Traduction des sens du Noble Coran - La traduction en swahili - 'Abd Allah Muhammad et Nâsir Khamîs

prev

Ad-Duha

next

1 : 93

وَٱلضُّحَىٰ

Allah Mtukufu Anaapa kwa wakati wa dhuha, na uliokusudiwa ni wakati wa mchana mzima. info
التفاسير: |

2 : 93

وَٱلَّيۡلِ إِذَا سَجَىٰ

Na kwa usiku utuliapo na viumbe na likakolea giza lake. «Allah Mtukufu Huapa kwa Atakacho katika viumbe vyake. Ama kiumbe, hafai kuapa kwa asiyekuwa Muumba wake, Kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu ni ushirikina». info
التفاسير: |

3 : 93

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ

Hakukuwacha Mola wako, (ewe Mtume), wala Hakukuchukia kwa kuchelewesha kukuteremshiaWahyi. info
التفاسير: |

4 : 93

وَلَلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لَّكَ مِنَ ٱلۡأُولَىٰ

Na Nyumba ya Akhera ni bora kwako kuliko nyumba ya ulimwengu. info
التفاسير: |

5 : 93

وَلَسَوۡفَ يُعۡطِيكَ رَبُّكَ فَتَرۡضَىٰٓ

Na Atakupa Mola wako, (ewe Mtume), neema ya kila sampuli uridhike. info
التفاسير: |

6 : 93

أَلَمۡ يَجِدۡكَ يَتِيمٗا فَـَٔاوَىٰ

Kwani hakukukuta, kabla ya hapo, ukiwa ni yatima, akakuhifadhi na kukutunza? info
التفاسير: |

7 : 93

وَوَجَدَكَ ضَآلّٗا فَهَدَىٰ

Na akakukuta hujui chochote kuhusu kitabu wala Imani, Akakufundisha yale amabayo ulikuwa huyajui na akakupa taufiki ya kufanya matendo mema? info
التفاسير: |

8 : 93

وَوَجَدَكَ عَآئِلٗا فَأَغۡنَىٰ

Na akakukuta masikini, Akakuletea riziki yako, na Akakutajirisha kwa kutosheka na kusubiri? info
التفاسير: |

9 : 93

فَأَمَّا ٱلۡيَتِيمَ فَلَا تَقۡهَرۡ

Basi yatima usimtendee ubaya. info
التفاسير: |

10 : 93

وَأَمَّا ٱلسَّآئِلَ فَلَا تَنۡهَرۡ

Na muombaji usimkaripie, bali mlishe na umtimizie haja zake. info
التفاسير: |

11 : 93

وَأَمَّا بِنِعۡمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثۡ

Na neema alizokupa mola wako zielezee. info
التفاسير: |
prev

Ad-Duha

next
:
0:00 0:00