Firo maanaaji Alqur'aana Teddunde nden - Eggo (nantino) ngo e Swahiliire - Abdullah Muhammad e Naasir Khamis.

Tonngoode hello ngon:close

6 : 61

وَإِذۡ قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُم مُّصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيَّ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَمُبَشِّرَۢا بِرَسُولٖ يَأۡتِي مِنۢ بَعۡدِي ٱسۡمُهُۥٓ أَحۡمَدُۖ فَلَمَّا جَآءَهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ قَالُواْ هَٰذَا سِحۡرٞ مُّبِينٞ

Na wakumbushe, (ewe Mtume), watu pindi ‘Ǐsâ, mwana wa Maryam, alipowaambia watu wake, «Mimi ni Mjumbe wa Allah Mtukufu kwenu, ni mwenye kusadikisha Taurati iliyokuja kabla yangu, na ni mwenye kushuhudilia ukweli wa Mtume atakayekuja baada yangu, jina lake ni Aḥmad» naye ni Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na ni mwenye kulingania watu wamuamini, basi alipowajia Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa aya zilizo wazi walisema, «Huu ni uchawi wa wazi». info
التفاسير: |

7 : 61

وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ وَهُوَ يُدۡعَىٰٓ إِلَى ٱلۡإِسۡلَٰمِۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلظَّٰلِمِينَ

Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi na adui zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu urongo na akamfanya kuwa ana washirika wa kuabudiwa, na hali yeye anaitwa aingie kwenye Uislamu na kumpwekesha Allah Mtukufu Peke Yake kwa ibada. Na Allah Mtukufu Hawaafikii, wale waliozidhulumu nafsi zao kwa kukufuru na kukanusha, kwenye njia ambayo ndani yake kuna kufaulu kwao. info
التفاسير: |

8 : 61

يُرِيدُونَ لِيُطۡفِـُٔواْ نُورَ ٱللَّهِ بِأَفۡوَٰهِهِمۡ وَٱللَّهُ مُتِمُّ نُورِهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡكَٰفِرُونَ

Hawa madhalimu wanataka kuitengua haki aliyotumwa kwayo Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), nayo ni Qur’ani, kwa maneno yao ya urongo. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuipa nguvu haki kwa kuitimiza Dini Yake, japokuwa wale wapingaji wenye kukanusha watachukia. info
التفاسير: |

9 : 61

هُوَ ٱلَّذِيٓ أَرۡسَلَ رَسُولَهُۥ بِٱلۡهُدَىٰ وَدِينِ ٱلۡحَقِّ لِيُظۡهِرَهُۥ عَلَى ٱلدِّينِ كُلِّهِۦ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُشۡرِكُونَ

Yeye Ndiye aliyemtuma Mtume Wake Muhammad kwa Qur’ani na Dini ya haki, ili Aifanye kuwa juu ya dini zilizo kinyume nayo, japokuwa washirikina watachukia hilo. info
التفاسير: |

10 : 61

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ تِجَٰرَةٖ تُنجِيكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٖ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Je niwaonyeshe biashara yenye mapato makubwa ambayo itawaokoa na adhabu yenye kuumiza? info
التفاسير: |

11 : 61

تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَٰهِدُونَ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٰلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ

Ni muendelee kumuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, na mpigane jihadi katika njia ya Allah Mtukufu kuinusuru Dini Yake kwa mali zenu na nafsi zenu, hilo ni bora kwenu kuliko biashara ya duniani. Basi mkiwa mnajua vitu venye madhara na manufaa, fuateni amri hiyo. info
التفاسير: |

12 : 61

يَغۡفِرۡ لَكُمۡ ذُنُوبَكُمۡ وَيُدۡخِلۡكُمۡ جَنَّٰتٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ وَمَسَٰكِنَ طَيِّبَةٗ فِي جَنَّٰتِ عَدۡنٖۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ

Mkifanya yale ambayo Allah Mtukufu Amewaamrisha, enyi Waumini, Atayasitiri madhambi yenu, na Atawatia kwenye mabustani ya Pepo ambayo chini ya miti yake inapita mito, na makazi yaliyotakasika na kusafishika ndani ya Mabustani ya kukaa daima, Huko ndiko kufaulu ambako hakuna kufaulu zaidi yake. info
التفاسير: |

13 : 61

وَأُخۡرَىٰ تُحِبُّونَهَاۖ نَصۡرٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتۡحٞ قَرِيبٞۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na kuna neema nyingine kwenu, (enyi Waumini), mtaipenda, nayo ni msaada kutoka kwa Allah Mtukufu utakaowajia na ushindi wa haraka mtakaoupata kwa mikono yenu. Na wape bishara Waumini, (ewe Mtume), ya kunusuriwa na kupata ushindi duniani na kupata Pepo kesho Akhera. info
التفاسير: |

14 : 61

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُوٓاْ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ لِلۡحَوَارِيِّـۧنَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٞ مِّنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٞۖ فَأَيَّدۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَىٰ عَدُوِّهِمۡ فَأَصۡبَحُواْ ظَٰهِرِينَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Kuweni watetezi wa dini ya Allah Mtukufu kama walivyokuwa marafiki wa kidhati wa ‘Ῐsā watetezi wa Dini ya Allah Mtukufu pale alipowaambia «Ni nani atakayesimama kunihami na kunisaidia katika mambo ya kujikurubisha kwa Allah Mtukufu?» Wakasema, «Sisi ndio watetezi wa Dini ya Allah Mtukufu.» Hapo kundi moja la Wana wa Isrãîl likaongoka na kundi lingine likapotea, tukawapa nguvu wale waliomuamini Allah Mtukufu na tukawapa ushindi juu ya wale waliowafanyia uadui miongoni mwa vipote vya manaswara, wakawa na nguvu juu yao kwa kupewa utume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). info
التفاسير: |
prev

As-Saff

next
:
0:00 0:00