prev

An-Nasr

next

1 : 110

إِذَا جَآءَ نَصۡرُ ٱللَّهِ وَٱلۡفَتۡحُ

Utakapotimia kwako , ewe Mtume, ushindi juu ya makafiri wa Kikureshi na ukafutahi Makkah. info
التفاسير: |

2 : 110

وَرَأَيۡتَ ٱلنَّاسَ يَدۡخُلُونَ فِي دِينِ ٱللَّهِ أَفۡوَاجٗا

Na ukaona watu wengi wanaingia kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi. info
التفاسير: |

3 : 110

فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُۚ إِنَّهُۥ كَانَ تَوَّابَۢا

Yatakapotokea hayo, jitayarishe kukutana na Mola Wako kwa kumtakasa na kumhimidi na kumuomba msamaha kwa wingi. Kwani Yeye ni Mwingi wa kuwakubalia toba wenye kumsabihi na kumuomba msamaha, kwa kuwasamehe na kuwarehemu. info
التفاسير: |
prev

An-Nasr

next
:
0:00 0:00