tefsiri na arapskom jeziku:
هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأۡوِيلَهُۥۚ يَوۡمَ يَأۡتِي تَأۡوِيلُهُۥ يَقُولُ ٱلَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبۡلُ قَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَآءَ فَيَشۡفَعُواْ لَنَآ أَوۡ نُرَدُّ فَنَعۡمَلَ غَيۡرَ ٱلَّذِي كُنَّا نَعۡمَلُۚ قَدۡ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ وَضَلَّ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Kwani kuna wanachokingojea makafiri isipokuwa mateso, ambayo ndiyo kikomo cha mambo yao, waliyoahidiwa katika Qur’ani? Siku kitakapokuja kikomo cha mambo yao, cha kuhesabiwa, kulipwa na mateso Siku ya Kiyama, watasema makafiri walioiacha Qur’ani na wakaikanusha duniani, «Sasa imetubainikia kwamba Mitume wa Mola wetu wamekuja na haki na wametupa ushauri mzuri. Je, tunaweza kupata marafiki na waombezi wapate kutuombea kwa Mola wetu? Au tunaweza kupewa nafasi ya kurudi duniani mara nyingine tupate kufanya matendo ya kumfanya Mwenyezi Mungu Awe radhi na sisi? Hakika wamepata hasara nafsi zao kwa kuingia Motoni na kukaa milele humo, na vimewaondokea vile ambavyo walikuwa wakiviabudu badala ya Mwenyezi Mungu na yale ambayo walikuwa wakiyazua miongoni mwa yale ambayo Shetani alikuwa akiwaadi nayo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ رَبَّكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ يُغۡشِي ٱلَّيۡلَ ٱلنَّهَارَ يَطۡلُبُهُۥ حَثِيثٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ وَٱلنُّجُومَ مُسَخَّرَٰتِۭ بِأَمۡرِهِۦٓۗ أَلَا لَهُ ٱلۡخَلۡقُ وَٱلۡأَمۡرُۗ تَبَارَكَ ٱللَّهُ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Hakika Mola wenu, enyi watu, ni Yule Aliyeanzisha mbingu na ardhi kutoka kwenye 'adam (hali ya kutokuwako) kwa Siku Sita, kisha Akalingana, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, juu ya 'Arsh, -yaani : Alikuwa juu- mlingano unaonasibiana na utukufu na ukubwa Wake. Yeye , kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anauingiza usiku kwenye mchana ukaufinika mpaka mwangaza wake ukaondoka, na Anauingiza usiku kwenye mchana mpaka giza lake likaondoka. Na daima kila mojawapo, kati ya viwili hivyi, kinafuata kingine kwa kasi. Na Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Ndiye Aliyeumba jua, mwezi na nyota zikiwa zinamtii Yeye, Anazipelekesha, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, vile Anavyotaka, nazo ni miongoni mwa alama kubwa za Mwenyezi Mungu. Jua utanabahi kwamba ni wake Yeye, kutakasika na sifa za upungufu na kutukuka ni Kwake, uumbaji wote, na ni Yake Yeye amri yote. Ametukuka Mwenyezi Mungu, umeendelea ukuu Wake na Ameepukana na kila upungufu, Bwana wa viumbe wote.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱدۡعُواْ رَبَّكُمۡ تَضَرُّعٗا وَخُفۡيَةًۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُعۡتَدِينَ
Muombeni, enyi Waumini, Mola wenu, kwa kujidhalilisha Kwake, kwa siri na kwa dhahiri.Na maombi yawe kwa unyenyekevu na yawe mbali na kujionyesha.Hakika Mwenyezi Mungu Hawapendi wanaokiuka mipaka ya sheria Zake. Na ukiukaji mkubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, kama vile kuwaomba wafu, masanamu na wengineo mfano wao wasiokuwa Mwenyezi Mungu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَا وَٱدۡعُوهُ خَوۡفٗا وَطَمَعًاۚ إِنَّ رَحۡمَتَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ مِّنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Wala msilete katika ardhi aina yoyote ya uharibifu, baada ya Mwenyezi Mungu kuitengeneza kwa kutuma Mitume, amani iwashukie, na kuimarika kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu. Na muombeni Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, mkimtakasia maombi yenu, kwa kuogopa mateso Yake na kuwa na matumaini kupata malipo Yake mazuri. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wenye kufanya wema.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَهُوَ ٱلَّذِي يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَقَلَّتۡ سَحَابٗا ثِقَالٗا سُقۡنَٰهُ لِبَلَدٖ مَّيِّتٖ فَأَنزَلۡنَا بِهِ ٱلۡمَآءَ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ كَذَٰلِكَ نُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Anayetuma upepo mzuri mororo wenye kubashiria mvua ambayo upepo huo unaisukuma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hapo viumbe vikangiwa na furaha kwa hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu. Na pindi ifikapo wakati ambapo upepo umebeba mawingu yaliyobebeshwa mvua, Mwenyezi Mungu Huyapeleka kwa upepo huo ili kuihuisha nchi iliyopigwa na ukame ardhi yake na kukauka miti yake na mimea yake ya nafaka, Mwenyezi Mungu hapo Akaiteremsha, kwa mawingu hayo, mvua, Akaitoa kwayo nyasi, miti na mimea ya nafaka, na miti ikarudi kujaa sampuli ya matunda. Kama tunavyoihuisha ardhi hii kwa mvua, vilevile tutawatoa wafu kutoka makabarini mwao baada ya kutoweka kwao, ili muwaidhike na mchukulie dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu na uwezo Wake wa kufufua.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلۡبَلَدُ ٱلطَّيِّبُ يَخۡرُجُ نَبَاتُهُۥ بِإِذۡنِ رَبِّهِۦۖ وَٱلَّذِي خَبُثَ لَا يَخۡرُجُ إِلَّا نَكِدٗاۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَشۡكُرُونَ
Na ardhi nzuri, ikiteremkiwa na mvua, inatoa mimea kwa idhini ya Mwenyezi Mungu na matakwa Yake, ikiwa mizuri na kwa njia ya wepesi. Hivyo ndivyo alivyo Muumini, zikiteremka aya za Mwenyezi Mungu kwake, hunufaika nazo na huzalisha kwake maisha mema. Ama ardhi ya chumvi iliyo mbovu; hiyo haitoi mimea isipokuwa mibovu isiyokuwa na faida, tena kwa shida, na haitoi mimea mizuri. Hivyo ndivyo alivyo kafiri, hanufaiki kwa aya za Mwenyezi Mungu. Mfano wa sampuli hiyo nzuri katika kueleza, ndiyo namna tunavyoleta hoja na dalili mbalimbali kuthibitisha haki kwa watu wanaozishukuru neema za Mwenyezi Mungu na wanaomtii.
Tefsiri na arapskom jeziku:
لَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ فَقَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓ إِنِّيٓ أَخَافُ عَلَيۡكُمۡ عَذَابَ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Hakika tulimtuma Nūḥ kwa watu wake, ili awalinganie kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa pungufu ni Kwake, na kumtakasia ibada, akasema, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na mumnyenyekee kwa kumtii, nyinyi hamna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada. Msipofanya na mkasalia kwenye kuabudu masanamu yenu, hakika mimi nawaogopea msishukiwe na adhabu ya Siku ambayo shida yenu itakuwa kubwa, nayo ni Siku ya Kiyama.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Mabwana wao na wakubwa wao walisema, «Sisi tunaitakidi, ewe Nūḥ, wewe uko kwenye upotevu waziwazi uko kando ya njia sawa.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي ضَلَٰلَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Nūḥ Akasema, «Enyi watu wangu, mimi si mpotevu katika jambo lolote kwa njia yoyote, lakini mimi ni mjumbe kutoka Mola wa viumbe wote; Mola wangu na Mola wenu na Mola wa viumbe wote.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمۡ وَأَعۡلَمُ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
«Nawafikishia nyinyi lile niliotumwa nalo kutoka kwa Mola wangu, na wapa ushauri kwa kuwaonya na adhabu ya Mwenyezi Mungu na kuwapa bishara njema ya malipo yake mema, na mimi nayajua, kuhusu sheria Yake, msiyoyajua.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡ وَلِتَتَّقُواْ وَلَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
«Je imewafanya nyinyi muone ajabu kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameteremsha kwenu yale ambayo yatawakumbusha mambo yenye kheri kwenu, kwa ulimi wa mtu miongoni mwenu, mnaoujua ukoo wake na ukweli wake, ili awaogopeshe adhabu ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na mateso Yake, na ili mujikinge na hasira Zake kwa kumuamini na kwa kutarajia kufaulu kupata rehema Zake na malipo Yake mema mengi?
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَأَغۡرَقۡنَا ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَوۡمًا عَمِينَ
Basi walimkanusha Nūḥ, tukamuokoa na wale walioamini pamoja na yeye katika jahazi, na tukawazamisha makafiri waliokanusha hoja zetu zilizowazi. Wao walikuwa vipofu wa nyoyo kwa kutoiona haki.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمۡ هُودٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥٓۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Hakika tulimtuma, kwenda kwa watu wa kabila la 'Ād, ndugu yao Hūd, walipoabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, akawaambia, «Muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hamna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwaYeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada. Je, hamuiogopi adhabu ya Mwenyezi Mungu na hasira Zake kwenu?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦٓ إِنَّا لَنَرَىٰكَ فِي سَفَاهَةٖ وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ ٱلۡكَٰذِبِينَ
Wakasema wale viongozi waliokufuru katika watu wa Hūd, «Sisi tunajua kwamba wewe, kwa kutuita sisi kuacha kuabudu waungu wetu na kumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, ni mpungufu wa akili, na sisi tunaamini kwamba wewe, kwa hayo usemayo, ni katika wale wanaomzuluia Mwenyezi Mungu warongo.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ يَٰقَوۡمِ لَيۡسَ بِي سَفَاهَةٞ وَلَٰكِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Hūd akasema, «Enyi watu wangu, sina upungufu katika akili yangu, isipokuwa mimi ni mjumbe kutoka kwa Mola wa viumbe wote.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أُبَلِّغُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَأَنَا۠ لَكُمۡ نَاصِحٌ أَمِينٌ
«Ninawafikishia nyinyi yale ambayo Amenituma nayo Mola wangu kwenu. Na mimi kwenu, katika yale niliyowaita kwayo ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kuitumia sheria Yake, ni mshauri mwenye imani, ni muaminifu juu ya wahyi wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَعَجِبۡتُمۡ أَن جَآءَكُمۡ ذِكۡرٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ مِّنكُمۡ لِيُنذِرَكُمۡۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ قَوۡمِ نُوحٖ وَزَادَكُمۡ فِي ٱلۡخَلۡقِ بَصۜۡطَةٗۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ لَعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Je, imewafanya nyinyi muone ajabu kwamba Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ameteremsha kwenu yale ambayo yanawakumbusha mambo yaliyo na kheri kwenu, kwa ulimi wa mtu katika nyinyi, mnaoujua ukoo wake na ukweli wake, ili awaogopeshe adhabu ya Mwenyezi mungu? Na kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, Alipowafanya nyinyi mshike nafasi ya waliokuwa kabla yenu katika ardhi baada ya kuwaangamiza kaumu ya Nūḥ, na akawazidishia miili yenu nguvu na ukubwa. Basi kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu nyingi juu yenu kwa kutarajia kufanikiwa mafanikio makubwa duniani na Akhera.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِنَعۡبُدَ ٱللَّهَ وَحۡدَهُۥ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُنَا فَأۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
’Ād walisema kumwambia Hūd, amani imshukie, «Je, umetuita tumuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, na tuihame ibada ya masanamu ambayo tumeirithi kutoka kwa mababa zetu? Basi tuletee adhabu ambayo unatutusha nayo iwapo wewe ni miongoni mwa wakweli katika hayo usemayo.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ قَدۡ وَقَعَ عَلَيۡكُم مِّن رَّبِّكُمۡ رِجۡسٞ وَغَضَبٌۖ أَتُجَٰدِلُونَنِي فِيٓ أَسۡمَآءٖ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّا نَزَّلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٖۚ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ
Hūd alisema kuwaambia watu wake, «Mshashukiwa na adhabu na ghadhabu kutoka kwa Mola wenu, Aliyetukuka na kuwa juu, «Mwajadiliana na mimi juu ya masanamu hawa mliowaita waungu, nyinyi na mababa zenu? Mwenyezi Mungu Hakuteremsha hoja yoyote wala dalili ya kuwa waabudiwe, kwani wao wameumbwa, Hawadhuru wala hawanufaishi; mwenye kuabudiwa peke yake si mwengine ni Muumba, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake. Basi ngojeni kuteremkiwa na adhabu, kwani mimi, pamoja na nyinyi, nangojea kuteremka kwake. Huu ni upeo wa kuonya na kutisha.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَنجَيۡنَٰهُ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَقَطَعۡنَا دَابِرَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۖ وَمَا كَانُواْ مُؤۡمِنِينَ
Basi adhabu ya Mwenyezi Mungu ikatukia kwa kutumwa upepo mkali juu yao. Mwenyezi Mungu akamuokoa Hūd na walioamini pamoja na yeye kwa rehema kubwa kutoka kwake, Aliyetukuka. Na Akawaangamiza makafiri wote miongoni mwa watu wake, Akawavunjavunja mpaka wa mwisho wao. Na wao hawakuwa ni Waumini kwa kuwa walikusanya baina ya kukanusha aya za Mwenyezi Mungu na kuacha kufanya vitendo vyema.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Na tulimtuma, kwenda kwa watu wa kabila la Thamūd, ndugu yao Ṣāliḥ, walipoabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Ṣāliḥ aliwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hamna mola anyestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada, nimewajia na hoja juu ya ukweli wa yale ninayowaitia kwayo. Nayo ni kuwa nilimuomba Mwenyezi Mungu mbele yenu, Akawatolea kutoka kwenye jiwe hili ngamia mkubwa kama mlivyoomba, basi muacheni ale kwenye malisho yaliyoko kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, na msimfanyie lolote la kumdhuru, mkifanya hivyo, mtapatwa na adhabu iumizayo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ جَعَلَكُمۡ خُلَفَآءَ مِنۢ بَعۡدِ عَادٖ وَبَوَّأَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورٗا وَتَنۡحِتُونَ ٱلۡجِبَالَ بُيُوتٗاۖ فَٱذۡكُرُوٓاْ ءَالَآءَ ٱللَّهِ وَلَا تَعۡثَوۡاْ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُفۡسِدِينَ
Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, Alipowafanya nyinyi mnashika nafasi za waliokuwa kabla yenu katika ardhi, baada ya kabila la ‘Ād, Akawamakinisha nyinyi katika ardhi nzuri, mkaifanya makao, mkajenga kwenye mabonde yake majumba makubwa na mkayachonga majabali yake ili mfanye majumba mengine. Basi kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu na msizunguke katika ardhi kwa uharibifu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لِلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِمَنۡ ءَامَنَ مِنۡهُمۡ أَتَعۡلَمُونَ أَنَّ صَٰلِحٗا مُّرۡسَلٞ مِّن رَّبِّهِۦۚ قَالُوٓاْ إِنَّا بِمَآ أُرۡسِلَ بِهِۦ مُؤۡمِنُونَ
Wakasema mabwana na wakubwa wa wale waliokuwa wakijiona kuwa ni wakubwa, miongoni mwa watu wa Ṣāliḥ, kuwaambia wale waliokuwa wakiwafanya wanyonge na kuwadharau, «Kwani mnajua kwamba Ṣāliḥ ametumwa kwetu na Mwenyezi Mungu?» Wale walioamini walisema, «Sisi tunayaamini yale ambayo Mwenyezi Mungu Amemtuma nayo na tunaifuata sheria aliyokuja nayo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُوٓاْ إِنَّا بِٱلَّذِيٓ ءَامَنتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ
Wakasema wale waliojiona, «Sisi ni wenye kuyakanusha hayo mliyoyaamini nyinyi na kuyafuata kuhusu unabii wa Ṣāliḥ.”
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَعَقَرُواْ ٱلنَّاقَةَ وَعَتَوۡاْ عَنۡ أَمۡرِ رَبِّهِمۡ وَقَالُواْ يَٰصَٰلِحُ ٱئۡتِنَا بِمَا تَعِدُنَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Wakamchinja ngamia kwa kutojali onyo la Ṣāliḥ, na wakaingiwa na kiburi kilichowafanya wasifuate amri ya Mola wao na wakasema, kwa njia ya shere na kwa kuona kuwa adhabu iko mbali na wao, «Ewe Ṣāliḥ, tuletee hiyo adhabu ambayo unatuonya nayo, iwapo wewe ni miongoni mwa Mitume wa Mwenyezi Mungu!»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Basi wale waliokufuru walishikwa na tetemeko kali ambalo lilizitoa nyoyo zao, wakawa wameangamia katika mji wao, wamegandama na ardhi kwa magoti yao na nyuso zao, hakuna yoyote kati yao aliyeponyoka.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَالَةَ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُحِبُّونَ ٱلنَّٰصِحِينَ
Ṣāliḥ, amani imshukie, alijiepusha na watu wake, walipomchinja ngamia, na maangamivu yakawa ni yenye kuwashukia, na akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu! Nimewafikishia yale Mola wangu Aliyoniamuru niwafikishie, kuhusu maamrisho Yake na makatazo Yake, na nimewafanyia bidii kiasi nilichoweza katika kuwavutia kwenye kheri na kuwakemea shari na kuwa muaminifu, lakini nyinyi hamuwapendi waaminifu kwenu, ndipo mkayakataa maneno yao na mkamtii kila shetani aliyelaaniwa.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلُوطًا إِذۡ قَالَ لِقَوۡمِهِۦٓ أَتَأۡتُونَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنۡ أَحَدٖ مِّنَ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na mkumbuke, ewe Mtume, Lūṭ, amani imshukie, pindi aliposema kuwaambia watu wake, «Je, mnafanya kitendo kibaya kilichofikia upeo wa ubaya? Hakuna yoyote, miongoni mwa viumbe, aliyefanya kitendo hiko kabla yenu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّكُمۡ لَتَأۡتُونَ ٱلرِّجَالَ شَهۡوَةٗ مِّن دُونِ ٱلنِّسَآءِۚ بَلۡ أَنتُمۡ قَوۡمٞ مُّسۡرِفُونَ
Nyinyi mnawaendea wanaume kwenye sehemu zao za nyuma, hali ya kuingiwa na matamanio ya kufanya hivyo, bila kujali uovu wake, huku mkiacha kile alichowahalalishia Mwenyezi Mungu kwa wake zenu. Bali nyinyi ni watu mliopita kiasi katika kukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Hakika kuwaendea wanaume badala ya wanawake ni miongoni mwa machafu ambayo yalianzishwa na kaumu ya Lūṭ, na hawakutanguliwa na yoyote katika viumbe.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوۡمِهِۦٓ إِلَّآ أَن قَالُوٓاْ أَخۡرِجُوهُم مِّن قَرۡيَتِكُمۡۖ إِنَّهُمۡ أُنَاسٞ يَتَطَهَّرُونَ
Hayakuwa majibu ya watu wa Lūṭ, alipowapinga kwa kitendo chao kilichofikia upeo wa ubaya, isipokuwa ni kuambiana wao kwa wao, «Mtoeni Lūṭ na wafuasi wake nchini mwenu, kwa kuwa yeye na wanaomfuata ni watu wanaojiepusha na kuwajia wanaume kwenye sehemu zao za nyuma.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَنجَيۡنَٰهُ وَأَهۡلَهُۥٓ إِلَّا ٱمۡرَأَتَهُۥ كَانَتۡ مِنَ ٱلۡغَٰبِرِينَ
Basi Mwenyezi Mungu Akamuokoa Lūṭ, na wafuasi wake na adhabu, Alimuamuru auhame mji ule, isipokuwa mke wake, kwani yeye alikuwa ni miongoni mwa walioangamia, waliosalia ndani ya adhabu ya Mwenyezi Mungu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِم مَّطَرٗاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Na Mwenyezi Mungu Akawaadhibu makafiri wa kaumu ya Lūṭ, kwa kuwateremshia wao mvua ya mawe, Akaigeuza nchi yao Akaifanya juu ni chini na chini ni juu. Tazama ulivyokuwa mwisho wa wale waliojasiri kufanya matendo ya kumuasi Mwenyezi Mungu na wakawakanusha Mitume Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ فَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَاۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ
Hakika tulimtuma, kwa watu wa kabila linalokaa Madyan, ndugu yao Shu'ayb, amani imshukie, akasema kuwaambia, «Enyi wtu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Hamna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Mtakasieni ibada.Hakika imewajia nyinyi hoja, kutoka kwa Mola wenu, juu ya ukweli wa yale ninayowaitia. Watekelezeeni watu haki zao kwa kutimiza vipimo na mizani. Na msiwapunguzie haki zao mkawadhulumu. Wala msifanye uharibifu katika ardhi, kwa ukafiri na kudhulumu, baada ya kuwa imetengenezwa kwa sheria za Mitume waliopita, amani iwashukie. Hayo niliyowaitia nyinyi ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu, iwapo nyinyi ni wenye kuniamini katika yale ninayowaitia, ni wenye kuzifuata sheria za Mwenyezi Mungu kivitendo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَا تَقۡعُدُواْ بِكُلِّ صِرَٰطٖ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ مَنۡ ءَامَنَ بِهِۦ وَتَبۡغُونَهَا عِوَجٗاۚ وَٱذۡكُرُوٓاْ إِذۡ كُنتُمۡ قَلِيلٗا فَكَثَّرَكُمۡۖ وَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
«Na wala msikae katika kila njia mkiwatisha watu kwa kuwaua wakitowapa mali yao, mkimzuia aliyemuamini Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, na akatenda mema asifuate njia iliyonyoka, na mkataka njia ya Mwenyezi Mungu iwe kombo, na mnaipotoa mkifuata matamanio yenu, na mnawafukuza watu wasiifuate. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, juu yenu ilipokuwa idadi yenu ni chache Mwenyezi Mungu akawafanya muwe wengi mkawa mna nguvu, wenye enzi. Na angalieni, ulikuwa vipi mwisho wa wale waharibifu katika ardhi na ni yapi yaliyowashukia ya maangamivu na kuvunjikiwa?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِن كَانَ طَآئِفَةٞ مِّنكُمۡ ءَامَنُواْ بِٱلَّذِيٓ أُرۡسِلۡتُ بِهِۦ وَطَآئِفَةٞ لَّمۡ يُؤۡمِنُواْ فَٱصۡبِرُواْ حَتَّىٰ يَحۡكُمَ ٱللَّهُ بَيۡنَنَاۚ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ
Na iwapo kundi miongoni mwenu waliyakubali yale Aliyonituma nayo Mwenyezi Mungu na kundi la watu wengine wasiyakubali hayo, basi ngojeni, enyi wakanushaji wa hukumu ya Mwenyezi Mungu inayotoa uamuzi baina yetu na nyinyi, itakapowashukia adhabu Yake ambayo aliwaonya nayo. Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka na kuwa juu, ni bora wa wenye kuhukumu baina ya waja Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ قَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَنُخۡرِجَنَّكَ يَٰشُعَيۡبُ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَكَ مِن قَرۡيَتِنَآ أَوۡ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۚ قَالَ أَوَلَوۡ كُنَّا كَٰرِهِينَ
Walisema watukufu na wakubwa wa watu wa Shu'ayb waliokataa, kwa kiburi, kumuamini Mwenyezi Mungu na kumfuata Mtume Wake Shu'ayb, amani imshukiye, «Tutakutoa, ewe Shu'ayb, wewe na walio pamoja na wewe kutoka kwenye miji yetu, isipokuwa ukiwa utarudi kwenye dini yetu.» Shu'ayb akasema akilipinga na kulionea ajabu neno lao, «Je, tuwafuate nyinyi kwenye dini yenu na mila yenu ya batili hata kama sisi tunaichukia kwa kujua kwetu ubatili wake?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَدِ ٱفۡتَرَيۡنَا عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا إِنۡ عُدۡنَا فِي مِلَّتِكُم بَعۡدَ إِذۡ نَجَّىٰنَا ٱللَّهُ مِنۡهَاۚ وَمَا يَكُونُ لَنَآ أَن نَّعُودَ فِيهَآ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ رَبُّنَاۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمًاۚ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَاۚ رَبَّنَا ٱفۡتَحۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَ قَوۡمِنَا بِٱلۡحَقِّ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡفَٰتِحِينَ
Akasema Shu'ayb kuwaambia watu wake, kwa kuongezea, «Tutakuwa tumemzulia Mwenyezi Mungu urongo tukirudi kwenye dini yenu baada ya Mwenyezi Mungu kutuokoa nayo. Haiwezekani kwetu kugeuka kuifuata dini isiyokuwa ya Mola wetu, isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu, Mola wetu, Ametaka. Hakika Mola wetu Amekienea kila kitu kwa ujuzi, kwa hivyo Anakijua kinachowafaa waja. Ni kwa Mwenyezi Mungu, Peke Yake, mategemeo yetu ya kupata uongofu na ushindi. Ewe Mola wetu, toa uamuzi wa haki kati yetu na watu wetu, na wewe ndiye bora wa wenye kutoa uamuzi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِن قَوۡمِهِۦ لَئِنِ ٱتَّبَعۡتُمۡ شُعَيۡبًا إِنَّكُمۡ إِذٗا لَّخَٰسِرُونَ
Wakasema watukufu na wakubwa wenye kukanusha, wenye kupinga ulinganizi wa Tawhīd (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) waliofikia kiwango cha juu katika ujeuri na uasi, wakitahadharisha kwamba Shu'ayb asifuatwe, «Kwa hakika, lau mnamfuata Shu'ayb, nyinyi kwa hivyo ni wenye kuangamia.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دَارِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Hapo watu wa Shu'ayb wakashikwa na mtetemeko mkali, wakawa wameangushwa kwenye mji wao hali ya kuwa wamekufa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَاۚ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ شُعَيۡبٗا كَانُواْ هُمُ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Wale ambao walimkanusha Shu'ayb walikuwa kama kwamba hawakukaa kwenye nyumba zao wala hawakustarehe humo. Kwani walimalizwa, isibaki alama yoyote yao, wakapatikana na hasara na maangamivu duniani na Akhera.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَتَوَلَّىٰ عَنۡهُمۡ وَقَالَ يَٰقَوۡمِ لَقَدۡ أَبۡلَغۡتُكُمۡ رِسَٰلَٰتِ رَبِّي وَنَصَحۡتُ لَكُمۡۖ فَكَيۡفَ ءَاسَىٰ عَلَىٰ قَوۡمٖ كَٰفِرِينَ
Shu'ayb alijiepusha na wao, alipokuwa na yakini kwamba adhabu ya Mwenyezi Mungu ni yenye kuwashukia, na akasema, «Enyi watu wangu, ‘Nimewafikishia ujumbe wa Mola wangu na nimewashauri muingie kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu na muache hayo mliyonayo; hamkusikia wala hamkutii. Vipi mimi niwasikitikie watu walioukataa upweke wa Mwenyezi Mungu na wakawakanusha Mitume Wake?’»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّآ أَخَذۡنَآ أَهۡلَهَا بِٱلۡبَأۡسَآءِ وَٱلضَّرَّآءِ لَعَلَّهُمۡ يَضَّرَّعُونَ
Na hatukumtuma Nabii kwenye kijiji chochote kuwalingania watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu na kuwakataza ushirikina ambao wanao, kisha wakamkanusha, isipokuwa tuliwapa mtihani wa shida na mikasa, tukawatia kwenye miili yao magonjwa na ndwele, na katika mali yao ufukara na uhitaji, kwa matumaini kwamba wanyenyekee, waelekee kwa Mwenyezi mungu na warudi kwenye haki.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ثُمَّ بَدَّلۡنَا مَكَانَ ٱلسَّيِّئَةِ ٱلۡحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَواْ وَّقَالُواْ قَدۡ مَسَّ ءَابَآءَنَا ٱلضَّرَّآءُ وَٱلسَّرَّآءُ فَأَخَذۡنَٰهُم بَغۡتَةٗ وَهُمۡ لَا يَشۡعُرُونَ
Kisha tukaigeuza hali nzuri ya mwanzo mahali pa hali mbaya, wakawa wana afya katika miili yao, na ukunjufu na neema katika mali zao, ili kuwapa muhula, kwani wakashukuru. Hayo yote hayakuwa na faida kwao, na hawakuzingatia wala hawakukomeka na ushirikina waliokuwa nao na wakasema, «Hii ndiyo hali ya ulimwengu kwa watu wake, kuna siku njema na siku mbaya; na hayo ndiyo yaliyowapitia baba zetu hapo nyuma.» Basi, punde si punde, tuliwashika kwa adhabu wakiwa wametulia, hawakuwa wakifikiria kuwa wataangamizwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَوۡ أَنَّ أَهۡلَ ٱلۡقُرَىٰٓ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَفَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَرَكَٰتٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِن كَذَّبُواْ فَأَخَذۡنَٰهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Na lau watu wa miji waliwaamini Mitume wao wakawafuata na kujiepusha na aliyoyakataza Mwenyezi Mungu, Angaliwafungulia Mwenyezi Mungu milango ya heri kwa kila njia. Lakini wao walikanusha, Mwenyezi Mungu Akawatesa kwa adhabu yenye kuangamiza kwa sababu ya ukafiri wao na maasia yao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَفَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا بَيَٰتٗا وَهُمۡ نَآئِمُونَ
Kwani wanadhani hawa watu wa mijini kuwa wao wameokoka na wamesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu kuwa haitawafika kipindi cha usiku wakiwa wamelala?
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا ضُحٗى وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ
Au kwani wanajiaminisha watu wa mijini kuwa wamesalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu kuwa haitawafika kipindi cha mchana wakiwa wameghafilika, wameshughulika na mambo ya dunia yao? Mwenyezi Mungu Amezihusu nyakati mbili hizi kwa kuzitaja, kwa kuwa mwanadamu nyakati hizi huwa wameghafilika zaidi, kwa hivyo kuja adhabu katika nyakati hizi huwa na kitisho zaidi na ni kali zaidi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَفَأَمِنُواْ مَكۡرَ ٱللَّهِۚ فَلَا يَأۡمَنُ مَكۡرَ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Je, wamejiaminisha, watu wa miji iliyokanusha, na vitimbi vya Mwenyezi Mungu kwao na kuwapa Kwake wao muhula, kwa kuwaachilia na yale Aliyowaneemesha nayo katika dunia yao, kwa njia ya kuwatesa sababu ya vitimbi vyao? Basi hawajiaminishi na vitimbi vya Mwenyezi Mungu isipokuwa watu wenye kuangamia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ
Kwani haikuwafunukia wale waliokaa kwenye nchi baada ya watu wake waliopita kuangamizwa kwa maasia yao, na wakafuata miendo yao, kwamba lau tunataka tungaliwaadhibu kwa makosa yao, kama tulivyowafanyia waliopita kabla yao, na kwamba tutazipiga chapa nyoyo zao, haki isiingie na wasisikie mawaidha wala makumbusho?
Tefsiri na arapskom jeziku:
تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Miji hiyo iliyotangulia kutajwa, nayo ni miji ya watu wa Nūḥ„ Hūd, Ṣāliḥ, Lūṭ, na Shu'ayb, tunakupatia, ewe Mtume, habari zake na zile zinazohusu mambo ya Mitume wa Mwenyezi Mungu waliotumwa kwa watu wa miji hiyo, zinazofanya mazingatio yapatikane kwa wenye kuzingatia na pia makemeo kwa madhalimu. Hakika watu wa miji hiyo walijiwa na Mitume wetu na hoja zilizo wazi juu ya ukweli wao, lakini hawakuwa ni wenye kuyaamini yale waliyokuja nayo hao Mitume kwao kwa sababu ya kupita mipaka kwao na kuikanusha haki. Na mfano Alivyopiga chapa Mwenyezi Mungu kwenye nyoyo za makafiri hawa waliotajwa, Atapiga mhuri kwenye nyoyo za wenye kumkanusha Muhammad (S.A.W.).
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَا وَجَدۡنَا لِأَكۡثَرِهِم مِّنۡ عَهۡدٖۖ وَإِن وَجَدۡنَآ أَكۡثَرَهُمۡ لَفَٰسِقِينَ
Na hatukuwapata wengi wa watu waliopita kuwa wana uaminifu wala utekelezaji ahadi, na hatukuwapata wengi wao isipokuwa ni watokaji nje ya utiifu wa Mwenyezi Mungu na ufuataji amri Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Kisha tulimtuma, baada ya Mitume waliotangulia kutajwa, Mūsā mwana wa 'Imrān kwa miujiza yetu iliyo wazi aende kwa Fir'awn na watu wake, wakaikataa na kuikanusha kwa udhalimu na upinzani. Tazama kwa mazingatio, namna gani tuliwafanya na tuliwazamisha hadi wa mwisho wao, huku Mūsā na watu wake wakiona? Na huo ndio mwisho wa waharibifu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na Mūsā alisema kumwambia Fir'awn akimzungumzia na akimfikishia ujumbe, «Mimi ni mjumbe kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Muumba viumbe wote na Mwenye kupanga hali zao na marejeo yao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
حَقِيقٌ عَلَىٰٓ أَن لَّآ أَقُولَ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ قَدۡ جِئۡتُكُم بِبَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَرۡسِلۡ مَعِيَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ
«Nastahili nisiseme kuhusu Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na inapasa kwangu nijilazimishe nayo. Nimewajia na dalili na hoja zenye ushindi kutoka kwa Mola wenu juu ya ukweli wa yale ninayowatajia. Basi waachilie, ewe Fir'awn, Wana wa Isrāīl pamoja na mimi kutoka kwenye kifungo chako na ukandamizaji wako, na wape uhuru wa kumuabudu Mwenyezi Mungu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ إِن كُنتَ جِئۡتَ بِـَٔايَةٖ فَأۡتِ بِهَآ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Fir'awn alisema kumwambia Mūsā, «Ukiwa umekuja na alama, kama unavyodai, basi niletee na uihudhurishe mbele yangu, ili madai yako yawe ya sawa na ukweli wako uthibiti, iwapo wewe ni mkweli katika madai yako kuwa wewe ni mjumbe wa Mola wa viumbe.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ
Hapo Mūsā aliitupa fimbo yake na ikageuka nyoka mkubwa anayeonekana waziwazi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ
Na akauvuta mkono wake kutoka kwenye uwazi wa kanzu iliyofunguliwa kifuani au chini ya kapwa lake, na papo hapo ukawa mweupe kama maziwa usio na mbalanga, ukiwa ni alama kwa Fir'awn; akiurejesha unarudi rangi yake ya mwanzo, kama ulivyo mwili wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
Watukufu wa watu wa Fir'awn walisema, «Hakika Mūsā ni mchawi, anayatawala macho ya watu kwa kuwadanganya mpaka ikawaingia kwenye fikira zao kuwa fimbo ni nyoka, na kukiona kitu kinyume na vile kilivyo, na yeye ana ujuzi mwingi wa uchawi na ana uhodari nao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُمۡۖ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ
«Yuwataka kuwatoa nyinyi nyote kwenye nchi yenu.» Fir'awn akasema, «Mnanipa shauri gani, enyi watu watukufu, juu ya mambo ya Mūsā?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَأَرۡسِلۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ
Wakasema waliohudhuria mjadala wa Mūsā miongoni mwa mabwana wa watu wa Fir’awn na wakubwa wao, «Mfanye Mūsā na Hārūn wangojee, na upeleke askari kwenye miji ya Misri na majimbo yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَٰحِرٍ عَلِيمٖ
«Ili wakukusanyie kila mchawi mwenye ujuzi mwingi wa uchawi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَجَآءَ ٱلسَّحَرَةُ فِرۡعَوۡنَ قَالُوٓاْ إِنَّ لَنَا لَأَجۡرًا إِن كُنَّا نَحۡنُ ٱلۡغَٰلِبِينَ
Wachawi wakamjia Fir'awn wakasema, «Je, tutakuwa na zawadi na mali tukimshinda Mūsā?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ نَعَمۡ وَإِنَّكُمۡ لَمِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Fir'awn akasema, «Ndio, mtakuwa na malipo na ukaribu na mimi mkimshinda.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ نَحۡنُ ٱلۡمُلۡقِينَ
Wakasema wachawi wa Fir'awn kumwambia Mūsā, kwa njia ya kujiona na kutojali. «Ewe Mūsā, chaguwa uwe ni wa mwanzo kutupa fimbo yako au tuwe sisi ni wa mwanzo kutupa.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ أَلۡقُواْۖ فَلَمَّآ أَلۡقَوۡاْ سَحَرُوٓاْ أَعۡيُنَ ٱلنَّاسِ وَٱسۡتَرۡهَبُوهُمۡ وَجَآءُو بِسِحۡرٍ عَظِيمٖ
Akasema Mūsā kuwaambia wachawi, «Tupeni nyinyi.» Walipotupa kamba na fimbo, waliyaroga macho ya watu yakaona kwamba yale waliyoyafanya ni ya kweli, na hali yalikuwa ni kiinimacho na vitu vya kudhania, na waliwatisha watu vitisho vikali na walikuja na uchawi wa nguvu ulio mwingi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَلۡقِ عَصَاكَۖ فَإِذَا هِيَ تَلۡقَفُ مَا يَأۡفِكُونَ
Hapo Mwenyezi Mungu Alimletea wahyi mja Wake na Mtume Wake Mūsā, amani imshukiye, katika kisimamo hicho kikubwa ambacho hapo Mwenyezi Mungu Alipambanua baina ya ukweli na urongo, akimuamuru akitupe kilichoko kwenye mkono wake wa kulia, nacho ni fimbo yake. Akaitupa na papo hapo ikawa inavimeza vile wanavyovitupa na kuwafanya watu wadhanie kuwa ni vya kweli na ilhali ni vya urongo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَوَقَعَ ٱلۡحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hapo haki ikajitokeza na ikafunuka kwa aliyehudhuria na kuiona kuhusu mambo ya Mūsā, amani imshukie, na kuwa yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, analingania haki, na ukabatilika urongo waliokuwa wakiufanya.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَغُلِبُواْ هُنَالِكَ وَٱنقَلَبُواْ صَٰغِرِينَ
Wakashindwa wachawi wote katika mahala walipokusanyika, na akaondoka Fir'awn na watu wake wakiwa wanyonge, waliozidiwa nguvu na kushindwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سَٰجِدِينَ
Wakapomoka wachawi kwa nyuso zao kwa kumsujudia Mola wa viumbe wote, kwa uwezo mkubwa wa Mwenyezi Mungu waliouona.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wakasema, «Tumemamini Mola wa viumbe wote.
Tefsiri na arapskom jeziku:
رَبِّ مُوسَىٰ وَهَٰرُونَ
«Naye ni Mola wa Mūsā na Hārūn.» Naye ni Ambaye ni lazima ibada ielekezwe Kwake, Peke Yake, si kwa mwingine.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ فِرۡعَوۡنُ ءَامَنتُم بِهِۦ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّ هَٰذَا لَمَكۡرٞ مَّكَرۡتُمُوهُ فِي ٱلۡمَدِينَةِ لِتُخۡرِجُواْ مِنۡهَآ أَهۡلَهَاۖ فَسَوۡفَ تَعۡلَمُونَ
Fir'awn akasema kuwaambia wachawi, «Mumemuamini Mwenyezi Mungu kabla sijawapa idhini mumuamini? Hakika kumuamini kwenu Mwenyezi Mungu, kumsadiki kwenu Mūsā na kuukubali kwenu unabii wake ni hila mlizozipanga nyinyi na Mūsā ili muwatoe watu wa mji wenu kutoka humo, na ili muzivamie heri zake na mufaidike nazo peke yenu.Basi mtajua, enyi wachawi, adhabu na mateso yatakayowashukia nyinyi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
لَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ ثُمَّ لَأُصَلِّبَنَّكُمۡ أَجۡمَعِينَ
«Nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu, enyi wachawi, kwa kupishana: kwa kuukata mkono wa kulia na mguu wa kushoto au mkono wa kushoto na mguu wa kulia, kisha nitawatungika nyinyi nyote juu ya vigogo vya mitende kwa njia ya kuwatesa na ili kuwafanya watu watishike.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُوٓاْ إِنَّآ إِلَىٰ رَبِّنَا مُنقَلِبُونَ
Walisema wachawi kumwambia Fir'awn, «Tuna uhakika kwamba sisi ni wenye kurejea kwa Mwenyezi mungu na kwamba adhabu Yake ni kali zaidi kushinda adhabu yako. Tutasuburi kikwelikweli leo kwa adhabu yako, tupate kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَا تَنقِمُ مِنَّآ إِلَّآ أَنۡ ءَامَنَّا بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا لَمَّا جَآءَتۡنَاۚ رَبَّنَآ أَفۡرِغۡ عَلَيۡنَا صَبۡرٗا وَتَوَفَّنَا مُسۡلِمِينَ
«Na wewe hukutupata na jambo lolote la kutuaibisha na kutupinga kwalo, ewe Fir'awn, isipokuwa ni kule kuamini kwetu na kukubali kwetu hoja za Mola wetu na dalili Zake alizokuja nazo Mūsā ambazo wewe huwezi kuleta mfano wake wala yoyote mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu Ambaye ni Yake mamlaka ya mbingu na ardhi. Mola wetu! Tumiminie subira kubwa na uthabiti juu yake, na utufishe tukiwa ni wenye kwndama amri yako, wenye kumfuata Mtume wako.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَالَ ٱلۡمَلَأُ مِن قَوۡمِ فِرۡعَوۡنَ أَتَذَرُ مُوسَىٰ وَقَوۡمَهُۥ لِيُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَيَذَرَكَ وَءَالِهَتَكَۚ قَالَ سَنُقَتِّلُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَنَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡ وَإِنَّا فَوۡقَهُمۡ قَٰهِرُونَ
Watukufu na wakubwa miongoni mwa watu wa Fir'awn walisema kumwambia Fir'awn, «Unamuacha Mūsā na watu wake, Wana wa Isrāīl, wawaharibu watu katika nchi ya Misri kwa kuwageuzia dini yao na kuwaletea ibada ya Mwenyezi Mungu Peke Yake, Asiye na mshirika, na kuacha kukuabudu wewe na kuwaabudu waungu wako?» Fir'awn akasema,»Tutawaua watoto wa kiume wa Wana wa Isrāīl, na tutawaacha watoto wao wa kike waishi ili watumike; na sisi tuko juu yao kwa nguvu za ufalme na mamlaka.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱللَّهِ وَٱصۡبِرُوٓاْۖ إِنَّ ٱلۡأَرۡضَ لِلَّهِ يُورِثُهَا مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلۡمُتَّقِينَ
Akasema Mūsā kuwaambia watu wake, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, «Takeni msaada kwa Mwenyezi Mungu Awaokoe na Fir'awn na watu wake, na subirini juu ya shida zinazowapata nyinyi na watoto wenu kutoka kwa Fir 'awn. Kwani ardhi yote ni ya Mwenyezi Mungu Anamrithisha Anayemtaka miongoni mwa waja Wake. Na mwisho mwema ni wa anyemcha Mwenyezi Mungu akafanya maamrisho Yake na akajiepusha na makatazo Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالُوٓاْ أُوذِينَا مِن قَبۡلِ أَن تَأۡتِيَنَا وَمِنۢ بَعۡدِ مَا جِئۡتَنَاۚ قَالَ عَسَىٰ رَبُّكُمۡ أَن يُهۡلِكَ عَدُوَّكُمۡ وَيَسۡتَخۡلِفَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرَ كَيۡفَ تَعۡمَلُونَ
Walisema watu wa Mūsā, miongoni mwa Wana wa Isrāīl, kumwambia Nabii wao Mūsā, «Tulisumbuliwa na tukaudhiwa na nguvu za Fir'awn na watu wake, kwa kuuawa watoto wetu wa kiume na kuachiliwa wanawake wetu, kabla hujatujia na baada ya kutujia.» Mūsā akawaambia, «Huenda Mola wenu Akamuangamiza adui yenu, Fir'awn na watu wake, na Awaweke nyinyi katika ardhi yao badala yao, baada ya kuangamia kwao, Aangalie namna mtakavyofanya: mtashukuru au mtakufuru?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ أَخَذۡنَآ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ بِٱلسِّنِينَ وَنَقۡصٖ مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Hakika tulimpa Fir'awn na watu wake mtihani wa chaka na ukame na upungufu wa matunda yao na nafaka zao ili wakumbuke na wakome, waache upotevu wao na wakimbilie kwa Mola wao kwa kutubia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَإِذَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡحَسَنَةُ قَالُواْ لَنَا هَٰذِهِۦۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَطَّيَّرُواْ بِمُوسَىٰ وَمَن مَّعَهُۥٓۗ أَلَآ إِنَّمَا طَٰٓئِرُهُمۡ عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Ukiwajia Fir'awn na watu wake urutuba na chakula huwa wakisema, «Hii ni yetu tunayoistahiki.» Na ukiwapata wao ukame na chaka huwa wakiona wameingiliwa na ukorofi na huwa wakisema, «Haya ni kwa sababu ya Mūsā na walio pamoja na yeye.»Jua utanabahi kwamba yanayowapata ya ukame na chaka ni kwa uamuzi wa Mwenyezi Mungu na makadirio Yake, na ni kwa sababu ya madhambi yao na ukafiri wao. Lakini wengi wa watu wa Fir'awn hawalijui hilo, kwa kuvama kwao kwenye ujinga na upotevu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَالُواْ مَهۡمَا تَأۡتِنَا بِهِۦ مِنۡ ءَايَةٖ لِّتَسۡحَرَنَا بِهَا فَمَا نَحۡنُ لَكَ بِمُؤۡمِنِينَ
Watu wa Fir'awn wakasema kumwambia Mūsā, «Alama yoyote utakayotuletea, na dalili na hoja zozote utakazotusimamishia ili utuepushe na dini ya Fir'awn tuliyonayo, sisi si wenye kukuamini,»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلطُّوفَانَ وَٱلۡجَرَادَ وَٱلۡقُمَّلَ وَٱلضَّفَادِعَ وَٱلدَّمَ ءَايَٰتٖ مُّفَصَّلَٰتٖ فَٱسۡتَكۡبَرُواْ وَكَانُواْ قَوۡمٗا مُّجۡرِمِينَ
Tukawapelekea wao mafuriko yenye kumaliza yaliyozamisha makulima na matunda; tukapeleka nzige wakazila nafaka zao, matunda yao, milango yao, sakafu zao na nguo zao; na tukapeleka chawa wanaoharibu matunda na kumaliza wanyama na mimea; tukapeleka vyura wakajaa kwenye vyombo vyao na vyakula vyao na malazi yao; na pia tukapeleka damu, ikawa mito yao na visima vyao vimegeuka damu, wasipate maji safi ya kunywa. Hii ni miujiza kati ya miujiza ya Mwenyezi Mungu, hakuna aiwezae isipokuwa Yeye, baadhi yake imetengwa na mingine. Pamoja na haya yote, watu wa Fir'awn walijiona watukufu, wakafanya kiburi kwa kukataa kumuamini Mwenyezi Mungu, wakawa ni watu wanatenda mambo Anayoyakataza Mwenyezi Mungu ya maasia na uhalifu kwa, ujeuri na uasi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ
Na adhabu ilipomteremkia Fir'awn na watu wake, walimkimbilia Mūsā na wakasema, «Ewe Mūsā, tuombee Mola wako, kwa wahyi aliokuletea Mwenyezi Mungu kwamba adhabu huondolewa kwa kutubia. Na ukituondolea adhabu tuliyonayo, tutayaamini uliyokuja nayo, na tutayafuata uliyotuitia kwayo, na tutawaachilia, pamoja na wewe, Wana wa Isrāīl, hatutawazuia waende na wewe pale wanapotaka.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَمَّا كَشَفۡنَا عَنۡهُمُ ٱلرِّجۡزَ إِلَىٰٓ أَجَلٍ هُم بَٰلِغُوهُ إِذَا هُمۡ يَنكُثُونَ
Mwenyezi Mungu Alipowaondolea adhabu Aliyoiteremsha kwao, mpaka muda ambao hapana budi wataufikia na waadhibiwe, ambapo hapo hakutawanufaisha kule kupewa muhula kuliotangulia na kuondolewa kwao adhabu mpaka wakati wa kufika kwake, punde si punde wanarudi kuvunja ahadi waliyomuahidi Mola wao na Mūsā na wanaendelea na kudumu na ukafiri wao na upotevu wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ فَأَغۡرَقۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡيَمِّ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ
Basi tukawalipiza ulipokuja muda uliowekwa kwa wao kuangamizwa, kwa kuwashushia mateso yetu, nayo ni kuwazamisha baharini, kwa sababu ya kuikanusha kwao miujiza iliyodhihiri kwa Mūsā na wakawa wanaipuuza; na kupuuza huko ndio sababu ya kukanusha.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَوۡرَثۡنَا ٱلۡقَوۡمَ ٱلَّذِينَ كَانُواْ يُسۡتَضۡعَفُونَ مَشَٰرِقَ ٱلۡأَرۡضِ وَمَغَٰرِبَهَا ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَاۖ وَتَمَّتۡ كَلِمَتُ رَبِّكَ ٱلۡحُسۡنَىٰ عَلَىٰ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ بِمَا صَبَرُواْۖ وَدَمَّرۡنَا مَا كَانَ يَصۡنَعُ فِرۡعَوۡنُ وَقَوۡمُهُۥ وَمَا كَانُواْ يَعۡرِشُونَ
Tukawarithisha Wana wa Isrāīl, waliokuwa wakifanywa wanyonge, pande za mashariki na magharibi ya ardhi, nazo ni sehemu za miji ya Sham, tulizozitia baraka kwa kutoa mazao na matunda na mito. Na limetimia neno jema la Mola wako, ewe Muhammad, kwa Wana wa Isrāīl kwa kuwapa utulivu katika ardhi kwa sababu ya kuvumilia kwao makero ya Fir'awn na watu wake. Na tukayavunjavunja yale maamirisho na mashamba ambayo Fir'awn na watu wake walikuwa wakiyatengeneza, na majengo na majumba na mengineyo waliokuwa wakiyajenga.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَجَٰوَزۡنَا بِبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ٱلۡبَحۡرَ فَأَتَوۡاْ عَلَىٰ قَوۡمٖ يَعۡكُفُونَ عَلَىٰٓ أَصۡنَامٖ لَّهُمۡۚ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱجۡعَل لَّنَآ إِلَٰهٗا كَمَا لَهُمۡ ءَالِهَةٞۚ قَالَ إِنَّكُمۡ قَوۡمٞ تَجۡهَلُونَ
Na tuliwakatia Wana wa Isrāīl bahari, wakapita kwa watu waliokuwa wamekaa na kuendelea kuabudu masanamu wao. Wana wa Isrāīl wakasema, «Tufanyie, ewe Mūsā, sanamu tupate kumuabudu na kumfanya mungu kama hawa watu walivyo na masanamu wanaowaabudu.» Mūsā akawaambia, «Hakika yenu nyinyi,enyi watu, ni wajinga wa kujua utukufu wa Mwenyezi Mungu, na hamjui kwamba ibada haifai kufanyiwa yoyote isipokuwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mmoja, Mwenye kutendesha nguvu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ مُتَبَّرٞ مَّا هُمۡ فِيهِ وَبَٰطِلٞ مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hakika hawa wanaowakalia hawa masanamu, ushirikina waliomo ndani yake umeangamizwa, na ni yenye kuangamiza na ni ya urongo yale waliokuwa wakiyafanya ya kuwaabudu masanamu hao ambao hawawazuilii adhabu ya Mwenyezi Mungu ikiwashukia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَبۡغِيكُمۡ إِلَٰهٗا وَهُوَ فَضَّلَكُمۡ عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Mūsā akasema kuwaambia watu wake, «Je, niwatafutie muabudiwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyewaumba na Akawatukuza juu ya walimwengu wa zama zenu kwa wingi wa Mitume watokanao na nyinyi, kumuangamiza adui yenu na kwa miujiza Aiyowahusu nayo.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ يَسُومُونَكُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِ يُقَتِّلُونَ أَبۡنَآءَكُمۡ وَيَسۡتَحۡيُونَ نِسَآءَكُمۡۚ وَفِي ذَٰلِكُم بَلَآءٞ مِّن رَّبِّكُمۡ عَظِيمٞ
Na kumbukeni, enyi Wana wa Isrāīl, neema zetu kwenu tulipowaokoa na kifungo cha Fir'awn na jamaa zake na unyonge na utwevu mliokuwa nao, wa kuchinjwa watoto wenu wa kiume na kuwaacha wanawake wenu ili watumike na wadharauliwe. Na katika kupitia kwenu mateso mabaya zaidi na maovu zaidi kisha kuwaokoa ni mtihani utokao kwa Mwenyezi Mungu kwenu na neema kubwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَوَٰعَدۡنَا مُوسَىٰ ثَلَٰثِينَ لَيۡلَةٗ وَأَتۡمَمۡنَٰهَا بِعَشۡرٖ فَتَمَّ مِيقَٰتُ رَبِّهِۦٓ أَرۡبَعِينَ لَيۡلَةٗۚ وَقَالَ مُوسَىٰ لِأَخِيهِ هَٰرُونَ ٱخۡلُفۡنِي فِي قَوۡمِي وَأَصۡلِحۡ وَلَا تَتَّبِعۡ سَبِيلَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Mwenyezi Mungu, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Alimpa ahadi Mūsā ya kuzungumza na Mola wake masiku thelathini, kisha Akamuengezea muda wa masiku kumi baada yake, ukakamilika wakati ambao Mwenyezi Mungu Alimuwekea Mūsā wa kusema na Yeye kuwa masiku arubaini. Na Mūsā alisema kumwambia ndugu yake Hārūn, alipotaka kwenda kuzungumza na Mola wake, «Kuwa ni badala yangu kwa watu wangu mpaka nitakaporudi, na uwahimize wamtii Mwenyezi Mungu na wamuabudu, na usifuate njia ya wale ambao wanaleta uharibifu katika ardhi.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَمَّا جَآءَ مُوسَىٰ لِمِيقَٰتِنَا وَكَلَّمَهُۥ رَبُّهُۥ قَالَ رَبِّ أَرِنِيٓ أَنظُرۡ إِلَيۡكَۚ قَالَ لَن تَرَىٰنِي وَلَٰكِنِ ٱنظُرۡ إِلَى ٱلۡجَبَلِ فَإِنِ ٱسۡتَقَرَّ مَكَانَهُۥ فَسَوۡفَ تَرَىٰنِيۚ فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُۥ لِلۡجَبَلِ جَعَلَهُۥ دَكّٗا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقٗاۚ فَلَمَّآ أَفَاقَ قَالَ سُبۡحَٰنَكَ تُبۡتُ إِلَيۡكَ وَأَنَا۠ أَوَّلُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na alipokuja Mūsā kwa wakati uliowekwa nao ni muda wa masiku arubaini na Akasema na yeye Mola wake kwa kumpa wahyi wake, maamrisho Yake na makatazo Yake, alifanya hamu ya kumuona Mwenyezi Mungu akataka amtazame. Mwenyezi Mungu Akamwambia, «Hutoniona!»Yaani hutaweza kuniona ulimwenguni. «Lakini liangalie jabali, likitulia mahali lilipo nitakapolitokezea, basi utaniona.» Alipojitokeza Mola wake kwa lile jabali alilifanya lipondeke liwe sawa na ardhi. Hapo Mūsā alianguka akiwa amezimia. Alipopata fahamu kutoka kwenye hali ya kuzimia alisema, «Kwa kukutakasisha, ewe Mola wangu, na kila sifa isiyolingana na utukufu wako, mimi natubia kwako kutokana na kuomba kwangu kukuona katika uhai huu wa kilimwengu, na mimi ni wa mwanzo wa wenye kukuamini miongoni mwa watu wangu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ يَٰمُوسَىٰٓ إِنِّي ٱصۡطَفَيۡتُكَ عَلَى ٱلنَّاسِ بِرِسَٰلَٰتِي وَبِكَلَٰمِي فَخُذۡ مَآ ءَاتَيۡتُكَ وَكُن مِّنَ ٱلشَّٰكِرِينَ
Mwenyezi Mungu Akasema, «Ewe Mūsā, Mimi nimekuchagua kati ya watu kwa ujumbe wangu kwa viumbe wangu niliokutuma kwao na kwa kusema kwangu na wewe pasi na mtu wa kati. Basi chukua niliyokupa kati ya maamrisho yangu na makatazo yangu, ushikamane nayo na uyatumie na uwe ni miongoni mwa wenye kumshukuru Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa utume aliokupa na Akakuhusu kwa maneno Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَكَتَبۡنَا لَهُۥ فِي ٱلۡأَلۡوَاحِ مِن كُلِّ شَيۡءٖ مَّوۡعِظَةٗ وَتَفۡصِيلٗا لِّكُلِّ شَيۡءٖ فَخُذۡهَا بِقُوَّةٖ وَأۡمُرۡ قَوۡمَكَ يَأۡخُذُواْ بِأَحۡسَنِهَاۚ سَأُوْرِيكُمۡ دَارَ ٱلۡفَٰسِقِينَ
Na tulimuandikia Mūsā katika Taurati mawaidha ya kila anachokihitajia katika hukumu za Dini yake, ili yapatikane makemeo na mazingatio, na maelezo yanayofafanua mambo ambayo walikalifishwa nayo ya halali na ya haramu, maamrisho na makatazo, visa, mambo ya itikadi, habari na mambo yasiyoonekana. Mwenyezi Mungu Alimwambia, «Basi yashike kwa nguvu.» Yaani, ishike Taurati kwa kwa bidii na hima. «Na uwaamrishe watu wako wazitumie sheria za Mwenyezi Mungu zilizomo humo. Hakika mwenye kushirikisha miongoni mwao na wengineo, mimi nitamuonesha huko Akhera nyumba ya waasi, nayo ni Moto wa Mwenyezi Mungu ambao Ameutayarisha kwa maadui Wake waliyotoka nje ya utiifu Wake.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
سَأَصۡرِفُ عَنۡ ءَايَٰتِيَ ٱلَّذِينَ يَتَكَبَّرُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَإِن يَرَوۡاْ كُلَّ ءَايَةٖ لَّا يُؤۡمِنُواْ بِهَا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلرُّشۡدِ لَا يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗا وَإِن يَرَوۡاْ سَبِيلَ ٱلۡغَيِّ يَتَّخِذُوهُ سَبِيلٗاۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَكَانُواْ عَنۡهَا غَٰفِلِينَ
Nitazipotoa nyoyo za wenye kufanya kiburi wakaacha kunitii na wenye kuwafanyia watu kiburi pasi na haki zisizielewe hoja na dalili zinazoonesha ukubwa wangu, sheria yangu na hukumu zangu, wawe hawamsikilizi Mtume yoyote kwa kiburi chao. Na wakiona, hawa wenye kuifanyia Imani kiburi, kila alama hawaiyamini, kwa sababu ya kupa mgongo kwao na kupingana kwao na Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Wakiiyona njia ya uongofu hawaifanyi ni njia, na wakiiyona njia ya upotevu wanaifanya kuwa ni njia na ni dini. Hayo ni kwa sababu ya kukanusha kwao aya za Mwenyezi Mungu na kughafilika kwao kuziangalia na kuyatia akilini maana yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَلِقَآءِ ٱلۡأٓخِرَةِ حَبِطَتۡ أَعۡمَٰلُهُمۡۚ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na wale ambao walizikanusha aya za Mwenyezi Mungu, hoja Zake na kukutana na Mwenyezi Mungu huko Akhera, matendo yao mema yatapomoka kwa sababu ya kukosekana sharti yake, nayo ni kumuamini Mwenyezi Mungu na kukubali kwamba malipo Yake ni kweli. Hawatalipwa huko Akhera isipokuwa malipo ya yale ambayo walikuwa wakiyafanya ulimwenguni ya ukafiri na maasia, nayo ni kukaa milele Motoni.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱتَّخَذَ قَوۡمُ مُوسَىٰ مِنۢ بَعۡدِهِۦ مِنۡ حُلِيِّهِمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٌۚ أَلَمۡ يَرَوۡاْ أَنَّهُۥ لَا يُكَلِّمُهُمۡ وَلَا يَهۡدِيهِمۡ سَبِيلًاۘ ٱتَّخَذُوهُ وَكَانُواْ ظَٰلِمِينَ
Na walitengeneza watu wa Mūsā, baada ya yeye kuwaacha kwenda kuzungumza na Mola Wake, sanamu wa kigombe asiye na roho anayetoa sauti, kutokana na dhahabu yao, wakamfanya ni muabudiwa. Kwani hawajui kwamba yeye hasemi na wao na hawaongozi wao kwenye kheri yoyote? Walijasiri kufanya jambo hili ovu, wakawa ni wenye kujidhulumu nafsi zao, ni wenye kuweka kitu mahala pasipokuwa pake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَمَّا سُقِطَ فِيٓ أَيۡدِيهِمۡ وَرَأَوۡاْ أَنَّهُمۡ قَدۡ ضَلُّواْ قَالُواْ لَئِن لَّمۡ يَرۡحَمۡنَا رَبُّنَا وَيَغۡفِرۡ لَنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Na walipojuta wale walioabudu kigombe badala ya Mwenyezi Mungu pale aliporudi Mūsā kwao, na wakaona kwamba walipotea njia ya sawa, na waliondoka kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, walianza kuukubali uja na kuomba kufutiwa makosa yao wakasema, «Mola wetu Asipoturehemu kwa kukubali toba yetu, na kufinika kwayo madhambi yetu, tutakuwa ni wenye kuangamia ambao matendo yao mema yamepita bure.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَمَّا رَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗا قَالَ بِئۡسَمَا خَلَفۡتُمُونِي مِنۢ بَعۡدِيٓۖ أَعَجِلۡتُمۡ أَمۡرَ رَبِّكُمۡۖ وَأَلۡقَى ٱلۡأَلۡوَاحَ وَأَخَذَ بِرَأۡسِ أَخِيهِ يَجُرُّهُۥٓ إِلَيۡهِۚ قَالَ ٱبۡنَ أُمَّ إِنَّ ٱلۡقَوۡمَ ٱسۡتَضۡعَفُونِي وَكَادُواْ يَقۡتُلُونَنِي فَلَا تُشۡمِتۡ بِيَ ٱلۡأَعۡدَآءَ وَلَا تَجۡعَلۡنِي مَعَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Aliporejea Mūsā kwa watu wake akiwa na hasira na huzuni, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Alimpa habari kwamba watu wake wamepatikana na mtihani na kwamba Sāmirīy amewapoteza. Mūsā alisema, «Ni ubaya ulioje mlioufanya nyuma yangu baada ya mimi kuondoka! Je mumeitangulia amri ya Mola wenu?» Yaani, mulikufanyia haraka kuja kwangu kwenu, na hali ni jambo lililopangwa na Mwenyezi Mungu Aliyetukuka?. Mūsā alizitupa mbao za Taurati kwa kuwakasirikia watu wake walioabudu kigombe na kwa kumkasirikia ndugu yake Hārūn. Akakishika kichwa cha Hārūn na akakivuta upande wake. Hārūn alisema kwa kubembeleza, «Ewe mwana wa mamangu, ‘Hakika hawa watu walinidharau, waliniona ni mnyonge na walikaribia kuniua, kwa hivyo usiwafurahishe maadui kwa unayonifanya na usiniingize katika hasira zako ukanifanya ni pamoja na wale walioenda kinyume na amri yako na wakaabudu kigombe.’»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قَالَ رَبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِأَخِي وَأَدۡخِلۡنَا فِي رَحۡمَتِكَۖ وَأَنتَ أَرۡحَمُ ٱلرَّٰحِمِينَ
Mūsā Alisema, ulipomfunukia udhuru wa ndugu yake na kujua kuwa yeye hakufanya uzembe katika kusimama imara juu ya amri ya Mwenyezi Mungu, «Mola wangu nisamehe ghadhabu zangu na umsamehe ndugu yangu yaliyopita kati yake na Wana wa Isrāīl, na ututie ndani ya rehema yako kunjufu, kwani wewe una huruma na sisi zaidi kuliko kila mwenye huruma.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ ٱلۡعِجۡلَ سَيَنَالُهُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّهِمۡ وَذِلَّةٞ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُفۡتَرِينَ
Hakika wale waliomfanya kigombe ni mungu itawapata wao ghadhabu kali kutoka kwa mola wao na unyonge katika uhai wa kilimwengu, kwa sababu ya kumkanusha kwao Mola wao. Na kama tulivyofanyia hawa, tutawafanyia wazushi wenye kuleta uzushi katika Dini ya Mwenyezi Mungu; na kila mwenye uzushi katika Dini ni mnyonge.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ عَمِلُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ ثُمَّ تَابُواْ مِنۢ بَعۡدِهَا وَءَامَنُوٓاْ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعۡدِهَا لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na wale waliofanya maovu ya ukafiri na maasia kisha wakarejea, baada ya kuyafanya, kwenye Imani na matendo mema, hakika Mola wako baada ya toba ya kidhati ni Msamehefu mno wa vitendo vyao viovu si Mwenye kuwafedhehi kwavyo, ni Mwenye kuwarehemu wao na kila aliye mfano wao miongoni mwa wenye kutubia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَمَّا سَكَتَ عَن مُّوسَى ٱلۡغَضَبُ أَخَذَ ٱلۡأَلۡوَاحَۖ وَفِي نُسۡخَتِهَا هُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّلَّذِينَ هُمۡ لِرَبِّهِمۡ يَرۡهَبُونَ
Zilipotulia hasira za Mūsā alizichukua mbao baada ya kuwa alizitupa chini, na ndani yake mlikuwa na maelezo ya haki na rehema kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu na kuogopa mateso Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱخۡتَارَ مُوسَىٰ قَوۡمَهُۥ سَبۡعِينَ رَجُلٗا لِّمِيقَٰتِنَاۖ فَلَمَّآ أَخَذَتۡهُمُ ٱلرَّجۡفَةُ قَالَ رَبِّ لَوۡ شِئۡتَ أَهۡلَكۡتَهُم مِّن قَبۡلُ وَإِيَّٰيَۖ أَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلسُّفَهَآءُ مِنَّآۖ إِنۡ هِيَ إِلَّا فِتۡنَتُكَ تُضِلُّ بِهَا مَن تَشَآءُ وَتَهۡدِي مَن تَشَآءُۖ أَنتَ وَلِيُّنَا فَٱغۡفِرۡ لَنَا وَٱرۡحَمۡنَاۖ وَأَنتَ خَيۡرُ ٱلۡغَٰفِرِينَ
Na Mūsā alichagua miongoni mwa watu wake wanaume sabiini walio bora kati yao, akatoka na wao akaenda hadi Tū,r Sīnā’ kwa wakati na muda ambao Mwenyezi Mungu Alimuagizia akutane na Yeye pamoja nao ili watubie kwa yale yaliyokuwa kwa wahuni wa Wana wa Isrāīl ya kuabudu kigombe. Walipokuja mahala hapo walisema, «Hatutakuamini, ewe Mūsā mpaka tumuone Mwenyezi Mungu waziwazi, basi utakaposema na Yeye tuoneshe.» Papo hapo walishikwa na mtetemeko mkali wakafa. Akasimama Mūsā akimnyenyekea Mwenyezi Mungu na akasema, «Ewe Mola wangu, niwaambie nini Wana wa Isrāīl nikiwajia na hali wewe umewaangamiza wabora wao? Lau unataka ungaliwaangamiza wote kabla ya hali hii ya kuwa mimi niko na wao. Hilo lingalikuwa sahali zaidi kwangu. Unatuangamiza kwa yale waliyoyafanya wachache wa akili miongoni mwetu? Kitendo hiki ambacho watu wangu wamekifanya cha kuabudu kigombe, hakikuwa isipokuwa ni majaribu na mtihani, unampoteza kwayo unayemtaka miongoni mwa viumbe wako na unamuongoza kwayo unayemtaka kumuongoza. Ni wewe mtegemewa wetu na mwenye kutunusuru, tughufirie dhambi zetu na uturehemu kwa rehema zako; na wewe ndiye bora wa wenye kusamehe makosa na kusitiri dhambi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَٱكۡتُبۡ لَنَا فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗ وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِ إِنَّا هُدۡنَآ إِلَيۡكَۚ قَالَ عَذَابِيٓ أُصِيبُ بِهِۦ مَنۡ أَشَآءُۖ وَرَحۡمَتِي وَسِعَتۡ كُلَّ شَيۡءٖۚ فَسَأَكۡتُبُهَا لِلَّذِينَ يَتَّقُونَ وَيُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلَّذِينَ هُم بِـَٔايَٰتِنَا يُؤۡمِنُونَ
«Na utujaalie ni miongoni mwa wale uliowaandikia matendo mema ulimwenguni na Akhera. Sisi tumerejea kwako hali ya kutubia.» Mwenyezi Mungu Aliyetukuka Akasema kumwambia Mūsā, «Adhabu yangu nitampatiliza kwayo ninayemtaka miongoni mwa viumbe wangu, kama nilivyowapatiliza hawa niliowapatia katika watu wako, na rehema yangu imewaenea viumbe wangu wote, nitawaandikia wale wanaomcha Mwenyezi Mungu na kuogopa mateso Yake, wakazitekeleza faradhi Zake na wakayaepuka mambo ya kumuasi, na wale ambao wao wanaziamini dalili za tawhīd (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) na hoja zake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلرَّسُولَ ٱلنَّبِيَّ ٱلۡأُمِّيَّ ٱلَّذِي يَجِدُونَهُۥ مَكۡتُوبًا عِندَهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَٱلۡإِنجِيلِ يَأۡمُرُهُم بِٱلۡمَعۡرُوفِ وَيَنۡهَىٰهُمۡ عَنِ ٱلۡمُنكَرِ وَيُحِلُّ لَهُمُ ٱلطَّيِّبَٰتِ وَيُحَرِّمُ عَلَيۡهِمُ ٱلۡخَبَٰٓئِثَ وَيَضَعُ عَنۡهُمۡ إِصۡرَهُمۡ وَٱلۡأَغۡلَٰلَ ٱلَّتِي كَانَتۡ عَلَيۡهِمۡۚ فَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِهِۦ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَٱتَّبَعُواْ ٱلنُّورَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ مَعَهُۥٓ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُفۡلِحُونَ
Rehema hii nitawaandikia wale wanaomuogopa Mwenyezi Mungu na kujiepusha na mambo ya kumuasi, na wanaomfuata Mtume aliye Nabii, ambaye hasomi wala haandiki, naye ni Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, ambaye wanazipata sifa zake na mambo yake yaandikwa huko kwao katika Taurati na Injili; anawaamrisha kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtii na kila lijulikanalo kuwa ni lema, na anawakataza ushirikina na maasia na kila lijulikanalo kuwa ni baya, na anawahalalishia vizuri vya vyakula na vinywaji na kuoana, na anawaharamishla vichafu vya hivyo kama nyama ya nguruwe na vile ambavyo walikuwa wakijihalalishia miongoni mwa vyakula na vinywaji ambavyo aliviharamisha Mwenyezi Mungu, na anawaondolea wao mambo magumu waliokalifishwa nayo kama kukata mahali pa najisi nguoni, kuzichoma moto ngawira, ulazimu wa kisasi juu ya aliyeua kwa kukusudia au kwa kukosea. Basi wale ambao walimuamini Nabii asiyejua kuandika wala kusoma kilichoandikwa, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, na wakaukubali unabii wake, wakamheshimu, wakamtukuza na wakamuhami na wakaifuata Qur’ani aliyoteremshiwa, wakaufuata mwendo wake kivitendo, hao ni wenye kufaulu kwa kupata yale ambayo Mwenyezi Mungu Aliwaahidi waja wake Waumini.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Waambie, ewe Mtume, watu wote, «Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote, si kwa baadhi yenu bila ya wengine, Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Haifai kuelekezwa uungu na ibada isipokuwa Kwake, zilizotukuka sifa Zake, Mwenye uwezo wa kupatisha viumbe, kuwaondosha na kuwafufua. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na kubalini upweke Wake, na muaminini Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, Nabii asiyesoma wala kwandika, anayemuamini Mwenyezi Mungu na yale aliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wake na yale waliyoteremshiwa manabii kabla yake; Mfuateni Mtume huyu na jilazimisheni kuyafanya anayowaamrisha kwayo ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kutaraji muafikiwe kufuata njia iliyolingana sawa.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمِن قَوۡمِ مُوسَىٰٓ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ
Na miongoni mwa Wana wa Isrāīl wanaotokana na jamaa za Mūsā kuna kundi la watu ambao wanasimama imara juu ya haki, wanawaongoza watu kwenye hiyo haki na wanafanya usawa katika kutoa uamuzi katika mambo yao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَطَّعۡنَٰهُمُ ٱثۡنَتَيۡ عَشۡرَةَ أَسۡبَاطًا أُمَمٗاۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ إِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰهُ قَوۡمُهُۥٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنۢبَجَسَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۚ وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡغَمَٰمَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ
Na tuliwagawa watu wa Mūsā miongoni mwa Wana wa Isrāīl makabila kumi na mbili, kwa idadi ya Asbāṭ- wana wa Ya’qūb-, kila kabila ikajulikana kupitia kiongozi wake. Na tulimpelekea wahyi Mūsā, walipotaka watu wake kwake maji ya kunywa waliposhikwa na kiu katika kuzunguka kwao, tukamwambia, «Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.» Akalipiga na pakabubujika chemchemi za maji sehemu kumi na mbili, na watu wa kila kabila, miongoni mwa yale makabila kumi na mbili, walijua mahali pao pa kunywa, hakuna kabila litakaloingia sehemu ya kunywa ya kabila lingine. Na tukawafinika kiwingu juu yenu, na tukawateremshia mann- kitu kinachofanana na gundi chenye ladha kama ya asali- na salwā- ndege wanaofanana na wale wanaoitwa sumānā (tomboro), na tukawaambia, «Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku.» Walivichukia na kuvichoka hivyo kwa muda mrefu wa kuvitumia na wakasema, «Hatutavumilia juu ya chakula kimoja.» Na wakataka kubadilishiwa kizuri walichonacho kwa ambacho ni kiovu. Na wao hawakutudhulumu sisi walipoacha kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuacha kusimama na yale Aliyoyalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao, kwa kuwa walizikosesha kila jema na kuzipeleka kwenye shari na mateso.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذۡ قِيلَ لَهُمُ ٱسۡكُنُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ وَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ وَقُولُواْ حِطَّةٞ وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطِيٓـَٰٔتِكُمۡۚ سَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na kumbuka, ewe Mtume, uasi kwa Wana wa Isrāīl Mola wao, kutakata na sifa pungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na Nabii wao Mūsā, amani imshukiye, na kugeuza kwao maneno waliyoamrishwa wayaseme pindi Alipowaambia Mwenyezi Mungu, «kaeni mji wa Baitul Maqdis na kuleni matunda yake, nafaka zake na mimea yake popote mtakapo na wakati wowote mtakao na semeni, ‘tuondoshee dhambi zetu,’ na ingieni mlangoni mkimnyenyekea Mwenyezi Mungu, tutawasamehe makosa yenu na hatutawaadhibu kwayo, na tutawaongezea walio wema kheri mbili: za ulimwengu na Akhera.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَبَدَّلَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ قَوۡلًا غَيۡرَ ٱلَّذِي قِيلَ لَهُمۡ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِجۡزٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ بِمَا كَانُواْ يَظۡلِمُونَ
Waliomkanusha Mwenyezi Mungu kati yao waliligeuza neno ambalo Mwenyezi Mungu Aliwaamrisha waliseme, wakaingia mlangoni wakijikokota kwa matako yao na wakasema, «habbah fī sha'rah» (mbegu kwenye unywele), hapo tukawateremshia adhabu kutoka mbinguni, tukawaangamiza kwayo, kwa sababu ya udhalimu wao na uasi wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَسۡـَٔلۡهُمۡ عَنِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلَّتِي كَانَتۡ حَاضِرَةَ ٱلۡبَحۡرِ إِذۡ يَعۡدُونَ فِي ٱلسَّبۡتِ إِذۡ تَأۡتِيهِمۡ حِيتَانُهُمۡ يَوۡمَ سَبۡتِهِمۡ شُرَّعٗا وَيَوۡمَ لَا يَسۡبِتُونَ لَا تَأۡتِيهِمۡۚ كَذَٰلِكَ نَبۡلُوهُم بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Na waulize, ewe Mtume, hawa Mayahudi kuhusu habari ya watu wa kijiji kilichokuwa karibu ya bahari, ambacho watu wake walikuwa wakipita mipaka siku ya Jumamosi kwa kufanya mambo yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, kwani Alikuwa Amewaamrisha waitukuze siku ya Jumamosi na wasivue samaki siku hiyo. Mwanyezi Mungu Akawajaribu na kuwapa mtihani, wakawa samaki wao wawajia siku ya Jumamosi kwa wingi wakiwa juu ya uso wa bahari, na Jumamosi ikipita wakawa samaki wanapotea na hawawaoni kabisa. Basi wakawa wafanya hila ya kuwatega siku ya Jumamosi kwenye mashimo na kuwavua baada yake. Na kama tulivyowaelezea vile Mwenyezi Mungu Alivyowajaribu na kuwapa mtihani kwa kuwatoa samake juu ya bahari katika siku ambayo waliharamishiwa kuwavua na kuwaficha wasiwaone katika siku ambazo ni halali kwao kuwavua, ndivyo tunavyowafanyia mtihani wao kwa sababu ya uasi wao na kutoka kwao kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذۡ قَالَتۡ أُمَّةٞ مِّنۡهُمۡ لِمَ تَعِظُونَ قَوۡمًا ٱللَّهُ مُهۡلِكُهُمۡ أَوۡ مُعَذِّبُهُمۡ عَذَابٗا شَدِيدٗاۖ قَالُواْ مَعۡذِرَةً إِلَىٰ رَبِّكُمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi kundi kati yao waliposema kuwaambia kundi lingine lililokuwa likiwapa mawaidhia wale waliopita mipaka siku ya Jumamosi na likiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu siku hiyo, «Kwa nini nyinyi mnawaidhia watu ambao Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangamiza ulimwenguni kwa kumuasi au ni Mwenye kuwaadhibu adhabu kali kesho Akhera?» Wakanena wale waliokuwa wakiwakataza wasimuasi Mwenyezi Mungu, «Tunawaidhia na tunawakataza ili tuwe na udhuru kuhusu wao na kwa ajili ya kutekeleza wajibu wa Mwenyezi Mungu juu yetu ya kuamrisha mema na kukataza maovu na kwa matumaini kwamba watamcha Mwenyezi Mungu, watamuogopa na watatubia kutokana na kumuasi kwao Mola wao na kupita mipaka ya mambo yaliyoharamishiwa kwao.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِۦٓ أَنجَيۡنَا ٱلَّذِينَ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلسُّوٓءِ وَأَخَذۡنَا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ بِعَذَابِۭ بَـِٔيسِۭ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Basi lilipoacha lile pote ambalo lilikiuka mipaka siku ya Jumamosi yale waliyokumbushwa na likaendelea kwenye upotevu wake na kukiuka mipaka kwake katika siku hiyo na lisiyakubali mawaidha waliyopewa na pote lenye kuwaidhia, Mwenyezi Mungu Aliwaokoa wale waliokuwa wanakataza maasia Yake na akawapatia wale waliokiuka mipaka siku ya Jumamosi adhabu kali mno kwa sababu ya kuenda kinyume kwao na amri ya Mwenyezi Mungu na kutoka kwao kwenye utiifu Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَمَّا عَتَوۡاْ عَن مَّا نُهُواْ عَنۡهُ قُلۡنَا لَهُمۡ كُونُواْ قِرَدَةً خَٰسِـِٔينَ
Basi pote hilo lilipoasi na likayakiuka yale ambayo Mwenyezi Mungu Alioyakataza ya kutowinda siku ya siku ya Jumamosi, Mwenyezi Mungu Aliwaambia (watu wa pote hilo), «Kuweni manyani hali ni wanyoge ni wenye kuwekwa mbali na kila jema.» Na wakawa hivyo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذۡ تَأَذَّنَ رَبُّكَ لَيَبۡعَثَنَّ عَلَيۡهِمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ مَن يَسُومُهُمۡ سُوٓءَ ٱلۡعَذَابِۗ إِنَّ رَبَّكَ لَسَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُۥ لَغَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Alipotangaza Mola wako, tangazo wazi, kwamba Atawapelekea Mayahudi mwenye kuwaonjesha adhabu mbaya na kuwadhalilisha mpaka Siku ya Kiyama. Hakika Mola wako ni Mpesi wa kutesa kwa anayestahili kuteswa kwa sababu ya ukafiri wake na uasi wake. Na hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kutubia, ni Mwnye huruma kwao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَقَطَّعۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُمَمٗاۖ مِّنۡهُمُ ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنۡهُمۡ دُونَ ذَٰلِكَۖ وَبَلَوۡنَٰهُم بِٱلۡحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na tuliwagawanya Wana wa Isrāīl makundi: kati yao kuna wanaosimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja Wake, na kati yao kuna wenye kufanya kasoro wenye kuzidhulumu nafsi zao. Na hawa tuliwapa mtihani wa maisha ya neema na ukunjufu wa riziki; na pia tuliwapa mtihani wa maisha ya dhiki, misiba na matatizo kwa matarajio kuwa watarudi kumtii Mola wao na watatubia kutokana na vitendo vya kumuasi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٞ وَرِثُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَأۡخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا ٱلۡأَدۡنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغۡفَرُ لَنَا وَإِن يَأۡتِهِمۡ عَرَضٞ مِّثۡلُهُۥ يَأۡخُذُوهُۚ أَلَمۡ يُؤۡخَذۡ عَلَيۡهِم مِّيثَٰقُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن لَّا يَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّ وَدَرَسُواْ مَا فِيهِۗ وَٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ
Wakaja, baada ya hawa ambao tulieleza sifa zao, badala mbovu. Walichukua Kitabu kutoka kwa wakale wao, wakakisoma na wakakijua, na wakaenda kinyume na hukumu zake, wakawa wanachukua kile wanacholetewa cha starahe ya ulimwenguni kinachotokana na njia mbaya za mapato kama hongo na mfano wake. Hayo ni kwa sababu ya wingi wa pupa lao na uroho wao, na wanasema pamoja na hayo, «Mwenyezi Mungu Atatusamehe,» wakitamani kwa Mwenyezi Mungu mambo yasiyofaa, na ikiwajia Mayahudi hawa starahe yenye kuondoka, miongoni mwa vitu vya haramu, huichukua na kuihalalisha, huku wakiendelea kufanya madhambi yao na kutumia haramu. Kwani hazikuchukuliwa kwao ahadi juu ya kuisimamisha Taurati na kufuata kivitendo yaliyomo ndani yake na kwamba hawatasema juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na kwamba hawatamzulia urongo, wakayajua yaliyomo Kitabuni, wakayapoteza na wakaenda kinyume na ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao katika hilo? Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu, wakafuata amri Zake na wakaepuka makatazo Yake. Kwani hawa wanaochukua mapato duni hawaelewi kwamba yaliyo mbele ya Mwenyezi Mungu ni bora zaidi na yenye kusalia zaidi kwa wachamungu?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ يُمَسِّكُونَ بِٱلۡكِتَٰبِ وَأَقَامُواْ ٱلصَّلَوٰةَ إِنَّا لَا نُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُصۡلِحِينَ
Na wanaoshikamana na Kitabu, wanaoyafuata kivitendo yaliyomo ndani yake miongoni mwa mambo ya itikadi na hukumu na wanaodumu na Swala kwa mipaka yake na wasiyozipoteza nyakati zake, Mwenyezi Mungu Atawalipa kwa matendo yao mema na hatayapoteza.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَإِذۡ نَتَقۡنَا ٱلۡجَبَلَ فَوۡقَهُمۡ كَأَنَّهُۥ ظُلَّةٞ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُۥ وَاقِعُۢ بِهِمۡ خُذُواْ مَآ ءَاتَيۡنَٰكُم بِقُوَّةٖ وَٱذۡكُرُواْ مَا فِيهِ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tulipoliinua jabali juu ya Wana wa Isrāīl likawa kama kwamba ni kiwingu kinachowafinika, wakawa na yakini kuwa kitawaangukia iwapo hawatazikubali hukumu zilizomo kwenye Taurati, na tukawaambia,»Chukueni tulichowapa kwa nguvu.» Yaani, fuateni kivitendo tulichowapa kwa bidii yenu, na yakumbukeni yaliyomo kwenye Kitabu chetu ya ahadi na masharti tuliyoyachukuwa kwenu kwamba mtayatekeleza yaliyomo ndani yake, ili mumche Mola wenu mpate kuokoka na mateso Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذۡ أَخَذَ رَبُّكَ مِنۢ بَنِيٓ ءَادَمَ مِن ظُهُورِهِمۡ ذُرِّيَّتَهُمۡ وَأَشۡهَدَهُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَلَسۡتُ بِرَبِّكُمۡۖ قَالُواْ بَلَىٰ شَهِدۡنَآۚ أَن تَقُولُواْ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ إِنَّا كُنَّا عَنۡ هَٰذَا غَٰفِلِينَ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Mola wako Alipowatoa wana wa Ādam kutoka kwenye migongo ya baba zao, Akawathibitishia upweke Wake kwa kuwatia tabia ya kimaumbile kwamba Yeye ni Mola wao, ni Muumba wao na ni Mmiliki wao; wakamkubalia hilo kwa kuchelea wasije kukanusha Siku ya Kiyama wasikubali chochote katika hilo na wasije wakadai kwamba hoja ya Mwenyezi Mungu haijasimama kwao na wala hawajui chochote juu yake, bali wao walikuwa wameghafilika na hilo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوۡ تَقُولُوٓاْ إِنَّمَآ أَشۡرَكَ ءَابَآؤُنَا مِن قَبۡلُ وَكُنَّا ذُرِّيَّةٗ مِّنۢ بَعۡدِهِمۡۖ أَفَتُهۡلِكُنَا بِمَا فَعَلَ ٱلۡمُبۡطِلُونَ
Na ili msiseme, «Hakika baba zetu walishirikisha kabla yetu na wakavunja ahadi, na sisi tukawafuata, basi je utatuadhibu kwa yale waliyoyafanya wale ambao waliyaharibu matendo yao kwa kumfanya Mwenyezi Mungu ana mshirika katika ibada?»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَكَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ وَلَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ
Na kama tulivyozipambanua hizo aya na tukaeleza ndani yake tulichowafanyia watu waliopita, ndivyo tunavyozipambanua aya na kuzieleza kwa watu wako, ewe Mtume, kwa kutazamia kwamba watarudi waache ushirikina wao na warajee kwa Mola wao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱتۡلُ عَلَيۡهِمۡ نَبَأَ ٱلَّذِيٓ ءَاتَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا فَٱنسَلَخَ مِنۡهَا فَأَتۡبَعَهُ ٱلشَّيۡطَٰنُ فَكَانَ مِنَ ٱلۡغَاوِينَ
Na wasimulie,ewe Mtume, watu wako habari ya mwanamume mmoja miongoni mwa Wana wa Isrāīl, tuliyompa hoja zetu na dalili zetu, akajifunza hizo kisha akazikanusha na akazitupa nyuma ya mgongo wake, akashindwa na Shetani na akawa ni miongoni mwa wapotevu wenye kuangamia, kwa sababu ya kuenda kinyume kwake na amri ya Mola wake na kumtii kwake Shetani.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَوۡ شِئۡنَا لَرَفَعۡنَٰهُ بِهَا وَلَٰكِنَّهُۥٓ أَخۡلَدَ إِلَى ٱلۡأَرۡضِ وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُۚ فَمَثَلُهُۥ كَمَثَلِ ٱلۡكَلۡبِ إِن تَحۡمِلۡ عَلَيۡهِ يَلۡهَثۡ أَوۡ تَتۡرُكۡهُ يَلۡهَثۚ ذَّٰلِكَ مَثَلُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَاۚ فَٱقۡصُصِ ٱلۡقَصَصَ لَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ
Na lau tulitaka kukitukuza cheo chake kwa aya tulizompa tungalifanya, lakini yeye alitegemea ulimwengu na akafuata matamanio yake, na akafadhilisha ladha zake na hawaa zake juu ya Akhera, na akakataa kumtii Mwenyezi Mungu na akaenda kinyume na amri Yake. Mfano wa mwanamume huyu ni mfano wa mbwa: ukimfukuza au ukimuacha hutoa ulimi wake katika hali zote mbili. Basi hivyo ndivyo alivyo yule aliyejivua aya za Mwenyezi Mungu kwa kuziacha, huwa akiendelea katika ukafiri wake ikiwa utafanya bidii kumlingania au utampuuza. Sifa hii, ewe Mtume, ndiyo sifa ya watu hawa waliokuwa wapotevu kabla hujawajia kwa uongofu na utume. Basi simulia, ewe Mtume, habari za watu waliopita, kwani katika kutolea kwako habari zao ni miujiza mikubwa zaidi; na huenda watu wako wakazingatia juu ya yale uliyowajia nayo na wakakuamini.
Tefsiri na arapskom jeziku:
سَآءَ مَثَلًا ٱلۡقَوۡمُ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَأَنفُسَهُمۡ كَانُواْ يَظۡلِمُونَ
Ni mfano mbaya ulioje! Mfano wa watu waliokanusha hoja za Mwenyezi Mungu na dalili Zake wakazikataa na hali kwamba ni nafsi zao wenyewe walikuwa wakizidhulumu kwa sababu ya kukanusha kwao hoja hizi na dalili.
Tefsiri na arapskom jeziku:
مَن يَهۡدِ ٱللَّهُ فَهُوَ ٱلۡمُهۡتَدِيۖ وَمَن يُضۡلِلۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Yule ambaye Mwenyezi Mungu Anamuafikia kumuamini Yeye na kumtii, huyo ndiye aliyeafikiwa; na yule ambaye Anamuachilia Asimuafikiye, huyo ndiye mwenye hasara, mwenye kuangamia. Kuongoza na kupoteza kunatokana na Mwenyezi Mungu Peke Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ ذَرَأۡنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِۖ لَهُمۡ قُلُوبٞ لَّا يَفۡقَهُونَ بِهَا وَلَهُمۡ أَعۡيُنٞ لَّا يُبۡصِرُونَ بِهَا وَلَهُمۡ ءَاذَانٞ لَّا يَسۡمَعُونَ بِهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ
Na kwa hakika tuliuumbia Moto - ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Atawaadhibu wanaostahili kuadhibiwa huko Akhera- majini na binadamu wengi, wana nyoyo lakini hawaelewi kwazo, hawatazamii malipo mazuri wala hawaogopi mateso; na wana macho hawaangalii kwayo aya za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, na wana masikio hawasikii kwayo aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuzitia akilini. Hawa ni kama wanyama wasioelewa waambiwacho, wasiofahamu wakionacho na wasiotia akilini kwa nyoyo zao kizuri na kibaya wakaweza kuzitenganisha. Bali wao wamepotea zaidi kuliko hao wanyama, kwani wanyama wanaona yanayowafaa na yanayowadhuru na wanamfuata mchungaji wao. Ama wao ni kinyume cha hilo, wao ndio wenye kughafilika na jambo la kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtii.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلِلَّهِ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ فَٱدۡعُوهُ بِهَاۖ وَذَرُواْ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ أَسۡمَٰٓئِهِۦۚ سَيُجۡزَوۡنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ana Majina Mazuri yanayoonyesha ukamilifu wa uwezo Wake, na majina Yake yote ni mazuri. Basi ombeni kutoka Kwake, kwa majina Yake, mnachotaka na muwaacheni wale wanaogeuza majina Yake kwa kuzidisha na kupunguza au kupotoa, kama kumuita kwa majina hayo asiyeyastahiki, kama vile washirikina wanavyowaita, kwa majina hayo, waungu wao, au ayape majina hayo maana ambayo Mwenyezi Mungu Hakuyataka wala Mtume Wake. Basi watapata malipo ya matendo yao mabaya waliokuwa wakiyafanya ulimwenguni ya kumkanusha Mwenyezi Mungu, kuyapotoa majina Yake na kuwafanya warongo Mitume Wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمِمَّنۡ خَلَقۡنَآ أُمَّةٞ يَهۡدُونَ بِٱلۡحَقِّ وَبِهِۦ يَعۡدِلُونَ
Na miongoni mwa wale tuliowaumba kuna kundi la watu bora wanaoongoka kwenye haki na wanaita watu waifuate, na kwa hiyo wanahukumu na wanafanyia watu uadilifu; na wao ni viongozi wa uongofu, kati ya wale ambao Mwenyezi Mungu Amewaneemesha kwa Imani na kufanya amali njema.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ
Na wale ambao walizikanusha aya zetu wakazikataa na wasiwaidhike nazo, tutawafungulia milango ya riziki na njia za maisha katika ulimwengu, kwa kuwavuta kidogo kidogo mpaka wahadaike kwa yale ambayo wako nayo na waitakidi kuwa wao wako kwenye kitu cha maana, kisha tutawatesa kwa ghafla kwa namna wasioijua. Haya ni mateso yatokao kwa Mwenyezi Mungu ya kukanusha hoja za Mwenyezi Mungu na aya Zake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأُمۡلِي لَهُمۡۚ إِنَّ كَيۡدِي مَتِينٌ
Na nitawapa muhula hawa ambao walizikanusha aya zetu mpaka wadhanie kwamba wao hawatateswa, waongeze ukafiri na uasi. Na kwa hivyo, waongezewe adhabu. Kwani vitimbi vyangu ni vigumu, yaani: ni vya nguvu na vikali havizuiliwi kwa nguvu wala kwa hila.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَلَمۡ يَتَفَكَّرُواْۗ مَا بِصَاحِبِهِم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Kwani hawafikirii hawa ambao walizikanusha aya zetu wakazingatia kwa akili zao na wakajua kwamba Muhammad hana wazimu? Yeye hakuwa isipokuwa ni mwenye kuwaonya wao mateso ya Mwenyezi Mungu kwa kumkanusha kwao Yeye, iwapo hawataamini, na ni mshauri muaminifu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَلَمۡ يَنظُرُواْ فِي مَلَكُوتِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ وَأَنۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَدِ ٱقۡتَرَبَ أَجَلُهُمۡۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Au kwani hawaangalii, hawa wakanushaji aya za Mwenyezi Mungu, kwenye ufalme wa Mwenyezi Mungu uliyo mkubwa na mamlaka Yake yenye uwezo wa kushinda, mbinguni na ardhini na chochote kile Alichokiumba Mwenyezi Mungu, zimetukuka sifa Zake, kwenye vitu viwili hivyo, wakalitia akilini hilo na wakalizingatia kwa akili zao na wakaangalia muda wa kikomo cha maisha yao ambao huenda ukawa umesongea karibu wakawa watakufa kwenye ukafiri wao na watakuwa kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu na mateso yake makali? Basi ni kitisho gani na onyo gani baada ya onyo la Qur’ani wataliamini na watalifanyia kazi?
Tefsiri na arapskom jeziku:
مَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَا هَادِيَ لَهُۥۚ وَيَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Yoyote ambaye Mwenyezi Mungu Anampoteza njia ya sawa hakuna mwenye kumuongoza, na Atawaacha wao ndani ya ukafiri wao wakiwa wanaduwaa na wanapigwa na bumbuazi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلسَّاعَةِ أَيَّانَ مُرۡسَىٰهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّيۖ لَا يُجَلِّيهَا لِوَقۡتِهَآ إِلَّا هُوَۚ ثَقُلَتۡ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ لَا تَأۡتِيكُمۡ إِلَّا بَغۡتَةٗۗ يَسۡـَٔلُونَكَ كَأَنَّكَ حَفِيٌّ عَنۡهَاۖ قُلۡ إِنَّمَا عِلۡمُهَا عِندَ ٱللَّهِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Wanakuuliza, ewe Mtume, makafiri wa Makkah kuhusu Kiyama: kusimama kwake ni lini? Waambie, elimu ya kusimama kwake iko kwa Mwenyezi Mungu, haitoi nje isipokuwa Yeye, imekuwa nzito kuijua na imefichika kwa watu wa mbinguni na ardhini. Hakuna Malaika aliyekaribishwa wala Mtume aliyetumilizwa anayejua wakati wa kusimama kwake. Hakiji isipokuwa kwa ghafla. Hawa watu wanakuuliza kuhusu hiko Kiyama kama kwamba wewe una pupa la kukijua, una bidii sana ya kukiuliza. Waambie, «Ujuzi wake uko kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Anayajua yaliyofichika kwenye mbingu na ardhi. Lakini wengi wa watu hawajui kwamba hilo hakuna anayelijua isipokuwa Mwenyezi Mungu.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي نَفۡعٗا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ وَلَوۡ كُنتُ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ لَٱسۡتَكۡثَرۡتُ مِنَ ٱلۡخَيۡرِ وَمَا مَسَّنِيَ ٱلسُّوٓءُۚ إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Sema, ewe Mtume, «Siwezi kuiletea mema nafsi yangu wala kuiepushia shari yenye kuifikia, isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Alitaka. Na lau mimi ningalikuwa najua yaliyofichika ningalifanya njia ambazo najua kwamba zitaniongezea maslahi na manufaa na ningalijikinga na shari yenye kuwa kabla haijatukia. Mimi si yoyote isipokuwa ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Amenituma kwenu, naogopesha mateso Yake na natoa bishara njema ya thawabu Zake kuwalipa watu wanaoamini kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakafuata sheria Yake kivitendo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَجَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا لِيَسۡكُنَ إِلَيۡهَاۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتۡ حَمۡلًا خَفِيفٗا فَمَرَّتۡ بِهِۦۖ فَلَمَّآ أَثۡقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنۡ ءَاتَيۡتَنَا صَٰلِحٗا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ
Yeye Ndiye ambaye Aliyewaumba nyinyi, enyi watu, kutokana na nafsi moja, nayo ni Ādam, amani imshukiye. Na akaumba kutokana na nafsi hiyo ya pili yake, nayo ni Ḥawwā’, ili aliwazike naye na ajitulize. Alipomuundama - makusudio ni jinsi ya mke na mume miongoni mwa kizazi cha Ādam - alibeba maji mapesi, akainuka nayo na akakaa nayo mpaka mimba ikatimia. Kilipokaribia kipindi cha kuzaa kwake na akawa mzito, walimuomba, mume na mke, Mola wao, «Tunaapa lau utatupatia mwanadamu aliye sawa, aliye mwema, hakika tutakuwa ni wenye kukushukuru kwa kutupa mtoto mwema.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُمَا صَٰلِحٗا جَعَلَا لَهُۥ شُرَكَآءَ فِيمَآ ءَاتَىٰهُمَاۚ فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Mwenyezi Mungu Alipowaruzuku, yule mume na mke, mtoto mwema walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika katika mtoto yule ambaye Mwenyezi Mungu Alipwekeka katika kumuumba wakamfanya ni mja wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; Ametukukuka Mwenyezi Mungu na Ameepukana na kila mshirika.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَيُشۡرِكُونَ مَا لَا يَخۡلُقُ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Je, washirikina hawa wawashirikisha viumbe vya Mwenyezi Mungu katika ibada ya Mwenyezi Mungu, hali washirikishwa hao hawawezi kuumba chochote, bali wao wameumbwa?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ لَهُمۡ نَصۡرٗا وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Wala hawawezi kuwanusuru wenye kuwaabudu au kuzilinda nafsi zao na ubaya. Iwapo wao hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa na hawawezi kuwalinda wanaowaabudu, wasipatikane na mambo wanayoyachukia, wala kuzilinda nafsi zao. Basi vipi wanafanywa ni waungu? Huu haukuwa isipokuwa ni upeo wa udhalimu na upeo wa uchache wa akili.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمۡۚ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡ أَدَعَوۡتُمُوهُمۡ أَمۡ أَنتُمۡ صَٰمِتُونَ
Na mnapowalingania, enyi washirikina, masanamu hawa ambao mliwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu kwenye uongofu, hawasikii ulinganizi wenu wala hawawafuati nyinyi; inalingana sawa kuwalingania au kuwanyamazia. Kwani wao hawasikii wala hawaoni wala hawaongozi wala hawaongozwi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Kwa hakika wale ambao mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, enyi washirikina, wamemilikiwa na Mola wao, kama mlivyomilikiwa nyinyi na Mola wenu. Basi iwapo nyinyi, kama mnavyodai, ni wakweli kwamba wao wanastahiki wafayiwe chochote kile cha ibada, waiteni wawaitikie. Iwapo watawaitikia na watawapatia matakwa yenu, mtakuwa ni wakweli, na isipokuwa hivyo, itakuwa wazi kwamba nyinyi ni warongo mnamzulia Mwenyezi Mungu uzushi mkubwa kabisa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ
Je, waungu hawa na masanamu wana miguu ya kutembelea na nyinyi katika haja zenu? Au wao wana mikono ya kuwatetea na kuwanusuru juu ya anayewatakia shari na maovu? Au wao wana macho ya kutazamia, wakapata kuwajulisha yale waliyoyashuhudia na wakayaona miongoni mwa yale yaliyofichika kwenu mkawa hamuyaoni? Au wao wana masikio ya kusikia kwayo, wapate kuwapa habari ya yale msiyoyasikia? Iwapo waungu wenu ambao mnawaabudu hawana vyombo hivi, kuna maana gani kuwaabudu, ilhali wao hawana vitu hivi ambavyo kwavyo kunapelekea kujipatia manufaa au kujiepushia madhara? Waambie, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wenye kuwaabudu masanamu, «Waiteni waungu wenu ambao mliwafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada, kisha kusanyikeni kunifanyia ubaya na maudhi, msinipe muhula na lifanyieni haraka hilo, kwani mimi siwajali waungu wenu kwa kuwa nategemea hifadhi ya Mwenyezi Mungu Peke Yake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ وَلِـِّۧيَ ٱللَّهُ ٱلَّذِي نَزَّلَ ٱلۡكِتَٰبَۖ وَهُوَ يَتَوَلَّى ٱلصَّٰلِحِينَ
«Hakika mtegemewa wangu ni Mwenyezi Mungu Ambaye Anasimamia kunihifadhi na kunipa ushindi. Yeye Ndiye Ambaye Aliniteremshia Qur’ani kwa haki na Yeye Anawasimamia walio wema miongoni mwa waja wake na anawapa ushindi juu ya maadui zao na Haachi kuwasaidia.»
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦ لَا يَسۡتَطِيعُونَ نَصۡرَكُمۡ وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Na wale waungu ambao nyinyi mnawaomba, enyi washirikina, badala ya Mwenyezi Mungu, hawawezi kuwanusuru nyinyi wala kuzinusuru nafsi zao.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَسۡمَعُواْۖ وَتَرَىٰهُمۡ يَنظُرُونَ إِلَيۡكَ وَهُمۡ لَا يُبۡصِرُونَ
Na iwapo mtawaita, enyi washirikina, hao waungu wenu kwenye kulingana sawa na haki hawatasikia mwito wenu. Na utawaona, ewe Mtume, waungu wa hawa washirikina miongoni mwa wenye kuabudu mizimu, wanakuelekea kama wanaokutazama na hali wao hawaoni kwa kuwa wao hawana macho wala busara.
Tefsiri na arapskom jeziku:
خُذِ ٱلۡعَفۡوَ وَأۡمُرۡ بِٱلۡعُرۡفِ وَأَعۡرِضۡ عَنِ ٱلۡجَٰهِلِينَ
Kubali, ewe Nabii, wewe na wafuasi wako kiwango cha kati cha tabia za watu na vitendo vyao, wala usitake kutoka kwao mambo magumu ili wasije wakachukia; na amrisha kwa kila neno jema na kitendo kizuri; na jiepushe na kushindana na mafidhuli na usijisawazishe na wajinga wenye uchache wa akili.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ نَزۡغٞ فَٱسۡتَعِذۡ بِٱللَّهِۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٌ عَلِيمٌ
Na iwapo utashikwa na hasira, ewe Nabii, zitokazo kwa Shetani au ukahisi, kutoka kwake, wasiwasi au ulegevu wa kufanya mema au himizo la kufanya ovu, basi tafuta himaya kwa Mola wako kwa kujilinda Kwake. Kwani Yeye ni Msikizi wa kila neno ni Mjuzi wa kila kitendo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ٱتَّقَوۡاْ إِذَا مَسَّهُمۡ طَٰٓئِفٞ مِّنَ ٱلشَّيۡطَٰنِ تَذَكَّرُواْ فَإِذَا هُم مُّبۡصِرُونَ
Hakika wale wanaomcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa viumbe wake, kwa kuogopa mateso Yake kwa kuzitekeleza faradhi Zake na kuyaepuka makatazo Yake, likiwapata tukio lolote la wasiwasi wa Shetani, wanayakumbuka yale Aliyowalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao ya kumtii na kutubia Kwake, na punde si punde wanakomeka na kumuasi Mwenyezi Mungu wakiwa kwenye hoja ya wazi, wenye kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na wenye kumuasi Shetani.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِخۡوَٰنُهُمۡ يَمُدُّونَهُمۡ فِي ٱلۡغَيِّ ثُمَّ لَا يُقۡصِرُونَ
Na ndugu wa mashetani, nao ni wapotofu miongoni mwa wapotevu wa wanadamu ambao mashetani wanawasukuma kwenye upotevu na upotofu. Na mashetani wa kijini hawaachi nafasi iwapite katika kuwasukuma kwao mashetani wa kibinadamu kwenye upotofu. Na mashetani wa kibinadamu hawaachi nafasi iwapite katika kuyafanya yale ambayo mashetani wa kijini wanayafanyia ushawishi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذَا لَمۡ تَأۡتِهِم بِـَٔايَةٖ قَالُواْ لَوۡلَا ٱجۡتَبَيۡتَهَاۚ قُلۡ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ مِن رَّبِّيۚ هَٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Na usipowajia, ewe Mtume, washirikina hawa na aya wanasema, «Si uitunge na uizue wewe mwenyewe.» Waambie, ewe Mtume, «Hili si langu, na haifai kwangu mimi nilifanye. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ameniamuru kufuata wahyi nilioletewa kutoka Kwake. Nao ni hii Qur’ani ninayowasomea, inayokusanya hoja na dalili zinazotoka kwa Mola wenu na yenye ufafanuzi, inayoongoza Waumini kwenye njia iliyolingana sawa, na ni rehema ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anawarehemu waja Wake Waumini.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذَا قُرِئَ ٱلۡقُرۡءَانُ فَٱسۡتَمِعُواْ لَهُۥ وَأَنصِتُواْ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ
Na isomwapo Qur’ani isikilizeni, enyi watu, na mnyamaze ili muielewe kwa matarajio kwamba Mwenyezi Mungu Awarehamu kwayo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱذۡكُر رَّبَّكَ فِي نَفۡسِكَ تَضَرُّعٗا وَخِيفَةٗ وَدُونَ ٱلۡجَهۡرِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ بِٱلۡغُدُوِّ وَٱلۡأٓصَالِ وَلَا تَكُن مِّنَ ٱلۡغَٰفِلِينَ
Na mtaje Mola wako, ewe Mtume, ndani ya nafsi yako kwa kumnyenyekea Mwenyezi Mungu na kumdhalilikia, hali ya kumcha Yeye moyoni, na umuombe kwa namna ya kati na kati baina ya kutoa sauti na kuifanya chini, katika mwanzo wa mchana na mwisho wake, na usiwe ni miongoni mwa wenye kughafilika kumtaja Mwenyezi Mungu na kupumbaa katika nyakati zao zinginezo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّ ٱلَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيُسَبِّحُونَهُۥ وَلَهُۥ يَسۡجُدُونَۤ۩
Hakika wale waliyoko mbele ya Mola Wako miongoni mwa Malaika hawafanyi kiburi kwa kuacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, bali wao wanaandama amri Zake, wanamtakasa mchana na usiku na wanamwepusha na mambo yasiyonasibiana na Yeye, na Yeye Peke Yake wanamsujudia.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: Sura el-A'araf
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - الترجمة السواحلية - عبد الله محمد وناصر خميس - Sadržaj prijevodā

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها الدكتور عبد الله محمد أبو بكر والشيخ ناصر خميس.

Zatvaranje