Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Alberwany * - Translations’ Index

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Translation of the meanings Surah: An-Nisā’   Ayah:

Surat An-Nisa

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ ٱتَّقُواْ رَبَّكُمُ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَخَلَقَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا وَبَثَّ مِنۡهُمَا رِجَالٗا كَثِيرٗا وَنِسَآءٗۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِي تَسَآءَلُونَ بِهِۦ وَٱلۡأَرۡحَامَۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَيۡكُمۡ رَقِيبٗا
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni.
Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na kutokana na nafsi hiyo akamuumba mkewe, na kutokana na hao wawili, wakaenea wanaume na wanawake wengi. Basi nyote mnatokana na nafsi moja. Mcheni Mwenyezi Mungu mnaye mtaka msaada kwa kila mnacho kihitajia, na kwa jina lake ndio mnaombana nyinyi kwa nyinyi katika mambo yenu. Pia tahadharini na kuacha kuwasaidia jamaa zenu, wa karibu na wa mbali. Kwani Mwenyezi Mungu daima anakuangalieni. Hapana chochote katika mambo yenu kinacho fichikana kwake. Na Yeye ndiye Mwenye kukulipeni.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَءَاتُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰٓ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَتَبَدَّلُواْ ٱلۡخَبِيثَ بِٱلطَّيِّبِۖ وَلَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَهُمۡ إِلَىٰٓ أَمۡوَٰلِكُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ حُوبٗا كَبِيرٗا
Na wapeni mayatima mali yao. Wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika yote hayo ni jukumu kubwa.
Na wapeni mayatima mali yao wanayo stahiki, na yalindeni mali yao vizuri, wala msiwape kilio duni mkawanyima kizuri. Wala msichukue mali yao mkaongezea kwenye mali yenu. Hakika kitendo hicho ni dhambi kubwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنۡ خِفۡتُمۡ أَلَّا تُقۡسِطُواْ فِي ٱلۡيَتَٰمَىٰ فَٱنكِحُواْ مَا طَابَ لَكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ مَثۡنَىٰ وَثُلَٰثَ وَرُبَٰعَۖ فَإِنۡ خِفۡتُمۡ أَلَّا تَعۡدِلُواْ فَوَٰحِدَةً أَوۡ مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۚ ذَٰلِكَ أَدۡنَىٰٓ أَلَّا تَعُولُواْ
Na ikiwa mnaogopa kuwa hamtowafanyia mayatima uadilifu, basi oeni mnao wapenda katika wanawake, wawili au watatu au wane. na mkiogopa kuwa hamwezi kufanya uadilifu, basi mmoja tu, au wale ambao mikono yenu ya kulia imewamiliki. Kufanya hivi ndiko kutapelekea msikithirishe wana.
Ilivyo kuwa mnakhofu kuwadhulumu mayatima kwa kuwa hiyo ni dhambi kubwa, basi kadhaalika khofuni machungu ya wake zenu kwa kuacha kuwafanyia uadilifu baina yao, na kuzidisha juu ya wane. Basi mnaweza kuoa wawili, au watatu, au wane, ikiwa mna imani kuwa mtaweza kufanya uadilifu. Mkiogopa kuwa hamtaweza kufanya uadilifu basi oeni mmoja tu, au jitoshelezeni na wajakazi walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hayo ni afadhali kuliko kwenda kuingia katika dhulma na ujeuri . Na ni afadhali msije mkawa na watoto wengi bila ya kiasi hata mshindwe kuwatazama. (Wafasiri wengi wamependelea kufasiri "Alla Tau'luu" kuwa "Kutofanya jeuri au dhulma." Lakini hii AL MUNTAKHAB imekhiari tafsiri hii ya "msikithirishe wana", ambayo ndiyo aliyo ifuata Imam Shaafii r.a., naye alitanguliwa na Maimamu wanazuoni wa Kiislamu, Zayd bin Aslam r.a.na Jabir bin Zayd r.a. kama alivyo simulia Daar Qut'ni, na imetajwa katika Tafsir ya Qurt'uby juzuu ya 5 sahifa 22.) Sharia ya Kiislamu si peke yake inayo ruhusu kuoa wake wengi, miongoni mwa sharia za dini za mbinguni. Sharia ya Taurati inamruhusu mwanamume kuoa idadi ya wanawake atakao. Na imetaja kuwa Manabii walikuwa wakioa wake kwa makumi na makumi. Na Taurati ni katika Agano la Kale la Biblia ambalo linafuatwa pia na Wakristo katika mambo ambayo hayakukatazwa katika Injili au Barua za Mitume. Na hakika iliopo ni kuwa hapana popote katika Agano Jipya panapo pinga sharia hiyo ya kuruhusu kuoa wake zaidi ya mmoja. Kanisa katika Karne za Kati liliruhusu hayo, na wafalme wa Ulaya wa Kikristo walio kuwa na wake wengi ni maarufu katika taarikh (historia). Khitilafu iliyopo ni kuwa Uislamu ndiyo dini ya kwanza kuweka idadi maalumu, isipindukiwe. Imeweka kiwango kwa mambo matatu. (Kwanza) wasipindukie hao wake kuliko wane. (Pili) asidhulumike mmoja katika hao wake, (Tatu) awe mtu anaweza kuwakimu hao wake. Shuruti mbili za mwisho zimelazimu kila ndoa, ijapokuwa ni ya kwanza. Wanazuoni wa Kiislamu wa sharia na wanga khitalifiana wanakubaliana pamoja kuwa mume ambaye anajua kuwa hawezi kuwafanyia uadilifu wakeze ni haramu kwake kidini kuongeza wake. Ila uharamu huu ni wa kidini, watawala na mahakimu hawawezi kumuingilia. Kwani uadilifu ni jambo la nafsi yake mtu, na dhamiri yake, na uwezo wa kutazama ni jambo la mnasaba halifungamani na mizani mojapo. Ni yeye mwenyewe atakaye pata adhabu Siku ya Kiyama akikhalifu amri hiyo. Dhulma au kutokuweza kukimu kunategemea hali ya siku zijazo, na mikataba haifungamani na mambo ambayo huenda yakawa au yasiwe, bali ni juu ya yaliyoko, na ilivyo kuwa dhaalimu huenda akawa muadilifu, na asiye weza sasa hueza akaweza baadae, kwani mali huja na kuondoka, juu ya hivyo Uislamu unasema mwanamume akimdhulumu mkewe au akashindwa kumkimu, basi mwanamke anaweza kutaka kufarikishwa na mume huyo, lakini hazuiliki na kuandikiana mkataba akifanya hayo kwa radhi yake na khiari yake. Na Uislamu kwa kufungua mlango wa kuoa wake zaidi ya mmoja lakini kwa mikazo kama hivyo ilivyo elezwa imekuwa umepiga vita magonjwa ya kijamii: Kwanza - Huenda ikawa idadi ya wanaume wanao faa kuoa ikawa chini kuliko wanawake wanao faa kuoelewa. Khasa huwa hayo baada ya vita. Imeonakana katika baadhi ya nchi za Ulaya imewahi kufika idadi ya wanawake kuwazidi wanaume baada ya vita kwa mara saba! Kwa hivyo ni hishima ya mwanamke katika hali kama hizo kuwa mke-mwenza kuliko kuwa akibahashika kama malaya, bila ya mume. Pili - Huenda kutokea baina ya mwanamume na mwanamke hali inayo walazimisha ama waingiane kiharamu au waoane kisharia. Ni maslaha kwa umma yawe hayo kwa mujibu wa sharia. Na ni bora kwa mwanamke kuwa mke kuliko kuwa hawara wa mwanamume huyu baada ya huyu. Ikiwa hii ni sura mbaya ya kuoa wake wengi, basi juu ya hivyo ni afadhali kuliko kuwa na mke mmoja. Kwani kuoa wake zaidi ya mmoja kama itavyo kuwa vibaya kunakinga shari kubwa zaidi kwa umma, nayo ni umalaya na maovu yanayo pandana nayo. Tatu - Mwanamke hakubali kuolewa na mume mwenye mke ila ikiwa ni kwa dharura iliyo kweli. Ikiwa mke wa kwanza atapata madhara kwa uke-wenza, basi huyu mwenzie atapata madhara makubwa zaidi kwa kuharimishwa mume kabisa, kwa kuwa ama ufe uke wake au apotee kwa wanaume majiani. Madhara makubwa hukingwa kwa madhara yaliyo akali (Kidogo). Nne - Imeonakana kuwa vijana wengi hawapendi kuoa, hata inakisiwa kuwa vijana wanao oa kwa kulinganisha na wafaao kuoa hawazidi kuliko 60%. Na haya yanazidi kila mwaka. Kupinga khatari hii hapana ila kuruhusu kuoa wake wengi. Tano - Huenda mke akapata maradhi ambayo hayamruhusu kulala na mumewe, au huenda akawa tasa. Ni maslaha ya umma na maslaha ya binafsi kuoa mke mwengine. (Wakati huo huo ikawa kumpa talaka huyo mke ni madhara makubwa zaidi kwa mke na ukatili kwa mume kufanya.) Kwa sababu kama hizi na nyenginezo Uislamu umeufungua mlango kwa shida na dhiki, na haukuufunga kabisa. Hivi sasa tunamwona Askofu Mkuu katika Uingereza anaona kuwa dawa ya pekee ya kuondoa uharibifu ulio uingilia ukoo wa Kiingereza ni kufungua mlango wa kuoa wake zaidi ya mmoja. Hakika Uislamu ni Sharia ya Mwenyezi Mungu ambaye anajua kila kitu. Kwani Yeye ndiye Mjuzi Mwenye hikima. (Haya tukijua kuwa dini ya Kikristo haikatazi kuoa wake wengi. Ni sharia zilizo tungwa na makanisa ya Kizungu tu kwa kufuata mila zao ndizo zinazo lazimisha kuoa mke mmoja. Basi hiyo ni mila ya Wazungu, wala si sharia ya dini yoyote duniani. Bali Uislamu ndiyo Dini pekee katika dini zote iliyo wekea kiwango, na kudhibiti idadi ya wanawake kuoa, kwa maslaha ya Umma.)
Arabic explanations of the Qur’an:
وَءَاتُواْ ٱلنِّسَآءَ صَدُقَٰتِهِنَّ نِحۡلَةٗۚ فَإِن طِبۡنَ لَكُمۡ عَن شَيۡءٖ مِّنۡهُ نَفۡسٗا فَكُلُوهُ هَنِيٓـٔٗا مَّرِيٓـٔٗا
Na wapeni wanawake mahari yao hali ya kuwa ni kipawa. Lakini wakikutunukieni kitu katika mahari, kwa radhi yao, basi kileni kiwashuke kwa raha.
Wapeni wanawake mahari yao kuwa ni kipawa, tunza iliyo safi. Na nyinyi hamna haki yoyote katika hayo mahari. Ikiwa hao wanawake kwa radhi ya nafsi zao wenyewe wakakubali kusamehe sehemu yoyote ya mahari mliyo kwisha ahadiana, basi hapo mnayo ruhusa kuchukua na mkatumia kwa kheri na salama.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تُؤۡتُواْ ٱلسُّفَهَآءَ أَمۡوَٰلَكُمُ ٱلَّتِي جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ قِيَٰمٗا وَٱرۡزُقُوهُمۡ فِيهَا وَٱكۡسُوهُمۡ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا
Wala msiwape wasio na akili mali yenu ambayo Mwenyezi Mungu ameyajaalia yawe ni kiamu yenu. Walisheni katika hayo na muwavike, na mseme nao maneno mazuri.
Wala msiwape wasio na akili ya kutosha kuendesha mambo yao mali yao, nayo ni mali yenu vile vile. Kwani mali ya yatima na ya mchache wa akili yamekulazimuni myatazame yasiharibike. Mwenyezi Mungu ameyajaalia mali hayo ya kukimu maisha. Wapeni kutokana na pato lake sehemu kama wanavyo hitajia kwa kula, na wavisheni na muwatendee vyema, na mseme nao maneno ya kuwaridhisha sio ya kuwaudhi au kuwadhili.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱبۡتَلُواْ ٱلۡيَتَٰمَىٰ حَتَّىٰٓ إِذَا بَلَغُواْ ٱلنِّكَاحَ فَإِنۡ ءَانَسۡتُم مِّنۡهُمۡ رُشۡدٗا فَٱدۡفَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡۖ وَلَا تَأۡكُلُوهَآ إِسۡرَافٗا وَبِدَارًا أَن يَكۡبَرُواْۚ وَمَن كَانَ غَنِيّٗا فَلۡيَسۡتَعۡفِفۡۖ وَمَن كَانَ فَقِيرٗا فَلۡيَأۡكُلۡ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِذَا دَفَعۡتُمۡ إِلَيۡهِمۡ أَمۡوَٰلَهُمۡ فَأَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ حَسِيبٗا
Na wajaribuni mayatima mpaka wafike umri wa kuoa. Mkiwaona ni wekevu, basi wapeni mali yao. Wala msiyale kwa fujo na pupa kwa kuwa watakuja kuwa watu wazima. Na aliye kuwa tajiri naajizuilie, na aliye fakiri basi naale kwa kadri ya ada. Na mtakapo wapa mali yao washuhudizieni. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mhasibu.
Na kabla ya hao mayatima kufika umri wa kubaalighi wajaribuni, mpate kujua akili zao na hali zao na maarifa yao katika kuendesha mambo. Hata wakifika wakati wa kusilihi kuoa na mkauona uwekevu wao, na matayarisho kuchukua jukumu, basi hapo wapeni mali yao wenyewe. Wala nyinyi msiyale mali yao kwa fujo, mkifanya haraka mpatilize kabla hawajabaalighi wakawa watu wazima ikabidi haki yao kurudi. Na akiwa katika mawasii anajitosha kwa utajiri, basi ajizuie asichukue chochote kuwa ni ujira kutazama mali ya mayatima. Na akiwa fakiri muhitaji basi ajitosheleze kuchukua ujira wa uangalizi kwa kadri ya ada ilivyo. Na mnapo wakabidhi mayatima mali yao wekeni mashahidi wa kushuhudia. Na mjue kuwa Mwenyezi Mungu daima yupo nyuma yenu, na Yeye ndiye Mhasibu, na Yeye ndiye Muangalizi. Na Yeye anatosha kuwa Mhasibu na Muangalizi.
Arabic explanations of the Qur’an:
لِّلرِّجَالِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٞ مِّمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنۡهُ أَوۡ كَثُرَۚ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا
Wanaume wana sehemu katika wanayo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Na wanawake wanayo sehemu katika waliyo yaacha wazazi na jamaa walio karibia. Ikiwa kidogo au kingi. Hizi ni sehemu zilizo faridhiwa.
Wanaume wanalo fungu lao katika mali waliyo yaacha kurithiwa wazazi wawili na jamaa walio karibia. Na wanawake, aidha, wana fungu lao, bila ya kunyimwa au kupunjwa. Na mafungu hayo yamethibiti, na yamefaridhiwa, na yamekadiriwa, yakiwa mali yenyewe kidogo au mengi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا حَضَرَ ٱلۡقِسۡمَةَ أُوْلُواْ ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينُ فَٱرۡزُقُوهُم مِّنۡهُ وَقُولُواْ لَهُمۡ قَوۡلٗا مَّعۡرُوفٗا
Na wakati wa kugawanya wakihudhuria jamaa na mayatima na masikini, wapeni katika hayo mali ya urithi, na semeni nao maneno mema.
Na pindi ikiwa wamehudhuria wakati ule wa kugawanya urithi baadhi ya jamaa ambao hawarithi, na ni mayatima na masikini, basi wakirimuni kwa kuwapa chochote katika huo urithi ili kuzipoza nafsi zao, na kuondoa uhasidi katika nyoyo zao. Na ni vizuri pia katika kuwapa kuleta maneno laini na udhuru mwema.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلۡيَخۡشَ ٱلَّذِينَ لَوۡ تَرَكُواْ مِنۡ خَلۡفِهِمۡ ذُرِّيَّةٗ ضِعَٰفًا خَافُواْ عَلَيۡهِمۡ فَلۡيَتَّقُواْ ٱللَّهَ وَلۡيَقُولُواْ قَوۡلٗا سَدِيدًا
Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli wakhofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa.
Watu watahadhari na kuwadhulumu mayatima, na wawaogopee watoto wao wanyonge wasije na wao wakadhulumiwa kwa watendavyo wazee kwa mayatima wa watu wengine. Na wamwogope Mwenyezi Mungu katika kuwatendea mayatima. Na waseme maneno yaliyo kaa sawa yanayo fuata haki, wala wasimdhulumu yeyote.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلۡيَتَٰمَىٰ ظُلۡمًا إِنَّمَا يَأۡكُلُونَ فِي بُطُونِهِمۡ نَارٗاۖ وَسَيَصۡلَوۡنَ سَعِيرٗا
Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhulma, hapana shaka yoyote wanakula matumboni mwao moto, na wataingia Motoni.
Hakika wanao wadhulumu mayatima kwa kuchukua mali yao bila ya haki, hakika wanakula yatakayo wapelekea Motoni. Na Mwenyezi Mungu atawaadhibu Siku ya Kiyama kwa moto mkali wenye kutia machungu.(Je, huwaje basi adhabu ya mwenye kudhulumu mali ya Mwenyezi Mungu? Wakfu za misikiti, madrasa n.k.? Na huwaje mwenye kuuwa ili apate kudhulumu mali ya mayatima wa hao alio wauwa?)
Arabic explanations of the Qur’an:
يُوصِيكُمُ ٱللَّهُ فِيٓ أَوۡلَٰدِكُمۡۖ لِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۚ فَإِن كُنَّ نِسَآءٗ فَوۡقَ ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُنَّ ثُلُثَا مَا تَرَكَۖ وَإِن كَانَتۡ وَٰحِدَةٗ فَلَهَا ٱلنِّصۡفُۚ وَلِأَبَوَيۡهِ لِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُ مِمَّا تَرَكَ إِن كَانَ لَهُۥ وَلَدٞۚ فَإِن لَّمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلَدٞ وَوَرِثَهُۥٓ أَبَوَاهُ فَلِأُمِّهِ ٱلثُّلُثُۚ فَإِن كَانَ لَهُۥٓ إِخۡوَةٞ فَلِأُمِّهِ ٱلسُّدُسُۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِي بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍۗ ءَابَآؤُكُمۡ وَأَبۡنَآؤُكُمۡ لَا تَدۡرُونَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ لَكُمۡ نَفۡعٗاۚ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu: Fungu la mwanamume ni kama fungu la wanawake wawili. Na ikiwa wanawake zaidi ya wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho kiacha maiti. Lakini akiwa mtoto mwanamke ni mmoja, basi fungu lake ni nusu. Na wazazi wake wawili, kila mmoja wao apate sudusi ya alicho kiacha, ikiwa anaye mtoto. Akiwa hana mtoto, na wazazi wake wawili wamekuwa ndio warithi wake, basi mama yake atapata thuluthi moja. Na akiwa anao ndugu, basi mama yake atapata sudusi. Haya ni baada ya kutolewa alicho usia au kulipa deni. Baba zenu na watoto wenu, nyinyi hamjui ni nani baina yao aliye karibia zaidi kwenu kwa manufaa. Hiyo ni Sharia iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Bila ya shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Mwenyezi Mungu anakuamrisheni katika mambo ya kuwarithisha watoto wenu na wazazi wenu, pindi mtakapo kufa, kwa njia inayo leta uadilifu na maslaha. Nayo ni kuwa sehemu ya mwanamume ni sawa na sehemu ya wanawake wawili, ikiwa watoto wanao rithi ni wanaume na wanawake. Ikiwa watoto wote ni wanawake watupu, na idadi yao imezidi wawili, basi sehemu yao ni thuluthi mbili za tirka, yaani mali yaliyo achwa na maiti. Inafahamika katika madhumuni ya Aya kuwa fungu la binti wawili ni kama fungu la walio zidi hapo. Na akiwa mtu amemuacha binti mmoja tu, basi fungu lake ni nusu ya alicho kiacha. Na akiwa mtu amemuacha baba na mama, basi kila mmojapo kati ya hao atapata sudusi, yaani sehemu moja katika sita, ikiwa huyo maiti alikuwa na mtoto mmoja - mwanamume au mwanamke - pamoja na hao wazazi wake. Akiwa hana mtoto na wakamrithi wazazi wake tu, basi mama sehemu yake ni thuluthi, na kilicho baki ni cha baba. Na ikiwa huyo maiti alikuwa na ndugu, basi mama yake atapata sudusi na kilicho baki ni cha baba, na wale ndugu hawapati chochote. Mafungu hayo hupewa wanao stahiki baada ya kwisha lipwa deni lilio kuwa juu ya maiti, na kutimiza yale aliyo yausia katika mipaka aliyo ruhusu Mwenyezi Mungu. Hii ni hukumu ya Mwenyezi Mungu. Na huu ndio uadilifu na ndio hikima. Na nyinyi hamjui ni nani kwenu mwenye manufaa zaidi kwenu, baina ya wazazi na wana. Na kheri khasa ni aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu, kwani Yeye ndiye Mwenye kuyajua maslaha yenu, na ndiye Mwenye hikima katika yale aliyo kulazimisheni.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَلَكُمۡ نِصۡفُ مَا تَرَكَ أَزۡوَٰجُكُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٞ فَلَكُمُ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡنَۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصِينَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۚ وَلَهُنَّ ٱلرُّبُعُ مِمَّا تَرَكۡتُمۡ إِن لَّمۡ يَكُن لَّكُمۡ وَلَدٞۚ فَإِن كَانَ لَكُمۡ وَلَدٞ فَلَهُنَّ ٱلثُّمُنُ مِمَّا تَرَكۡتُمۚ مِّنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ تُوصُونَ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٖۗ وَإِن كَانَ رَجُلٞ يُورَثُ كَلَٰلَةً أَوِ ٱمۡرَأَةٞ وَلَهُۥٓ أَخٌ أَوۡ أُخۡتٞ فَلِكُلِّ وَٰحِدٖ مِّنۡهُمَا ٱلسُّدُسُۚ فَإِن كَانُوٓاْ أَكۡثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمۡ شُرَكَآءُ فِي ٱلثُّلُثِۚ مِنۢ بَعۡدِ وَصِيَّةٖ يُوصَىٰ بِهَآ أَوۡ دَيۡنٍ غَيۡرَ مُضَآرّٖۚ وَصِيَّةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَلِيمٞ
Na fungu lenu ni nusu walicho acha wake zenu ikiwa hawana mtoto. Wakiwa na mtoto basi fungu lenu ni robo ya walicho acha, baada ya wasia waliyo usia au kulipa deni. Na wake zenu watapata robo mlicho kiacha, ikiwa hamna mtoto. Mkiwa mna mtoto basi sehemu yao ni thumni ya mlicho kiacha, baada ya wasia mlio usia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anaye rithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye ndugu mume au ndugu mke, basi kila mmoja katika hawa atapata sudusi. Na wakiwa zaidi kuliko hivyo basi watashirikiana katika thuluthi, baada ya wasia ulio usiwa au kulipa deni, pasio kuleta dhara. Huu ndio wasia ulio toka kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mpole.
Fungu la mume ni nusu ya alicho acha mke ikiwa huyo mke hakuacha mtoto kutokana na mume huyo au mwenginewe. Akiwa huyo mke ana mtoto, basi mumewe atapata robo baada ya kutolewa wasia aliye uusia huyo mwanamke au kulipwa deni lake. Na fungu la mke au wake ni robo ya alicho acha mume ikiwa hakuacha mtoto kwa wake hao au wenginewe. Akiwa anaye mwana kutokana na hao au wake wenginewe basi mke huyu au wake hawa watapata thumni ya tirka baada ya wasia alio usia au deni. Na mwana wa mwana, yaani mjukuu, ni kama mwana katika haya yaliyo tangulia. Na akiwa maiti ni mwanamume au mwanamke, naye hana mwana wala mzazi, na kamwacha ndugu mume kwa mama, au ndugu wawili wa kike kwa mama, basi kila mmoja wao atapata sudusi, yaani sehemu moja katika sita. Na wakiwa wengi kuliko hivyo watashirikiana katika thuluthi, watagawana sawa sawa wanaume na wanawake kwa mujibu wa ushirika, baada ya kulipa madeni yaliyo kuwa juu yake, na kutimiza wasia ambao haudhuru urithi, nao ni wasia usio pindukia thuluthi iliyo baki baada ya kulipa madeni. Basi, enyi Waumini! Jilazimisheni kufuata aliyo kuusieni Mwenyezi Mungu; kwani Yeye hakika ni Mwenye kujua vyema nani miongoni mwenu anaye dhulumu na nani anaye fanya uadilifu, Yeye ni Mpole hafanyi haraka kutoa adhabu.
Arabic explanations of the Qur’an:
تِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۚ وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ يُدۡخِلۡهُ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ
Hiyo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na anaye mt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, Yeye atamtia katika Pepo zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na huko ndiko kufuzu kukubwa.
Hizo ni hukumu zilizo tajwa kueleza khabari ya mirathi na mengine yaliyo tangulia ni Sharia za Mwenyezi Mungu aliye zipanga kwa ajili ya waja wake wazijue wala wasizikiuke. Na Mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika alivyo hukumu Yeye malipwa yake yatakuwa ni Pepo ipitayo mito kati yake, na atakaa humo daima dawamu. Na huko ndiko kushinda kukubwa. Mpango wa mirathi uliyo bainishwa na Qur'ani Tukufu ni mpango wa uadilifu na haki kuliko kanuni zote za mirathi nyenginezo duniani. Na haya wameyakiri wataalamu wa sharia wote wa Ulaya. Na huu ni mmoja katika ushahidi wa kuwa Qur'ani inatokana na Mwenyezi Mungu, kwani haya au yaliyo karibia haya hayakuwa yakijuulikana kwa Waajemi wala kwa Warumi wala katika sharia zozote za kabla ya Uislamu. Na sharia hii ya Kiislamu imefuata mipango hii ya uadilifu: Kwanza - Umefanywa urithi kwa mujibu apendavyo Mwenyezi Mungu, sivyo apendavyo mwenye mali, bila ya kupuuza kabisa mapenzi yake huyo. Amepewa huyo ruhusa ya kufanya wasia kwa thuluthi ya mali kwa ajili ya mambo mema, kama kutimiza kasoro katika waajibu wake wa dini, kama Zaka ambazo alikuwa hakuzitoa, au kuwajaalia kitu wahitaji alio khusiana nao kwa ujamaa au mapenzi nao hawastahiki urithi. Na amezuiliwa kufanya wasia ikiwa hayo yatapelekea maasi au yatachochea kuendelea maasia. Na thuluthi mbili zilizo baki baada ya wasia, au mali yote ikiwa hapana wasia, Mwenyezi Mungu Mtunga sharia, amejipa Yeye kuzigawa kwa haki. Pili - Katika kuchukua madaraka ya ugawaji tirka, Mwenyezi Mungu Aliye takasika, amempa aliye karibu zaidi kuliko mwenginewe, bila ya kuzingatia ukubwa au udogo. Kwa hivyo ndio ikawa watoto wana sehemu kubwa zaidi katika mirathi, kwani wao ndio kiendelezo cha yule maiti, na pia kuwa wao aghlabu ni wanyonge. Juu ya hivyo hawakukoseshwa, bali wameshirikiana nao, mama na bibi, baba na babu, ijapokuwa wanachukua akalli kuliko watoto. Tatu - Yaonekana kuwa mirathi ni kwa kadri ya haja. Kwa hivyo sehemu ya watoto ni kubwa kwa sababu haja yao ni kubwa zaidi, na wao ndio wanayakabili maisha, na kina baba na mama wanayapa mgongo maisha. Ama zingatio la haja ndilo lililo pelekea kuwa fungu la mwanamke liwe nusu ya fungu la mwanamume katika aghlabu ya hali za mirathi. Haya ni kwa kuwa mwanamume inambdi zaidi kukabili matumizi, kwa kuwa yeye anatakikana awalishe watoto na awatazame, amtumilie mwanamke. Maumbile ya kibinaadamu yamemfanya mwanamke ndiye asimamie kazi za nyumbani na kulea watoto, kuangalia raha zao, na mwanmume awe ni wa kuhangaika nje kiuchumi alete fedha za kutumia nyumba nzima. Kumpa kila mmoja kwa kadri ya haja ndio uadilifu. Kuweka sawa kwa wenye haja mbali mbali ni udhalimu. Nne - Sharia ya Kiislamu katika kugawa kwake tirka ya maiti inakusudia kugawa sio kurundika. Kwa hivyo haikufanya urithi wende kwa mtoto mkubwa peke yake, wala haikuwapa wanaume tu na kuwachilia mbali wanawake, wala watoto wakaachwa wazazi. Wala hawakukoseshwa wasio kuwa katika uti wa nasaba, kama ndugu, na maami, na banu-ami n.k. Urithi unaendelea mpaka kwa wanao karibia ukoo, lakini aliye karibu hufadhilika zaidi. Na shida kutokea kuwa mrithi ni mmoja tu. Tano - Mwanamke hakoseshwi kurithi, kama ilivyo kuwa ada ya Waarabu. Hivi ni kumhishimu mwanamke na kumpa haki yake. Na juu ya haya Uislamu hauzuii kurithi ujamaa wa mwanamke, bali hurithi jamaa walio kuwa upande wake, kama wanavyo rithi jamaa upande wa baba. Makaka na madada kwa upande wa mama wanachukua pale wanapo chukua ndugu wa baba na mama, bali katika hali nyengine wanachukua watoto wa kwa mama na kuchukua ndugu wanaume na wanawake. Na haya bila ya shaka ni kuutukuza umama, na kuutambua ukaribu wake. Haya hayakuwa yakijuulikana kabla yake, walakini hii ni Sharia ya Mwenyezi Mungu aliye Mjuzi na Mwenye hikima.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَعۡصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ وَيَتَعَدَّ حُدُودَهُۥ يُدۡخِلۡهُ نَارًا خَٰلِدٗا فِيهَا وَلَهُۥ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha.
Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akaikiuka mipaka aliyo iweka Mwenyezi Mungu, na huku akihalalisha kukiuka huko basi mtu huyo atalipwa Moto, na humo atakaa milele, akiadhibiwa mwili wake juu ya kuadhibiwa roho yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّٰتِي يَأۡتِينَ ٱلۡفَٰحِشَةَ مِن نِّسَآئِكُمۡ فَٱسۡتَشۡهِدُواْ عَلَيۡهِنَّ أَرۡبَعَةٗ مِّنكُمۡۖ فَإِن شَهِدُواْ فَأَمۡسِكُوهُنَّ فِي ٱلۡبُيُوتِ حَتَّىٰ يَتَوَفَّىٰهُنَّ ٱلۡمَوۡتُ أَوۡ يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لَهُنَّ سَبِيلٗا
Na ambao wanafanya uchafu miongoni mwa wanawake wenu, washuhudizieni watu wane katika nyinyi. Watakapo shuhudia, basi wazuieni majumbani mpaka wafishwe na mauti au Mwenyezi Mungu awatolee njia nyengine.
Na wale wanawake wanao zini wakishuhudiwa na mashahidi wanaume wane walio waadilifu, basi wazuieni wasitoke nyumbani kwa ajili ya kuwalinda na kuzuia usiendelee ufisadi na shari mpaka wafe, au Mwenyezi Mungu awafungulie njia ya maisha yaliyo sawa kwa kuolewa na kutubu. (Wafasiri wengine wanasema hukumu hii ni kwa wanawake wanao fanya mambo machafu wenyewe kwa wenyewe, sio ya zina baina ya mwanamke na mwanamume. Kwa kuhifadhi heshima ya wanawake inalazimu wapatikane mashahidi wane, badala ya wawili, walio ona kitendo khasa, sio kuwatuhumu watu kwa jambo ovu kama hilo bila ya mashahidi wane walio shuhudia kwa macho yao.)
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذَانِ يَأۡتِيَٰنِهَا مِنكُمۡ فَـَٔاذُوهُمَاۖ فَإِن تَابَا وَأَصۡلَحَا فَأَعۡرِضُواْ عَنۡهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ تَوَّابٗا رَّحِيمًا
Na wawili kati yenu wafanyao hayo waadhibuni. Na wakitubia wakatengenea basi waacheni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kupokea toba, Mwenye kurehemu.
Mwanamume na mwanamke walio zini, nao hawajaoa (au kuolewa), wapewe adhabu maalumu, pindi ikithibiti hiyo zina kwa mashahidi wane waadilifu. Wakitubu baada ya kupewa adhabu, basi msiwatajie hayo maasi waliyo yatenda, wala msiwaaziri. Hakika Mwenyezi Mungu kwa rehema yake anakubali toba ya wenye kutubu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّمَا ٱلتَّوۡبَةُ عَلَى ٱللَّهِ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَٰلَةٖ ثُمَّ يَتُوبُونَ مِن قَرِيبٖ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَتُوبُ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Hakika toba inayo kubaliwa na Mwenyezi Mungu ni ya wale wafanyao uovu kwa ujinga, kisha wakatubia kwa haraka. Hao ndio Mwenyezi Mungu huwakubalia toba yao, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na ni Mwenye hikima.
Hakika toba imedhaminiwa na Mwenyezi Mungu kwa watendao maovu katika hali ya ujinga, na kupitikiwa na kutoangalia vyema, kisha wakafanya haraka ya kutubu kabla ya kufikiwa na mauti. Hawa basi Mwenyezi Mungu anaikubali toba yao, naye ni Mjuzi, haumfichikii ukweli wa toba, ni Mwenye hikima, hakosei katika kupima.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَيۡسَتِ ٱلتَّوۡبَةُ لِلَّذِينَ يَعۡمَلُونَ ٱلسَّيِّـَٔاتِ حَتَّىٰٓ إِذَا حَضَرَ أَحَدَهُمُ ٱلۡمَوۡتُ قَالَ إِنِّي تُبۡتُ ٱلۡـَٰٔنَ وَلَا ٱلَّذِينَ يَمُوتُونَ وَهُمۡ كُفَّارٌۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَعۡتَدۡنَا لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا
Wala hawana toba wale wafanyao maovu mpaka yakamfikia mmoja wao mauti, kisha hapo akasema: Hakika mimi sasa nimetubia. Wala wale wanao kufa na hali wao ni makafiri. Hao tumewaandalia adhabu chungu.
Toba isiyo kubaliwa ni ya wanao fanya maasi kisha hawafanyi haraka kuyajutia mpaka mmoja afikwapo na mauti. Tena hapo husema: Sasa mimi natangaza majuto na toba. Kadhaalika toba haikubaliwi kutokana na wanao kufa katika ukafiri. Mwenyezi Mungu ameyaandalia makundi mawili hayo adhabu ya kutia uchungu huko kwenye nyumba ya malipo, Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَحِلُّ لَكُمۡ أَن تَرِثُواْ ٱلنِّسَآءَ كَرۡهٗاۖ وَلَا تَعۡضُلُوهُنَّ لِتَذۡهَبُواْ بِبَعۡضِ مَآ ءَاتَيۡتُمُوهُنَّ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَٰحِشَةٖ مُّبَيِّنَةٖۚ وَعَاشِرُوهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِۚ فَإِن كَرِهۡتُمُوهُنَّ فَعَسَىٰٓ أَن تَكۡرَهُواْ شَيۡـٔٗا وَيَجۡعَلَ ٱللَّهُ فِيهِ خَيۡرٗا كَثِيرٗا
Enyi mlio amini! Si halali kwenu kuwarithi wanawake kwa nguvu. Wala msiwadhikishe ili mwapokonye baadhi ya mlivyo wapa - isipo kuwa wakifanya uchafu ulio wazi. Na kaeni nao kwa wema, na ikiwa mmewachukia, basi huenda mkakichukia kitu, na Mwenyezi Mungu ametia kheri nyingi ndani yake.
Enyi mlio amini! Haikujuziini kuwafanya wanawake kama bidhaa, mkiwarithi wake zenu bila ya mahari na bila ya ridhaa yao. Wala msiwadhulumu kwa kuwadhikisha ili wapate kusamehe baadhi ya mahari mlio wapa. Wala msiwadhiki ili wapate kukurejesheeni mali mlio wapa, ila ikiwa wakifanya kosa wazi la kuwacha ut'iifu, au la tabia mbovu, au la ukahaba. Hapo mnaweza kuwadhikisha au kuchukua baadhi ya mlicho wapa wakati wa kufarikiana nao. Na ni waajibu wenu, enyi Waumini, kukaa na wake zenu kwa vizuri, kwa maneno mema na vitendo vyema. Ikiwa mtawachukia kwa aibu fulani katika tabia au katika umbo au mengineyo, basi juu ya hivyo subirini. Msifanye haraka kuwaacha, kwani asaa Mwenyezi Mungu akajaalia kheri nyingi katika hicho hicho mkichukiacho. Na ujuzi wa mambo yote uko kwa Mwenyezi Mungu tu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنۡ أَرَدتُّمُ ٱسۡتِبۡدَالَ زَوۡجٖ مَّكَانَ زَوۡجٖ وَءَاتَيۡتُمۡ إِحۡدَىٰهُنَّ قِنطَارٗا فَلَا تَأۡخُذُواْ مِنۡهُ شَيۡـًٔاۚ أَتَأۡخُذُونَهُۥ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا
Na mkitaka kubadilisha mke mahali pa mke, na hali mmoja wao mmempa chungu ya mali, basi msichukue katika hayo kitu chochote. Je, mtachukua kwa dhulma na kosa lilio wazi?
Na pindi ikiwa mnataka kubadili mke pahala pa mke mwengine, na ikawa mmempa mmoja wao mali mengi basi si halali kwenu kuchukua chochote katika hayo. Jee mtachukua hayo kwa njia ya upotovu na kwa dhambi iliyo wazi?
Arabic explanations of the Qur’an:
وَكَيۡفَ تَأۡخُذُونَهُۥ وَقَدۡ أَفۡضَىٰ بَعۡضُكُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٖ وَأَخَذۡنَ مِنكُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا
Na mtachukuaje na ilhali mmekwisha ingiliana nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wamechukua kwenu ahadi iliyo madhubuti?
Na vipi ikufalieni nyinyi kutaka kurudishiwa mahari mliyo kwisha yatoa, na hali mlikwisha changanyika nyinyi kwa nyinyi, na wao wanawake wakafungamana nanyi kwa agano lenye nguvu ambalo kwalo Mwenyezi Mungu amewajibisha muingiane nao kwa ndoa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَنكِحُواْ مَا نَكَحَ ءَابَآؤُكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا قَدۡ سَلَفَۚ إِنَّهُۥ كَانَ فَٰحِشَةٗ وَمَقۡتٗا وَسَآءَ سَبِيلًا
Wala msiwaoe wake walio waoa baba zenu, ila yaliyo kwisha pita. Hakika huo ni uchafu na uchukizo na ni njia mbaya.
Wala nyinyi, watoto, msiwaoe wanawake walio wahi kuolewa na baba zenu. Jambo hilo ni uchafu na linachusha, na linakirihiwa na Mwenyezi Mungu na watu. Na hiyo ni njia ovu kabisa. Lakini Mwenyezi Mungu anasamehe yaliyo kwisha tendeka katika zama za ujahili. Waarabu katika zama za ujahili walikuwa na ada zisio mpa heshima mwanamke, bali zikimdhulumu sana, na zikikata makhusiano mema katika ukoo. Ilikuwa mtu akifa baba yake na akawa na wake wasio kuwa mama yake mzazi, akilazimishwa kuwaoa, au akiwarithi wake za baba yake bila ya ndoa mpya. Na ilikuwa mtu akimwacha mke basi humpokonya kwa dhulma na uadui mahari yote aliyo mpa. Na walikuwapo walio kuwa wakimzuia huyo mt'laka asiolewe na mtu mwengine, kwa jeuri na inda. Ukaja Uislamu, ukamlinda mwanamke na dhulma hii iliyo wazi, ukakataza kurithiwa mke, na kumpokonya mahari yake hata chembe, ijapo kuwa ni mali mengi, na ukakataza kumzuia mt'alaka asiolewe, au kumkera ili apate kutaka yeye mke t'alaka kwa kutoa mali. Na katika mtindo wao Waarabu wa jahiliya ilikuwa yafaa mtu kumwoa aliye kuwa mke wa baba yake na akafarikiana naye kwa t'alaka au mfano wake. Uislamu ukakataza hayo, na ukauwita mtindo huo ni uchafu, kwa sababu ni jambo baya analo lichukia Mwenyezi Mungu na kila mwenye akili sawa. Huo ndio uadilifu wa Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
حُرِّمَتۡ عَلَيۡكُمۡ أُمَّهَٰتُكُمۡ وَبَنَاتُكُمۡ وَأَخَوَٰتُكُمۡ وَعَمَّٰتُكُمۡ وَخَٰلَٰتُكُمۡ وَبَنَاتُ ٱلۡأَخِ وَبَنَاتُ ٱلۡأُخۡتِ وَأُمَّهَٰتُكُمُ ٱلَّٰتِيٓ أَرۡضَعۡنَكُمۡ وَأَخَوَٰتُكُم مِّنَ ٱلرَّضَٰعَةِ وَأُمَّهَٰتُ نِسَآئِكُمۡ وَرَبَٰٓئِبُكُمُ ٱلَّٰتِي فِي حُجُورِكُم مِّن نِّسَآئِكُمُ ٱلَّٰتِي دَخَلۡتُم بِهِنَّ فَإِن لَّمۡ تَكُونُواْ دَخَلۡتُم بِهِنَّ فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ وَحَلَٰٓئِلُ أَبۡنَآئِكُمُ ٱلَّذِينَ مِنۡ أَصۡلَٰبِكُمۡ وَأَن تَجۡمَعُواْ بَيۡنَ ٱلۡأُخۡتَيۡنِ إِلَّا مَا قَدۡ سَلَفَۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Mmeharimishiwa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu, na shangazi zenu, na khaalati zenu, na binti wa ndugu mume, na binti wa dada, na mama zenu walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wa wake zenu, na watoto wenu wa kambo walio katika ulinzi wenu walio zaliwa na wake zenu mlio waingilia. Ikiwa hamkuwaingilia basi hapana lawama juu yenu. (Pia mmeharimishwa) wake wa watoto wenu walio toka katika migongo yenu. Na kuwaoa pamoja dada wawili isipo kuwa yale yaliyo kwisha pita. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
Mwenyezi Mungu amekuharimishieni kuwaoa mama zenu, na binti zenu, na dada zenu (ndugu wanawake) na shangazi zenu, na khaalati zenu (mama wadogo) na binti wa ndugu, na binti wa dada, na mama walio kunyonyesheni, na dada zenu kwa kunyonya, na mama wakwe. Na walio harimishwa bila ya kunasibiana kwa damu ni: mama wa kunyonyesha, dada wa kunyonya, mama mkwe, binti za wake kwa waume wengine ikiwa hao wake wameingiliwa, na wake wa watoto mlio wazaa, na kuwaoa pamoja ndugu wawili. Yaliyo pita katika siku za ujahili yamesamehewa. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe kwa yaliyo pita kabla ya mpango huu, na Mwenye kuwarehemu katika aliyo kuwekeeni sharia. Ni Sharia ya Kiislamu pekee iliyo harimisha kwa sababu ya kunyonyesha. Anaye nyonya anakula kutokana na mwili wa mnyonyeshaji kama anavyo kula kutokana na mama yake ndani ya tumbo lake. Wote hao wawili wanakuwa ni sehemu yake huyo mtoto. Hapana khitilafu baina ya kukua ndani ya chumba na ndani ya tumbo. Na katika kuharimisha kwa kunyonyesha ni kumtukuza mnyonyeshaji, kwani anakuwa kama mama. Na haya ni kuzidi kushajiisha kunyonyesha kimaumbile, sio kwa chupa, kwa watoto wachanga.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۖ كِتَٰبَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَآءَ ذَٰلِكُمۡ أَن تَبۡتَغُواْ بِأَمۡوَٰلِكُم مُّحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَۚ فَمَا ٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِهِۦ مِنۡهُنَّ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا تَرَٰضَيۡتُم بِهِۦ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡفَرِيضَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا
NA WANAWAKE wenye waume, isipo kuwa walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sharia ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasio kuwa hao, mtafute kwa mali yenu kwa kuowa pasina kuzini. Kama mnavyo starehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni waajibu. Wala hapana lawama juu yenu kwa mtakacho kubaliana baada ya kutimiza waajibu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua na Mwenye hikima.
Haramu kwenu kuoa wake za watu wote, waungwana na wasio waungwana, ila mateka mlio wateka katika vita baina yenu na makafiri. Kwani ndoa zao zilizo pita zinafutika kwa kutekwa. Wanakuwa halali kwenu baada ya kuhakikisha hawana mimba. Basi shikeni aliyo kuandikieni Mwenyezi Mungu kuhishimu mlicho katazwa. Isipo kuwa hao wanawake Waumini walio maharimu yenu, mwaweza kutafuta wanawake mkawaoa kwa mali yenu, bila ya kuzini au kuweka kinyumba. Kila mwanamke mliye starehe naye baada ya kumwoa mpeni mahari yake kama mlivyo patana. Hapana ubaya kwenu ikiwa watakuridhieni kupunguza au kuongeza. Mwenyezi Mungu daima anayaangalia mambo ya waja wake, na ni mwenye kuwapangia hukumu zinazo wasilihi kwa maisha yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ مِنكُمۡ طَوۡلًا أَن يَنكِحَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ فَمِن مَّا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُم مِّن فَتَيَٰتِكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِكُمۚ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ فَٱنكِحُوهُنَّ بِإِذۡنِ أَهۡلِهِنَّ وَءَاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِ مُحۡصَنَٰتٍ غَيۡرَ مُسَٰفِحَٰتٖ وَلَا مُتَّخِذَٰتِ أَخۡدَانٖۚ فَإِذَآ أُحۡصِنَّ فَإِنۡ أَتَيۡنَ بِفَٰحِشَةٖ فَعَلَيۡهِنَّ نِصۡفُ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ مِنَ ٱلۡعَذَابِۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَشِيَ ٱلۡعَنَتَ مِنكُمۡۚ وَأَن تَصۡبِرُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, na aoe katika vijakazi Waumini iliyo wamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kama ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapo olewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyo wekewa waungwana. Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anaye ogopa kuingia katika zina. Na mkisubiri ndio bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu.
Asiye weza kati yenu kuwaoa wanawake Waumini wa kiungwana basi na aowe anaye muweza katika wanawake Waumini walio milikiwa. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema ukweli wa Imani yenu na ikhlasi yenu. Wala msione uvunjifu kuwaowa hao vijakazi, kwani nyinyi na wao ni sawa katika Dini. Basi waoweni kwa idhini ya watu wao, na muwape mahari yao mliyo wakadiria kwa mujibu ya ilivyo zowewa kati yenu kwa ajili ya kutendeana mema na kutimiza haki. Na chagueni wanawake walio safi, msichague wazinifu kwa dhaahiri wala mahawara wa kinyumba. Na hao wakija zini baada ya kuolewa basi adabu yao ni nusu ya muungwana. Na huku kuhalalishiwa kuowa wajakazi mnapo kuwa hamuwezi kunajuzu kwa anaye ogopa taabu zinazo pelekea zina. Na mkisubiri kuto owa wajakazi na mkakaa safi ni bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mkubwa wa kurehemu.
Arabic explanations of the Qur’an:
يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمۡ وَيَهۡدِيَكُمۡ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَيَتُوبَ عَلَيۡكُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Mwenyezi Mungu anataka kukubainishieni na kukuongozeni nyendo za walio kuwa kabla yenu, na akurejezeni kwenye ut'iifu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima.
Mwenyezi Mungu anataka kukuwekeeni wazi njia yenye maslaha kabisa, na akuongoeni kwenye nyendo njema za walio kuwa kabla yenu, na akurejesheni kwenye njia ya ut'iifu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua vyema mambo yenu, ni Mwenye kupanga baraabara katika hukumu zake kwa yanayo silihi mambo yenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱللَّهُ يُرِيدُ أَن يَتُوبَ عَلَيۡكُمۡ وَيُرِيدُ ٱلَّذِينَ يَتَّبِعُونَ ٱلشَّهَوَٰتِ أَن تَمِيلُواْ مَيۡلًا عَظِيمٗا
Na Mwenyezi Mungu anataka kukurejezeni kwenye ut'iifu wake, na wanao taka kufuata matamanio wanataka mkengeuke makengeuko makubwa.
Na Mwenyezi Mungu anataka mrejee katika ut'iifu wake, na wale wanao fuata ladha zao, na matamanio yao machafu, miongoni mwa makafiri na waasi, wanataka muwe mbali kabisa na njia ya haki.
Arabic explanations of the Qur’an:
يُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُخَفِّفَ عَنكُمۡۚ وَخُلِقَ ٱلۡإِنسَٰنُ ضَعِيفٗا
Mwenyezi Mungu anataka kukupunguzieni taabu, na mwanaadamu ameumbwa dhaifu.
Mwenyezi Mungu anataka kukufanyieni wepesi katika kutunga sharia ambazo ndani yake zina sahala na takhfifu kwenu. Kwani hakika Mwenyezi Mungu amemuumba mwanaadamu kiumbe dhaifu katika kupambana na matamanio na maelekeo ya nafsi. Kwa hivyo yanayo mlazimu katika sharia yana wepesi na wasaa. Na hayo kwa fadhila yake na taisiri yake Mwenyezi Mungu ndiyo anayo walazimisha waja wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَأۡكُلُوٓاْ أَمۡوَٰلَكُم بَيۡنَكُم بِٱلۡبَٰطِلِ إِلَّآ أَن تَكُونَ تِجَٰرَةً عَن تَرَاضٖ مِّنكُمۡۚ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُمۡ رَحِيمٗا
Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe. Wala msijiuwe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwarehemuni.
Enyi mlio amini! Msinyang'anyane mali nyinyi kwa nyinyi. Lakini ipo ruhusa kufanya biashara kwa kuridhiana. Wala msijiteketeze kwa kuacha amri za Mola wenu Mlezi. Wala mmoja wenu asimtende uwovu mwenziwe, kwani nyote ni nafsi moja. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye rehema daima kwenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ عُدۡوَٰنٗا وَظُلۡمٗا فَسَوۡفَ نُصۡلِيهِ نَارٗاۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرًا
Na mwenye kutenda hayo kwa uadui na udhaalimu, basi huyo tutamwingiza Motoni. Na hilo ni jepesi kwa Mwenyezi Mungu.
Na mwenye kuyatenda aliyo yaharimisha Mwenyezi Mungu kwa uvamizi na kupindukia haki yake, basi tutamtia Motoni ateketee huko. Na hayo ni madogo na mepesi kabisa kwa Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِن تَجۡتَنِبُواْ كَبَآئِرَ مَا تُنۡهَوۡنَ عَنۡهُ نُكَفِّرۡ عَنكُمۡ سَيِّـَٔاتِكُمۡ وَنُدۡخِلۡكُم مُّدۡخَلٗا كَرِيمٗا
Mkiyaepuka makubwa mnayo katazwa, tutakufutieni makosa yenu madogo, na tutakuingizeni mahali patukufu.
Mkiyaachilia mbali madhambi makubwa makubwa anayo kukatazeni Mwenyezi Mungu, tutakusameheni makosa yaliyo duni ya hayo, maadamu mnafanya ukomo wa juhudi yenu kwenda sawa; na tutakuwekeni duniani na Akhera mwahali penye ihsani na hishima kwenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَتَمَنَّوۡاْ مَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بِهِۦ بَعۡضَكُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖۚ لِّلرِّجَالِ نَصِيبٞ مِّمَّا ٱكۡتَسَبُواْۖ وَلِلنِّسَآءِ نَصِيبٞ مِّمَّا ٱكۡتَسَبۡنَۚ وَسۡـَٔلُواْ ٱللَّهَ مِن فَضۡلِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمٗا
Wala msitamani alicho wafadhili Mwenyezi Mungu baadhi yenu kuliko wengine. Wanaume wana fungu katika walio vichuma, na wanawake wana fungu katika walio vichuma. Na muombeni Mwenyezi Mungu fadhila zake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Wala haifai wanaume kutamani yale waliyo khusishwa nayo wanawake, wala haiwafalii wanawake kutamani waliyo khusishwa nayo wanaume. Kwani kila kikundi kina sehemu yake kwa mujibu wa tabia ya maumbile ya kazi zinazo wawajibikia, na haki wanazo ongezewa. Basi kila mmoja ajielekeze kutaraji ziada ya fadhila za Mwenyezi Mungu kwa kukuza vipawa alivyo pewa yeye na kutafuta msaada juu ya waajibu ulio juu yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi timamu wa kila kitu, na mtu amepewa namna ya kila kitu kinacho msilihi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِكُلّٖ جَعَلۡنَا مَوَٰلِيَ مِمَّا تَرَكَ ٱلۡوَٰلِدَانِ وَٱلۡأَقۡرَبُونَۚ وَٱلَّذِينَ عَقَدَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡ فَـَٔاتُوهُمۡ نَصِيبَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدًا
Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu.
Na wote, wanaume na wanawake, tumewajaalia kuwa wanastahiki urithi wao wa kuwarithi wazazi wawili, na jamaa, na wale ambao mfiliwa amefungamana nao kwa agano ambalo matokeo yake ni kuwa amrithi ijapokuwa si jamaa, na amsaidie pindi anahitajia msaada kuwa ni badala yake. Basi mpeni haki yake kila mwenye haki, wala msipunguze kitu. Hakika Mwenyezi Mungu anakuangalieni kwa kila kitu, na yuko pamoja nanyi, anashuhudia yote myafanyayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلرِّجَالُ قَوَّٰمُونَ عَلَى ٱلنِّسَآءِ بِمَا فَضَّلَ ٱللَّهُ بَعۡضَهُمۡ عَلَىٰ بَعۡضٖ وَبِمَآ أَنفَقُواْ مِنۡ أَمۡوَٰلِهِمۡۚ فَٱلصَّٰلِحَٰتُ قَٰنِتَٰتٌ حَٰفِظَٰتٞ لِّلۡغَيۡبِ بِمَا حَفِظَ ٱللَّهُۚ وَٱلَّٰتِي تَخَافُونَ نُشُوزَهُنَّ فَعِظُوهُنَّ وَٱهۡجُرُوهُنَّ فِي ٱلۡمَضَاجِعِ وَٱضۡرِبُوهُنَّۖ فَإِنۡ أَطَعۡنَكُمۡ فَلَا تَبۡغُواْ عَلَيۡهِنَّ سَبِيلًاۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيّٗا كَبِيرٗا
Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.
Wanaume wana haki ya kuwaangalia na kuwachunga wanawake, na kuwasimamia katika mambo yao kwa vile Mwenyezi Mungu amewapa wao wanaume sifa za kuweza kuisimamia haki hii, na kwa kuwa wao ndio wanao hangaika na kufanya juhudi ya kutafuta mali ya kuutumilia ukoo mzima. Basi wanawake wema wanakuwa ni wat'iifu kwa Mwenyezi Mungu na waume zao. Ni wenye kuhifadhi vyote ambavyo waume zao hawavioni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameamrisha vihifadhiwe, na kwa kuwapa wao tawfiki. Na wanawake wanao onyesha kuanza uasi wanasihini kwa maneno yenye kuathiri. Kama hawakusikia tenganeni nao kitandani. Hawakusikia, watieni adabu kwa pigo dogo, si la kuwajuruhi wala kuwadhalilisha. Wakirejea kwenye ut'iifu wenu kwa njia mojapo katika hizi tatu basi msiwatafutie kisababu cha kuwatesa zaidi kuliko haya. Hakika Mwenyezi Mungu yuko juu yenu, naye atakupatilizeni pindi mkiwaudhi wake zenu au mkawafanyia jeuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنۡ خِفۡتُمۡ شِقَاقَ بَيۡنِهِمَا فَٱبۡعَثُواْ حَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهِۦ وَحَكَمٗا مِّنۡ أَهۡلِهَآ إِن يُرِيدَآ إِصۡلَٰحٗا يُوَفِّقِ ٱللَّهُ بَيۡنَهُمَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا خَبِيرٗا
Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari.
Pindi pakitokea kukhitalifiana baina ya mke na mume, na mkakhofia kutokea kufarikiana kutako leta t'alaka, chagueni waamuzi wawili. Mmoja kutokana na upande wa mume na mwengine upande wa mke. Wakitaka kusuluhiana Mwenyezi Mungu atawawafikisha wafikilie lilio kheri kwa wote wawili, nako ama kukaa kwa wema au kuachana kwa ihsani. Hakika Mwenyezi Mungu anachungua kila kitu cha waja wake, kilicho dhihiri na kilicho fichikana.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَلَا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗا وَبِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱلۡجَارِ ذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡجَارِ ٱلۡجُنُبِ وَٱلصَّاحِبِ بِٱلۡجَنۢبِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخۡتَالٗا فَخُورًا
Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri,
Nanyi muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake, wala msimfanyie washirika katika Ungu na kuabudiwa. Na watendeeni wema wazazi wenu bila ya taksiri yoyote, na pia jamaa zenu, na mayatima, na walio fakirika kwa sababu ya kuemewa au kupata masaibu katika mali yao, na jirani mliye karibiana naye kwa nasaba, na jirani mtu mbali, na mwenzio katika kazi au njia au majlisi, na msafiri mhitaji asiye kuwa na kituo katika nchi maalumu, na watumwa wenu wanaume na wanawake mlio wamiliki. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi anaye jipa ubora juu ya watu wengine, na hawachukulii watu kwa huruma, na anakithirisha kujisifu mwenyewe kwa kujifakhiri.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ يَبۡخَلُونَ وَيَأۡمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلۡبُخۡلِ وَيَكۡتُمُونَ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۗ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا
Ambao wanafanya ubakhili na wanaamrisha watu ubakhili, na wanaficha fadhila alizo wapa Mwenyezi Mungu. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya fedheha,
Hao ndio wanao ongeza juu ya takaburi na tafakhuri yao ila ya kuwafanyia watu ubakhili kwa mali yao na juhudi yao. Tena ikawa wanawataka watu wafanye ubakhili kama wao. Kazi yao ni kukhofia neema na fadhila ya Mwenyezi Mungu isiwatoke. Kwa hivyo, basi, hawajifai wenyewe wala hawawafai watu. Wapinzani kama hao tumekwisha waandalia adhabu ya kutia machungu na ya kudhalilisha.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمۡوَٰلَهُمۡ رِئَآءَ ٱلنَّاسِ وَلَا يُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَلَا بِٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۗ وَمَن يَكُنِ ٱلشَّيۡطَٰنُ لَهُۥ قَرِينٗا فَسَآءَ قَرِينٗا
Na ambao hutoa mali yao kwa kuonyesha watu, wala hawamuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Mwisho; na yule ambaye Shet'ani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya mno.
Na Mwenyezi Mungu hawapendi wanao toa mali kwa ajili ya kuonekana na watu, wapate kuwasifu na kuwatukuza, na ilhali wao si wenye kumuamini Mwenyezi Mungu wala Siku ya Malipo. Kwani hao wamemfuata Shetani naye amewapoteza. Na mwenye kuwa rafiki yake ni Shetani basi ana rafiki mbaya kweli.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَاذَا عَلَيۡهِمۡ لَوۡ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَأَنفَقُواْ مِمَّا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِهِمۡ عَلِيمًا
Na ingeli wadhuru nini wao lau wangeli muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho, na wakatoa katika aliyo waruzuku Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwajua vyema.
Ama wamelaanika watu hawa! Kingewadhuru nini wao lau kuwa wamemuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Akhera, na wakatoa katika alicho wapa Mwenyezi Mungu kwa kufuatana na Imani hii, na usafi wa niya, na kutaraji thawabu kama ilivyo wajibikia? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kwa ujuzi kaamili mambo yote yaliyo wazi na yaliyo fichikana ndani.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَظۡلِمُ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖۖ وَإِن تَكُ حَسَنَةٗ يُضَٰعِفۡهَا وَيُؤۡتِ مِن لَّدُنۡهُ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Hakika Mwenyezi Mungu hadhulumu hata uzito wa chembe moja. Na ikiwa ni jambo jema basi Yeye hulizidisha na hutoa kutoka kwake malipo makubwa.
Hakika Mwenyezi Mungu hamdhulumu mtu hata kidogo. Basi hampunguzii ujira wake mtu, wala adhabu yake hamzidishii kabisa. Bali humzidishia mtenda mema thawabu zake mardufu hata zikiwa kidogo vipi. Na humpa kwa fadhila yake malipo makubwa yasiyo lingana na hayo mema yake ambayo yamekwisha zidishwa mardufu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَكَيۡفَ إِذَا جِئۡنَا مِن كُلِّ أُمَّةِۭ بِشَهِيدٖ وَجِئۡنَا بِكَ عَلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِ شَهِيدٗا
Basi itakuwaje pindi tukiwaletea kutoka kila umma shahidi, na tukakuleta wewe kuwa shahidi wa hawa?
Vipi basi itakuwa hali ya hao mabakhili wanao pingana na aliyo yaamrisha Mwenyezi Mungu, tutapo mleta Siku ya Kiyama kila Nabii awe ni shahidi juu ya kaumu yake, na tukakuleta wewe, ewe Nabii Muhammad, kuwa ni shahidi juu ya kaumu yako, na hali miongoni mwao wapo hao wanao zuia mali yao na wanao pinga?
Arabic explanations of the Qur’an:
يَوۡمَئِذٖ يَوَدُّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَعَصَوُاْ ٱلرَّسُولَ لَوۡ تُسَوَّىٰ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضُ وَلَا يَكۡتُمُونَ ٱللَّهَ حَدِيثٗا
Siku hiyo walio kufuru na wakamuasi Mtume watatamani Ardhi isawazishwe juu yao. Wala hawataweza kumficha Mwenyezi Mungu neno lolote.
Yatapo tokea haya watatamani hao wapinzani wanao pinga lau kuwa wangeli potea chini ya Ardhi kama wanavyo potea maiti makaburini! Na wao hawawezi kumficha Mwenyezi Mungu kitu chochote katika mambo yao, na hali zao na vitendo vyao vitadhihiri.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَقۡرَبُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَأَنتُمۡ سُكَٰرَىٰ حَتَّىٰ تَعۡلَمُواْ مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغۡتَسِلُواْۚ وَإِن كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوۡ جَآءَ أَحَدٞ مِّنكُم مِّنَ ٱلۡغَآئِطِ أَوۡ لَٰمَسۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَلَمۡ تَجِدُواْ مَآءٗ فَتَيَمَّمُواْ صَعِيدٗا طَيِّبٗا فَٱمۡسَحُواْ بِوُجُوهِكُمۡ وَأَيۡدِيكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوًّا غَفُورًا
Enyi mlio amini! Msikaribie Sala, hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba - isipo kuwa mmo safarini - mpaka mkoge. Na mkiwa wagonjwa, au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake - na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi, mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Msamehevu na Mwenye kughufiria.
Enyi mlioamini! Msende kusali misikitini nanyi mmo katika hali ya ulevi mpaka muwe mnafahamu myasemayo. Wala msiingie misikitini nanyi mna janaba, ila ikiwa ni kupita njia tu bila ya kusita, mpaka mtahirike kwa kukoga. Na mkiwa ni wagonjwa hamuwezi kutumia maji kwa kuogopa maradhi yasikuzidini au kuchelewa kupona, au mkiwa mmo safarini na ipo shida ya kupata maji, basi tumieni mchanga ulio safi. Kadhaalika mmoja wenu akitoka chooni, au mkawaingilia wanawake na mkawa hamkupata maji ya kujitahirishia kwa kukosekana kwake, basi vile vile chukueni mchanga safi upigeni kwa mikono yenu, na mpangusie nyuso zenu na mikono yenu. Hakika ni shani ya Mwenyezi Mungu kuwa ni Mwenye kusamehe sana na Mwenye kufuta dhambi.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يَشۡتَرُونَ ٱلضَّلَٰلَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّواْ ٱلسَّبِيلَ
Huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wananunua upotovu na wanakutakeni nanyi mupotee Njia?
Hebu huyastaajabii mambo ya hawa walio pewa sehemu ya Vitabu vilivyo tangulia wanavyo acha uwongofu na wakatafuta upotovu katika mambo yaliyo wakhusu nafsi zao! Na wao tena wanakutakeni nyinyi mjitenge na Haki ambayo ndiyo Njia ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka!
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِأَعۡدَآئِكُمۡۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَلِيّٗا وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ نَصِيرٗا
Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema maadui zenu. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni Mlinzi, na anatosha kuwa ni Mwenye kukunusuruni.
Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi kuliko nyinyi kuwajua maadui zenu wa kweli, na anatambua zaidi yaliyo ndani ya nafsi zao. Ulinzi wa Mwenyezi Mungu unakulindeni, na unakuangalieni, na unakutosheni. Basi msitafute ulinzi wa mwenginewe usio kuwa wake. Msaada na nusura yake inakutoshelezeni; basi msiwe kutaka msaada wa mwenginewe.
Arabic explanations of the Qur’an:
مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْ يُحَرِّفُونَ ٱلۡكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِۦ وَيَقُولُونَ سَمِعۡنَا وَعَصَيۡنَا وَٱسۡمَعۡ غَيۡرَ مُسۡمَعٖ وَرَٰعِنَا لَيَّۢا بِأَلۡسِنَتِهِمۡ وَطَعۡنٗا فِي ٱلدِّينِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ قَالُواْ سَمِعۡنَا وَأَطَعۡنَا وَٱسۡمَعۡ وَٱنظُرۡنَا لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ وَأَقۡوَمَ وَلَٰكِن لَّعَنَهُمُ ٱللَّهُ بِكُفۡرِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُونَ إِلَّا قَلِيلٗا
Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangeli sema: Tumesikia na tumet'ii, na usikie na "Undhurna" (Utuangalie), ingeli kuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu.
Miongoni mwa Mayahudi kipo kikundi kazi yao kugeuza geuza maana ya maneno. Wao husema kimoyomoyo kumwambia Mtume s.a.w.: Tumesikia hayo maneno, na hatuifati hiyo amri. Na pia husema: Sikia maneno yetu - hukusikia wito. Wakikusudia kwa hayo kumuapiza Mtume. Na husema: Sikia bila ya kusikilizwa. Tamko hilo wanalipindua maana. Muradi wao ni kumuapiza, na wanajidai kuwa muradi wao ni kumwombea dua. Na husema: "Raai'na", wakipindua ndimi zao wakijitia kuwa wanakusudia "Undhurna" yaani "Tuangalie". Wanaonyesha kuwa wanataka uangalizi wake, na kumbe wanakusudia neno la Kiyahudi lenye maana ya "Mpumbavu" ili kuibeza Dini ya Kiislamu. Na lau kuwa wangeli nyooka sawa wakasema: "Tumesikia na tumet'ii" badala ya hiyo kauli yao ya "Tumesikia na tumeasi", na wakasema: "Sikia" na wasiseme "Bila ya kusikilizwa", na wakasema :"Undhurna" yaani "Tuangalie", badala ya "Raa'ina", ingeli kuwa bora kwao kuliko hayo wayasemayo, na ingeli kuwa ndiyo njia ya uadilifu zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu amewatoa katika rehema yake kwa ule upinzani wao. Kwa hivyo huwaoni miongoni mwao wanao mwitikia mwenye kuwaitia Imani ila wachache tu.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ ءَامِنُواْ بِمَا نَزَّلۡنَا مُصَدِّقٗا لِّمَا مَعَكُم مِّن قَبۡلِ أَن نَّطۡمِسَ وُجُوهٗا فَنَرُدَّهَا عَلَىٰٓ أَدۡبَارِهَآ أَوۡ نَلۡعَنَهُمۡ كَمَا لَعَنَّآ أَصۡحَٰبَ ٱلسَّبۡتِۚ وَكَانَ أَمۡرُ ٱللَّهِ مَفۡعُولًا
Enyi mlio pewa Kitabu! Aminini tuliyo yateremsha yenye kusadikisha yale mliyo nayo, kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni, au tukawalaani kama tulivyo walaani watu wa Sabato (Jumaamosi). Na amri ya Mwenyezi Mungu ni lazima ifanyike.
Enyi mlio pewa Kitabu alicho teremsha Mwenyezi Mungu! Iaminini Qur'ani tuliyo mteremshia Muhammad, inayo sadikisha mliyo nayo, kabla hatujawateremshia adhabu ya kufutwa nyuso zenu zikawa kama visogo, hazina pua, wala macho, wala nyusi. Au tukakutoeni katika rehema yetu kama tulivyo watoa wale walio ikhalifu amri yetu wakatenda waliyo katazwa ya kuvua samaki siku ya mapumziko,(Sabt au Sabato) siku ya Jumaamosi. Na hukumu ya Mwenyezi Mungu ni yenye kutimizwa tu, wala hapana cha kuipinga.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا
Hakika Mwenyezi Mungu hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika amezua dhambi kubwa.
Hakika Mwenyezi Mungu hafuti dhambi za ushirikina, kumfanya Yeye ana mshirika yeyote. Na husamehe dhambi zilio chini ya huo ushirikina kwa amtakaye miongoni mwa waja wake. Na mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi amemzulia Mwenyezi Mungu na ametenda dhambi kubwa mno isiyo stahiki kusamehewa.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يُزَكُّونَ أَنفُسَهُمۚ بَلِ ٱللَّهُ يُزَكِّي مَن يَشَآءُ وَلَا يُظۡلَمُونَ فَتِيلًا
Jee huwaoni wale wanao dai kuwa ati wametakasika? Bali Mwenyezi Mungu humtakasa amtakaye. Na hawatadhulumiwa hata kadiri ya kijiuzi kilichomo ndani ya uwazi wa kokwa ya tende.
Hustaajabii hali ya hao makafiri wanao zua kwa vitendo vyao? Vitendo vyao viovu wao wanaviona kuwa ni vizuri. Wanajisifu kuwa kwa vitendo hivyo wao wametakasika. Na ni Mwenyezi Mungu tu peke yake ndiye anaye jua jema na baya. Yeye ndiye wa kumtakasa amtakaye, na wala hamdhulumu mtu yeyote kadiri yake hata chembe.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱنظُرۡ كَيۡفَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَۖ وَكَفَىٰ بِهِۦٓ إِثۡمٗا مُّبِينًا
Tazama vipi wanavyo mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na haya yatosha kuwa dhambi iliyo dhaahiri.
Vipi watu hawa wanavyo mzulia Mwenyezi Mungu uwongo kwa haya na mengineyo mfano wa haya! Yatosha uwovu ulio wazi kwa huu uwongo wao kuyakashifu maovu yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبٗا مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡجِبۡتِ وَٱلطَّٰغُوتِ وَيَقُولُونَ لِلَّذِينَ كَفَرُواْ هَٰٓؤُلَآءِ أَهۡدَىٰ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ سَبِيلًا
Huwaoni wale walio pewa sehemu ya Kitabu? Wanaamini masanamu na Shet'ani! Na wanawasema walio kufuru, kuwa hao wameongoka zaidi katika njia kuliko Walio amini.
Hebu huwastaajabii hawa walio pewa sehemu ya ujuzi wa Kitabu wanavyo ridhia ibada ya masanamu na Shetani, na wanavyo sema kuwa hao waabuduo masanamu ni afadhali wameongoka kwenye Njia kuliko Waislamu wenye kuamini?
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ لَعَنَهُمُ ٱللَّهُۖ وَمَن يَلۡعَنِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ نَصِيرًا
Hao ndio Mwenyezi Mungu amewalaani. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemlaani basi hutamwona kuwa na mwenye kumnusuru.
Hao ndio alio watupa Mwenyezi Mungu na akawafukuzilia mbali kutoka kwenye rehema yake. Na mwenye kutupwa na Mwenyezi Mungu na akatolewa kwenye rehema yake basi kabisa huyo hana wa kumnusuru na kumlinda na ghadhabu ya Mola wake Mlezi.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ لَهُمۡ نَصِيبٞ مِّنَ ٱلۡمُلۡكِ فَإِذٗا لَّا يُؤۡتُونَ ٱلنَّاسَ نَقِيرًا
Au wanayo sehemu ya utawala? Basi hapo wasingewapa watu hata tundu ya kokwa ya tende.
Hao wamekoseshwa neema ya kuifuata haki, kama walivyo koseshwa na utawala. Na lau wakipewa utawala hawanufaishi watu hata chembe.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَمۡ يَحۡسُدُونَ ٱلنَّاسَ عَلَىٰ مَآ ءَاتَىٰهُمُ ٱللَّهُ مِن فَضۡلِهِۦۖ فَقَدۡ ءَاتَيۡنَآ ءَالَ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَءَاتَيۡنَٰهُم مُّلۡكًا عَظِيمٗا
Au wanawahusudu watu kwa yale aliyo wapa Mwenyezi Mungu kwa fadhila yake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikima na tukawapa utawala mkubwa.
Na vipi watu hawa wanavyo waonea maya Waarabu? Na wakaona ni jambo kuu kuwa Mwenyezi Mungu alivyo wapa fadhila yake kwa kuwatolea Nabii kutokana nao, na ilhali Mwenyezi Mungu alimpa Ibrahim na ukoo wake - naye ni baba yenu (Mayahudi na Wakristo), na baba yao (Waislamu pia) - Kitabu kilicho teremshwa kwa ufunuo, na Unabii na Utawala ulio mkubwa!
Arabic explanations of the Qur’an:
فَمِنۡهُم مَّنۡ ءَامَنَ بِهِۦ وَمِنۡهُم مَّن صَدَّ عَنۡهُۚ وَكَفَىٰ بِجَهَنَّمَ سَعِيرًا
Basi wapo miongoni mwao waliyo yaamini, na wapo walio yakataa. Na Jahannamu yatosha kuwa ni moto wa kuwateketeza.
Miongoni mwa walio pelekewa Nabii Ibrahim na ukoo wake wapo wenye kukiamini Kitabu kilicho teremshiwa kwao, na wapo walio kipa nyongo wakajitenga nacho. Na jaza ya hawa wenye kujitenga na wito wa Haki ni Jahannamu yenye moto wa kuteketeza.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَوۡفَ نُصۡلِيهِمۡ نَارٗا كُلَّمَا نَضِجَتۡ جُلُودُهُم بَدَّلۡنَٰهُمۡ جُلُودًا غَيۡرَهَا لِيَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَزِيزًا حَكِيمٗا
Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima.
Hakika wanao pinga hoja zetu zenye kubainisha wazi wazi, na wakawakanusha Manabii, tutakuja watia kwenye Moto utakao babua ngozi zao. Na kila zikisita kuhisi adhabu Mwenyezi Mungu atawabadilishia ngozi nyengine mpya ili machungu ya adhabu yabaki yakiendelea. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye ushindi katika mambo yake, na Mwenye hikima katika vitendo vyake. Humuadhibu mwenye kumpinga na akabaki na upinzani mpaka kufa kwake. Qur'an Tukufu imeitangulia sayansi ya kisasa, ikathibitisha kuwa katika ngozi mishipa ya kuhisi, Navo, imetanda kama wavu, na hiyo hupokea mishipa yote ya kuhisi machungu, joto na baridi na mengineyo. Na hayo hayakujuulikana ila hivi karibuni.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ لَّهُمۡ فِيهَآ أَزۡوَٰجٞ مُّطَهَّرَةٞۖ وَنُدۡخِلُهُمۡ ظِلّٗا ظَلِيلًا
Na wale walio amini na wakatenda mema tutawaingiza katika Pepo zipitazo mito kati yake kwa kudumu humo milele. Huko watakuwa na wake walio takasika, na tutawaingiza katika vivuli vizuri kweli.
Na ambao walio yasadiki yaliyo wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi, na wakatenda vitendo vyema, tutawalipa kwa Imani yao na vitendo vyao na tutawaingiza katika Mabustani ya Peponi yapitayo mito chini ya miti yake. Uhai wao hauna kikomo kabisa. Nao humo watakuwa na wake walio t'ahirika na kila la aibu na uchafu. Tutawapa uhai wa starehe chini ya vivuli vizuri vya kudumu, waishi maisha mema yenye neema isiyo kwisha.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ إِنَّ ٱللَّهَ يَأۡمُرُكُمۡ أَن تُؤَدُّواْ ٱلۡأَمَٰنَٰتِ إِلَىٰٓ أَهۡلِهَا وَإِذَا حَكَمۡتُم بَيۡنَ ٱلنَّاسِ أَن تَحۡكُمُواْ بِٱلۡعَدۡلِۚ إِنَّ ٱللَّهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِۦٓۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا
Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni nyinyi Waumini mrejeshe vyote mlio pewa amana, kutokana na Mwenyezi Mungu au kutokana na watu, kwa wenyewe kwa uadilifu. Basi msifanye jeuri katika kuhukumu. Haya ni mawaidha yanayo toka kwa Mola wenu Mlezi. Basi yafanyieni pupa kuyafuata. Bora ya mawaidha ni yanayo tokana naye Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu daima ni Mwenye kusikia yasemwayo, ni Mwenye kuyaona yatendwayo. Basi anamjua anaye rejesha amana, na anaye fanya khiana, na anaye hukumu kwa uadilifu, na anaye fanya jeuri. Na kila mmoja atamlipa kwa atendalo.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَأُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنكُمۡۖ فَإِن تَنَٰزَعۡتُمۡ فِي شَيۡءٖ فَرُدُّوهُ إِلَى ٱللَّهِ وَٱلرَّسُولِ إِن كُنتُمۡ تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِۚ ذَٰلِكَ خَيۡرٞ وَأَحۡسَنُ تَأۡوِيلًا
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.
Enyi mlio sadiki aliyo kuja nayo Muhammad! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, na wale wanao tawala mambo yenu miongoni mwa Waislamu wanao simama juu ya haki na uadilifu, na wanatekeleza Sharia ya Mwenyezi Mungu. Na mkizozana katika jambo baina yenu basi rejeeni kwenye Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake ili mpate kujua hukumu yake. Kwani Yeye Mwenyezi Mungu amekuteremshieni Kitabu chake na Mtume wake amebainisha hicho Kitabu. Na katika hayo ipo hukumu ya hayo mnayo khitalifiana kwayo. Haya ni kwa mujibu wa Imani yenu kumuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na haya ndio bora kwenu ili mpate kuongoka kwendea uadilifu katika mnayo khitalifiana kwayo, na mwisho wake ndio mzuri zaidi. Kwani hivyo ndio kuzuia zisitokee khilafu zinazo pelekea ugomvi na upotovu.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ يَزۡعُمُونَ أَنَّهُمۡ ءَامَنُواْ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُوٓاْ إِلَى ٱلطَّٰغُوتِ وَقَدۡ أُمِرُوٓاْ أَن يَكۡفُرُواْ بِهِۦۖ وَيُرِيدُ ٱلشَّيۡطَٰنُ أَن يُضِلَّهُمۡ ضَلَٰلَۢا بَعِيدٗا
Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yale yaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu, na hali wameamrishwa wakatae hayo! Na Shet'ani anataka kuwapotezelea mbali.
Ewe Nabii! Huwastaajabii hao wanao dai kuwa wanasadiki Kitabu ulicho teremshiwa wewe na vilivyo teremshwa kabla yako wewe, wanataka wahukumiwe katika ugomvi wao kwenye upotovu na uharibifu na hukumu isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu? Na Mwenyezi Mungu amekwisha waamrisha wayapinge hayo, wala wasitake kuhukumiwa kwa hayo. Na Shetani anataka awaachishe Njia ya Haki na Uwongofu, awapotezelee mbali.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ إِلَىٰ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ وَإِلَى ٱلرَّسُولِ رَأَيۡتَ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودٗا
Na wanapo ambiwa: Njooni kwenye yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, na njooni kwa Mtume; utawaona wanaafiki wanakukwepa kwa upinzani.
Na wakiambiwa: Njooni kwenye Qur'ani na Sharia aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu, na njooni kwa Mtume wake akubainishieni, utaona hao wanaafiki wanajitenga nawe kabisa wanakukataa.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَكَيۡفَ إِذَآ أَصَٰبَتۡهُم مُّصِيبَةُۢ بِمَا قَدَّمَتۡ أَيۡدِيهِمۡ ثُمَّ جَآءُوكَ يَحۡلِفُونَ بِٱللَّهِ إِنۡ أَرَدۡنَآ إِلَّآ إِحۡسَٰنٗا وَتَوۡفِيقًا
Basi inakuwaje unapo wasibu msiba kwa sababu ya yale iliyo tanguliza mikono yao? Hapo tena hukujia wakiapa kwa Mwenyezi Mungu wakisema: Hatukutaka ila wema na mapatano.
Itakuwaje hali basi yakiwateremkia masaibu kwa sababu ya uovu wao na upotovu wa vitendo vyao, na wasipate pa kukimbilia ila kwako! Hapo basi watakuapia Mungu mbele yako kuwa wao hawakukusudia kwa maneno yao na vitendo vyao ila wema tu na kutaka mapatano.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَعۡلَمُ ٱللَّهُ مَا فِي قُلُوبِهِمۡ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَعِظۡهُمۡ وَقُل لَّهُمۡ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَوۡلَۢا بَلِيغٗا
Hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu anayajua yaliyomo ndani ya nyoyo zao. Basi waachilie mbali, uwape mawaidha na uwaambie maneno ya kuathiri na kuingia katika nafsi zao.
Hao ndio wanao kula yamini kuwa hawakutaka ila wema na vitendo vya muwafaka. Mwenyezi Mungu anayajua vyema yaliyomo katika nyoyo zao, na anaujua uwongo wa hiyo kauli yao. Basi wewe usishughulike na maneno yao. Waite kwenye haki kwa mawaidha yaliyo mema, na sema nao maneno yenye hikima yenye kuathiri yanayo fika ndani ya nyoyo zao.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا لِيُطَاعَ بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ إِذ ظَّلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ جَآءُوكَ فَٱسۡتَغۡفَرُواْ ٱللَّهَ وَٱسۡتَغۡفَرَ لَهُمُ ٱلرَّسُولُ لَوَجَدُواْ ٱللَّهَ تَوَّابٗا رَّحِيمٗا
Na hatukumtuma Mtume yeyote ila at'iiwe kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na lau pale walipo jidhulumu nafsi zao wangeli kujia, wakamwomba Mwenyezi Mungu msamaha, na Mtume akawaombea msamaha, hapana shaka wangeli mkuta Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba na Mwenye kurehemu.
Na Sisi hatukumtuma Mtume yeyote ila jambo lake kuu ni kuwa at'iiwe, na ut'iifu huo ni kwa ruhusa iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu. Na hakika mwenye kwenda kinyume, au kukanusha, au kukhaalifu, anakuwa ni mwenye kujidhulumu mwenyewe. Na lau kuwa hawa walio jidhulumu wakirejea kwenye uwongofu, wakakujia wakiomba msamaha kutokana na Mwenyezi Mungu kwa yale waliyo yatenda, na wewe ukawaombea msamaha kwa mujibu wa ujumbe wako na kwa ulivyo ona ilivyo geuka hali yao, basi hapana shaka watamkuta Mwenyezi Mungu, Aliye takasika na kutukuka, ni Mwingi wa kukubali toba, na Mwenye kuwarehemu waja wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤۡمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيۡنَهُمۡ ثُمَّ لَا يَجِدُواْ فِيٓ أَنفُسِهِمۡ حَرَجٗا مِّمَّا قَضَيۡتَ وَيُسَلِّمُواْ تَسۡلِيمٗا
La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.
Naapa kwa jina la Mola wako Mlezi! Hawahisabiwi kuwa ni Waumini wa Haki na wenye kuinyenyekea, mpaka watakapo kufanya wewe hakimu muamuzi wa mizozo inayo tokea baina yao. Kisha nafsi zao zisione dhiki kwa utavyo hukumu, na wakunyenyekee kama wanavyo nyenyekea Waumini wa kweli.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَوۡ أَنَّا كَتَبۡنَا عَلَيۡهِمۡ أَنِ ٱقۡتُلُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ أَوِ ٱخۡرُجُواْ مِن دِيَٰرِكُم مَّا فَعَلُوهُ إِلَّا قَلِيلٞ مِّنۡهُمۡۖ وَلَوۡ أَنَّهُمۡ فَعَلُواْ مَا يُوعَظُونَ بِهِۦ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡ وَأَشَدَّ تَثۡبِيتٗا
Na lau kuwa tumewaamrisha: Jiueni, au tokeni majumbani kwenu, wasingeli fanya hayo ila wachache tu miongoni mwao. Na lau kama wangeli fanya walio waidhiwa ingeli kuwa bora kwao na uthibitisho wa nguvu zaidi.
Na lau kuwa Sisi tumewalazimisha mashaka ya mwisho, kwa kuwaamrisha wapigane Jihadi moja kwa moja, na wajitolee nafsi zao kutilifu, au watoke nje waache majumba yao kwenda pigana Jihadi daima, wasinge kubali kut'ii ila wachache tu. Lakini Mwenyezi Mungu, Aliye takasika na kutukuka, hakalifishi ila linalo wezekana. Na lau kuwa wange fanya hayo na wakafuata haki yake ingeli kuwa ni kheri yao ya duniani na Akhera. Na hivyo ndiyo inavyo pelekea kuthibiti Imani, na kuingia imara, na kuleta utulivu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذٗا لَّأٓتَيۡنَٰهُم مِّن لَّدُنَّآ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Na hapo tunge wapa malipo makubwa kutoka kwetu.
Na lau kuwa wamesimama juu ya Haki aliyo ilazimisha Mwenyezi Mungu kwa kadri ya uweza wao, Mwenyezi Mungu angeli wapa malipo makubwa kwa fadhila yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَهَدَيۡنَٰهُمۡ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا
Na tungeli waongoa Njia iliyo nyooka.
Na kwa sababu ya kut'ii kwao kwa uweza wao inakuwa hakika Mwenyezi Mungu amewaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka isio pindukia kiasi kwa kuzidi au kupungua.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يُطِعِ ٱللَّهَ وَٱلرَّسُولَ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلَّذِينَ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِم مِّنَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ وَٱلصِّدِّيقِينَ وَٱلشُّهَدَآءِ وَٱلصَّٰلِحِينَۚ وَحَسُنَ أُوْلَٰٓئِكَ رَفِيقٗا
Na wenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao wa pamoja na wale alio waneemesha Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii, na Masiddiqi, na Mashahidi, na Watu wema. Na uzuri ulioje kuwa pamoja na watu hao!
Na mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume kwa kuzifuata kwa unyenyekevu amri zao na kuridhia hukumu yao, basi huyo yu pamoja na alio waneemesha Mwenyezi Mungu kwa uwongofu na kuwawezesha duniani na Akhera. Na watu hao ni Manabii wake, na wafuasi wao walio wasadiki na kuwakubali na wakafuata nyendo zao, na Mashahidi walio kufa katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na watu wema watendao mema kwa siri na dhaahiri. Na hapana la kushinda uzuri kuliko kuwa pamoja na watu hawa - haingii mashakani mwenye kukaa nao, wala hayachoshi mazungumzo yao.
Arabic explanations of the Qur’an:
ذَٰلِكَ ٱلۡفَضۡلُ مِنَ ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ عَلِيمٗا
Hiyo ni fadhila itokayo kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kutosha.
Hayo ni makao matukufu kwa mwenye kumt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hiyo ni fadhila kubwa inayo tokana na Mwenyezi Mungu. Naye anavijua sana vitendo vyenu, naye atakulipeni kwavyo. Yamtosha Muumini kuwa Mwenyezi Mungu anamjua, naye lake ni kumt'ii Mola wake Mlezi na kutafuta radhi zake.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ خُذُواْ حِذۡرَكُمۡ فَٱنفِرُواْ ثُبَاتٍ أَوِ ٱنفِرُواْ جَمِيعٗا
Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu! Na mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!
Enyi Mlio amini! Daima kuweni na hadhari na maadui wenu. Jizatitini kupambana na vitimbi vyao. Na mkitoka kwenda vitani tokeni kwa vikosi vikosi, au tokeni nyote pamoja.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنَّ مِنكُمۡ لَمَن لَّيُبَطِّئَنَّ فَإِنۡ أَصَٰبَتۡكُم مُّصِيبَةٞ قَالَ قَدۡ أَنۡعَمَ ٱللَّهُ عَلَيَّ إِذۡ لَمۡ أَكُن مَّعَهُمۡ شَهِيدٗا
Na yupo kati yenu anaye bakia nyuma; na ukikusibuni msiba husema: Mwenyezi Mungu kanifanyia kheri sikuwa nao.
Na wahadharisheni wanao kaa nyuma wasende nanyi vitani. Miongoni mwa hao mnao ishi nao wakajizuia wasifuatane nanyi kwenda kupigana, mkipatwa na shida na masaibu katika Jihadi, wao wa kikundi hicho, kwa kufurahia yaliyo kusibuni, husema: Mwenyezi Mungu katufanyia kheri kwa kuwa hatukwenda nao vitani.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَئِنۡ أَصَٰبَكُمۡ فَضۡلٞ مِّنَ ٱللَّهِ لَيَقُولَنَّ كَأَن لَّمۡ تَكُنۢ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُۥ مَوَدَّةٞ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ مَعَهُمۡ فَأَفُوزَ فَوۡزًا عَظِيمٗا
Na ikIkufikieni Fadhila kutoka kwa Mwenezi Mungu husema, kama kwamba hapakuwa mapenzi baina yenu naye, laiti ni ngekuwa baina yao nikafanikiwa Mafanikio makubwa
Na mnapo pata fadhila ya ushindi kutokana na Mwenyezi Mungu, mkapata ngawira za vita, kikundi hicho hicho, kwa kuona maya na kutamani, husema: Laiti tungeli kuwa nao katika vita hivi, nasi tukapata mafanikio ya ngawira nzuri. Na husema haya na hayo kama kwamba hapakuwepo mapenzi yoyote yaliyo wafunga wao na nyinyi.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ فَلۡيُقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ ٱلَّذِينَ يَشۡرُونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا بِٱلۡأٓخِرَةِۚ وَمَن يُقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَيُقۡتَلۡ أَوۡ يَغۡلِبۡ فَسَوۡفَ نُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Basi nawapigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu wale ambao wanao uza uhai wa dunia kwa Akhera. Na anaye pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kisha akauliwa au akashinda basi tutakuja mpa ujira mkubwa.
Ikiwa yupo kati yenu anaye bakia nyuma asende kupigana kutokana na udhaifu wa Imani yake, au ulegevu wa azma yake, basi na wapigane, kuinua Neno la Mwenyezi Mungu na kuwania Haki, wale walio uza uhai wao wa dunia kutafuta uhai wa Akhera. Na mwenye kupigana vita kwa ajili ya kunyanyua Neno la Mwenyezi Mungu na kuwania Haki, atapata moja ya mema mawili. Ama atauliwa apate fadhila ya kufa shahidi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, au atashinda, apate fadhila ya kufuzu katika dunia. Naye katika hali zote mbili atapewa na Mwenyezi Mungu ujira mkubwa katika Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا لَكُمۡ لَا تُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخۡرِجۡنَا مِنۡ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهۡلُهَا وَٱجۡعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيّٗا وَٱجۡعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا
Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.
Vipi inakufalieni kuwa msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na hali wanyonge, wanaume na wanawake na watoto wao, wanayayatika kuomba msaada wa kuwanusuru, huku wakimwomba Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu wakisema: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutoe kwenye utawala wa hawa madhaalimu, na kwa nguvu zako na rehema yako tuwezeshe tuwe chini ya utawala wa Waumini; na tujaalie kutoka kwako mgombozi wa kutunusuru!
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِ ٱلطَّٰغُوتِ فَقَٰتِلُوٓاْ أَوۡلِيَآءَ ٱلشَّيۡطَٰنِۖ إِنَّ كَيۡدَ ٱلشَّيۡطَٰنِ كَانَ ضَعِيفًا
Walio amini wanapigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio kufuru wanapiana katika njia ya upotofu. Basi piganeni na marafiki wa Shet'ani. Hakika hila za Shet'ani ni dhaifu.
Walio isadiki Haki na wakaifuata, hupigana kwa ajili ya kulitukuza Neno la Mwenyezi Mungu, na uadilifu, na Haki. Na wale wanao pinga wakafanya inadi hupigana kwa ajili ya dhulma na uharibifu. Kwa hivyo hawa wamekuwa ni vipenzi vya Shetani. Basi enyi Waumini! Wapigeni vita hao, kwani wao ni wenzake Shetani na wasaidizi wake. Na jueni kuwa nyinyi mtawashinda tu kwa kuungwa mkono na Mwenyezi Mungu, kwani mpango wa Shetani, na ingawa mkubwa vipi ufisadi wake, ni dhaifu, hauna nguvu. Na Haki ndiyo yenye ushindi.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَلَمۡ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ قِيلَ لَهُمۡ كُفُّوٓاْ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَءَاتُواْ ٱلزَّكَوٰةَ فَلَمَّا كُتِبَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقِتَالُ إِذَا فَرِيقٞ مِّنۡهُمۡ يَخۡشَوۡنَ ٱلنَّاسَ كَخَشۡيَةِ ٱللَّهِ أَوۡ أَشَدَّ خَشۡيَةٗۚ وَقَالُواْ رَبَّنَا لِمَ كَتَبۡتَ عَلَيۡنَا ٱلۡقِتَالَ لَوۡلَآ أَخَّرۡتَنَآ إِلَىٰٓ أَجَلٖ قَرِيبٖۗ قُلۡ مَتَٰعُ ٱلدُّنۡيَا قَلِيلٞ وَٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّمَنِ ٱتَّقَىٰ وَلَا تُظۡلَمُونَ فَتِيلًا
Je, huwaoni wale walio ambiwa: Izuieni mikono yenu, na mshike Swala na mtoe Zaka. Na walipo amrishwa kupigana, mara kundi moja kati yao liliwaogopa watu kama kumwogopa Mwenyezi Mungu, au kwa khofu kubwa zaidi. Na wakasema: Mola Mlezi wetu! Kwa nini umetuamrisha kupigana? Laiti unge tuakhirishia kiasi ya muda kidogo hivi! Sema: Starehe ya dunia ni ndogo, na Akhera ni bora zaidi kwa mwenye kuchamngu. Wala hamtadhulumiwa hata uzi wa kokwa ya tende.
Ewe Muhammad! Hebu huwaangalii ukawastaajabia wale walio taka kupigana kabla ya kuja ruhusa, wakaambiwa: Bado haujafika wakati wa vita. Basi izuieni mikono yenu msipigane. Bali shughulikieni kushika Swala, na kutoa Zaka. Na Mwenyezi Mungu alipo waamrisha wapigane kikawa kikundi kimoja kati yao kikawa kinawaogopa watu kama kumkhofu Mwenyezi Mungu, au zaidi. Wakasema kwa kuona ni mageni hayo: Kwa nini ukatuamrisha kupigana? Wao walidhani kuwa kuamrishwa vita kunahimiza ajali yao, na kwa hivyo wakasema: Hebu lau ungeli tungojea muda kidogo tupate kustarehe na ulimwengu! Waambie: Songeni mbele mkapigane hata ikiwa mtakufa mashahidi, kwani starehe ya dunia, ingawa ni kubwa vipi, ni chache ukilinganisha na starehe ya Akhera. Na Akhera ni bora na kubwa zaidi kwa mwenye kumcha Mwenyezi Mungu, na huko mtakuja lipwa kwa vitendo vyenu vya duniani, wala hampunguziwi hata chembe katika ujira wenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَيۡنَمَا تَكُونُواْ يُدۡرِككُّمُ ٱلۡمَوۡتُ وَلَوۡ كُنتُمۡ فِي بُرُوجٖ مُّشَيَّدَةٖۗ وَإِن تُصِبۡهُمۡ حَسَنَةٞ يَقُولُواْ هَٰذِهِۦ مِنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ وَإِن تُصِبۡهُمۡ سَيِّئَةٞ يَقُولُواْ هَٰذِهِۦ مِنۡ عِندِكَۚ قُلۡ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ ٱللَّهِۖ فَمَالِ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلۡقَوۡمِ لَا يَكَادُونَ يَفۡقَهُونَ حَدِيثٗا
Popote mlipo mauti yatakufikieni, na hata mkiwa katika ngome zilizo na nguvu. Na likiwafikilia jema wanasema: Hili limetoka kwa Mwenyezi Mungu. Na likiwafikilia ovu wanasema: Hili limetoka kwako wewe. Sema: Yote yanatokana na Mwenyezi Mungu. Basi wana nini watu hawa hata hawakaribii kufahamu maneno?
Hakika hayo mauti mnayo yakimbia yatakukuteni popote pale mlipo, na hata mkikaa ndani ya ngome zilizo jengwa madhubuti imara. Na hao wenye imani legevu na dhaifu husema pindi wapatapo ushindi na ngawira: Haya yametoka kwa Mwenyezi Mungu. Na pindi wapatapo lawama au kushindwa wao hukwambia wewe: Ewe Muhammad! Haya yanatokana na wewe. Haya si lolote ila kukufanya kuwa wewe ni mkorofi, na kukutupia lawama wewe badala ya nafsi zao. Basi waambie: Kila linalo kupateni, mnalo lipenda na mnalo lichukia, linatokana na kudra ya Mwenyezi Mungu, na linatokana na majaribio yake na mitihani yake. Wana nini watu hawa madhaifu hata hawajakaribia kujua usawa wa maneno wanayo ambiwa?
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّآ أَصَابَكَ مِنۡ حَسَنَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ وَمَآ أَصَابَكَ مِن سَيِّئَةٖ فَمِن نَّفۡسِكَۚ وَأَرۡسَلۡنَٰكَ لِلنَّاسِ رَسُولٗاۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدٗا
Jema lilio kufikia limetokana na Mwenyezi Mungu. Na ovu lilio kusibu linatokana na nafsi yako. Nasi tumekutuma kwa watu uwe ni Mtume. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kutosha.
Ewe Nabii! Kufanikiwa, na neema, na afya, na salama unayo ipata inatokana na fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako. Yeye anafanya haya kukufadhili kukufanyia hisani. Na inapo kusibu shida, na mashaka, na udhiya, na ya karaha, basi yanatokana na nafsi yako mwenyewe kwa sababu ya upungufu fulani au makosa uliyo yatenda. Haya anaambiwa Mtume s.a.w. ni kama mfano wa wanaadamu wote ijapo kuwa halikutokea kwake la uovu. Kwani Mtume anaambiwa: Tumekutuma kuwa Mtume kutoka kwetu kwa watu wote. Na Mwenyezi Mungu ni shahidi wa kufikisha kwako huo ujumbe na juu ya kuitikia kwao hao watu. Na Yeye ni Mjuzi wa kutosha.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّن يُطِعِ ٱلرَّسُولَ فَقَدۡ أَطَاعَ ٱللَّهَۖ وَمَن تَوَلَّىٰ فَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ حَفِيظٗا
Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu. Na anaye kengeuka, basi Sisi hatukukutuma wewe uwe ni mlinzi wao.
Mwenye kumt'ii Mtume basi ndio amemt'ii Mwenyezi Mungu, kwani yeye haamrishi ila alicho amrisha Mwenyezi Mungu. Wala hakatazi ila alicho kataza Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo kumt'ii yeye (Mtume s.a.w.) ndio kutenda na kuacha kwa ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. Na mwenye kukataa kukut'ii wewe basi, kwani Sisi hatukukupeleka wewe ila uwe ni mbashiri na mwonyaji tu, sio uwe ni mlinzi wao na muangalizi wao, uwalindie vitendo vyao. Hayo ni yetu Sisi sio yako.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَقُولُونَ طَاعَةٞ فَإِذَا بَرَزُواْ مِنۡ عِندِكَ بَيَّتَ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ غَيۡرَ ٱلَّذِي تَقُولُۖ وَٱللَّهُ يَكۡتُبُ مَا يُبَيِّتُونَۖ فَأَعۡرِضۡ عَنۡهُمۡ وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱللَّهِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا
Na wanasema: Tunat'ii. Lakini wanapo toka kwako kundi moja miongoni mwao hupanga njama usiku kinyume na unayo yasema. Na Mwenyezi Mungu anayaandika yote hayo wanayo yapangia njama za usiku. Basi waachilie mbali, na umtegemee Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.
Na kikundi hichi kinacho tapatapa husema: Amri yako tunait'ii. Hatuna kwako ila kut'ii unayo amrisha na kukataza. Lakini wakisha toka kwako wakawa mbali nawe, baadhi yao hupanga vijambo vyao usiku usiku, kinyume na unavyo waambia ya kuwaamrisha na kuwakataza. Na Mwenyezi Mungu, Subhanahu wa Taa'la, Aliye takasika na Kutukuka, anayadhibiti yote wanayo yapanga kwa siri. Basi usiwashughulikie, na wapuuze, na mwachie mambo yao Mwenyezi Mungu, na wewe mtegemee Yeye. Na Mwenyezi Mungu ni wa kutosha kuwa ni Mtegemewa wako, na Mlinzi wako wa kumwachilia mambo yako yote.
Arabic explanations of the Qur’an:
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ ٱلۡقُرۡءَانَۚ وَلَوۡ كَانَ مِنۡ عِندِ غَيۡرِ ٱللَّهِ لَوَجَدُواْ فِيهِ ٱخۡتِلَٰفٗا كَثِيرٗا
Hebu hawaizingatii hii Qur'ani? Na lau kuwa imetoka kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangeli kuta ndani yake khitilafu nyingi.
Basi hao wanaafiki hawakizingatii Kitabu cha Mwenyezi Mungu wakajua hoja za Mwenyezi Mungu zilio juu yao kuwa ni waajibu kut'ii na kufuata amri yako? Na kwamba Kitabu hichi kinatoka kwa Mwenyezi Mungu kwa yalivyo shikamana maana yake na hukumu zake, na kinavyo fungamana wenyewe kwa wenyewe? Hii ni dalili kuwa ni kweli kinatoka kwa Mwenyezi Mungu; kwani lau kuwa kinatokana na mwenginewe basi maana yake yangeli gongana, na hukumu zake zingeli khitalifiana sana.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا جَآءَهُمۡ أَمۡرٞ مِّنَ ٱلۡأَمۡنِ أَوِ ٱلۡخَوۡفِ أَذَاعُواْ بِهِۦۖ وَلَوۡ رَدُّوهُ إِلَى ٱلرَّسُولِ وَإِلَىٰٓ أُوْلِي ٱلۡأَمۡرِ مِنۡهُمۡ لَعَلِمَهُ ٱلَّذِينَ يَسۡتَنۢبِطُونَهُۥ مِنۡهُمۡۗ وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ وَرَحۡمَتُهُۥ لَٱتَّبَعۡتُمُ ٱلشَّيۡطَٰنَ إِلَّا قَلِيلٗا
Na linapo wafikia jambo lolote lilio khusu amani au la kitisho wao hulitangaza. Na lau kuwa wangeli lipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanao chunguza wangeli lijua. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu na rehema yake mngeli mfuata Shet'ani ila wachache wenu tu.
Na hichi kikundi cha wanaafiki kikipata khabari zozote zilio khusu nguvu au udhaifu wa Waislamu huzitangaza na kuzieneza nje, ili kuwababaisha Waislamu au kuwatia khofu katika nyoyo zao, au ili zifike khabari zao kwa maadui wao. Na lau kuwa hawa wanaafiki watangazao wamerudisha jambo lilio kuhusu usalama au kitisho kwa Mtume na kwa wakuu wa mambo miongoni mwa waongozi na Masahaba wakubwa, wakataka kwao kujua hakika, wangeli jua hao wanao jitahidi kuchungua mambo na kuyatangaza, kuwa yaliyo kweli yanatokana na Mtume na waongozi wengine. Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yenu kwa alivyo zithibitisha nyoyo zenu juu ya Imani, na kuzuia fitina, na rehema yake kwa kukupeni sababu na njia za ushindi, wengi wenu wangeli fuata upotovu wa Shetani, na wasingeli okoka kutokana na upotovu wake ila wachache tu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَقَٰتِلۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ لَا تُكَلَّفُ إِلَّا نَفۡسَكَۚ وَحَرِّضِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَكُفَّ بَأۡسَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۚ وَٱللَّهُ أَشَدُّ بَأۡسٗا وَأَشَدُّ تَنكِيلٗا
Basi pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Hukalifishwi ila nafsi yako tu. Na wahimize Waumini. Huenda Mwenyezi Mungu akayazuia mashambulio ya walio kufuru. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mkali zaidi wa kushambulia na Mkali zaidi wa kuadhibu.
Na kama wapo kati yenu mfano wa hawa wanaafiki basi wapuuzilie mbali. Na wewe pigana kwa ajili ya Neno la Mwenyezi Mungu na kwa ajili ya Haki. Wewe huna jukumu ila la nafsi yako tu. Kisha waite Waumini wende vitani, na wahimize. Huenda Mwenyezi Mungu kwa kupitia kwako na kwao akazuia hayo mashambulio ya makafiri. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kukuungeni mkono, na ni Mwenye kukunusuruni. Na Yeye ana nguvu kuliko wote, na mkali kuliko wote katika kuwaadhibu makafiri.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّن يَشۡفَعۡ شَفَٰعَةً حَسَنَةٗ يَكُن لَّهُۥ نَصِيبٞ مِّنۡهَاۖ وَمَن يَشۡفَعۡ شَفَٰعَةٗ سَيِّئَةٗ يَكُن لَّهُۥ كِفۡلٞ مِّنۡهَاۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ مُّقِيتٗا
Mwenye kusaidia msaada mwema ana fungu lake katika hayo, na mwenye kusaidia msaada mwovu naye ana sehemu yake katika hayo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza na ujuzi juu ya kila kitu.
Na hawa wanaafiki husaidia ufisadi, na watu wa Imani husaidia Haki. Na mwenye kusaidia jambo jema ana fungu lake la thawabu. Na mwenye kuwasaidia watu waovu naye ana mzigo wake wa dhambi katika malipo yake. Na Mwenyezi Mungu ana uweza juu ya kila kitu, na Mwenye kujua kila kitu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا حُيِّيتُم بِتَحِيَّةٖ فَحَيُّواْ بِأَحۡسَنَ مِنۡهَآ أَوۡ رُدُّوهَآۗ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَسِيبًا
Na mnapo amkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuhisabu kila kitu.
Akikuamkieni mtu yeyote kwa maamkio ya salamu, au dua, au ya namna yoyote ya hishima, au namna nyengine yoyote ile, basi mjibuni kwa maamkio yaliyo mazuri zaidi, au kwa uchache mjibuni kama alivyo kuamkieni yeye. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kutia hisabuni kila kitu, kikubwa na kidogo.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ لَيَجۡمَعَنَّكُمۡ إِلَىٰ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا رَيۡبَ فِيهِۗ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ حَدِيثٗا
Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Kwa yakini atakukusanyeni Siku ya Kiyama. Halina shaka hilo. Na ni nani msema kweli kuliko Mwenyezi Mungu?
Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu ila Yeye, wala hapana mwenye uweza ila Yeye, hapana shaka atakufufueni baada ya kufa kwenu, na atakukusanyeni kwenye kituo cha kuhisabiwa kwa ajili ya malipo. Hayo hayana shaka. Yeye anasema hayo, basi msiyatilie shaka maneno yake. Na kauli gani iliyo ya kweli zaidi kuliko kauli ya Mwenyezi Mungu?
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ فَمَا لَكُمۡ فِي ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِئَتَيۡنِ وَٱللَّهُ أَرۡكَسَهُم بِمَا كَسَبُوٓاْۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَهۡدُواْ مَنۡ أَضَلَّ ٱللَّهُۖ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا
Mmekuwaje kuwa makundi mawili kwa khabari ya wanaafiki, na hali Mwenyezi Mungu amewageuza kwa sababu ya yale waliyo yachuma? Je! Mnataka kumwona mwongofu ambaye Mwenyezi Mungu amemhukumu kuwa kapotea? Na aliye mhukumu Mwenyezi Mungu kuwa amekwisha potea wewe hutampatia njia.
Haikufaliini, enyi Waumini, kukhitalifiana katika mas-ala yaliyo khusu wanaafiki, ambao wanadhihirisha Uislamu na wanaficha ukafiri. Haikufaliini kukhitalifiana kwa mas-ala yao, kuwa ati wao ni Waumini au makafiri? Wauwawe au waachiliwe? Je, wameelekea kuongoka au hawatarajiwi uwongofu? Fahamu zao zimegeuzwa kwa yaliyo chumwa na vitendo vyao. Shari imekuwa ndio inayo wahukumu, basi usimtarajie kuongoka yule ambaye Mwenyezi Mungu kwa ujuzi wake wa tangu na tangu kesha mkadiria asiongoke. Kwani aliye andikwa katika ujuzi wa Mwenyezi Mungu wa tangu azali kuwa ni mwenye kupotea basi huna njia ya kumwongoa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ كَمَا كَفَرُواْ فَتَكُونُونَ سَوَآءٗۖ فَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ أَوۡلِيَآءَ حَتَّىٰ يُهَاجِرُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِۚ فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ وَجَدتُّمُوهُمۡۖ وَلَا تَتَّخِذُواْ مِنۡهُمۡ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرًا
Wanapenda lau kuwa nanyi mnge kufuru kama walivyo kufuru wao, ili muwe sawa sawa. Basi msiwafanye marafiki miongoni mwao mpaka wahame kwa ajili ya Dini ya Mwenyezi Mungu. Na wakikengeuka basi wakamateni na wauweni popote mnapo wapata. Wala msimfanye rafiki katika wao wala msaidizi.
Hakika nyinyi mnapenda kuwaongoa hawa wanaafiki, na wao wanapenda nyinyi mkufuru kama wao, ili muwe nyote sawa kwa ukafiri. Ilivyo kuwa hivyo basi msitake wa kukuungeni mkono miongoni mwao. Wala msiwafanye wenzenu, mpaka wakubali kutoka huko kwao kuwania Jihadi kwa ajili ya Uislamu. Hivyo tu ndio itawatoka sifa ya unaafiki. Lakini wakiyakataa hayo, wakaungana na maadui zenu, basi wauweni popote mtapo wapata, wala msiwaone kuwa ni wenzenu, wala msiwachukulie kuwa ndio wasaidizi wenu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا ٱلَّذِينَ يَصِلُونَ إِلَىٰ قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٌ أَوۡ جَآءُوكُمۡ حَصِرَتۡ صُدُورُهُمۡ أَن يُقَٰتِلُوكُمۡ أَوۡ يُقَٰتِلُواْ قَوۡمَهُمۡۚ وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَسَلَّطَهُمۡ عَلَيۡكُمۡ فَلَقَٰتَلُوكُمۡۚ فَإِنِ ٱعۡتَزَلُوكُمۡ فَلَمۡ يُقَٰتِلُوكُمۡ وَأَلۡقَوۡاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ فَمَا جَعَلَ ٱللَّهُ لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سَبِيلٗا
Isipokuwa wale walio fungamana na watu ambao mna ahadi baina yenu na wao, au wanakujieni na vifua vyao vina dhiki kupigana nanyi, au kupigana na watu wao. Na lau angeli penda Mwenyezi Mungu angeli wasaliti juu yenu wakapigana nanyi. Basi wakijitenga nanyi, wasipigane nanyi, na wakakuleteeni amani, basi Mwenyezi Mungu hakukupeni njia kupigana nao.
Katika wanaafiki, wanao stahiki kuuliwa kwa fisadi yao kuwafisidi umma wa Waumini, watoe wale ambao wamefungamana na kaumu ambao baina yao na Waumini yapo mapatano ya kuzuia kuuliwa aliye fungamana na upande mmoja wapo. Au vile vile ambao wametatizwa hawajui wapigane pamoja na watu wao, ambao ni maadui wa Waislamu wasio na mkataba nao, au wapigane pamoja na Waumini? Kwani hakika wale wa kwanza inakatazwa kuwauwa kwa ajili ya mkataba, na wengine inakatazwa kuwauwa kwa kuwa hawajui moja wapo la kutenda. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amependa angeli wajaalia hao wakupigeni vita. Ilivyo kuwa wamekhiari kukaa tu wasikupigeni na wakaingiana nanyi kwa salama na amani, basi haikufaliini nyinyi kuwauwa. Hapana ruhusa kufanya hayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
سَتَجِدُونَ ءَاخَرِينَ يُرِيدُونَ أَن يَأۡمَنُوكُمۡ وَيَأۡمَنُواْ قَوۡمَهُمۡ كُلَّ مَا رُدُّوٓاْ إِلَى ٱلۡفِتۡنَةِ أُرۡكِسُواْ فِيهَاۚ فَإِن لَّمۡ يَعۡتَزِلُوكُمۡ وَيُلۡقُوٓاْ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَمَ وَيَكُفُّوٓاْ أَيۡدِيَهُمۡ فَخُذُوهُمۡ وَٱقۡتُلُوهُمۡ حَيۡثُ ثَقِفۡتُمُوهُمۡۚ وَأُوْلَٰٓئِكُمۡ جَعَلۡنَا لَكُمۡ عَلَيۡهِمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينٗا
Mtawakuta wengine wanataka wapate salama kwenu na salama kwa watu wao. Kila wakirudishwa kwenye fitna hudidimizwa humo. Ikiwa hawajitengi nanyi, na wakakuleteeni salama, na wakazuia mikono yao, basi wakamateni na wauweni popote mnapo wakuta. Na juu ya hao ndio tumekupeni hoja zilizo wazi.
Mkiwashinda washirikina, hao wanaafiki huwa pamoja nanyi; na washirikina wakiwashinda Waislamu, wao huwa pamoja na washirikina. Wao hutaka wapate amani kwa Waislamu na wapate amani kwa jamaa zao washirikina. Hawa wamo katika upotovu na unaafiki wa moja kwa moja. Ikiwa hawatoacha kukupigeni vita na wakakutangazieni amani na salama, basi wauweni popote muwapatapo. Kwani kwa kuto kujitenga na kukupigeni vita, basi inakuwa Waumini wana haki kuwauwa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewapa Waumini hoja iliyo wazi kuwapiga vita.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَا كَانَ لِمُؤۡمِنٍ أَن يَقۡتُلَ مُؤۡمِنًا إِلَّا خَطَـٔٗاۚ وَمَن قَتَلَ مُؤۡمِنًا خَطَـٔٗا فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖ وَدِيَةٞ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦٓ إِلَّآ أَن يَصَّدَّقُواْۚ فَإِن كَانَ مِن قَوۡمٍ عَدُوّٖ لَّكُمۡ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖۖ وَإِن كَانَ مِن قَوۡمِۭ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَهُم مِّيثَٰقٞ فَدِيَةٞ مُّسَلَّمَةٌ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ وَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مُّؤۡمِنَةٖۖ فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ تَوۡبَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Kuwagawa wanaafiki namna hii ni kwa ajili ya kutoka shakani, ili Muumini asimuuwe Muumini mwenziwe kwa kumdhania kuwa ni mnaafiki. Na haijuzu kumuuwa Muumini ila kwa kukosea, bila ya kukusudia. Na katika hali ya kumuuwa Muumini kwa kukosea akiwa anaishi chini ya utawala wa dola ya Kiislamu, basi atatoa muuwaji diya kuwapa walio fiwa kuwa ni fidia kwa mtu waliye mkosa, na tena amkomboe mtumwa aliye Muumini iwe ni kuwafidia umma wa Kiislamu kwa walicho kosa. Kwani kumkomboa Muumini ni kama kumhuisha mtu kwa kumpatia uhuru. Inakuwa kwa kukomboa shingo ya Muumini ni kuulipa umma wa Kiislamu kwa walicho kosa. Ikiwa aliye uliwa yumo katika watu ambao wana mapatano ya amani na Waislamu, basi yapasa kumpa uhuru mtumwa na kuwalipa watu wa maiti diya, kwani inakuwa hawaichukui hiyo diya kwa kuwaudhi Waislamu kwa sababu ya mapatano yao. Na ikiwa mwenye kuuwa bila ya kukusudia hakupata mtumwa Muumini wa kumkomboa, basi afunge miezi miwili mfululizo, asile mchana hata siku moja. Hayo yawe ni kuitengeza nafsi na kujizoesha kuwa na hadhari zaidi. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka anazijua sana nafsi za watu na niya zao. Naye ni Mwenye hikima, anajua kuzipanga adhabu zake. "Kuulipa" kwa kuwa utumwa ni amana ya mtu, na kumkomboa mtumwa ni kumhuisha mtu. Akiuliwa Muumini kwa kukosea, na mwenye kuuwa akakomboa shingo ya Muumini basi huyo amehuisha na kuulipa umma.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَقۡتُلۡ مُؤۡمِنٗا مُّتَعَمِّدٗا فَجَزَآؤُهُۥ جَهَنَّمُ خَٰلِدٗا فِيهَا وَغَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِ وَلَعَنَهُۥ وَأَعَدَّ لَهُۥ عَذَابًا عَظِيمٗا
Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.
Hakika mwenye kumuuwa Muumini kwa mauwaji ya kukusudia na kuona ndio ndivyo mauwaji hayo, Jaza yake inayo lingana na ukhalifu huo ni kuingizwa Motoni milele, na kughadhibikiwa na Mwenyezi Mungu na afukuzwe kutokana na rehema yake. Na Mwenyezi Mungu amemtengezea Akhera adhabu kubwa, kwani kitendo hichi ndio ukhalifu mkubwa kabisa katika dunia.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَتَبَيَّنُواْ وَلَا تَقُولُواْ لِمَنۡ أَلۡقَىٰٓ إِلَيۡكُمُ ٱلسَّلَٰمَ لَسۡتَ مُؤۡمِنٗا تَبۡتَغُونَ عَرَضَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ مَغَانِمُ كَثِيرَةٞۚ كَذَٰلِكَ كُنتُم مِّن قَبۡلُ فَمَنَّ ٱللَّهُ عَلَيۡكُمۡ فَتَبَيَّنُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا
Enyi mlio amini! Mnapo safiri katika Njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni, wala msimwambie anaye kutoleeni salamu: Wewe si Muumini; kwa kutaka manufaa ya maisha ya dunia hii, hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu zipo ghanima nyingi. Hivyo ndivyo mlivyo kuwa nyinyi zamani, na Mwenyezi Mungu akakuneemesheni. Basi chunguzeni sawa sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda
Kutahadhari msije mkamuuwa Muumini ni waajibu katika wakati wa kwenda vitani. Mkisafiri kwa ajili ya Jihadi ya Njia ya Mwenyezi Mungu jijuvyeni hakika ya hao mnao pigana nao kabla ya kupambana. Je, hao wamesilimu au bado ni washirikina. Wala msimwambie anaye kutoleeni salamu kuwa ni ishara ya amani: Wewe si Muumini, kwa kuwa mnataka kumnyang'anya mali yake na kondoo wake. Bali ipokeeni salamu yake, kwani kwa Mwenyezi Mungu amekuahidini kupata ngawira nyingi nyenginezo. Na nyinyi, enyi Waumini! Mlikuwa hivyo hivyo katika ukafiri kabla ya hayo, na Mwenyezi Mungu amekuhidini. Basi hakikisheni mambo ya hao mnao wakuta. Na Mwenyezi Mungu anajua baraabara, na hapana chochote kinacho fichikana kwake. Na Yeye hakika ni Mwenye kuhisabu kwa mujibu wa ujuzi wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّا يَسۡتَوِي ٱلۡقَٰعِدُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ غَيۡرُ أُوْلِي ٱلضَّرَرِ وَٱلۡمُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡۚ فَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ بِأَمۡوَٰلِهِمۡ وَأَنفُسِهِمۡ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ دَرَجَةٗۚ وَكُلّٗا وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلۡحُسۡنَىٰۚ وَفَضَّلَ ٱللَّهُ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ عَلَى ٱلۡقَٰعِدِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Hawawi sawa Waumini wanao kaa tu wala hawanadharura, na wale wanao pigana katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Mwenyezi Mungu amewatukuza cheo wale wanao pigana kwa mali yao na nafsi zao kuliko wale wanao kaa tu. Ingawa Mwenyezi Mungu amewaahidi wote mashukio mema, lakini Mwenyezi Mungu amewafadhili wanao pigana kwa ujira mkubwa kuliko wanao kaa tu.
Na hakika Jihadi pamoja na kuchukua hadhari inayo takikana ina fadhila kubwa sana. Basi hawawi sawa wanao kaa majumbani mwao wasende kupigana Jihadi na wale Mujaahidiina, wanao pigana kwa mali yao na nafsi zao. Kwani Mwenyezi Mungu amewanyanyua wale Mujaahidiina daraja, cheo cha juu kuwashinda wale wanao kaa nyuma; ila ikiwa wale wanao kaa nyuma wana udhuru unao wazuia kutoka kwenda vitani. Hapo inakuwa udhuru wao unawatoa lawamani, juu ya kuwa wanao pigana wana fadhila na cheo makhsusi. Mwenyezi Mungu amewaahidi makundi yote mawili mashukio mema, na matokeo mazuri.
Arabic explanations of the Qur’an:
دَرَجَٰتٖ مِّنۡهُ وَمَغۡفِرَةٗ وَرَحۡمَةٗۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمًا
Ni vyeo hivyo vinavyo toka kwake, na maghfira na rehema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.
Na cheo hichi walicho khusishwa nacho hao wanao pigana Jihadi ni cheo kikubwa, cha juu, hata imekuwa ni kama cheo cha kutafautisha sana baina yao na wengineo. Na kwa ajili ya cheo hichi watapata maghfira makubwa na rehema kunjufu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَوَفَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ظَالِمِيٓ أَنفُسِهِمۡ قَالُواْ فِيمَ كُنتُمۡۖ قَالُواْ كُنَّا مُسۡتَضۡعَفِينَ فِي ٱلۡأَرۡضِۚ قَالُوٓاْ أَلَمۡ تَكُنۡ أَرۡضُ ٱللَّهِ وَٰسِعَةٗ فَتُهَاجِرُواْ فِيهَاۚ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا
Hakika Malaika watawaambia wale ambao wamewafisha nao wamejidhulumu nafsi zao: Mlikuwa vipi? Watasema: Tulikuwa tunaonewa. Watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa na wasaa wa kuhamia humo? Basi hao makaazi yao ni Jahannamu, nayo ni marejeo mabaya kabisa.
Na hakika ni waajibu wa Muislamu kuhamia kwenye dola ya Kiislamu asiishi katika udhalili. Malaika watawauliza wakisha kufa: Mlikuwaje hata mkaridhia maisha ya unyonge na kudharauliwa? Na wao watajibu: Tulikuwa wanyonge katika nchi hiyo tukionewa. Malaika watawaambia: Kwani ardhi ya Mwenyezi Mungu haikuwa kunjufu ina wasaa, mkaweza kuhama badala ya kuishi katika uonevu? Watu hao wanao kubali uonevu, na wao wanaweza kuondoka, makao yao yatakuwa ni Jahannamu. Na hayo ni mashukio maovu kabisa. Basi Muislamu haimfalii kuishi katika udhalili, bali aishi na utukufu wake na hishima yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا ٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلۡوِلۡدَٰنِ لَا يَسۡتَطِيعُونَ حِيلَةٗ وَلَا يَهۡتَدُونَ سَبِيلٗا
Isipo kuwa wale walio kuwa wanyonge miongoni mwa wanaume na wanawake na watoto wasio na uweza wa hila ya kuongoza njia ya kuhama.
Juu ya hivyo wanasameheka na adhabu hii wale wasio weza kusafiri miongoni mwa wanaume, na wanawake, na watoto, wasio na nguvu, na hawana hila, wala hawakupata njia ya kutoka.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأُوْلَٰٓئِكَ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَعۡفُوَ عَنۡهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَفُوًّا غَفُورٗا
Basi hao huenda Mwenyezi Mungu akawasamehe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa maghfira
Na hao wanatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu. Na ni shani yake Mwenyezi Mungu kusamehe na kughufiria.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ وَمَن يُهَاجِرۡ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ يَجِدۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُرَٰغَمٗا كَثِيرٗا وَسَعَةٗۚ وَمَن يَخۡرُجۡ مِنۢ بَيۡتِهِۦ مُهَاجِرًا إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ثُمَّ يُدۡرِكۡهُ ٱلۡمَوۡتُ فَقَدۡ وَقَعَ أَجۡرُهُۥ عَلَى ٱللَّهِۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na mwenye kuhama katika Njia ya Mwenyezi Mungu atapata pengi duniani pa kukimbilia, na atapata wasaa. Na anaye toka nyumbani kwake kuhama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha yakamfika mauti njiani basi umethibiti ujira wake kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu.
Anaye hama kutafuta njia za kuiwania Haki na kuiunga mkono, atakuta duniani kwingi endako ambako maadui wa Haki wanahizika. Na atapata wasaa wa uhuru, na makao ya hishima,na thawabu, na ujira mkubwa. Aliye toka kwake kuhamia dola ya hishima, ambayo ndiyo dola ya Mwenyezi Mungu na Mtumewe, kisha yakamdiriki mauti kabla hajafika endako, basi ujira wake umethibiti. Mwenyezi Mungu amemkirimu kwa kujiwajibishia kumlipa ujira wake, na kumghufiria na kumrehemu. Ni shani yake kughufiria na kurehemu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا ضَرَبۡتُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَلَيۡسَ عَلَيۡكُمۡ جُنَاحٌ أَن تَقۡصُرُواْ مِنَ ٱلصَّلَوٰةِ إِنۡ خِفۡتُمۡ أَن يَفۡتِنَكُمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْۚ إِنَّ ٱلۡكَٰفِرِينَ كَانُواْ لَكُمۡ عَدُوّٗا مُّبِينٗا
Na mnapo safiri katika nchi si vibaya kwenu kama mkifupisha Swala, iwapo mnachelea wasije wale walio kufuru wakakuleteeni maudhi. Hakika makafiri ni maadui zenu walio wazi wazi.
Swala ni faridha isiyo epukika. Haiachiki Swala kwa ajili ya safari, lakini hana dhambi anaye fupisha Swala safarini. Watokao kwenda safari wakikhofia kuwa makafiri watawaletea ya kuwaudhi, wanaweza kufupisha Swala. Swala za rakaa nne zisaliwe rakaa mbili. Kutahadhari na kuingiliwa na makafiri ni waajibu, kwani wao ni maadui, na uadui wao uwazi.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِذَا كُنتَ فِيهِمۡ فَأَقَمۡتَ لَهُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَلۡتَقُمۡ طَآئِفَةٞ مِّنۡهُم مَّعَكَ وَلۡيَأۡخُذُوٓاْ أَسۡلِحَتَهُمۡۖ فَإِذَا سَجَدُواْ فَلۡيَكُونُواْ مِن وَرَآئِكُمۡ وَلۡتَأۡتِ طَآئِفَةٌ أُخۡرَىٰ لَمۡ يُصَلُّواْ فَلۡيُصَلُّواْ مَعَكَ وَلۡيَأۡخُذُواْ حِذۡرَهُمۡ وَأَسۡلِحَتَهُمۡۗ وَدَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَوۡ تَغۡفُلُونَ عَنۡ أَسۡلِحَتِكُمۡ وَأَمۡتِعَتِكُمۡ فَيَمِيلُونَ عَلَيۡكُم مَّيۡلَةٗ وَٰحِدَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ إِن كَانَ بِكُمۡ أَذٗى مِّن مَّطَرٍ أَوۡ كُنتُم مَّرۡضَىٰٓ أَن تَضَعُوٓاْ أَسۡلِحَتَكُمۡۖ وَخُذُواْ حِذۡرَكُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ أَعَدَّ لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا
Na unapo kuwa pamoja nao, ukawasalisha, basi kundi moja miongoni mwao wasimame pamoja nawe na wachukue silaha zao. Na watakapo maliza sijida zao, basi nawende nyuma yenu, na lije kundi jingine ambalo halijasali, lisali pamoja nawe. Nao wachukue hadhari yao na silaha zao. Walio kufuru wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu ili wakuvamieni mvamio wa mara moja. Wala si vibaya kwenu ikiwa mnaona udhia kwa sababu ya mvua au mkawa wagonjwa, mkaziweka silaha zenu. Na chukueni hadhari yenu. Hakika Mwenyezi Mungu amewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
Ewe Nabii Muaminifu, ukiwa nao na Swala ya Jamaa inasaliwa, msisahau kutahadhari na maadui. Na hayo ni kuwagawa Waislamu makundi mawili. Moja lianze kuswali kwa kukufuata wewe, na wakati huo la pili lisimame kwa hadhari na silaha likilinda vifaa. Ukisha nusu ya Swala, kundi lilio sali nawe lende nyuma yako, na lije jengine lisali nawe Swala iliyo bakia. Kisha litimize sehemu waliyo ikosa. Na lile la kwanza lisali baki ya Swala. Na hii huitwa "Laahiqah", yaani iliyo kutwa na nyengine inaitwa "Masbuuqah", yaani iliyo tanguliwa ,kwa kuwa inasaliwa mwanzo wa Swala ya Jamaa; na "Laahiqah" inasaliwa mwisho wa Swala ya Jamaa. Mpango huu ni kwa sababu isikosekane Swala, na kutahadhari na makafiri ambao wanapenda mghafilike na silaha zenu na vifaa vyenu wapate kukuvamieni kwa ghafla, na wakumalizeni nanyi mmo katika Swala. Vita na washirikina ni waajibu, na havina ukomo. Lakini hapana dhambi juu yenu kusita kwa ajili ya udhuru kama mvua au maradhi, juu ya kuwa lazima muwe na hadhari ya kudumu. Na hii ni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa makafiri hapa duniani, na Akhera amewaandalia adhabu ya fedheha na udhalili. "Laahiq" ni anaye swali na Imam mwanzo wa Swala na akalazimika kusali iliyo baki peke yake, na "Masbuuq" anaye iwahi sehemu ya mwisho ya Swala ya Jamaa, kisha akatimiza sehemu aliyo ikosa peke yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَإِذَا قَضَيۡتُمُ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ قِيَٰمٗا وَقُعُودٗا وَعَلَىٰ جُنُوبِكُمۡۚ فَإِذَا ٱطۡمَأۡنَنتُمۡ فَأَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَۚ إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ كَانَتۡ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ كِتَٰبٗا مَّوۡقُوتٗا
Mkisha sali basi mkumbukeni Mwenyezi Mungu mkisimama, na mkikaa, na mnapo jinyoosha kwa kulala. Na mtapo tulia basi shikeni Sala kama dasturi. Kwani hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyo wekewa nyakati maalumu.
Na mkisha Swala ya vita, inayo itwa Swala ya Khofu, msisahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu daima. Mkumbukeni nanyi mmesimama, mnapigana, mmekaa, na mmelala. Kwani kumkumbuka Mwenyezi Mungu Mtukufu kunatia nguvu nyoyo, na kuzituliza. Khofu ikiondoka pakawa na utulivu basi timizeni Swala kwa ukamilifu, kwani Swala imefaridhiwa juu ya Waumini isaliwe kwa nyakati zake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تَهِنُواْ فِي ٱبۡتِغَآءِ ٱلۡقَوۡمِۖ إِن تَكُونُواْ تَأۡلَمُونَ فَإِنَّهُمۡ يَأۡلَمُونَ كَمَا تَأۡلَمُونَۖ وَتَرۡجُونَ مِنَ ٱللَّهِ مَا لَا يَرۡجُونَۗ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا
Wala msifanye ulegevu kuwafukuzia kaumu ya maadui. Ikiwa mnaumia, basi nao pia wanaumia kama mnavyo umia nyinyi. Nanyi mnataraji kwa Mwenyezi Mungu wasio yataraji wao. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima.
Msilegee kuwafukuzia makafiri walio kwisha kukutangazieni vita na wanajaribu kukushambulieni kila pahala. Hakika vita havikosi maumivu. Ikiwa nyinyi Waumini mmepata majaraha na mengineyo, na wao makafiri pia wameyapata machungu. Khitilafu yenu ni kuwa wao hawapiganii Haki, wala hawataraji kitu kwa Mwenyezi Mungu; na nyinyi mnataka Haki na mnataraji radhi za Mwenyezi Mungu na neema za kudumu. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu na vyao, naye ni Mwenye hikima, anamlipa kila mtu kwa alitendalo.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّآ أَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ لِتَحۡكُمَ بَيۡنَ ٱلنَّاسِ بِمَآ أَرَىٰكَ ٱللَّهُۚ وَلَا تَكُن لِّلۡخَآئِنِينَ خَصِيمٗا
Hakika Sisi tumekuteremshia Kitabu hiki kwa haki ili upate kuhukumu baina ya watu kwa alivyo kuonyesha Mwenyezi Mungu. Wala usiwe mtetezi wa makhaaini.
Tumekuteremshia hii Qur'ani kwa haki na kwa kweli. Imekusanya kila lilio la haki. Inabainisha haki mpaka Siku ya Kiyama, ili iwe ni taa yako ya kukupa mwangaza kuwahukumu watu. Basi hukumu baina yao, wala usiwepiganie walio makhaaini.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
Na unapo hukumu baina ya watu muelekee Mwenyezi Mungu, na ukumbuke utukufu wake, na uombe maghfira yake na rehema yake. Kwani kughufiria na kurehemu ndio shani yake Subhanahu wa Taa'la.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَا تُجَٰدِلۡ عَنِ ٱلَّذِينَ يَخۡتَانُونَ أَنفُسَهُمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ خَوَّانًا أَثِيمٗا
Wala usiwatetee wanao khini nafsi zao. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi aliye khaaini, mwenye dhambi.
Wala usiwatetee wale wanao fanya khiana, na wakaendelea mno katika kuificha hiyo khiana katika nafsi zao. Kwani Mwenyezi Mungu hampendi ambaye mtindo wake ni khiana na kufanya madhambi.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱلنَّاسِ وَلَا يَسۡتَخۡفُونَ مِنَ ٱللَّهِ وَهُوَ مَعَهُمۡ إِذۡ يُبَيِّتُونَ مَا لَا يَرۡضَىٰ مِنَ ٱلۡقَوۡلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِمَا يَعۡمَلُونَ مُحِيطًا
Wanataka kujificha kwa watu, wala hawataki kujificha kwa Mwenyezi Mungu, naye yu pamoja nao pale wanapo panga njama usiku kwa maneno asiyo yapenda. Na Mwenyezi Mungu anayajua vyema wanayo yatenda.
Wanajificha, na wanataka kujisitiri kwa watu wasiione khiana yao. Wala hayumkini kuzificha khiana zao kwa Mwenyezi Mungu, na ilhali Yeye daima yu pamoja nao. Na wao usiku usiku hukubaliana kwa maneno yasiyo mridhi Mwenyezi Mungu ya kuwasingizia tuhuma watu wasio na makosa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu anajua vyema, na hapana kitu kinacho weza kujificha na ujuzi wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ جَٰدَلۡتُمۡ عَنۡهُمۡ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا فَمَن يُجَٰدِلُ ٱللَّهَ عَنۡهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَم مَّن يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا
Hivyo nyinyi mmewatetea hawa katika uhai huu wa duniani. Basi nani atakaye watetea kwa Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama? Au ni nani atakuwa wakili wao wa kumtegemea?.
Ikiwa nyinyi mnawatetea hao wakosa wasipate adhabu ya duniani, basi hatopatikana wa kuwatetea Siku ya Kiyama mbele ya Mwenyezi Mungu na kukubali kuwa ni mlinzi wao wa kuwasaidia.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَعۡمَلۡ سُوٓءًا أَوۡ يَظۡلِمۡ نَفۡسَهُۥ ثُمَّ يَسۡتَغۡفِرِ ٱللَّهَ يَجِدِ ٱللَّهَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na anaye tenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Mwenyezi Mungu, atamkuta Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
Mlango wa toba, hakika, uwazi. Anaye tenda kitendo kiovu cho chote, au akajidhulumu nafsi yake kwa kufanya maasi, kisha akamtaka msamaha Mwenyezi Mungu Mtukufu, atamkuta Mwenyezi Mungu yu tayari kukubali toba yake, na kumghufiria madhambi yake. Kwani ndio mwendo wake Mwenyezi Mungu kughufiria na kurehemu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَكۡسِبۡ إِثۡمٗا فَإِنَّمَا يَكۡسِبُهُۥ عَلَىٰ نَفۡسِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Na anaye chuma dhambi, basi ameichumia nafsi yake mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hikima.
Hakika madhara ya madhambi ni juu ya yule yule ayatendayo. Mwenye kuchuma madhambi basi anajidhuru mwenyewe. Na alitendalo linamuangukia mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na kutukuka anajua aliyo yatenda, na atamchukulia kwa mujibu wa hikima yake. Atamuadhibu au atamsamehe kwa mujibu wa hikima yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَكۡسِبۡ خَطِيٓـَٔةً أَوۡ إِثۡمٗا ثُمَّ يَرۡمِ بِهِۦ بَرِيٓـٔٗا فَقَدِ ٱحۡتَمَلَ بُهۡتَٰنٗا وَإِثۡمٗا مُّبِينٗا
Na atendaye kosa au dhambi kisha akamsingizia asiye na kosa, basi amejitwika dhulma na dhambi iliyo wazi.
Na mwenye kutenda makosa na madhambi kisha akamsingizia mwenginewe asiye na kosa alilo litenda - kama vile mwizi kaiba kitu kisha akamsingizia wizi mtu mwengine - mtu huyo ana dhambi mbili. Moja ni uwongo na uzushi, na la pili lile kosa lilio wazi la kuiba.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَوۡلَا فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ وَرَحۡمَتُهُۥ لَهَمَّت طَّآئِفَةٞ مِّنۡهُمۡ أَن يُضِلُّوكَ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡۖ وَمَا يَضُرُّونَكَ مِن شَيۡءٖۚ وَأَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمۡ تَكُن تَعۡلَمُۚ وَكَانَ فَضۡلُ ٱللَّهِ عَلَيۡكَ عَظِيمٗا
Na lau kuwa si fadhila ya Mwenyezi Mungu juu yako na rehema yake, kundi moja kati yao linge dhamiria kukupoteza. Wala hawapotezi ila nafsi zao, wala hawawezi kukudhuru kwa lolote. Na Mwenyezi Mungu amekuteremshia Kitabu na hikima na amekufundisha uliyo kuwa huyajui. Na fadhila za Mwenyezi Mungu zilizo juu yako ni kubwa.
Lau kuwa Mwenyezi Mungu hakukufadhili kwa kukuteremshia Wahyi, Ufunuo, na akakupa rehema ya kutambua na kufahamu hakika, kikundi cha wapotovu kingependa kukupoteza. Lakini hawapotezi ila nafsi zao. Kwani Mwenyezi Mungu ni muangalizi wako, na ndiye mwenye kukuonyesha haki. Hayakufikilii madhara ya mipango yao na upotezi wao. Yeye Mwenyezi Mungu amekuteremshia Qur'ani Tukufu ambayo hiyo ndiyo mizani ya haki, na ameutuza moyo wako kwa hikima, na amekufundisha Sharia na hukumu ambazo ulikuwa hukuzijua ila kwa kufunuliwa na Yeye. Hakika fadhila za Mwenyezi Mungu juu yako daima ni kubwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ لَّا خَيۡرَ فِي كَثِيرٖ مِّن نَّجۡوَىٰهُمۡ إِلَّا مَنۡ أَمَرَ بِصَدَقَةٍ أَوۡ مَعۡرُوفٍ أَوۡ إِصۡلَٰحِۭ بَيۡنَ ٱلنَّاسِۚ وَمَن يَفۡعَلۡ ذَٰلِكَ ٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِ ٱللَّهِ فَسَوۡفَ نُؤۡتِيهِ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Hakuna kheri katika mengi ya wanayo shauriana kwa siri, isipo kuwa kwa yule anaye amrisha kutoa sadaka, au kutenda mema, au kupatanisha baina ya watu. Na mwenye kufanya hayo kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, basi tutakuja mpa ujira mkubwa.
Hakika wale wanao kaa wakipanga mambo yao kisirisiri, mambo hayo hayana kheri, kwa sababu shari ndio huchipuka katika ufichoni. Lakini ikiwa mazungumzo hayo ni kwa jambo la sadaka ya kuwapa watu, au kufanya jambo lolote lisio baya, au kupanga mipango ya kusuluhisha baina ya watu, hayo si mabaya. Kwani hayo ni mambo ya kheri. Na mwenye kufanya hivyo kwa kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Subhanahu Wataa'la, basi Mwenyezi Mungu atampa malipo makubwa duniani na Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يُشَاقِقِ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ ٱلۡهُدَىٰ وَيَتَّبِعۡ غَيۡرَ سَبِيلِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ نُوَلِّهِۦ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصۡلِهِۦ جَهَنَّمَۖ وَسَآءَتۡ مَصِيرًا
Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu.
Na anaye mpinga Mtume s.a.w. baada ya kwisha itambua Njia ya Haki na Uwongofu, na akaifuata njia isiyo kuwa ya Waumini, na akaingia kwenye urafiki na maadui wa Waumini, basi huyo atakuwa na hao. Kwani amekhiari kuwa hao ndio wawe marafiki zake na walinzi wake. Mwenyezi Mungu atakuja mtia Motoni Siku ya Kiyama.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا
Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu basi huyo amepotea upotovu wa mbali.
Hakika mwisho huu wa kuumiza ni wao hao vile vile, kwani hao ni maadui wa Uislamu. Mfano wake ni mfano wa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Hakika kila dhambi yaweza kughufiriwa, ila kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kumuabudu mwenginewe asiye kuwa Yeye, na kumpinga Mtume katika Haki. Ni shani ya Mwenyezi Mungu kusamehe madhambi, ila dhambi ya kumshirikisha Yeye katika ibada. Kwa jenginelo lisilo kuwa hili Yeye humsamehe amtakaye. Anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada na kumtegemea, basi huyo ameipotea Haki, na amekuwa mbali nayo mno; kwani mtu huyo ameifisidi akili yake na nafsi yake pia.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِن يَدۡعُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ إِنَٰثٗا وَإِن يَدۡعُونَ إِلَّا شَيۡطَٰنٗا مَّرِيدٗا
Wao hawawaombi badala yake Yeye ila wanawake, wala hawamuombi ila Shet'ani aliye asi.
Katika upotovu ulio wazi kabisa ambao uko mbali na Haki ni ule wa mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu. Huyo anaabudu kitu ambacho hakisikii wala hakioni, hakidhuru wala hakinafiishi. Na huita hiyo miungu yake kwa majina ya kike, kama Laata na Uzza na Manaata na mengineyo ya majina ya kike. Yeye hakika kwa hivyo anamuabudu Shetani.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّعَنَهُ ٱللَّهُۘ وَقَالَ لَأَتَّخِذَنَّ مِنۡ عِبَادِكَ نَصِيبٗا مَّفۡرُوضٗا
Mwenyezi Mungu amemlaani. Naye Shet'ani alisema: Kwa yakini nitawachukua sehemu maalumu katika waja wako.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha mfukuza huyu Shetani kutokana na kivuli cha rehema yake, na amemjaalia awe katika njia ya upotovu. Na Shetani ameapa, na amejichukulia ahadi mwenyewe, kuwa atachota miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu idadi maalumu awapumbaze kwa upotovu wake na awatie wasiwasi kwa shari yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَأُضِلَّنَّهُمۡ وَلَأُمَنِّيَنَّهُمۡ وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ فَلَيُبَتِّكُنَّ ءَاذَانَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ وَلَأٓمُرَنَّهُمۡ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلۡقَ ٱللَّهِۚ وَمَن يَتَّخِذِ ٱلشَّيۡطَٰنَ وَلِيّٗا مِّن دُونِ ٱللَّهِ فَقَدۡ خَسِرَ خُسۡرَانٗا مُّبِينٗا
Na hakika nitawapoteza na nitawatia matamanio, na nitawaamrisha, basi watakata masikio ya wanyama, na nitawaamrisha, basi watabadili aliyo umba Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shet'ani kuwa ni mlinzi wake badala ya Mwenyezi Mungu, basi huyo amekhasiri khasara ya dhaahiri.
Hakika kiapo chake Shetani ni kuwa atawapoteza wale anao wapumbaza kwa kuwatenga mbali na Haki, na kuchochea pumbao lao na matamanio yao, mpaka wakawa wamepotea wanatanga tanga katika mawazo na tamaa za uwongo. Wakisha kuwa katika kuzainiwa huku na tamaa hizo chini ya utawala wake Shetani, tena huwatokomeza kwenye mambo yasiyo ingia akilini, na huwapelekea hao wafikiri kufanya hayo ni ibada. Na ilhali haya yote ni mawazo ya uwongo tu. Basi huwatia wasiwasi wakatenda mambo, kama kwa mfano kuwakata masikio baadhi ya ngamia wao, wageuze khulka aliyo iumba Mwenyezi Mungu. Wakafanya kuwa ngamia aliye katwa masikio yake hachinjwi, wala hafanyishwi kazi, wala hazuiliwi kwenda machungani atakavyo. Yote haya ni kwa amri yake Shetani kuwazaini. Tena huwatia wasiwasi mpaka wakaona kuwa hayo ni katika dini. Na hakika wao inakuwa wanamfuata yeye Shetani, na wanamfanya yeye ndiye wa kuwanusuru, na ndiye wa kumfuata badala ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumfanya Shetani ndiye msaidizi wake wa kumfuata, basi amekhasiri khasara kubwa iliyo wazi. Kwani hapo anakuwa amepotea njia ya Haki, na ameipumbaza akili yake, na utampata ufisadi duniani, na adhabu Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَعِدُهُمۡ وَيُمَنِّيهِمۡۖ وَمَا يَعِدُهُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ إِلَّا غُرُورًا
Anawaahidi na anawatia tamaa. Na Shet'ani hawaahidi ila udanganyifu.
Shetani huwapambia shari, wakaiona nzuri, na huwaahidi manufaa watayo pata pindi wakitenda kitendo fulani, na huwatia katika nafsi zao matumaini ya kuyatumai. Na hapana lolote analo waahidi na analo wapambia ila ni udanganyifu mtupu.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ مَأۡوَىٰهُمۡ جَهَنَّمُ وَلَا يَجِدُونَ عَنۡهَا مَحِيصٗا
Hao makao yao ni Jahannamu, na wala hawapati makimbilio kutoka humo.
Hakika hao walio zipoteza akili zao na wakafuata wasiwasi wa Shetani anao watia katika nafsi zao, mwisho wao ni kuendea Jahannamu, wala hawatapata njia ya kutoka huko.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ سَنُدۡخِلُهُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۖ وَعۡدَ ٱللَّهِ حَقّٗاۚ وَمَنۡ أَصۡدَقُ مِنَ ٱللَّهِ قِيلٗا
Na wale walio amini na wakatenda mema, tutawaingiza katika Bustani zipitayo mito kati yake. Watadumu humo milele. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo kweli. Na nani mkweli zaidi kwa usemi kuliko Mwenyezi Mungu.
Huu ndio mwisho wa wafuasi wa Shetani. Ama mwisho wa wafuasi wa Mwenyezi Mungu ni mzuri. Wao ndio walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakatenda mema, wala hawazugwi na mawazo ya uwongo. Hakika Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu Mtukufu atawatia katika mabustani yapitayo mito kati yake, chini ya vivuli. Na hayo ni makubwa mno kuliko bustani hizi za duniani. Na hayo ni yakini, kwani ahadi hizo ni ahadi za Mwenyezi Mungu, na ahadi zake haziwi ila ni hakika isiyo geuka, wala haina udanganyifu. Yeye ni mmiliki wa kila kitu. Wala haiwezi kufikirika kuwa yupo yeyote yule aliye mkweli kwa neno lake na ahadi yake kuliko Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّيۡسَ بِأَمَانِيِّكُمۡ وَلَآ أَمَانِيِّ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِۗ مَن يَعۡمَلۡ سُوٓءٗا يُجۡزَ بِهِۦ وَلَا يَجِدۡ لَهُۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Si kwa matamanio yenu, wala matamanio ya Watu wa Kitabu! Anaye fanya ubaya atalipwa kwalo, wala hatajipatia mlinzi wala wa kumnusuru, isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
Malipo siyo ayatamaniyo mtu na kuyaota bila ya vitendo vyema vizaavyo matunda. Malipo siyo myatamaniyo nyinyi, Waislamu. Wala siyo wayatamaniayo na kuyaota Ahlu-l-Kitabi, Watu wa Biblia, Mayahudi na Wakristo. Bali malipo na kuepukana na adhabu ni kwa Imani na Vitendo Vyema. Atendaye maovu atalipwa kwa vitendo vyake. Wala hampati mlinzi wala wa kumnusuru ila Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِن ذَكَرٍ أَوۡ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَأُوْلَٰٓئِكَ يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ وَلَا يُظۡلَمُونَ نَقِيرٗا
Na anaye fanya mema, akiwa mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini - basi hao wataingia Peponi wala hawatadhulumiwa hata kadiri ya tundu ya kokwa ya tende.
Watendao mema, kwa kadiri ya uwezo wao nao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wataingia kwenye Pepo ya neema, wala hawatapunguziwa hata chembe. Na hapana khitilafu baina ya malipo ya mwanamume na ya mwanamke, kwani mwanamke naye ana waajibu wake, malipo ya vitendo vyema, na adhabu kwa vitendo vibaya.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَمَنۡ أَحۡسَنُ دِينٗا مِّمَّنۡ أَسۡلَمَ وَجۡهَهُۥ لِلَّهِ وَهُوَ مُحۡسِنٞ وَٱتَّبَعَ مِلَّةَ إِبۡرَٰهِيمَ حَنِيفٗاۗ وَٱتَّخَذَ ٱللَّهُ إِبۡرَٰهِيمَ خَلِيلٗا
Na nani aliye bora kwa dini kuliko yule aliye usilimisha uso wake kwa Mwenyezi Mungu, naye akawa mwema, na anafuata mila ya Ibrahim mwongofu? Na Mwenyezi Mungu alimfanya Ibrahim kuwa ni rafiki mwendani.
Msingi wa vitendo vyema ni itikadi iliyo sawa. Na bora ya dini ni kumtakasikia niya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ukawa uso wako, na akili yako, na nafsi yako, yote haitaki kitu isipo kuwa kumridhi Mwenyezi Mungu Subhanahu. Kwa hivyo basi ndio fahamu zako zitanyooka sawa kuufahamu ujumbe wa Mitume, na ndio utaweza kushika daima vitendo vilivyo bora, na ukamfuata Baba wa Manabii, Ibrahim a.s. Kwani dini yake Ibrahim ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu, na ndiyo Dini inayo elekeza kutaka Haki daima. Na kwa Ibrahim ndiyo umekutana umoja wa Dini, kwa Waislamu, na Mayahudi na Wakristo. Basi ifuateni njia yake. Mwenyezi Mungu hakika amemkirimu Ibrahim, akamwita "Rafiki Mwendani".
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٖ مُّحِيطٗا
Ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote vilivyomo mbinguni na vilivyomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni mwenye kuvizunguka vitu vyote.
Hakika wa kumtakasia niya ni Mwenyezi Mungu, na ndio kwake Yeye inapasa uusilimishe uso wako, yaani umuelekee na umnyenyekee. Huko ndiko kumsafia niya Mwenyezi Mungu aliye umba ulimwengu wote, na ndiye mwenye kuumiliki. Vitu vyote viliomo mbinguni na duniani - nyota, sayari, jua, mwezi, milima, mabonde, majangwa, mashamba n.k. ni vya Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mwenye kubainikiwa na kila kitu, Mwenye kujua kwa ujuzi mkamilifu wa kuvizunguka vitu vyote avitendavyo mwanaadamu. Na Yeye atamlipa kheri akitenda kheri, na shari akitenda shari.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَيَسۡتَفۡتُونَكَ فِي ٱلنِّسَآءِۖ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِيهِنَّ وَمَا يُتۡلَىٰ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ فِي يَتَٰمَى ٱلنِّسَآءِ ٱلَّٰتِي لَا تُؤۡتُونَهُنَّ مَا كُتِبَ لَهُنَّ وَتَرۡغَبُونَ أَن تَنكِحُوهُنَّ وَٱلۡمُسۡتَضۡعَفِينَ مِنَ ٱلۡوِلۡدَٰنِ وَأَن تَقُومُواْ لِلۡيَتَٰمَىٰ بِٱلۡقِسۡطِۚ وَمَا تَفۡعَلُواْ مِنۡ خَيۡرٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِهِۦ عَلِيمٗا
Wanakuuliza nini sharia ya wanawake. Sema: Mwenyezi Mungu ana kutoleeni fatwa juu yao, na mnayo somewa humu Kitabuni kukhusu mayatima wanawake ambao hamwapi walicho andikiwa, na mnapenda kuwaoa, na kukhusu wanyonge katika watoto, na kwamba mwasimamie mayatima kwa uadilifu. Na kheri yoyote mnayo fanya Mwenyezi Mungu anaijua.
Watu walimtaka Mtume s.a.w. awambie nini hukumu ya sharia juu ya wanawake. Na wanawake walikuwa, na wangali bado kuwa, ni watu wanyonge. Basi Mwenyezi Mungu amembainishia Nabii wake ili naye abainishe hali ya wanawake, na hali ya wanyonge wengine katika ukoo miongoni mwa watoto na mayatima. Na akataja kuwa mayatima wanawake ambao wanaolewa wala hawachukui mahari yao, na watoto, na mayatima, wote hao watendewe kwa uadilifu na huruma na kuraiwa. Na kwamba kila kheri itendwayo basi hakika Mwenyezi Mungu anaijua, na Yeye ndiye atakaye ilipa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِنِ ٱمۡرَأَةٌ خَافَتۡ مِنۢ بَعۡلِهَا نُشُوزًا أَوۡ إِعۡرَاضٗا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يُصۡلِحَا بَيۡنَهُمَا صُلۡحٗاۚ وَٱلصُّلۡحُ خَيۡرٞۗ وَأُحۡضِرَتِ ٱلۡأَنفُسُ ٱلشُّحَّۚ وَإِن تُحۡسِنُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا
Na mwanamke akichelea kutupwa au kutojaliwa na mumewe, basi si vibaya kwao wakisikizana kwa suluhu. Na suluhu ni bora. Na nafsi zimewekewa machoni mwake tamaa na choyo. Na mkifanya wema na mkamchamngu basi hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za yote mnayo yatenda.
Na mwanamke akikhofia kuwa mumewe anapuuza mambo ya nyumbani au anayatupa, hayajali, wala hayashughulikii, basi hapana dhambi kwa wote hao wawili kutafuta njia za kusuluhiana kwa mapatano mema na kukurubiana. Na mwenye akili kati yao ni yule anaye anza kutaka masikizano. Na suluhu daima ina kheri, haina shari ndani yake. Linalo zuia masikizano ni kule kuwa kila mmoja kung'ang'ania haki yake kwa ukamilifu, na ugumu na uchoyo wa nafsi unapo wamiliki watu. Wala hapana njia ya kurejeza mapenzi ila mmojapo kati ya wawili kulegeza kamba. Na huyo ndiye mwema, mchamngu, mwenye kujihifadhi na dhulma. Na mwenye kutenda vitendo vyema na akamcha Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu anayo khabari ya vitendo vyake, na atamlipa kwavyo.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلَن تَسۡتَطِيعُوٓاْ أَن تَعۡدِلُواْ بَيۡنَ ٱلنِّسَآءِ وَلَوۡ حَرَصۡتُمۡۖ فَلَا تَمِيلُواْ كُلَّ ٱلۡمَيۡلِ فَتَذَرُوهَا كَٱلۡمُعَلَّقَةِۚ وَإِن تُصۡلِحُواْ وَتَتَّقُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Wala hamtaweza kufanya uadilifu baina ya wake, hata mkikakamia. Kwa hivyo msimili moja kwa moja mkamwacha (mmojapo) kama aliye tundikwa. Na mkisikizana na mkamchamungu basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Mwenye kurehemu.
Kuwafanyia uadilifu wake kwa mapenzi ya daima yasiyo chafuliwa na udanganyifu, na kutendeana usawa katika mapenzi ikawa nipe nikupe, ni jambo lisilo wezekana kuwa. Kadhaalika haiwezi kuwepo usawa katika kuwapenda wake, ikiwa kuna zaidi kuliko mke mmoja. Walakini mkijitahidi, basi msimfanyie ujeuri mmoja wapo, mkamili upande mmoja, na mkamwacha mwengine si mke si mt'alaka. Yapasa mjitengeneze, na muendeshe nyumba zenu kwa wema si kwa ufisadi. Na mcheni Mwenyezi Mungu apate kughufirieni na akurehemuni. Ni shani yake kughufiria na kurehemu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِن يَتَفَرَّقَا يُغۡنِ ٱللَّهُ كُلّٗا مِّن سَعَتِهِۦۚ وَكَانَ ٱللَّهُ وَٰسِعًا حَكِيمٗا
Na wakitengana Mwenyezi Mungu atamtosheleza kila mmoja katika wao kwa ukunjufu wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu Mwenye hikima.
Ikiwa suluhu haikumkinika na ikawa chuki (au karaha) imeshika nguvu zaidi, basi inalazimika kufarikiana. Na wakifarikiana Mwenyezi Mungu atawatosheleza kila mmoja wao kutokana na ukunjufu wa rehema yake na fadhila yake. Na riziki ziko katika mikono ya Mwenyezi Mungu, na Yeye ndiye Mwenye hikima, na hupanga mambo yote kwa mipango yake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ وَصَّيۡنَا ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَإِيَّاكُمۡ أَنِ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَنِيًّا حَمِيدٗا
Na ni vya Mwenyezi Mungu tu vyote viliomo katik mbingu na viliomo katika dunia. Na kwa hakika tuliwausia walio pewa Kitabu kabla yenu, na nyinyi pia, kwamba mumche Mwenyezi Mungu. Na mkikataa, basi ni vya Mwenyezi Mungu viliomo mbinguni na viliomo duniani. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, anajitosha, na Msifiwa.
Kiini cha Dini ni kumnyenyekea Mwenye kuumba ulimwengu, Mwenye utukufu na ukarimu, na kuukubali ufalme wake usio na ukomo. Kwani ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na katika ardhi. Na kwa huu Ufalme usio na ukomo amesema: Tumewausia watu wa dini zilizo toka mbinguni, katika Watu wa Kitabu na nyinyi Waislamu, mumkhofu Mwenyezi Mungu, na mumuabudu Yeye, na msiwe mnakufuru katika ibada yake, maana Yeye ndiye Mwenye utawala mkubwa kushinda wote. Hapana kitu kilicho toka nje ya utawala wake. Yeye ni Mkwasi, yaani mwenye kujitosha wala hakuhitajiini nyinyi. Juu ya hivyo Yeye anakuhimidini kwa imani yenu, kwani kwa kuwa Yeye ni Mwenye kujitosheleza mwenyewe, juu ya hivyo anasifu na kushukuru vitendo vyema vya waja wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلًا
Na ni vya Mwenyezi Mungu viliomo katika mbingu na viliomo katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa Mlinzi.
Kupanga kila kitu cha mbinguni na duniani ni kazi ya Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka. Yeye ndiye Mwenye madaraka, Mwenye kuendesha, Mwenye kupanga. Yatosha kuwa Yeye ndiye Mtawala aliye amrisha ulimwengu ukajipanga ulivyo jipanga, na akawaamrisha watu wamuabudu, na wamtegemezee Yeye mambo yao, na wamche Yeye.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِن يَشَأۡ يُذۡهِبۡكُمۡ أَيُّهَا ٱلنَّاسُ وَيَأۡتِ بِـَٔاخَرِينَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلَىٰ ذَٰلِكَ قَدِيرٗا
Akitaka atakuondoeni, enyi watu! Na awalete wengineo. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa hayo.
Hakika nyinyi enyi waja wa Mwenyezi Mungu! Mko chini ya ufalme wa Mwenyezi Mungu Mwenye uweza na Mwenye nguvu. Akipenda atakufisheni na alete wengine kabisa. Na Yeye Mwingi wa Utukufu ni Muweza wa hayo, na Muweza wa kila kitu.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّن كَانَ يُرِيدُ ثَوَابَ ٱلدُّنۡيَا فَعِندَ ٱللَّهِ ثَوَابُ ٱلدُّنۡيَا وَٱلۡأٓخِرَةِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعَۢا بَصِيرٗا
Anaye taka malipo ya dunia, basi kwa Mwenyezi Mungu yapo malipo ya dunia na Akhera. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia na Mwenye kuona.
Na watu, pindi wakitafuta neema za dunia zilizo halali kwa njia ya haki iliyo nyooka sawa, basi hakika Mwenyezi Mungu atawapa neema za duniani na Akhera; kwani Yeye ndiye aliye miliki neema zote mbili.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُواْ قَوَّٰمِينَ بِٱلۡقِسۡطِ شُهَدَآءَ لِلَّهِ وَلَوۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۡ أَوِ ٱلۡوَٰلِدَيۡنِ وَٱلۡأَقۡرَبِينَۚ إِن يَكُنۡ غَنِيًّا أَوۡ فَقِيرٗا فَٱللَّهُ أَوۡلَىٰ بِهِمَاۖ فَلَا تَتَّبِعُواْ ٱلۡهَوَىٰٓ أَن تَعۡدِلُواْۚ وَإِن تَلۡوُۥٓاْ أَوۡ تُعۡرِضُواْ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٗا
Enyi mlio amini! Kuweni wenye kusimamisha uadilifu, mtowao ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ijapo kuwa ni juu ya nafsi zenu, au wazazi wawili na jamaa zenu. Akiwa tajiri au masikini Mwenyezi Mungu anawastahikia zaidi. Basi msifuate matamanio, mkaacha kufanya uadilifu. Na mkiupotoa au mkajitenga nao basi Mwenyezi Mungu anajua vyema mnayo yatenda.
Uadilifu ndio nidhamu ya maumbile. Na hiyo ndiyo sharia ambayo haiwezi kuwapo ndani yake maoni ya kukhitalifiana. Basi enyi mlio mt'ii Mwenyezi Mungu wa Haki, na wito wa Mitume wake, kuweni macho nafsi zenu katika kuut'ii uadilifu, na kuweni macho kwa ajili ya watu. Mfanyieni insafu aliye dhulumiwa, na msimame imara, si kwa ajili ya kumpendelea tajiri, au kumwonea huruma masikini. Kwani Mwenyezi Mungu aliye waumba matajiri na masikini anastahiki zaidi kuangalia hali ya tajiri au fakiri. Matamanio ndiyo yanayo mpelekea mtu kumili nafsi yake, basi msiyafuate matamanio mkaacha uadilifu. Na mkikengeuka mkaacha uadilifu, au mkapuuza kusimamisha uadilifu, basi mjue Mwenyezi Mungu anayajua myatendayo, tena anayajua kwa ujuzi wa ndani. Naye atakulipeni kwa mujibu wa a'mali yenu; ikiwa njema mtalipwa wema, ikiwa ovu mtalipwa shari.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ ءَامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِي نَزَّلَ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ مِن قَبۡلُۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِٱللَّهِ وَمَلَٰٓئِكَتِهِۦ وَكُتُبِهِۦ وَرُسُلِهِۦ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا
Enyi mlio amini! Muaminini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha juu ya Mtume wake, na Kitabu alicho kiteremsha kabla yake. Na anaye mkataa Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume wake, na Siku ya Akhera, basi huyo amekwisha potelea mbali.
Kwa hakika Ujumbe wa mbinguni ni mmoja, kwa kuwa yule Mwenye kutuma ni Mmoja, naye ni Mwenyezi Mungu. Basi enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu na mumsafie niya. Na msadikini Mtume wake Muhammad, na msadiki yaliyo kuja katika Kitabu chake alicho mteremshia, na mtende yaliyo amrishwa humo. Na sadikini Vitabu vilivyo teremshwa kabla yake kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu bila ya mageuzo wala kusahau. Aminini yote hayo. Kwani mwenye kumkanusha Mwenyezi Mungu, Muumba wa viumbe vyote, na Malaika, na Mwenye kuyajua yaliyo fichikana, na Vitabu vya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na akaikanusha Siku ya Mwisho, basi huyo ameipotea Njia Iliyo Nyooka, na ametokomea mbali katika njia ya upotovu.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ءَامَنُواْ ثُمَّ كَفَرُواْ ثُمَّ ٱزۡدَادُواْ كُفۡرٗا لَّمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ سَبِيلَۢا
Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Mwenyezi Mungu hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia.
Hakika Imani ni kuit'ii Haki kusio kuwa na ukomo, na kunako endelea daima. Basi wanao taradadi wakababaika si Waumini. Hao ambao wanaamini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakakufuru, na kwa hivyo wakazidi ukafiri wao - Mwenyezi Mungu hatakuwa wa kuwaghufiria watu hao hivyo vitendo vyao viovu, wala hatawaongoa kwenye Haki. Kwani kusamehe kwa Mwenyezi Mungu kunahitajia toba, na kujing'oa na shari, na uwongofu wake ni kwa wale wanao ielekea Haki na wanaitaka.
Arabic explanations of the Qur’an:
بَشِّرِ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ بِأَنَّ لَهُمۡ عَذَابًا أَلِيمًا
Wabashirie wanaafiki kwamba watapata adhabu chungu,.
Ewe Mtume Mtukufu! Waonye wanaafiki kwamba Siku ya Kiyama watapata adhabu chungu yenye kuumiza.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ يَتَّخِذُونَ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَيَبۡتَغُونَ عِندَهُمُ ٱلۡعِزَّةَ فَإِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعٗا
Wale ambao huwafanya makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.
Hao wanaafiki huufanya utawala wa makafiri uwe juu yao, na wanawawacha Waumini. Basi hebu hivyo wanataka wapate utukufu kwa hawa makafiri? Hakika utukufu uko kwa Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye huwapa waja wake wenye kuamini. Na mwenye kutaka utukufu kwa Mwenyezi Mungu atatukuka, na mwenye kutaka utukufu kwa mwenginewe atadhalilika.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَدۡ نَزَّلَ عَلَيۡكُمۡ فِي ٱلۡكِتَٰبِ أَنۡ إِذَا سَمِعۡتُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ يُكۡفَرُ بِهَا وَيُسۡتَهۡزَأُ بِهَا فَلَا تَقۡعُدُواْ مَعَهُمۡ حَتَّىٰ يَخُوضُواْ فِي حَدِيثٍ غَيۡرِهِۦٓ إِنَّكُمۡ إِذٗا مِّثۡلُهُمۡۗ إِنَّ ٱللَّهَ جَامِعُ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ وَٱلۡكَٰفِرِينَ فِي جَهَنَّمَ جَمِيعًا
Naye amekwisha kuteremshieni katika Kitabu hiki ya kwamba mnapo sikia Aya za Mwenyezi Mungu zinakanushwa na zinafanyiwa kejeli, basi msikae pamoja nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine. Hivyo mtakuwa nanyi mfano wao hao. Hakika Mwenyezi Mungu atawakusanya wanaafiki na makafiri wote pamoja katika Jahannamu.
Mwenyezi Mungu amekwisha kuteremshieni katika Qur'ani Tukufu kwamba kila mkisikia Aya za Kitabu nyinyi mnaamini, na makafiri wanapinga na wanakejeli. Na ikiwa hivyo ndiyo hali ya makafiri na wanaafiki, na mkasikia kejeli zao, basi msikae nao, mpaka waingie katika mazungumzo mengine waache dhihaki zao. Na nyinyi ikiwa hamtofanya hivyo, mkawa mnasikiliza kejeli zao, basi mtakuwa nanyi kama wao katika kuifanyia maskhara Qur'ani. Mwisho wa makafiri na wanaafiki ni muovu mno, kwani Mwenyezi Mungu atawakusanya wote hao katika Moto wa Siku ya Kiyama.
Arabic explanations of the Qur’an:
ٱلَّذِينَ يَتَرَبَّصُونَ بِكُمۡ فَإِن كَانَ لَكُمۡ فَتۡحٞ مِّنَ ٱللَّهِ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَكُن مَّعَكُمۡ وَإِن كَانَ لِلۡكَٰفِرِينَ نَصِيبٞ قَالُوٓاْ أَلَمۡ نَسۡتَحۡوِذۡ عَلَيۡكُمۡ وَنَمۡنَعۡكُم مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ فَٱللَّهُ يَحۡكُمُ بَيۡنَكُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۚ وَلَن يَجۡعَلَ ٱللَّهُ لِلۡكَٰفِرِينَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ سَبِيلًا
Wale ambao wanakungojeeni, mkipata ushindi unao toka kwa Mwenyezi Mungu wao husema: Si tulikuwa pamoja nanyi vile? Na ikiwa ni sehemu ya makafiri kushinda wao huwaambia: Hatukuwa ni waweza wa kukushindeni, nasi tukakukingeni na hawa Waumini? Basi Mwenyezi Mungu atahukumu baina yenu Siku ya Kiyama, wala Mwenyezi Mungu hatawapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.
Mtindo wa wanaafiki ni kukungojeeni kama anavyo ngojea mwenye husda na maya anaye tamani mpate masaibu mnapo kuwa katika vita na maadui. Mkishinda kwa nusra ya Mwenyezi Mungu, na mkafungukiwa njia ya Haki, wao huwaambia Waumini - na hali wao ule ushindi walio pewa wenye Imani na Mwenyezi Mungu umewashtusha : Sisi hatukuwa nanyi? Kwa maana sisi ni jamaa zenu! Na ikiwa ni zamu ya makafiri kupata ushindi, basi wao huwaendea na kuwaambia: Sisi hatukuyashughulikia mambo yenu hata yakawa ni yetu? Na hatukukupeni mapenzi yetu, na tukakulindeni na hawa Waumini? (yaani sisi ni wenzenu). Na Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la atakuhukumuni baina yenu na hawa wanaafiki Siku ya Kiyama. Wala Mwenyezi Mungu hatowapa makafiri njia kuwashinda Waumini maadamu Waumini watashikamana na sifa ya Imani ya kweli na vitendo vyema.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَهُوَ خَٰدِعُهُمۡ وَإِذَا قَامُوٓاْ إِلَى ٱلصَّلَوٰةِ قَامُواْ كُسَالَىٰ يُرَآءُونَ ٱلنَّاسَ وَلَا يَذۡكُرُونَ ٱللَّهَ إِلَّا قَلِيلٗا
Hakika wanaafiki wanamkhadaa Mwenyezi Mungu, na hali ni Yeye ndiye mwenye kuwakhadaa wao. Na wanapo inuka kuswali huinuka kwa unyong'onyo, wanajionyesha kwa watu tu, wala hawamdhukuru Mwenyezi Mungu ila kidogo tu.
Hakika wanaafiki, kwa ule unaafiki wao, wanadhani kuwa wanamkhadaa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wanamficha hakika ya nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Yeye ndiye anaye wakhadaa wao. Basi Yeye huwapururia kuwapa muhula, na anawawacha mpaka wabobee katika maovu yao, kisha ndio awahisabu kwa waliyo yatenda. Na hawa wanaafiki wana dhaahiri ya kuonekana, na ya ndani ya nafsi zao. Yale ya kuonekana ni vile kuwa wakiinuka kwenda kuswali huinuka kwa uvivu, kwa unyong'onyo. Na Swala yao ni riya tu, kuonyesha, si ya kweli. Na ya ndani ni kuwa hawakumbuki kumtaja Mwenyezi Mungu ila kwa nadra, kwa tukizi. Na lau kuwa wanamkumbuka vilivyo wangeli uacha unaafiki
Arabic explanations of the Qur’an:
مُّذَبۡذَبِينَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ لَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِ وَلَآ إِلَىٰ هَٰٓؤُلَآءِۚ وَمَن يُضۡلِلِ ٱللَّهُ فَلَن تَجِدَ لَهُۥ سَبِيلٗا
Wanayumba yumba baina ya huku na huko. Huku hawako na huko hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha kupotea, kabisa hutompatia njia.
Na hawa wanaafiki ni watu wanao taradadi, wanababaika. Kwenu hawapo, na kwao makafiri hawapo katika kila hali. Na hayo ni kwa sababu ya udhaifu wa imani, na udhaifu wa nafsi, na kwa sababu ya kupotoka na Haki. Na mwenye kuandikiwa kupotoka na Mwenyezi Mungu tangu hapo azali, basi huna njia wewe ya kumwongoa sawa.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۚ أَتُرِيدُونَ أَن تَجۡعَلُواْ لِلَّهِ عَلَيۡكُمۡ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينًا
Enyi mlio amini! Msiwafanye makafiri kuwa ndio marafiki badala ya Waumini. Je, mnataka Mwenyezi Mungu awe na hoja iliyo wazi juu yenu?.
Hakika katika sababu za unaafiki ni kuwa wanaafiki wamewafanya watu wasio kuwa Waumini kuwa ndio walinzi wao, marafiki zao, watawala wao, na ndio wa kuwanusuru. Enyi Waumini! Yaacheni haya, muepukane nayo. Wala msiwafanye makafiri ndio wa kukunusuruni, wakukutawalini, mkawanyenyekea. Na hapana shaka yoyote mkifanya hivyo mnampa Mwenyezi Mungu hoja iliyo wazi ya kukuhojini. Mtakuja ingia pamoja na wanaafiki, na mtadhalilika. Kwani inakuwa hamfanyi utukufu wenu utoke kwa Mwenyezi Mungu, na kwa haki, na vitendo vyema.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلۡمُنَٰفِقِينَ فِي ٱلدَّرۡكِ ٱلۡأَسۡفَلِ مِنَ ٱلنَّارِ وَلَن تَجِدَ لَهُمۡ نَصِيرًا
Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru.
Hakika wanaafiki kwa sababu ya unaafiki wao watakuwa katika vina vya Jahannamu. Wao wako chini kabisa huko, na daraja ya mwisho kabisa. Wala hutompata wa kuwanusuru, wa kuwatetea na adhabu hiyo.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا ٱلَّذِينَ تَابُواْ وَأَصۡلَحُواْ وَٱعۡتَصَمُواْ بِٱللَّهِ وَأَخۡلَصُواْ دِينَهُمۡ لِلَّهِ فَأُوْلَٰٓئِكَ مَعَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَۖ وَسَوۡفَ يُؤۡتِ ٱللَّهُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ أَجۡرًا عَظِيمٗا
Isipo kuwa wale walio tubu, na wakatengeneza na wakashikamana na Mwenyezi Mungu, na wakamtakasia Dini yao Mwenyezi Mungu. Basi hao ni pamoja na Waumini. Na Mwenyezi Mungu atakuja wapa Waumini ujira mkubwa.
Isipo kuwa wale katika wao walio tubia, na wakarejea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakaungana naye Yeye peke yake, na wakajitakasa, na wakaelekeza nyuso zao kwake, na wakatenda mema. Wakifanya haya basi ndio wanakuwa miongoni mwa Waumini. Watapata malipo ya Waumini. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha waahidi Waumini malipo makubwa duniani na Akhera.
Arabic explanations of the Qur’an:
مَّا يَفۡعَلُ ٱللَّهُ بِعَذَابِكُمۡ إِن شَكَرۡتُمۡ وَءَامَنتُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ شَاكِرًا عَلِيمٗا
Mwenyezi Mungu hakuadhibuni mkimshukuru na mkamuamini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kupokea shukrani na ndiye Mwenye kujua.
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu hana alitakalo kwenu ila mumuamini Yeye, na muishukuru neema yake. Mkiwa hivyo basi hampati adhabu, bali mtapata malipo ya kheri na shukrani. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mwenye kushukuria waja wake kwa vitendo vyema, na ni Mjuzi, anajua hali zao zote njema na mbaya.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ لَّا يُحِبُّ ٱللَّهُ ٱلۡجَهۡرَ بِٱلسُّوٓءِ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ إِلَّا مَن ظُلِمَۚ وَكَانَ ٱللَّهُ سَمِيعًا عَلِيمًا
MWENYEZI MUNGU hapendi uovu uenezwe kwa maneno ila kwa mwenye kudhulumiwa. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua.
Mwenyezi Mungu anawakataza waja wake wasiseme maneno maovu, ila yule aliye patwa na dhulma. Ni halali kwake kumshitaki aliye mdhulumu, na autaje uovu aliyo tendewa. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni Mwenye kusikia vyema maneno ya aliye dhulumiwa. Na ni Mjuzi wa dhulma ya mwenye kudhulumu. Na atamlipa kwa kitendo chake hicho.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِن تُبۡدُواْ خَيۡرًا أَوۡ تُخۡفُوهُ أَوۡ تَعۡفُواْ عَن سُوٓءٖ فَإِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَفُوّٗا قَدِيرًا
Mkidhihirisha wema au mkiuficha, au mkiyasamehe maovu, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira na Muweza.
Mkiyadhihirisha mema myatendayo, au mkayaficha, au mkamsamehe anaye kufanyieni uovu, Mwenyezi Mungu atakulipeni kwa kufuata khulka yake Mtukufu, ya kusamehe na hali ana uwezo kaamili. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu ni mwingi mno wa kusamehe, Mwenye kukamilika uwezo wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ يَكۡفُرُونَ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيُرِيدُونَ أَن يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ ٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَيَقُولُونَ نُؤۡمِنُ بِبَعۡضٖ وَنَكۡفُرُ بِبَعۡضٖ وَيُرِيدُونَ أَن يَتَّخِذُواْ بَيۡنَ ذَٰلِكَ سَبِيلًا
Hakika wale wanao mkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya.
Hakika wasio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanao taka kufanya ubaguzi katika imani ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanasema: Tunawaamini baadhi ya Mitume, sio wote, hao wanawaamini wawapendao na wanawakataa wasio wapenda. Na lilio waajibu ni kuwaamini wote, kwani Imani haikubali kukatwa mapande mapande.
Arabic explanations of the Qur’an:
أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡكَٰفِرُونَ حَقّٗاۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٗا مُّهِينٗا
Hao ndio makafiri kweli. Na tumewaandalia makafiri adhabu ya kudhalilisha.
Hawa wote ndio walio ungama ukafiri wao ulio wazi. Na Mwenyezi Mungu amekwisha waahidi wao na mifano ya hao adhabu kali yenye kudhalilisha.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ وَلَمۡ يُفَرِّقُواْ بَيۡنَ أَحَدٖ مِّنۡهُمۡ أُوْلَٰٓئِكَ سَوۡفَ يُؤۡتِيهِمۡ أُجُورَهُمۡۚ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورٗا رَّحِيمٗا
Na walio muamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu.
Na ama wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala hawakumkanusha hata mmoja wapo kati yao, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu atawalipa malipo makubwa kwa ajili ya Imani yao iliyo kamilika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira kwa wenye kutubu, na ni Mwenye kuwarehemu waja wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَسۡـَٔلُكَ أَهۡلُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن تُنَزِّلَ عَلَيۡهِمۡ كِتَٰبٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِۚ فَقَدۡ سَأَلُواْ مُوسَىٰٓ أَكۡبَرَ مِن ذَٰلِكَ فَقَالُوٓاْ أَرِنَا ٱللَّهَ جَهۡرَةٗ فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّٰعِقَةُ بِظُلۡمِهِمۡۚ ثُمَّ ٱتَّخَذُواْ ٱلۡعِجۡلَ مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَٰتُ فَعَفَوۡنَا عَن ذَٰلِكَۚ وَءَاتَيۡنَا مُوسَىٰ سُلۡطَٰنٗا مُّبِينٗا
Watu wa Kitabu wanakutaka uwateremshia kitabu kutoka mbinguni. Na kwa hakika walikwisha mtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walisema: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu wazi wazi. Wakapigwa na radi kwa hiyo dhulma yao. Kisha wakamchukua ndama kumuabudu, baada ya kwisha wajia hoja zilizo wazi. Nasi tukasamehe hayo, na tukampa Musa nguvu zilizo dhaahiri.
Ewe Mtume! Watu wa Kitabu, yaani Mayahudi wapendao kuudhi, wanakutaka ulete dalili ya ukweli wa unabii wako. Uwaletee kitabu makhsusi kiwateremkie kutoka mbinguni kithibitishe ukweli wa utume wako, na kiwatake wakuamini na kukut'ii! Ukiyaona makuu hayo wayatakayo, wewe usifanye haraka. Kwani wenzao walio tangulia walifanya kero vile vile, wakamtaka Musa makubwa kuliko hayo. Walimwambia: Tuonyeshe Mwenyezi Mungu tumwone kwa macho. Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa lile kero lao na dhulma yao kwa kuwapiga radi iliyo wateketeza!! Kisha watajie hawa watu kosa kubwa zaidi na ovu zaidi, nalo ni pale walipo mfanya ndama kuwa ni Mungu wao, wakamwacha Mwenyezi Mungu aliye waumba. Haya baada ya kwisha ona dalili zote alizo zionyesha Musa kwa Firauni na kaumu yake!! Kisha juu ya hayo Mwenyezi Mungu akawakunjulia usamehevu wake kwao, na Mwenyezi Mungu akampa nguvu Musa kwa hoja zilio wazi, na neno madhubuti.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَرَفَعۡنَا فَوۡقَهُمُ ٱلطُّورَ بِمِيثَٰقِهِمۡ وَقُلۡنَا لَهُمُ ٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا وَقُلۡنَا لَهُمۡ لَا تَعۡدُواْ فِي ٱلسَّبۡتِ وَأَخَذۡنَا مِنۡهُم مِّيثَٰقًا غَلِيظٗا
Na tukanyanyua mlima juu yao kwa kufanya agano nao. Na tukawaambia: Ingilieni mlangoni kwa unyenyekevu. Na tukawaambia: Msiivunje Siku ya Sabato (Jumaa mosi). Na tukachukua kwao ahadi iliyo madhubuti.
Mwenyezi Mungu akaunyanyua mlima juu ya Wana wa Israili ili kuwatisha kwa kule kuikataa kwao sharia ya Taurati, mpaka wakaikubali. Akachukua kwao agano, na akawaamrisha waingie mjini hali wakimnyenyekea Mwenyezi Mungu. Wala wasiyakiuke aliyo waamrisha kushika ibada katika siku ya Sabato, yaani Jumaamosi.(Imeitwa "Sabt" Kiarabu, "Shabbath" Kiyahudi, "Sabbath" Kiingereza, na "Sabato" Kiswahili, maana yake "Mapumziko" kwa kuwa ni siku ya mapumziko kwa Mayahudi.) Na Mwenyezi Mungu alichukua kwao ahadi ya nguvu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَبِمَا نَقۡضِهِم مِّيثَٰقَهُمۡ وَكُفۡرِهِم بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ وَقَتۡلِهِمُ ٱلۡأَنۢبِيَآءَ بِغَيۡرِ حَقّٖ وَقَوۡلِهِمۡ قُلُوبُنَا غُلۡفُۢۚ بَلۡ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَيۡهَا بِكُفۡرِهِمۡ فَلَا يُؤۡمِنُونَ إِلَّا قَلِيلٗا
Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi zao, na kuzikataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri kwa kufuru zao, basi hawaamini ila kidogo tu.
Mwenyezi Mungu akawakasirikia kwa sababu ya kuvunja agano hili, na kuzikataa ishara za Mwenyezi Mungu, na kwa kuwauwa Manabii kwa dhulma, na kuendelea katika upotovu wao kwa kusema: Nyoyo zetu zimefungwa hazikubali hayo unayo tuitia! Nao hawasemi kweli katika kauli yao hiyo, bali Mwenyezi Mungu amezifuta nyoyo zao kwa ukafiri wao, basi ni wachache tu kati yao wanao amini.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَبِكُفۡرِهِمۡ وَقَوۡلِهِمۡ عَلَىٰ مَرۡيَمَ بُهۡتَٰنًا عَظِيمٗا
Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa.
Na Mwenyezi Mungu amewaghadhibikia Mayahudi kwa sababu ya kufru yao na kumzulia Maryam uzushi mkubwa.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَقَوۡلِهِمۡ إِنَّا قَتَلۡنَا ٱلۡمَسِيحَ عِيسَى ٱبۡنَ مَرۡيَمَ رَسُولَ ٱللَّهِ وَمَا قَتَلُوهُ وَمَا صَلَبُوهُ وَلَٰكِن شُبِّهَ لَهُمۡۚ وَإِنَّ ٱلَّذِينَ ٱخۡتَلَفُواْ فِيهِ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُۚ مَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍ إِلَّا ٱتِّبَاعَ ٱلظَّنِّۚ وَمَا قَتَلُوهُ يَقِينَۢا
Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.
Na Mwenyezi Mungu pia amewaghadhibikia kwa kusema kwao uwongo: Hakika sisi tumemuuwa Masihi Isa bin Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na kweli ya yakini ni kuwa hawakumuuwa kama wanavyo zua. Wala hawakumsulubu kama wanavyo dai. Lakini walifananishiwa, nao wakadhani kuwa wamemuuwa na wamemsalibu. Na hakika walimuuwa na kumsalibu aliye shabihiana naye. Nao wakaja kukhitalifiana baada ya hayo, kuwa aliyeuwawa ni Isa au mtu mwengine? Na wote hao, kwa hakika, wamo katika shaka tu juu ya jambo hilo. Kweli iliyopo ni kuwa hawana ujuzi nayo mambo haya, ila ni dhana tu. Kabisa hawakumuuwa Isa. (Wataalamu wa Biblia mpaka hii leo wamo kuzozana katika jambo hili. Mwenye kuzichungua Injili zinazo kubaliwa na Wakristo ataona kuwa hazina uthibitisho kuwa aliye salibiwa ndiye Yesu, au hata huyo naye alikufa msalabani au la.)
Arabic explanations of the Qur’an:
بَل رَّفَعَهُ ٱللَّهُ إِلَيۡهِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا
Bali Mwenyezi Mungu alim- tukuza kwake, na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Bali Mwenyezi Mungu alimtukuza kwake, akamwokoa na maadui zake, wasimsalibu na wasimuuwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushinda, hashindiki, ni Mwenye hikima katika vitendo vyake. (Taaurati inayo kubaliwa na Mayahudi na Wakristo imesema kuwa anaye kufa kwa kutundikwa msalabani amelaaniwa. Ndio maana Mayahudi wakawa na hamu wamtundike Nabii Isa ili wathibitishe kuwa huyo si chochote ila ni mlaanifu. Je, Mwenyezi Mungu Mtukufu vipi aachilie jambo hilo liwe kwa Mtume wake?)
Arabic explanations of the Qur’an:
وَإِن مِّنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ إِلَّا لَيُؤۡمِنَنَّ بِهِۦ قَبۡلَ مَوۡتِهِۦۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَكُونُ عَلَيۡهِمۡ شَهِيدٗا
Na hawi katika Watu wa Kitabu ila hakika atamuamini yeye kabla ya kufa kwake. Naye Siku ya Kiyama atakuwa shahidi juu yao.
Na hapana mmojapo katika Watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo) ila atakuja tambua uhakika wa Isa (kuwa ni Nabii wa kweli wa Mwenyezi Mungu, si mwana haramu, wala si mwana wa Mungu) kabla ya kufa kwake, na kuwa yeye Isa ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na atakuja amini imani ambayo haitomfaa kitu, kwa kuwa wakati wake umekwisha pita. Na Siku ya Kiyama Isa atatoa ushahidi juu yao kuwa yeye alifikisha ujumbe, na kuwa yeye ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَبِظُلۡمٖ مِّنَ ٱلَّذِينَ هَادُواْ حَرَّمۡنَا عَلَيۡهِمۡ طَيِّبَٰتٍ أُحِلَّتۡ لَهُمۡ وَبِصَدِّهِمۡ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ كَثِيرٗا
Basi kwa dhulma yao Mayahudi tuliwaharimishia vitu vizuri walivyo halalishiwa. Na kwa sababu ya kuwazuilia kwao watu wengi na Njia ya Mwenyezi Mungu.
Kwa sababu ya udhalimu wao Mayahudi Mwenyezi Mungu amewapa adabu - amewakataza vyakula mbali mbali vilivyo vizuri, vimekuwa kwao ni haramu, na ilhali kwanza vilikuwa halali kwao. Na kwa udhalimu wao wamewazuia watu wengi wasiingie katika Dini ya Mwenyezi Mungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَأَخۡذِهِمُ ٱلرِّبَوٰاْ وَقَدۡ نُهُواْ عَنۡهُ وَأَكۡلِهِمۡ أَمۡوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَٰطِلِۚ وَأَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ مِنۡهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا
Na kuchukua kwao riba, nao wamekatazwa, na kula kwao mali ya watu kwa dhulma. Basi tumewaandalia makafiri katika wao adhabu yenye uchungu.
Na kwa sababu ya kupenda kula riba - na Mwenyezi Mungu alikwisha wakataza hayo - na kuchukua mali ya watu kwa njia isiyo ya haki, ndio ikawa adabu ya dini ni kuwazuilia na kula vyakula vilivyo vizuri. Na Mwenyezi Mungu amewawekea hao walio kufuru adhabu yenye kutia machungu.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّٰكِنِ ٱلرَّٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ مِنۡهُمۡ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَۚ وَٱلۡمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَۚ وَٱلۡمُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ أُوْلَٰٓئِكَ سَنُؤۡتِيهِمۡ أَجۡرًا عَظِيمًا
Lakini walio bobea katika ilimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini uliyo teremshiwa wewe, na yaliyo teremshwa kabla yako. Na wanao shika Swala, na wakatoa Zaka, na wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho - hao tutawapa malipo makubwa.
Lakini walio bobea katika ilimu, yaani wataalamu kweli kweli, miongoni mwa Mayahudi, na Waumini katika umma wako, Ewe Nabii, wanasadiki wahyi ulio funuliwa wewe, na walio letewa Mitume wa kabla yako. Na wanao shika Swala baraabara, na wanatoa Zaka, na wanamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuliwa na hisabu, hao Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kabisa kwa imani yao na ut'iifu wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
۞ إِنَّآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ كَمَآ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ نُوحٖ وَٱلنَّبِيِّـۧنَ مِنۢ بَعۡدِهِۦۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَإِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَ وَٱلۡأَسۡبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَٰرُونَ وَسُلَيۡمَٰنَۚ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا
Hakika Sisi tumekuletea wahyi wewe kama tulivyo wapelekea wahyi Nuhu na Manabii walio kuwa baada yake. Na tulimpelekea wahyi Ibrahim na Ismail na Is-haka na Yaakub na wajukuu zake, na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman, na Daud tukampa Zaburi.
Hakika Sisi tumekufunulia wewe, ewe Nabii! (tumekuteremshia Wahyi), Qur'ani na Sharia, kama tulivyo wafunulia kabla yako Nuhu na Manabii wa baada yake, na kama tulivyo wapa Wahyi Ibrahim, na Ismail, na Is-haq, na Yaakub, na wajukuu zake, nao wale walio kuwa Manabii wa Mwenyezi Mungu miongoni mwa dhuriya (wazao) wa Yaakub, na Isa, na Ayubu, na Yunus, na Haarun, na Suleiman, na kama tulivyo mfunulia Daud tukamteremshia Kitabu cha Zabur.
Arabic explanations of the Qur’an:
وَرُسُلٗا قَدۡ قَصَصۡنَٰهُمۡ عَلَيۡكَ مِن قَبۡلُ وَرُسُلٗا لَّمۡ نَقۡصُصۡهُمۡ عَلَيۡكَۚ وَكَلَّمَ ٱللَّهُ مُوسَىٰ تَكۡلِيمٗا
Na Mitume tulio kwisha kukuhadithia kabla yake, na Mitume wengine hatukukuhadithia. Na Mwenyezi Mungu alinena na Musa kwa maneno.
Kadhaalika tumewatuma Mitume wengi ambao tumekwisha taja khabari zao kabla yake. Na Mitume wengine hatukukusimulia hadithi zao. Na njia ya kumpa Wahyi Musa ilikuwa Mwenyezi Mungu akisema naye moja kwa moja nyuma ya pazia, lakini bila ya kuwepo mwengine kati.
Arabic explanations of the Qur’an:
رُّسُلٗا مُّبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَى ٱللَّهِ حُجَّةُۢ بَعۡدَ ٱلرُّسُلِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَزِيزًا حَكِيمٗا
Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu baada ya kuletewa Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Tuliwapeleka Mitume hao kuwapa bishara njema ya thawabu wenye kuamini, na kuwaonya adhabu wale walio kufuru, ili watu wasiwe na hoja ya kumtafutia kisababu Mwenyezi Mungu baada ya kwisha wapeleka Mitume. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, ni Mshindi, wala hana yeyote madaraka pamoja naye, na ni Mwenye hikima kwa atendayo.
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّٰكِنِ ٱللَّهُ يَشۡهَدُ بِمَآ أَنزَلَ إِلَيۡكَۖ أَنزَلَهُۥ بِعِلۡمِهِۦۖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يَشۡهَدُونَۚ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدًا
Lakini Mwenyezi Mungu anayashuhudia aliyo kuteremshia wewe. Ameyateremsha kwa kujua kwake - na Malaika pia wanashuhudia. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi.
Lakini ikiwa hao watu hawashuhudii kukusadikisha, basi Mwenyezi Mungu Mwenyewe anashuhudia kuwa aliyo kuteremshia ni sahihi. Hakika Yeye amekuteremshia hayo kwa hikima, na kwa mujibu wa ujuzi wake. Na Malaika nao wanashuhudia hayo kadhaalika. Na ewe Mtume! Yakutosha wewe ushahidi wa Mwenyezi Mungu, kuliko ushahidi wowote mwenginewe.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ قَدۡ ضَلُّواْ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا
Hakika walio kufuru na wakazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, wamekwisha potelea mbali.
Hakika wale ambao wamekufuru wasikusadiki wewe, na wakawazuia watu wasiingie katika Dini ya Mwenyezi Mungu, bila ya shaka wamekuwa mbali mno na Haki.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَظَلَمُواْ لَمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ طَرِيقًا
Hakika wale walio kufuru na wakadhulumu hawi Mwenyezi Mungu kuwasamehe wala kuwaongoa njia.
Wale walio kufuru, na wakajidhulumu nafsi zao, na wakamdhulumu Mtume kwa kuupinga ujumbe wake, na wakawadhulumu watu walipo wafichia Haki, Mwenyezi Mungu hatowasamehe kamwe maadamu watabaki katika ukafiri wao. Wala hatawapa uwongofu wa kuijua njia ya kuvuka. Sio mtindo wake Subhanahu kuwasamehe watu kama hao nao wangali kubaki katika upotovu wao.
Arabic explanations of the Qur’an:
إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدٗاۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى ٱللَّهِ يَسِيرٗا
Isipo kuwa njia ya Jahannamu. Humo watadumu milele. Na hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi.
Lakini atawapeleka kwenye njia ya Motoni, na humo wabakie daima dawamu. Na hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jambo jepesi.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلرَّسُولُ بِٱلۡحَقِّ مِن رَّبِّكُمۡ فَـَٔامِنُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ وَإِن تَكۡفُرُواْ فَإِنَّ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَكَانَ ٱللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Enyi Watu! Amekwisha kujieni Mtume huyu na haki itokayo kwa Mola wenu Mlezi. Basi aminini, ndiyo kheri yenu. Na mkikakanusha basi hakika viliomo mbinguni na duniani ni vya Mwenyezi Mungu tu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye hikima.
Enyi watu! Amekwisha kukujieni Mtume huyu, Muhammad, na Dini ya Haki kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi yaaminini aliyo kuja nayo; ndiyo itakuwa kheri yenu. Na pindi mkikataa ila kukufuru tu, basi mjue kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkwasi na imani yenu, hana haja nayo. Yeye ndiye Mwenye kukumilikini nyinyi. Kwani vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vyake Yeye, kwa kuvimiliki, kuviumba na kuviendesha atakavyo. Naye ni Mwenye kuvijua vyema viumbe vyake, ni Mwenye hikima katika uendeshaji wake. Haupotezi ujira wa mwema, wala hapuuzi kumlipa mwovu.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَهۡلَ ٱلۡكِتَٰبِ لَا تَغۡلُواْ فِي دِينِكُمۡ وَلَا تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّۚ إِنَّمَا ٱلۡمَسِيحُ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ رَسُولُ ٱللَّهِ وَكَلِمَتُهُۥٓ أَلۡقَىٰهَآ إِلَىٰ مَرۡيَمَ وَرُوحٞ مِّنۡهُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦۖ وَلَا تَقُولُواْ ثَلَٰثَةٌۚ ٱنتَهُواْ خَيۡرٗا لَّكُمۡۚ إِنَّمَا ٱللَّهُ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ سُبۡحَٰنَهُۥٓ أَن يَكُونَ لَهُۥ وَلَدٞۘ لَّهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَكَفَىٰ بِٱللَّهِ وَكِيلٗا
Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha.
Enyi Watu wa Kitabu! Msipindukie haki, mkazidisha kupita kiasi katika dini yenu, wala msimzulie uwongo Mwenyezi Mungu, mkaukanya utume wa Isa, au mkamfanya kuwa ni Mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Kwani Masihi ni Mtume kama walivyo Mitume wengine. Mwenyezi Mungu amemuumba kwa uwezo wake na neno lake alilo mbashiria kwalo, na Jibrili akampulizia Maryamu roho ya Mwenyezi Mungu. Hii ni siri katika siri za uwezo wake Mwenyezi Mungu. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake wote imani ya kweli. Wala msidai kuwa katika Ungu kuna Utatu!! Tokeni katika upotovu huu, itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu, wala hana mshirika wake. Naye ametakasika na kuwa na mwana! Na kila kilioko katika mbingu na ardhi ni chake. Na Yeye Mwenyewe anajitosha peke yake kuwa ni Mwendeshaji wa Ufalme wake. (Kuitwa Nabii Isa Neno au Roho iliyo toka kwa Mungu, hakumpi Ungu. Yeye ni neno kwa kuumbwa kwa amri ya "Kun", "Kuwa" akawa. Haya ni kuwapinga Mayahudi walio dai kuwa yeye ni mwanaharamu. Basi wanaambiwa kuwa ameumbwa kama vilivyo umbwa vitu vyote, kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Naye ni Roho iliyo toka kwa Mwenyezi Mungu kama walivyo pewa Waumini wote (58.22) na alivyo puliziwa Adam (15.29) na kwa hivyo wanaadamu wote (32.7-9). Hapana hata pahala pamoja katika Injili ziliomo katika Biblia ambapo Yesu (Nabii Isa a.s.) alijiita mwenyewe Mwana wa Mungu. Kila mara akijiita Mwana wa Adamu. Na alipo mwita Mungu Baba, alikusudia ni Baba wa watu wote, kama alipo sema: "Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Injili ya Yohana 10.33-36.)
Arabic explanations of the Qur’an:
لَّن يَسۡتَنكِفَ ٱلۡمَسِيحُ أَن يَكُونَ عَبۡدٗا لِّلَّهِ وَلَا ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ ٱلۡمُقَرَّبُونَۚ وَمَن يَسۡتَنكِفۡ عَنۡ عِبَادَتِهِۦ وَيَسۡتَكۡبِرۡ فَسَيَحۡشُرُهُمۡ إِلَيۡهِ جَمِيعٗا
Masihi hataona uvunjifu kuwa mtumwa wa Mwenyezi Mungu, wala Malaika walio karibishwa. Na watakao ona uvunjifu utumwa wa Mwenyezi Mungu na kufanya kiburi, basi atawakusanya wote kwake.
Masihi hakujiona bora hata akatae kuwa ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu, wala hawakujiona bora Malaika walio karibishwa. Na mwenye kutakabari na kujiona mtu wa juu hataweza kuikimbia adhabu ya Mwenyezi Mungu Siku atakayo wakusanya watu kwa ajili ya hisabu.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَيُوَفِّيهِمۡ أُجُورَهُمۡ وَيَزِيدُهُم مِّن فَضۡلِهِۦۖ وَأَمَّا ٱلَّذِينَ ٱسۡتَنكَفُواْ وَٱسۡتَكۡبَرُواْ فَيُعَذِّبُهُمۡ عَذَابًا أَلِيمٗا وَلَا يَجِدُونَ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٗا وَلَا نَصِيرٗا
Na ama walio amini na wakatenda mema atawalipa ujira wao sawa sawa, na atawazidishia kwa fadhila yake. Na ama wale walio ona uvunjifu na wakafanya kiburi, basi atawaadhibu adhabu iliyo chungu. Wala hawatopata mlinzi wala wa kuwanusuru asiye kuwa Mwenyezi Mungu.
Ama walio amini wakatenda mema atawalipa thawabu za vitendo vyao, na atawazidishia kwa fadhila yake, kwa kuwakirimu na kuwaneemesha. Na ama wale walio kataa kumuabudu, na wakajiona bora wasimshukuru, hao amewaandalia adhabu yenye machungu makali. Hapana msaidizi wa kuwakinga nayo wala wa kuwanusuru.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُم بُرۡهَٰنٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ نُورٗا مُّبِينٗا
Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi.
Enyi watu wote! Zimekwisha kujieni dalili zilizo wazi za ukweli wa Mtume Muhammad. Na tumekuteremshieni kwa ulimi wake Qur'ani iliyo wazi kama mwangaza, unao angaza Njia, na inayo kuongozeni kwendea mafanikio.
Arabic explanations of the Qur’an:
فَأَمَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ بِٱللَّهِ وَٱعۡتَصَمُواْ بِهِۦ فَسَيُدۡخِلُهُمۡ فِي رَحۡمَةٖ مِّنۡهُ وَفَضۡلٖ وَيَهۡدِيهِمۡ إِلَيۡهِ صِرَٰطٗا مُّسۡتَقِيمٗا
Ama wale walio muamini Mwenyezi Mungu, na wakashikamana naye, basi atawatia katika rehema yake na fadhila, na atawaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Ama walio msadiki Mwenyezi Mungu na ujumbe wake alio leta, na wakaifuata Dini yake, atawatia katika Bustani zake Akhera, na atawamiminia rehema yake, na atawakusanya katika ukunjufu wa fadhila yake, na atawawezesha hapa duniani kuthibiti katika Njia yake Iliyo Nyooka.
Arabic explanations of the Qur’an:
يَسۡتَفۡتُونَكَ قُلِ ٱللَّهُ يُفۡتِيكُمۡ فِي ٱلۡكَلَٰلَةِۚ إِنِ ٱمۡرُؤٌاْ هَلَكَ لَيۡسَ لَهُۥ وَلَدٞ وَلَهُۥٓ أُخۡتٞ فَلَهَا نِصۡفُ مَا تَرَكَۚ وَهُوَ يَرِثُهَآ إِن لَّمۡ يَكُن لَّهَا وَلَدٞۚ فَإِن كَانَتَا ٱثۡنَتَيۡنِ فَلَهُمَا ٱلثُّلُثَانِ مِمَّا تَرَكَۚ وَإِن كَانُوٓاْ إِخۡوَةٗ رِّجَالٗا وَنِسَآءٗ فَلِلذَّكَرِ مِثۡلُ حَظِّ ٱلۡأُنثَيَيۡنِۗ يُبَيِّنُ ٱللَّهُ لَكُمۡ أَن تَضِلُّواْۗ وَٱللَّهُ بِكُلِّ شَيۡءٍ عَلِيمُۢ
Wanakuomba uhukumu, sema: Mwenyezi Mungu anakupeni hukumu juu ya mkiwa. Ikiwa mtu amekufa, naye hana mtoto, lakini anaye ndugu wa kike, basi huyo atapata nusu alicho acha maiti. Na mwanamume atamrithi ndugu wa kike ikiwa hana mwana. Na ikiwa wao ni ndugu wa kike wawili, basi watapata thuluthi mbili za alicho acha maiti. Na wakiwa ndugu wanaume na wanawake, basi mwanamume atapata sehemu iliyo sawa na ya wanawake wawili. Mwenyezi Mungu anakubainishieni ili msipotee; na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
Ewe Nabii! Wanakuuliza vipi atarithiwa aliye kufa naye akawa hana mwana, wala mzazi. Sema: Hakika hukumu ya Mwenyezi Mungu katika urithi wa hawa ni kuwa, akiwa maiti ana ndugu wa kike basi atapata nusu ya tirka. Na akiwa maiti ni mwanamke naye ana ndugu wa kiume basi atarithi mali yote. Na ikiwa ameacha ndugu wawili wa kike, basi watapata hao thuluthi mbili ya urithi. Na ikiwa hao ndugu ni mchanganyiko wanaume na wanawake, basi fungu la mwanamume ni sawa na mafungu mawili ya wanawake. Mwenyezi Mungu anakubainishieni haya msije mkapotea katika kugawa mafungu ya urithi. Na Mwenyezi Mungu ni Mkamilifu wa ujuzi wa a'mali zenu na vitendo vyenu vyote. Na atakulipeni kwavyo. (Angalia: Urithi wa ndugu katika Aya hii ni wa ndugu khalisa, yaani ndugu kwa baba na mama, au ndugu kwa baba. Ama urithi wa ndugu kwa mama tu umekwisha tajwa katika Aya 12 ya Sura hii ya Annisaa.) Na Sunna (Mafunzo ya Mtume) imebainisha kuwa wakizidi kuliko ndugu wa kike wawili, pamoja na Aya ya mirathi iliyo tajwa, kuwa wakizidi kuliko binti wawili, watachukua thuluthi mbili. Ni bora kuwa zaidi kuliko ndugu wawili wa kike, kwa sababu mabinti ni karibu zaidi kwa maiti. Tuzingatie kuwa kwa mujibu wa kanuni za Kizungu za kurithi, ambazo zimetokana na kanuni ya Kirumi, ndugu wanaume wala wa kike wala watoto wao hawarithi. Na juu ya hivyo mwenye mali anayo ruhusa kumkata yeyote asipate urithi wake. Uislamu umekataza haya. Warithi lazima wapate urithi wao, ila mtu anayo haki ya kuandika wasia kujihukumia kisicho zidi thuluthi moja ya mali yake.(W.H. Ingrams katika kitabu chake Zanzibar Its History and Its People ameandika: "Hakika Sharia Takatifu yaonekana kuwa ni ya haki zaidi sana kuliko hata mpango wa Kiingereza wa kugawanya mali. Katika Zanzibar [na bila ya shaka katika Waislamu wote] hapana mwendo wa kuwa mtu "kukatwa urithi akabakishwa na shilingi moja tu"; vyo vyote vile, ni sehemu ndogo tu ndiyo inaweza kuandikiwa wasia, na yaliyo baki lazima yagawiwe kwa warithi kwa mujibu wa kiwango maalumu.")
Arabic explanations of the Qur’an:
 
Translation of the meanings Surah: An-Nisā’
Surahs’ Index Page Number
 
Translation of the Meanings of the Noble Qur'an - Swahili translation - Ali Muhsen Alberwany - Translations’ Index

Translation of the Quran meanings into Swahili by Ali Muhsen Alberwany

close