Übersetzung der Bedeutungen des edlen Qurans - Die Übersetzung in Swahili

prev

Al-Alaq

next

1 : 96

ٱقۡرَأۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلَّذِي خَلَقَ

Soma, ewe Nabii, Qur’ani uliyoteremshiwa ukianza kwa Jina la Mola wako Aliyepwekeka kwa kuumba. info
التفاسير: |

2 : 96

خَلَقَ ٱلۡإِنسَٰنَ مِنۡ عَلَقٍ

Aliyemuumba kila binadamu kwa pande la damu nzito nyekundu. info
التفاسير: |

3 : 96

ٱقۡرَأۡ وَرَبُّكَ ٱلۡأَكۡرَمُ

Soma, (ewe Nabii), kile ulichoteremshiwa, na Mola wako ni Mwingi wa wema, Mwingi wa ukarimu. info
التفاسير: |

4 : 96

ٱلَّذِي عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ

Aliyewafundisha viumbe vyake kuandika kwa kalamu. info
التفاسير: |

5 : 96

عَلَّمَ ٱلۡإِنسَٰنَ مَا لَمۡ يَعۡلَمۡ

Alimfundisha binadamu vitu ambavyo hakuwa akivijua. Akamtoa kwenye giza la ujinga, Akampeleka kwenye nuru ya elimu. info
التفاسير: |

6 : 96

كَلَّآ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَيَطۡغَىٰٓ

Kweli, binadamu hukiuka mipaka ya Allah Mtukufu info
التفاسير: |

7 : 96

أَن رَّءَاهُ ٱسۡتَغۡنَىٰٓ

Akijiona ametosheka kwa utajiri wake. info
التفاسير: |

8 : 96

إِنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلرُّجۡعَىٰٓ

Basi, ajue kila mwenye kuchupa mipaka kuwa uhakika ni kuwa atarudi kwa Allah Mtukufu Ambaye Atamlipa kila binadamu kwa alilolitenda. info
التفاسير: |

9 : 96

أَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي يَنۡهَىٰ

Je, umeona ujeuri wa ajabu zaidi kuliko wa mtu huyu, (Abû jahl), Anayemkataza mja wetu? «Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie», info
التفاسير: |

10 : 96

عَبۡدًا إِذَا صَلَّىٰٓ

Unamuona anavyomkataza mja wetu pale anaposwali? info
التفاسير: |

11 : 96

أَرَءَيۡتَ إِن كَانَ عَلَى ٱلۡهُدَىٰٓ

Waonaje iwapo mwenye kukatazwa kuswali yuko kwenye uongofu, vipi anamkataza? info
التفاسير: |

12 : 96

أَوۡ أَمَرَ بِٱلتَّقۡوَىٰٓ

Au iwapo anaamrisha mwingine kumcha Mungu, vipi anamkataza hilo? info
التفاسير: |
prev

Al-Alaq

next
:
0:00 0:00