Traducción de los significados del Sagrado Corán - Traducción al idioma swahili- Abdullah Mohamad y Naser Jamis

Número de la página:close

11 : 14

قَالَتۡ لَهُمۡ رُسُلُهُمۡ إِن نَّحۡنُ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۖ وَمَا كَانَ لَنَآ أَن نَّأۡتِيَكُم بِسُلۡطَٰنٍ إِلَّا بِإِذۡنِ ٱللَّهِۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Mitume waliposikia yale yaliyosemwa na watu wao waliwaambia, Ni kweli kwamba sisi hatukuwa isipokuwa ni binadamu kama nyinyi, kama mlivyosema. Lakini Allah Mtukufu Anawafanyia wema Anaowataka miongoni mwa waja wake kwa kuwapa neema Zake na kuwateua kwa kuwapa utume Wake. Na hizo dalili waziwazi mlizozitaka, haiwezekani sisi kuwaletea isipokuwa kwa idhini ya Allah Mtukufu na taufiki Yake. Na kwa Allah Mtukufu Peke Yake wanategemea Waumini katika mambo yao yote. info
التفاسير: |

12 : 14

وَمَا لَنَآ أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى ٱللَّهِ وَقَدۡ هَدَىٰنَا سُبُلَنَاۚ وَلَنَصۡبِرَنَّ عَلَىٰ مَآ ءَاذَيۡتُمُونَاۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُتَوَكِّلُونَ

«Na vipi sisi tusimtegemee Allah Mtukufu, na hali Yeye Ndiye Aliyetuongoza njia ya kuokoka na adhabu Yake kwa kufuata hukumu za dini Yake? Na sisi tutavumilia sana makero yenu kwetu kwa maneno maovu na mengineyo. Na kwa Allah Mtukufu Peke Yake ni lazima Waumini wamtegemee Awapatie nusura na ushindi juu ya maadui zao». info
التفاسير: |

13 : 14

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِرُسُلِهِمۡ لَنُخۡرِجَنَّكُم مِّنۡ أَرۡضِنَآ أَوۡ لَتَعُودُنَّ فِي مِلَّتِنَاۖ فَأَوۡحَىٰٓ إِلَيۡهِمۡ رَبُّهُمۡ لَنُهۡلِكَنَّ ٱلظَّٰلِمِينَ

Nyoyo za makafiri ziliingia dhiki kwa maneno ya Mitume na wakasema kuwaambia, «Hakika tutawatoa kutoka miji yetu mpaka mrudi kwenye dini yetu.» Allah Mtukufu Akatuma wahyi kwa Mitume kwamba Atawaangamiza wenye kukataa, wenye kumkanusha Yeye na Mitume Wake. info
التفاسير: |

14 : 14

وَلَنُسۡكِنَنَّكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَافَ مَقَامِي وَخَافَ وَعِيدِ

«Na tutaufanya mwisho mwema uwe ni wa Mitume na wafuasi wao kwa kuwakalisha kwenye ardhi ya makafiri baada ya kuwaangamiza. Kuwaangamiza huko na kuwakalisha Waumini ardhi yao ni jambo la uhakika kwa anayeogopa kisimamo chake mbele yangu Siku ya Kiyama na akaogopa onyo langu na adhabu yangu». info
التفاسير: |

15 : 14

وَٱسۡتَفۡتَحُواْ وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٖ

Mitume wakaelekea kwa Mola wao wakamuomba Awape ushindi juu ya maadui wao na Ahukumu baina yao, na Yeye Akawakubalia na Akamwangamiza kila mwenye kujiona asiyekubali haki, Asiyeifuata na Asiyetaka kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtakasia ibada. info
التفاسير: |

16 : 14

مِّن وَرَآئِهِۦ جَهَنَّمُ وَيُسۡقَىٰ مِن مَّآءٖ صَدِيدٖ

Mbele yake, huyu kafiri, patakuwa na Jahanamu, ataikuta na adhabu yake na atanyweshwa humo usaha na damu zinazotoka kwenye miili ya watu wa Motoni. info
التفاسير: |

17 : 14

يَتَجَرَّعُهُۥ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُۥ وَيَأۡتِيهِ ٱلۡمَوۡتُ مِن كُلِّ مَكَانٖ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٖۖ وَمِن وَرَآئِهِۦ عَذَابٌ غَلِيظٞ

Mwenye kiburi atajaribu kumeza usaha na damu na vinginevyo vinavyotiririka mara kwa mara kutoka kwa watu wa Motoni, na hataweza kuzimeza kwa uchafu wake, kuunguza kwake na uchungu wake. Na adhabu kali ya kila aina itamjia kwenye kila kiungo katika mwili wake. Hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika. Na baada ya adhabu hii atapatiwa adhabu nyingine yenye kuumiza. info
التفاسير: |

18 : 14

مَّثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِرَبِّهِمۡۖ أَعۡمَٰلُهُمۡ كَرَمَادٍ ٱشۡتَدَّتۡ بِهِ ٱلرِّيحُ فِي يَوۡمٍ عَاصِفٖۖ لَّا يَقۡدِرُونَ مِمَّا كَسَبُواْ عَلَىٰ شَيۡءٖۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَٰلُ ٱلۡبَعِيدُ

Hali ya matendo mazuri ya makafiri ulimwenguni, kama vile kufanya wema na kuunga udugu, ni kama hali ya jivu lililopigwa na upepo wa nguvu katika siku yenye upepo mkali usiache hata alama yake. Hivyo ndivyo yatakavyokuwa matendo yao, hawatapata kwa matendo hayo kitu cha kuwanufaisha mbele ya Allah Mtukufu; kwani ukafiri umeyaondoa kama vile upepo ulivyoondoa jivu. Kushughulika huko na kufanya matendo mema huko bila ya msingi, ndio kupotea kuliko mbali na njia ya sawa info
التفاسير: |
prev

Ibrahim

next
:
0:00 0:00