Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman * - Translations’ Index


Translation of the meanings Surah: Tā-ha   Ayah:

Surat Taha

طه
«Ṭā, Hā» Yametangulia maelezo kuhusu herufi za mkato mwanzo wa sura ya Al -Bqarah.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لِتَشۡقَىٰٓ
Hatukuiteremsha Qur’ani kwako, ewe Mtume, ujisumbue kwa jambo usiloliweza kulifanya.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا تَذۡكِرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰ
Lakini tumeiteremsha iwe ni mawaidha, ili ajikumbushe nayo mwenye kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu apate kujikinga nayo kwa kutekelaza faradhi na kujiepusha na mambo ya haramu.
Arabic explanations of the Qur’an:
تَنزِيلٗا مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلۡعُلَى
Hii Qur’ani ni teremsho kutoka kwa Mwenyezi Mungu Ambaye Ameumba ardhi na mbingu zilizo juu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلرَّحۡمَٰنُ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ ٱسۡتَوَىٰ
Mwingi wa rehema, juu ya 'Arsh Amelingana, yaani Amekuwa juu na Ameangatika, kulingana kunakonasibiana na utukufu Wake na ukubwa Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَمَا تَحۡتَ ٱلثَّرَىٰ
Ni Vyake vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini na vilivyoko baina yake na vilivyoko ndani yake, kwa kuviumba, kuvitamalaki na kuviendesha.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِن تَجۡهَرۡ بِٱلۡقَوۡلِ فَإِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ وَأَخۡفَى
Na ukitoa sauti, ewe Mtume, katika kusema ukaifanya ya juu au ya chini, basi hakuna chochote kinachofichika kwa Mwenyezi Mungu, Anajua siri na kilichofichika zaidi kuliko siri katika vitu ambavyo nafsi yako inakuzungumzia.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ
Mwenyezi Mungu Ambaye hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, ni Yake Peke Yake majina yaliyokamilika katika uzuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَهَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Na je, imekujia, ewe Mtume, habari ya Mūsā bin ‘Imrān, amani imshukie, katika kurudi kwake kutoka Madyan na kuelekea Misri.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِذۡ رَءَا نَارٗا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدٗى
Alipouona moto usiko umewashwa, akasema kuwaambia watu wa nyumbani kwake, «Ngojeni! Mimi nimeuona moto, huenda nikawaletea kinga cha moto mkapata kujitoa ubaridi na mkawasha moto mwingine kwa kinga hiko, au nikapata mtu wa kutuongoza njia.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِيَ يَٰمُوسَىٰٓ
Mūsā alipoufikia ule moto, Mwenyezi Mungu Alimuita, «Ewe Mūsā!
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنِّيٓ أَنَا۠ رَبُّكَ فَٱخۡلَعۡ نَعۡلَيۡكَ إِنَّكَ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوٗى
Mimi ni Mola wako, vua viatu vyako, wewe sasa uko kwenye bonde la Tuwā nililolipa baraka. Hivyo ni ili ajiandae kusema na Mola wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَنَا ٱخۡتَرۡتُكَ فَٱسۡتَمِعۡ لِمَا يُوحَىٰٓ
Na mimi nimekuteua , ewe Mūsā, kwa ujumbe wangu, basi sikiliza yale unayoletewa ya wahyi kutoka kwangu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّنِيٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدۡنِي وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكۡرِيٓ
Mimi Ndiye Mwenyezi Mungu, hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa mimi, sina mshirika, basi niabudu mimi na usimamishe Swala ili unikumbuke ndani yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ
Hakika Kiyama ambacho watu hapo watafufuliwa hapana budi ni chenye kutukia. Nakaribia kukificha kwangu mimi mwenyewe, basi ni vipi atakijua mtu yoyote miongoni mwa viumbe. Hivyo ni apate kulipwa kila mtu kwa alilolitenda ulimwenguni, liwe zuri au baya.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنۡهَا مَن لَّا يُؤۡمِنُ بِهَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَتَرۡدَىٰ
Basi asikuepushe, ewe Mūsā, na kukiamini na kujitayarisha nacho, asiyekikubali kuwa kitatukia na asiyetenda ya kumfaa huko na akayafuata matamanio ya nafsi yake na akakikanusha, kwani ukifanya hivyo utaangamia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَٰمُوسَىٰ
Na ni nini hii iliyo kwenye mkono wako wa kulia, ewe Mūsā?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّؤُاْ عَلَيۡهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ
Akasema Mūsā, «Hii ni ni fimbo yangu, naitegemea katika kwenda na ninapigia miti ili mbuzi wangu walishe majani yake yanayoanguka na pia nina maslahi nayo mengine.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ أَلۡقِهَا يَٰمُوسَىٰ
Mwenyezi Mungu Akamwambia Mūsā, «Itupe fimbo yako!»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَلۡقَىٰهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٞ تَسۡعَىٰ
Mūsā akaitupa chini, ikageuka kwa amri ya Mwenyezi Mungu ikawa nyoka anayetembea, na Mūsā akaona jambo kubwa na akazunguka kukimbia.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ
Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Mūsā, «Mshike huyo nyoka na usimuogope, tutamrudisha kuwa fimbo vile alivyokuwa mwanzo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ
Na ukumbatie mkono wako kwenye ubavu wako chini ya shina la mkono utatoka hali ni mweupe kama barafu bila ya kuwa na mbalanga, ili iwe ni alama nyingine.
Arabic explanations of the Qur’an:
لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى
Tumefanya hivyo ili kukuonesha , ewe Mūsā, dalili zetu kubwa zenye kutolea ushahidi uweza wetu, ukubwa wa ufalme wetu na usahihi wa utume wako.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Enda, ewe Mūsā, kwa Fir'awn, kwa kuwa yeye amepitisha kipimo chake na ametoka kwenye utiifu wa Mola wake, umuite kwenye kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumuabudu.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِي صَدۡرِي
Mūsā akasema, «Ewe Mola wangu! Nikunjulie kifua changu,
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَسِّرۡ لِيٓ أَمۡرِي
nirahisishie mambo yangu
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةٗ مِّن لِّسَانِي
na nifungulie ulimi wangu uwe na ufasaha wa matamshi,
Arabic explanations of the Qur’an:
يَفۡقَهُواْ قَوۡلِي
ili waelewe maneno yangu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي
Na unipatie msaidizi miongoni mwa watu wangu,
Arabic explanations of the Qur’an:
هَٰرُونَ أَخِي
naye ni Hārūn ndugu yangu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱشۡدُدۡ بِهِۦٓ أَزۡرِي
Nitilie nguvu kwa yeye na uuthibitishe mgongo wangu kwa ajili yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَشۡرِكۡهُ فِيٓ أَمۡرِي
Na umshirikishe na mimi katika unabii na ufikishaji ujumbe.
Arabic explanations of the Qur’an:
كَيۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرٗا
Tupate kukuepusha na kila sifa ya upungufu na tukutakase kwa wingi,
Arabic explanations of the Qur’an:
وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا
na tukutaje kwa wingi na tukushukuru.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرٗا
Kwa hakika, wewe ni mwenye kutuona, hakuna chochote kinachofichika kwako miongoni mwa vitendo vyetu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَٰمُوسَىٰ
Mwenyezi Mungu Akasema, «Nishakupa kila ulichokiomba, ewe Mūsā.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَيۡكَ مَرَّةً أُخۡرَىٰٓ
«Na tulikupa , ewe Mūsā, kabla ya neema hii, neema nyingine ulipokuwa ni mtoto wa kunyonya tukakuokoa na unyanyasaji wa Fir'awn.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِذۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰٓ
«Na hilo ni pale tulipomfahamisha mamako kwa kumtia mawazo kwamba:
Arabic explanations of the Qur’an:
أَنِ ٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلتَّابُوتِ فَٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ فَلۡيُلۡقِهِ ٱلۡيَمُّ بِٱلسَّاحِلِ يَأۡخُذۡهُ عَدُوّٞ لِّي وَعَدُوّٞ لَّهُۥۚ وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةٗ مِّنِّي وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِيٓ
muweke mwanao, Mūsā, baada ya kuzaliwa, katika sanduku, kisha ulitie kwenye mto wa Nail. Hapo mto wa Nail utalipeleka hadi ufuoni, na hapo Fir'awn atalichukua, adui yangu na adui yake (huyo aliyomo sandukuni). Na nikayaingiza mapenzi kwako kutoka kwangu, ukawa kwa hilo, ni mwenye kupendwa na waja, na ili ulelewe chini ya uangalizi wangu na ulinzi wangu. Kwenye aya hii kuna kuthibitisha sifa ya jicho ('ayn) kwa Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, kama inavyonasibiana na utukufu Wake na ukamilifu Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِذۡ تَمۡشِيٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُۥۖ فَرَجَعۡنَٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا فَنَجَّيۡنَٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّٰكَ فُتُونٗاۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٖ يَٰمُوسَىٰ
«Na pia tulikuneemesha pindi alipokwenda dadako kufuatilia mambo yako, kisha akasema akiwaambia waliokuchukua, ‘Je, niwajulishe nyinyi yule anayeweza kuwalelea na kuwanyonyeshea?’ Basi tukakurudisha kwa mamako baada ya kwamba ulikuwa kwenye mikono ya Fir'awn ili nafsi yake itulie kwa kuokoka kwako na kuzama na kuuawa na asiwe na masikitiko ya kukukosa. Na ulimuua mtu wa kabila la Kibti kimakosa tukakuokoa na makero ya kitendo chako hiko na kuogopa kuuawa. Na tulikuonja maonjo mengi, ukatoka kwa kuogopa ukaenda kwa watu wa Madyan, ukaketi kwao miaka mingi, kisha ukaja kutoka Madyan katika kipindi tulichokipanga kwa kukutumiliza, kuja kulikofikiana na mpango wa Mwenyezi Mungu na matakwa Yake. Na mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu Mwingi wa baraka Aliyetukuka.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱصۡطَنَعۡتُكَ لِنَفۡسِي
«Nimekupa neema hizi, ewe Mūsā, zikiwa ni chaguo langu kwako na uteuzi ili ubebe utume wangu na ufikishe ujumbe wangu na usimame kutekeleza maamrisho yangu na makatazo yangu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱذۡهَبۡ أَنتَ وَأَخُوكَ بِـَٔايَٰتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكۡرِي
«Enda, ewe Mūsā, wewe na ndugu yako Hārūn, ukiwa na aya zangu zinazoonyesha uungu wangu na ukamilifu wa uweza wangu na ukweli wa utume wako, wala msiwe wanyonge katika kuendeleza utajo wangu.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Endeni, mkiwa pamoja, kwa Fir'awn, kwa kuwa yeye amekiuka mipaka katika ukafiri na udhalimu,
Arabic explanations of the Qur’an:
فَقُولَا لَهُۥ قَوۡلٗا لَّيِّنٗا لَّعَلَّهُۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ
na mumwambie maneno laini, kwani huenda akakumbuka au akamuogopa Mola wake.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَا رَبَّنَآ إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفۡرُطَ عَلَيۡنَآ أَوۡ أَن يَطۡغَىٰ
Mūsā na Hārūn wakasema, «Ewe Mola wetu! Sisi tunaogopa asije akakimbilia kutuadhibu au akajitolea kuipinga haki asiikubali.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ لَا تَخَافَآۖ إِنَّنِي مَعَكُمَآ أَسۡمَعُ وَأَرَىٰ
Mwenyezi Mungu Akasema kumwambia Mūsā na Hārūn, «Msimuogope Fir'awn, kwani mimi niko na nyinyi, nasikia maneno yenu na naona vitendo vyenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأۡتِيَاهُ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَا تُعَذِّبۡهُمۡۖ قَدۡ جِئۡنَٰكَ بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكَۖ وَٱلسَّلَٰمُ عَلَىٰ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلۡهُدَىٰٓ
Basi endeni kwake na mumwambie, ‘Sisi ni wajumbe wawili kutoka kwa Mola wako kwamba uwaache Wana wa Isrāīl na usiwakalifishe matendo wasiyoyaweza. Kwa hakika tumekujilia na ushahidi wa kimiujiza kutoka kwa Mola wako wenye kuonesha ukweli wetu katika ulinganizi wetu. Na kusalimika na adhabu ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, ni kwa mwenye kuufuata uongofu Wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّا قَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡنَآ أَنَّ ٱلۡعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Mola wako Ametuletea wahyi kwamba adhabu Yake itamshukia aliyekanusha na akaupa mgongo ulinganizi Wake na sheria Yake.’»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَٰمُوسَىٰ
Fir'awn akawaambia wote wawili kwa njia ya kukanusha, «Basi ni nani Mola wenu, ewe Mūsā?»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ رَبُّنَا ٱلَّذِيٓ أَعۡطَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ خَلۡقَهُۥ ثُمَّ هَدَىٰ
Mūsā akamwambia, «Mola wetu ni Yule Ambaye Alikipa kila kitu umbile linalokifaa kulingana na uzuri wa utengezaji Wake kisha akamuongoza kila kiumbe uongofu kamili wa kunufaika kwa kile alichomuumbia Mwenyezi Mungu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ فَمَا بَالُ ٱلۡقُرُونِ ٱلۡأُولَىٰ
Fir'awn akasema kumwambia Mūsā kwa njia ya kukosoa na kuteta, «Mambo yalikuwa vipi kwa ummah waliopita? Na ni vipi habari za kame zilizopita, kwani wao wametutangulia katika ukanushaji na ukafiri?»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَٰبٖۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى
Mūsā alisema kumwambia Fir'awn, «Hilo uliloliuliza halimo kwenye yale tunayoyazungumza, isipokuwa ujuzi wa watu wa hizo kame na mambo waliyoyafanya iko kwa Mola wangu kwenye Kitabu Kilichohifadhiwa (Al-Lawh (al-Mah,fūd) na mimi sina ujuzi nalo. Na Mola wangu Hapotei kwenye vitendo Vyake na hukumu Zake na Hasahau chochote Alichokijua katika hivyo.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مَهۡدٗا وَسَلَكَ لَكُمۡ فِيهَا سُبُلٗا وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّن نَّبَاتٖ شَتَّىٰ
Yeye Ndiye Ambaye Amewafanyia ardhi nyepesi ili mnufaike nayo, na Amewatolea kwenye ardhi hiyo njia nyingi, na Ameteremsha kutoka juu mvua, akaitoa kwayo aina tafauti za mimea.
Arabic explanations of the Qur’an:
كُلُواْ وَٱرۡعَوۡاْ أَنۡعَٰمَكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ
Kuleni, enyi watu, miongoni mwa vizuri tulivyowaoteshea, na muwalishe wanyama howa wenu na wa mstuni. Kwa kweli, katika yote yaliyotajwa pana alama nyingi za uweza wa Mwenyezi Mungu na ni ulinganizi wa umoja Wake na kumpwekesha Yeye kwa kumuabudu kwa wenye akili timamu.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ مِنۡهَا خَلَقۡنَٰكُمۡ وَفِيهَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡهَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ
Kutoka kwenye ardhi tumewaumba nyinyi, enyi watu, na humo tutawarudisha baada ya kufa, na kutoka humo tutawatoa mkiwa hai ili muhisabiwe na mulipwe.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ أَرَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ
Na kwa kweli, tulimuonyesha Fir'awn dalili zetu na hoja zetu zote zenye kujulisha uungu wetu na uweza wetu na ukweli wa ujumbe wa Mūsā, akazikanusha na akakataa kuikubali haki.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ أَجِئۡتَنَا لِتُخۡرِجَنَا مِنۡ أَرۡضِنَا بِسِحۡرِكَ يَٰمُوسَىٰ
Fir'awn akasema, «Je, ewe Mūsā, umetujia ili upate kututoa majumbani mwetu kwa uchawi wako huu?
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَنَأۡتِيَنَّكَ بِسِحۡرٖ مِّثۡلِهِۦ فَٱجۡعَلۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكَ مَوۡعِدٗا لَّا نُخۡلِفُهُۥ نَحۡنُ وَلَآ أَنتَ مَكَانٗا سُوٗى
«Basi tutakuletea uchawi mfano wa uchawi wako. Weka wakati maalumu kati yetu na wewe, ambao sisi tusiende kinyume nao na pia wewe usiende kinyume nao, katika mahali palipolingana palipo sawa kati yetu na wewe.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ مَوۡعِدُكُمۡ يَوۡمُ ٱلزِّينَةِ وَأَن يُحۡشَرَ ٱلنَّاسُ ضُحٗى
Mūsā akasema kumwambia Fir'awm, «Ahadi yenu ya mkusanyiko ni suku ya sikukuu, pindi watu watakapojipamba na kukusanyika kutoka kila sehemu na upande kipindi cha asubuhi.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَتَوَلَّىٰ فِرۡعَوۡنُ فَجَمَعَ كَيۡدَهُۥ ثُمَّ أَتَىٰ
Hapo Fir'awn aliyapa mgongo hali ya kuyapuuza yale ya ukweli aliyoletewa na Mūsā na akawakusanya wachawi wake, na baada yake akaja katika kipindi cha mkusanyiko.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيۡلَكُمۡ لَا تَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا فَيُسۡحِتَكُم بِعَذَابٖۖ وَقَدۡ خَابَ مَنِ ٱفۡتَرَىٰ
Mūsā akasema kuwaambia wachawi wa Fir'awn akiwapa mawaidha, «Jihadharini, msimzulie Mwenyezi Mungu urongo, Asije Akawamaliza nyinyi kwa adhabu itokayo Kwake na Akawaondoa kabisa. Na kwa kweli, amepata hasara mwenye kumzulia Mwenyezi Mungu urongo.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَتَنَٰزَعُوٓاْ أَمۡرَهُم بَيۡنَهُمۡ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّجۡوَىٰ
Hapo wachawi walivutana na wakizungumza kwa siri kuhusu mambo yao. Walisema, «Kwa kweli, Mūsā na Hārūn ni wachawi,
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَٰنِ لَسَٰحِرَٰنِ يُرِيدَانِ أَن يُخۡرِجَاكُم مِّنۡ أَرۡضِكُم بِسِحۡرِهِمَا وَيَذۡهَبَا بِطَرِيقَتِكُمُ ٱلۡمُثۡلَىٰ
wanataka kuwatoa nyinyi nchini mwenu kwa uchawi wao na kuuondoa mfumo mkubwa mnaoushikilia wa uchawi.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَجۡمِعُواْ كَيۡدَكُمۡ ثُمَّ ٱئۡتُواْ صَفّٗاۚ وَقَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡيَوۡمَ مَنِ ٱسۡتَعۡلَىٰ
Basi vithibitisheni vitimbi vyenu na muwe na nia moja juu ya hilo pasi na kutengana kati yenu, kisha njooni mkiwa ni safu moja na mvirushe vilivyomo mikononi mwenu kwa mara moja ili muyashangaze macho ya watu na muushinde uchawi wa Mūsā na ndugu yake. Na kwa kweli, leo amepata matakwa yake yule atakayekuwa juu ya mwenzake akamshinda na akambana.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَلۡقَىٰ
Wachawi wakasema, «Ewe Mūsā! Ima uirushe fimbo yako mwanzo au tuanze sisi kuvirusha tulivyonavyo.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ بَلۡ أَلۡقُواْۖ فَإِذَا حِبَالُهُمۡ وَعِصِيُّهُمۡ يُخَيَّلُ إِلَيۡهِ مِن سِحۡرِهِمۡ أَنَّهَا تَسۡعَىٰ
Mūsā aliwaambia, «Basi rusheni nyinyi mwanzo hivyo mlivyonavyo.« Hapo wakazirusha kamba zao na fimbo zao,
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَوۡجَسَ فِي نَفۡسِهِۦ خِيفَةٗ مُّوسَىٰ
na ikamsawirikia Mūsā kuwa zile ni nyoka wanatembea na akaingiwa na kicho rohoni mwake.
Arabic explanations of the Qur’an:
قُلۡنَا لَا تَخَفۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Mwenyezi Mungu Akamwambia Mūsā wakati huo, «Usiogope chochote, kwani wewe ndiye uliye juu ya hawa wachawi na uliye juu ya Fir'awn na askari wake, na utawashinda.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَلۡقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلۡقَفۡ مَا صَنَعُوٓاْۖ إِنَّمَا صَنَعُواْ كَيۡدُ سَٰحِرٖۖ وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّاحِرُ حَيۡثُ أَتَىٰ
«Na irushe fimbo yako iliyoko kwenye mkono wako wa kulia, itazimeza kamba zao na fimbo zao, kwani walichokifanya mbele yako si chochote isipokuwa ni vitimbi vya mchawi na kiinimacho cha uchawi. Na hafaulu mchawi kwa uchawi wake popote anapokuwa.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سُجَّدٗا قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ هَٰرُونَ وَمُوسَىٰ
Hapo Mūsā aliirusha fimbo yake, ikavimeza walivyovifanya, haki ikajitokeza na hoja ikasimama juu yao. Hapo wachawi walijitupa chini wakiwa katika hali ya kusujudu na wakasema, «Tumemuamini Mola wa Hārūn na Mūsā. Lau huu ulikuwa ni uchawi hatungalishindwa.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ ءَامَنتُمۡ لَهُۥ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِي عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحۡرَۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمۡ فِي جُذُوعِ ٱلنَّخۡلِ وَلَتَعۡلَمُنَّ أَيُّنَآ أَشَدُّ عَذَابٗا وَأَبۡقَىٰ
Fir'awn akasema kuwaambia wachawi, «Mumemkubali vipi Mūsā, mkamfuata na mkamtambua kabla sijawaruhusu kufanya hivyo? Kwa kweli, Mūsā ndiye mkubwa wenu aliyewafundisha uchawi, kwa hivyo mumemfuata. Basi nitaikatakata mikono yenu na miguu yenu kinyume: mkono wa upande huu na mguu wa upande mwingine, na nitawasulubu kwa kuifunga miili yenu kwenye vigogo vya mitende. Na hapo mtajua, tena mtajua, enyi wachawi, ni yupi kati yetu, ni mimi au Mola wa Mūsā, mwenye adhabu kali zaidi na yenye kudumu zaidi kuliko mwingine?»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ لَن نُّؤۡثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلَّذِي فَطَرَنَاۖ فَٱقۡضِ مَآ أَنتَ قَاضٍۖ إِنَّمَا تَقۡضِي هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَآ
wachawi wakasema kumwambia Fir'awn,« Hatutakutanguliza wewe tukakusikiliza na tukaifuata dini yako juu ya yale aliyotuletea Mūsā yaliyo waziwazi yanayojulisha ukweli wake na ulazima wa kumfuata na kumtii Mola wake. Na hatutautanguliza uola wako wa kujipangia juu ya uola wa Mwenyezi Mungu Aliyetuumba. Basi fanya kile utakachotufanya. Ukweli ni kwamba utawala wako ni hapa katika maisha ya duniani. Na utakachokifanya kwetu si kitu isipokuwa ni adhabu itakayokoma kwa kukoma dunia hii.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّآ ءَامَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغۡفِرَ لَنَا خَطَٰيَٰنَا وَمَآ أَكۡرَهۡتَنَا عَلَيۡهِ مِنَ ٱلسِّحۡرِۗ وَٱللَّهُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ
«Kwa kweli, sisi tumemuamini Mola wetu, tumemkubali Mtume Wake na tumeyatumia aliyokuja nayo ili Mola wetu Atusamehe dhambi zetu na yale uliyotulazimisha nayo ya kufanya uchawi wa kupingana na Mūsā. Na Mwenyezi Mungu ni bora kwetu kuliko wewe, ewe Fir'awn, kwa kumlipa aliyemtii na ni mwenye adhabu ya kudumu zaidi kwa anayemuasi na kuenda kinyume na amri Yake.»
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّهُۥ مَن يَأۡتِ رَبَّهُۥ مُجۡرِمٗا فَإِنَّ لَهُۥ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ
Ukweli wa mambo ni kwamba mwenye kumjia Mola wake hali ya kuwa amemkanusha, basi atapata moto wa Jahanamu atakaoteswa nao; hatakufa humo akapumzika wala hataishi maisha ambayo atayafurahia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَأۡتِهِۦ مُؤۡمِنٗا قَدۡ عَمِلَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلدَّرَجَٰتُ ٱلۡعُلَىٰ
Na mwenye kumjia Mola wake hali ya kuwa amemuamini na ametenda matendo mema, basi atapata daraja za juu
Arabic explanations of the Qur’an:
جَنَّٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ مَن تَزَكَّىٰ
katika mabustani ya Pepo ya kukaa daima ambayo mito inapita chini ya miti yake, wakiwa ni wenye kukaa humo milele. Neema hiyo ya daima ni malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mwenye kujisafisha nafsi yake na uchafu, uovu na ushirikina, na akamuabudu Mwenyezi Mungu, Peke Yake, akamtii na akajiepusha na matendo ya kumuasi na akakutana na Mola wake na huku hamshirikishi yoyote kati ya viumbe Vyake katika kumuabudu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَسۡرِ بِعِبَادِي فَٱضۡرِبۡ لَهُمۡ طَرِيقٗا فِي ٱلۡبَحۡرِ يَبَسٗا لَّا تَخَٰفُ دَرَكٗا وَلَا تَخۡشَىٰ
Na kwa hakika tulimpelekea wahyi Mūsā tukamwambia, «Toka Misri usiku ukiwa pamoja na waja wangu miongoni mwa Wana wa Isrāīl, na uwatolee njia kavu baharini, bila kumuogopa Fir'awn na askari wake kuwa watawaandama na kuwakuta na bila ya kuogopa kuzama.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ بِجُنُودِهِۦ فَغَشِيَهُم مِّنَ ٱلۡيَمِّ مَا غَشِيَهُمۡ
Basi Mūsā alikwenda usiku pamoja na Wana wa Isrāīl akavuka nao kwenye njia ya bahari, hapo Fir'awn pamoja na askari wake wakawafuata, maji yakawafinika, kwa namna ambayo hakuna anayoijua isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wote walizama isipokuwa Mūsā na watu wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَضَلَّ فِرۡعَوۡنُ قَوۡمَهُۥ وَمَا هَدَىٰ
Na aliwapoteza Fir'awn watu wake kwa ukafiri aliyowapambia na ukanushaji, na hakuwafanya waandame njia ya uongofu.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ قَدۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ عَدُوِّكُمۡ وَوَٰعَدۡنَٰكُمۡ جَانِبَ ٱلطُّورِ ٱلۡأَيۡمَنَ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰ
Enyi Wana wa Isrāīl, kumbukeni tulipowaokoa na adui yenu Fir'awn na tukafanya agano lenu ni upande wa kulia wa jabali la Tūr ili muteremshiwe Taurati, na tutukawateremshia jangwani vitu vya nyinyi kuvila vinavyofanana na gundi vyenye utamu wa asali, na ndege wanaofanana na tomboro.
Arabic explanations of the Qur’an:
كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ وَلَا تَطۡغَوۡاْ فِيهِ فَيَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبِيۖ وَمَن يَحۡلِلۡ عَلَيۡهِ غَضَبِي فَقَدۡ هَوَىٰ
Kuleni riziki yetu nzuri na msifanye uadui kwa kuoneana nyinyi kwa nyinyi, kwani mkifanya hivyo hasira zangu zitawashukia, na yoyote mwenye kushukiwa na hasira zangu, basi yeye ameangamia na amepata hasara.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنِّي لَغَفَّارٞ لِّمَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا ثُمَّ ٱهۡتَدَىٰ
Na mimi ni Mwingi wa kusamehe kwa anayetubia kutokana na dhambi zake na ukanushaji wake, akaniamini mimi na akafanya matendo mema kisha akaongoka kufuata njia ya ukweli na akasimama imara juu yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَمَآ أَعۡجَلَكَ عَن قَوۡمِكَ يَٰمُوسَىٰ
Na ni kitu gani kilichokuharakisha, ewe Mūsā, ukawatangulia watu wako kwenda upande wa kulia wa jabali la Tūr na ukawaacha nyuma yako?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ هُمۡ أُوْلَآءِ عَلَىٰٓ أَثَرِي وَعَجِلۡتُ إِلَيۡكَ رَبِّ لِتَرۡضَىٰ
Akasema, «Wao wako nyuma yangu watanifikia. Na nimewatangulia kuja kwako, ewe Mola wangu, ili uridhike na mimi.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ فَإِنَّا قَدۡ فَتَنَّا قَوۡمَكَ مِنۢ بَعۡدِكَ وَأَضَلَّهُمُ ٱلسَّامِرِيُّ
Mwenyezi Mungu akasema kumwambia Mūsā, «Hakika sisi tumewatahini watu wako, baada ya wewe kuwaepuka, kwa kuabudu kigombe, na Sāmirīy amewapoteza.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَرَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ أَلَمۡ يَعِدۡكُمۡ رَبُّكُمۡ وَعۡدًا حَسَنًاۚ أَفَطَالَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡعَهۡدُ أَمۡ أَرَدتُّمۡ أَن يَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَخۡلَفۡتُم مَّوۡعِدِي
Hapo Mūsā akarudi kwa watu wake akiwa ni mwenye hasira na masikitiko na akawaambia, «Enyi watu wangu, Si Mwenyezi Mungu Amewaagiza agizo zuri la kuiteremsha Taurati? Kwani hiyo ahadi imepitiwa na kipindi kirefu mkaona kuwa agizo limechelewa au mlitaka kufanya jambo ambalo kwalo zitawashukia hasira kutoka kwa Mola wenu ndipo mkaenda kinyume na agizo langu nililowaahidi, mkaabudu kigombe na mkaacha kujilazimisha na amri zangu?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ مَآ أَخۡلَفۡنَا مَوۡعِدَكَ بِمَلۡكِنَا وَلَٰكِنَّا حُمِّلۡنَآ أَوۡزَارٗا مِّن زِينَةِ ٱلۡقَوۡمِ فَقَذَفۡنَٰهَا فَكَذَٰلِكَ أَلۡقَى ٱلسَّامِرِيُّ
Wakasema, «Ewe Mūsā, sisi hatukwenda kinyume na agizo lako la kutuchagua, lakini sisi tulibebeshwa mizigo mizito ya pambo la watu wa Fir'awn, tukaitupa kwenye shimo lenye moto kwa amri ya Sāmirīy, na pia Sāmirīy alitupa mchanga aliokuwa nao wa kwato za farasi wa Jibrili, amani imshukiye.»
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَخۡرَجَ لَهُمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٞ فَقَالُواْ هَٰذَآ إِلَٰهُكُمۡ وَإِلَٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ
Hivyo basi Sāmirīy aliwatengenezea Wana wa Isrāīl kutokana na dhahabu kigombe ambacho ni mwili unaotoa sauti ya ng’ombe. Hapo wakasema waliofitinika nacho , «Huyu ndiye mola wenu na mola wa Mūsā aliyemsahau na kughafilika naye.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَفَلَا يَرَوۡنَ أَلَّا يَرۡجِعُ إِلَيۡهِمۡ قَوۡلٗا وَلَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا
Je, hawaoni hawa walioabudu kigombe kwamba hicho hakianzi kusema nao wala hakiwapi jawabu na hakiwezi kuwaondolea madhara wala kuwaletea manufaa?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ قَالَ لَهُمۡ هَٰرُونُ مِن قَبۡلُ يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِۦۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَٱتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوٓاْ أَمۡرِي
Kwa kweli, Hārūn aliwaambia Wana wa Isrāīl kabla Mūsā hajarudi kuwajia, «Enyi watu wangu, hakika nyinyi mumetahiniwa na huyu kigombe, ili aonekana wazi mwenye Imani miongoni mwenu apate kujitenga na mwenye kukanusha. Kwa hakika Mola wenu ni Al-Rahmān (Mwingi wa Rehema) si mwingine. Basi nifuateni katika lile ninalowaitia la kumuabudu Mwenyezi Mungu na muitii amri yangu katika kufuata sheria Yake.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالُواْ لَن نَّبۡرَحَ عَلَيۡهِ عَٰكِفِينَ حَتَّىٰ يَرۡجِعَ إِلَيۡنَا مُوسَىٰ
Walisema wenye kuabudu kigombe miongoni mwao, «Hatutaacha kusimama kukiabudu kigombe mpaka Mūsā arudi kwetu.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَٰهَٰرُونُ مَا مَنَعَكَ إِذۡ رَأَيۡتَهُمۡ ضَلُّوٓاْ
Mūsā akasema kumwambia ndugu yake Hārūn, «Ni jambo gani lililokuzuia ulipowaona wamepotea na kuwa kando na Dini yao
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَّا تَتَّبِعَنِۖ أَفَعَصَيۡتَ أَمۡرِي
usinifuate ukawa na mimi na ukawaacha? Je, umeasi amri yangu niliyokuamrisha kwayo ya kushika mahali pangu na kutengeneza baada ya mimi kuondoka?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ يَبۡنَؤُمَّ لَا تَأۡخُذۡ بِلِحۡيَتِي وَلَا بِرَأۡسِيٓۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقۡتَ بَيۡنَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَمۡ تَرۡقُبۡ قَوۡلِي
Kisha Mūsā alishika ndevu za Hārūn na kichwa chake akawa amvuta upande wake. Hārūn akamwambia, «Ewe mwana wa mamangu, usinishike ndevu zangu wala nywele za kichwa changu! Mimi niliogopa, lau niliwaacha na nikakutana na wewe, usije ukasema, «Umewagawanya Wana wa Isrāīl na hukutunza wasia wangu wa kukaa nao vizuri.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ فَمَا خَطۡبُكَ يَٰسَٰمِرِيُّ
Mūsā akasema kumwambia Sāmirīy, «Una jambo gani, ewe Sāmirīy? Na ni lipi lililokupelekea kufanya hilo ulilolifanya?
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ بَصُرۡتُ بِمَا لَمۡ يَبۡصُرُواْ بِهِۦ فَقَبَضۡتُ قَبۡضَةٗ مِّنۡ أَثَرِ ٱلرَّسُولِ فَنَبَذۡتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتۡ لِي نَفۡسِي
Sāmirīy akasema, «Nilimuona ambaye hawakumuona, naye ni Jibrili, amani imshukiye, juu ya farasi, wakati walipotoka baharini na Fir'awn akazamishwa na askari wake, hapo niliteka kwa kitanga changu cha mkono mchanga wa athari ya kwato za farasi wa Jibrili nikaurusha kwenye pambo ambalo kwalo nimetengeneza kigombe, kikawa ni kigombe chenye mwili, chenye kutoa sauti ya ng’ombe, na kikawa ni kisirani na mtihani. Kufanya hivyo ndivyo nafsi yangu inayoamrisha maovu ilivyonipambia.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ فَٱذۡهَبۡ فَإِنَّ لَكَ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَۖ وَإِنَّ لَكَ مَوۡعِدٗا لَّن تُخۡلَفَهُۥۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰٓ إِلَٰهِكَ ٱلَّذِي ظَلۡتَ عَلَيۡهِ عَاكِفٗاۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُۥ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُۥ فِي ٱلۡيَمِّ نَسۡفًا
Mūsā akasema kumwambia Sāmirīy, «Basi enda! Mateso yako katika uhai wa duniani ni uishi ukiwa umetengwa na umwambie kila mtu, ‘ Sigusi wala siguswi’, na una agizo huko Akhera la wewe kuadhibiwa na kuteswa, Mwenyezi Mungu Hataenda kinyume na agizo hilo na utalikuta. Na muangalie muabudiwa wako ambaye umesimama kumuabudu, tutamchoma kwa moto kisha tutampeperusha baharini achukuliwe na upepo kusiwe na athari yake yoyote yenye kusalia.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّمَآ إِلَٰهُكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَسِعَ كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمٗا
Kwa kweli, mola wenu, enyi watu, ni Mola Mmoja Ambaye hakuna muabudiwa isipokuwa Yeye, ujuzi Wake umeenea kila kitu.
Arabic explanations of the Qur’an:
كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ مَا قَدۡ سَبَقَۚ وَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ مِن لَّدُنَّا ذِكۡرٗا
Na kama tulivyokusimulia, ewe Mtume, habari za Mūsā na Fir'awn na watu wao, tunakupa habari za waliokutangulia wewe. Na tumekuletea hii Qur’ani kutoka kwetu iwe ni ukumbusho kwa mwenye kujikumbusha.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّنۡ أَعۡرَضَ عَنۡهُ فَإِنَّهُۥ يَحۡمِلُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وِزۡرًا
Mwenye kuipa mgongo hii Qur’ani, asiiamini na asiitumie, atakuja Siku ya Kiyama akiwa amebeba dhambi kubwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
خَٰلِدِينَ فِيهِۖ وَسَآءَ لَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ حِمۡلٗا
Hao watakaa milele kwenye adhabu, na utawakera mzigo huo mzito wa madhambi kwa kuwa umewatia Motoni.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ وَنَحۡشُرُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ يَوۡمَئِذٖ زُرۡقٗا
Siku Malaika watakapovuvia kwenye pembe ili kutoa ukulele wa kufufuliwa na tuwaongoze makafiri siku hiyo wakiwa rangi ya buluu, miili yao imegeuka na pia macho yao kwa matukio makubwa yaliyojiri.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَتَخَٰفَتُونَ بَيۡنَهُمۡ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا عَشۡرٗا
Huku wakinong’onezana baina yao na wakiambiana wao kwa wao, «Hamkukaa kwenye uhai wa ulimwenguni isipokuwa siku kumi.
Arabic explanations of the Qur’an:
نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذۡ يَقُولُ أَمۡثَلُهُمۡ طَرِيقَةً إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا يَوۡمٗا
Sisi ni wajuzi zaidi kwa wanayoyasema na wanayoyaficha pindi anaposema mjuzi wao zaidi na mwenye akili nyingi miongoni mwao, «Hamkuishi isipokuwa siku moja,» kwa ufupi wa kipindi cha duniani watakaouhisi ndani ya nafsi zao Siku ya Kiyama.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡجِبَالِ فَقُلۡ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسۡفٗا
Na wanakuuliza watu wako, ewe Mtume, kuhusu hatima ya majabali Siku ya Kiyama. Basi waambie, «Mola wangu Atayaondoa mahali pake na atyafanya ni vumbi lililopeperushwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَيَذَرُهَا قَاعٗا صَفۡصَفٗا
«Aiwache ardhi wakati huo imetandazika, imelingana na imekuwa kavu haina mimea.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجٗا وَلَآ أَمۡتٗا
Mwenye kuiangalia haoni, kwa kulingana kwake, mbeteko wala muinuko wala mteremko.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَئِذٖ يَتَّبِعُونَ ٱلدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُۥۖ وَخَشَعَتِ ٱلۡأَصۡوَاتُ لِلرَّحۡمَٰنِ فَلَا تَسۡمَعُ إِلَّا هَمۡسٗا
Katika siku hiyo, watu wataifuata sauti ya mlinganizi kuelekea kwenye kisimamo cha Kiyama, hakuna njia ya kuepuka ulinganizi wa mwenye kulingania, kwani huo ni haki na kweli kwa viumbe wote. Hapo sauti zitatulia kwa kumnyenyekea Mwingi wa rehema, hutasikia kutoka kwao isipokuwa sauti ya ndani isiyosikika.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَئِذٖ لَّا تَنفَعُ ٱلشَّفَٰعَةُ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَرَضِيَ لَهُۥ قَوۡلٗا
Katika siku hiyo, hayatamfaa maombezi kiumbe yoyote, mpaka iwapo Mwingi wa rehema Ataruhusu na Ataridhika na mwenye kuombewa, na hiyo haiwi isipokuwa kwa mwenye Imani mwenye ikhlasi.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِۦ عِلۡمٗا
Anayajuwa mambo ya Kiyama yaliyoko mbele ya watu na mambo ya dunia yaliyoko nyuma yao, na viumbe Vyake hawamzunguki kwa kumjua, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَعَنَتِ ٱلۡوُجُوهُ لِلۡحَيِّ ٱلۡقَيُّومِۖ وَقَدۡ خَابَ مَنۡ حَمَلَ ظُلۡمٗا
Na nyuso za viumbe zitamnyenyekea na kumdhalilikia mwenye kuziumba, Mwenye kila maana ya uhai mkamilifu kama inavyonasibiana na utukufu Wake, Ambaye Hafi , Anayesimama kuendesha kila kitu, Aliye Mkwasi wa kutomuhitajia asiyekuwa Yeye. Kwa kweli, amepata hasara Siku ya Kiyama mwenye kumfanya ni mshirika wa Mwenyezi Mungu yoyote kati ya viumbe Vyake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَا يَخَافُ ظُلۡمٗا وَلَا هَضۡمٗا
Na mwenye kufanya matendo mema na hali yeye anamuamini Mola wake, hataogopa maonevu ya kuongezwa maovu yake wala unyanyasaji wa kupunguziwa mema yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا وَصَرَّفۡنَا فِيهِ مِنَ ٱلۡوَعِيدِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ أَوۡ يُحۡدِثُ لَهُمۡ ذِكۡرٗا
Na kama tulivyowapendekezea wenye Imani kufanya matendo mema na tukawaonya makafiri kuendelea kwenye maasia yao na ukanushaji wao aya zetu, tuliiteremsha hii Qur’an kwa lugha ya Kiarabu wapate kuielewa. Na tumefafanua ndani yake aina za maonyo kwa matarajio wamuogope Mola wao, au hii Qur’ani iwaletee ukumbusho wapate kuwaidhika na kuzingatia.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُۥۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِي عِلۡمٗا
Ameepukana Mwenyezi Mungu, kutakata ni Kwake, na Amekuwa juu na ametakasika na kila upungufu, Aliye Mfalme Ambaye mamlaka Yake yamemtendesha nguvu kila mfalme na mjeuri, Mwenye kuendesha kila kitu, Ambaye Yeye Ndiye ukweli, na agizo Lake ni kweli, na onyo Lake ni kweli, na kila kitu kinachotoka Kwake ni kweli. Na usifanye haraka, ewe Mtume, ya kushindana na Jibrili katika kuipokea Qur’ani kabla hajaimaliza, na useme, «Mola wangu! Niongezee elimu juu ya ile uliyonifundisha.»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَقَدۡ عَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ ءَادَمَ مِن قَبۡلُ فَنَسِيَ وَلَمۡ نَجِدۡ لَهُۥ عَزۡمٗا
Na kwa hakika tulimuusia Ādam kabla hajakula kutoka kwenye ule mti, asile kutoka kwenye mti huo na tukamwambia kwamba Iblisi ni adui yako na mke wako, basi wasiwatoe nyinyi wawili kutoka Peponi, mkajasumbuka wewe na mke wako duniani. Basi Shetani akamshawishi, naye akamtii na akausahau wasia. Na hatukumpata na nia ya nguvu yenye kumfanya aitunze ile amri aliyopewa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tuliposema kuwaambia Malaika, «Msujudieni Ādam sijida ya maamkizi na kutoa heshima, nao wakatii na wakasujudu, lakini Iblisi alikataa kusujudu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَقُلۡنَا يَٰٓـَٔادَمُ إِنَّ هَٰذَا عَدُوّٞ لَّكَ وَلِزَوۡجِكَ فَلَا يُخۡرِجَنَّكُمَا مِنَ ٱلۡجَنَّةِ فَتَشۡقَىٰٓ
Tukasema, «Ewe Ādam! Kwa hakika, huyu Iblisi ni adui yako na mke wako, basi jihadharini naye na msimtii kwa kuniasi mimi, asije akawatoa Peponi ukasumbuka ukitolewa humo.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعۡرَىٰ
Hakika yako wewe, ewe Ādam, una neema ya kula kwenye Pepo hii na hutashikwa na njaa, na pia kuvaa na hutakaa tupu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَنَّكَ لَا تَظۡمَؤُاْ فِيهَا وَلَا تَضۡحَىٰ
na una neema ya kutoshikwa na kiu katika hii Pepo na kutopatwa na joto la jua.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَوَسۡوَسَ إِلَيۡهِ ٱلشَّيۡطَٰنُ قَالَ يَٰٓـَٔادَمُ هَلۡ أَدُلُّكَ عَلَىٰ شَجَرَةِ ٱلۡخُلۡدِ وَمُلۡكٖ لَّا يَبۡلَىٰ
Hapo Shetani akamshawishi Ādam na akamwambia, «Je, nikushauri kwa kukuonesha mti ambao lau utakula kutoka mti huo utakaa milele na hutakufa na utakuwa na ufalme usiokoma na usiokatika?
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَكَلَا مِنۡهَا فَبَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۚ وَعَصَىٰٓ ءَادَمُ رَبَّهُۥ فَغَوَىٰ
Basi Ādam na Ḥawwā’ wakala kutoka kwenye mti ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza nao, na papo hapo tupu zao zikafunuka, na kabla ya hapo zilikuwa zimesitiriwa na macho yao hayazioni. Hapo wakawa wanakata majani ya miti ya Peponi na kujiambisa nayo ili kufinika tupu zao zilizowafunuka. Na Ādam alienda kinyume na amri ya Mola wake na akapotea kwa kula kutoka kwenye mti ambao Mwenyezi Mungu Alimkataza asiukaribie.
Arabic explanations of the Qur’an:
ثُمَّ ٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَتَابَ عَلَيۡهِ وَهَدَىٰ
Kisha Mwenyezi Mungu Akamteua Ādam, Akamkaribisha, Akaikubali toba yake na Akamuongoza njia njema ya kuifuata.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ ٱهۡبِطَا مِنۡهَا جَمِيعَۢاۖ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَنِ ٱتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشۡقَىٰ
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akamwambia Ādam na Ḥawwā’ «Shukeni kutoka kwenye Pepo muende ardhini nyote pamoja na Iblisi, kwani nyinyi na yeye ni maadui. Mtakapojiwa na uongofu na maelezo kutoka kwangu, basi mwenye kufuata uongofu wangu na maelezo yangu na akayatumia yote mawili, yeye atakuwa amefuata usawa duniani na ataongoka, na hatasumbuka huko Akhera kwa kuteswa na Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِكۡرِي فَإِنَّ لَهُۥ مَعِيشَةٗ ضَنكٗا وَنَحۡشُرُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَعۡمَىٰ
Na mwenye kuupa mgongo utajo wangu ambao ninamkumbusha nao, atakuwa na maisha ya dhiki na usumbufu katika uhai wa kilimwengu, hata kama inaonekana kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa utajiri na nafasi, na kaburi yake itambana na aadhibiwe humo, na tutamfufua Siku ya Kiyama akiwa kipofu wa kutoona na wa hoja.
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرۡتَنِيٓ أَعۡمَىٰ وَقَدۡ كُنتُ بَصِيرٗا
Atasema huyo mwenye kuupa mgongo utajo wa Mwenyezi Mungu , «Mola wangu! Kwa nini umenifufua nikiwa kipofu na hali nilikuwa nikiona duniani?»
Arabic explanations of the Qur’an:
قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتۡكَ ءَايَٰتُنَا فَنَسِيتَهَاۖ وَكَذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمَ تُنسَىٰ
Mwenyezi Mungu Atasema kumwambia, «Nimekufufua ukiwa kipofu, kwa kuwa wewe zilikujia aya zetu zikiwa na hoja waziwazi, ukazipa mgongo na usiziamini. Na kama ulivyoziacha ulimwenguni, basi leo vilevile utaachwa Motoni.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَنۡ أَسۡرَفَ وَلَمۡ يُؤۡمِنۢ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦۚ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبۡقَىٰٓ
«Hivyo ndivyo tutakavyomtesa, kwa mateso ya hapa duniani, yule aliyepita kiasi katika kujidhulumu nafsi yake akamuasi Mola wake na asiziamini aya zake. Na kwa kweli, adhabu ya kesho Akhera waliyoandaliwa ina uchungu mkali zaidi na inadumu na kujikita zaidi, kwa kuwa haikatika na haimaliziki.»
Arabic explanations of the Qur’an:
أَفَلَمۡ يَهۡدِ لَهُمۡ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ يَمۡشُونَ فِي مَسَٰكِنِهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ
Kwani haukuwaongoza watu wako kwenye njia ya sawa, Ewe mtume, ule wingi watu waliokanusha kabala yao tuliowaangamiza na hali wao wanatembea kwenye nyumba zao na wanaziona athari za kuangamia kwao? Kwa hakika, katika wingi wa watu hao na mabaki ya adhabu waliyopewa pana mazingatio na mawaidha kwa wenye akili za kuelewa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَكَانَ لِزَامٗا وَأَجَلٞ مُّسَمّٗى
Na lau si neno litokalo kwa Mola wako na muda uliotajwa mbele Yake, wangalipata maangamivu yenye kulazimiana na wao hapa ulimwenguni, kwa kuwa wao wanastahili kuyapata kwa sababu ya ukafiri wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ غُرُوبِهَاۖ وَمِنۡ ءَانَآيِٕ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡ وَأَطۡرَافَ ٱلنَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرۡضَىٰ
Basi vumilia, ewe Mtume, juu ya yale wanayoyasema wakanushaji kuhusu wewe ya sifa mbaya na urongo, umtakase Mola wako kwa kumshukuru katika Swala ya alfajiri kabla jua halijachomoza, na katika Swala ya alasiri kabla ya jua kuzama, na katika Swala ya ishai nyakati za usiku, na umtakase Mola wako kwa kumshukuru katika Swala ya adhuhuri, kwani kipindi chake kiko nchani mwa nusu ya kwanza ya mchana na nusu ya pili, na katika Swala ya magaribi, ili ulipwe kwa matendo haya kwa namna ambayo utaridhika nayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ زَهۡرَةَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا لِنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَرِزۡقُ رَبِّكَ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰ
Na usivitazame vitu ambavyo tumewastarehesha navyo hawa washirikina na wanaofanana na wao miongoni mwa aina ya starehe. Kwani hivyo ni pambo lenye kuondoka katika uhai huu wa kilimwengu. Tumewastarehesha navyo,ili tuwatahini navyo. Na riziki ya Mola wako na malipo yake ni bora kwako kuliko hivyo tulivyowastarehesha navyo na ni vya kudumu zaidi, kwani havina kukatika wala kumalizika.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأۡمُرۡ أَهۡلَكَ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱصۡطَبِرۡ عَلَيۡهَاۖ لَا نَسۡـَٔلُكَ رِزۡقٗاۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكَۗ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلتَّقۡوَىٰ
Na waamrishe watu wako, ewe Nabii, kuswali na ujisubirishe nayo. Sisi hatutaki kutoka kwako mali, kwani sisi ndio tunaokuruzuku na kukupa. Na mwisho mwema ulimwenguni na Akhera ni wa wachajimungu
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَالُواْ لَوۡلَا يَأۡتِينَا بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّهِۦٓۚ أَوَلَمۡ تَأۡتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ
Na walisema wenye kukukanusha, ewe Mtume, «Basi si utuletee alama itokayo kwa Mola wako yenye kuonesha ukweli wako?» Kwani hikuwajia hii Qur’ani yenye kuisadukisha haki iliyomo kwenye Vitabu vilivyopita?»
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَوۡ أَنَّآ أَهۡلَكۡنَٰهُم بِعَذَابٖ مِّن قَبۡلِهِۦ لَقَالُواْ رَبَّنَا لَوۡلَآ أَرۡسَلۡتَ إِلَيۡنَا رَسُولٗا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ مِن قَبۡلِ أَن نَّذِلَّ وَنَخۡزَىٰ
Na lau sisi tuliwaangamiza wenye kukanusha kwa adhabu kabla hatujawapelekea Mtume na kuwateremshia Kitabu, wanagalisema, «Mola wetu! Si utuletee Mtume kutoka kwako tupate kumuamini na tufuate aya zako na Sheria yako, kabla ya sisi kudhalilika na kuhizika kwa adhabu yako.»
Arabic explanations of the Qur’an:
قُلۡ كُلّٞ مُّتَرَبِّصٞ فَتَرَبَّصُواْۖ فَسَتَعۡلَمُونَ مَنۡ أَصۡحَٰبُ ٱلصِّرَٰطِ ٱلسَّوِيِّ وَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ
Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, «Kila mmoja kati yetu sisi na nyinyi anagojea matukio ya ulimengu na ni nani atakayepata ushindi na kufaulu. Basi ngojeni, mtajua ni watu gani walioko kwenye njia iliyokaa sawa na nani, kati yetu sisi na nyinyi, aliyeongoka kwenye haki.»
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: Tā-ha
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis Abdurahman - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Dr. Abdalla Mohamed Abubakar and Nassor Khamis

close