કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષાતર - અલી મોહસીન અલ્ બરવાની * - ભાષાંતરોની અનુક્રમણિકા

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

શબ્દોનું ભાષાંતર સૂરહ: અલ્ મુર્સલાત   આયત:

Surat Al-Mursalat

وَٱلۡمُرۡسَلَٰتِ عُرۡفٗا
Naapa kwa zinazo tumwa kwa upole! 
Naapa kwa Aya zilizo tumwa kwa ulimi wa Jibrili kumpelekea Muhammad kwa upole wa kawaida na kheri,
અરબી તફસીરો:
فَٱلۡعَٰصِفَٰتِ عَصۡفٗا
Na zinazo vuma kwa kasi!
Na kwa Aya zenye kuzitwaa kwa nguvu dini nyengine zote za uwongo zikizipeperushia mbali,
અરબી તફસીરો:
وَٱلنَّٰشِرَٰتِ نَشۡرٗا
Na zikaeneza maeneo yote!
Na kwa Aya zenye kueneza hikima na uwongofu katika nyoyo za walimwengu kwa uenezi mkubwa mno,
અરબી તફસીરો:
فَٱلۡفَٰرِقَٰتِ فَرۡقٗا
Na zinazo farikisha zikatawanya!
Na zenye kufarikisha baina ya kweli na uwongo kwa mfarakano ulio wazi kabisa,
અરબી તફસીરો:
فَٱلۡمُلۡقِيَٰتِ ذِكۡرًا
Na zinazo peleka mawaidha!
Na zenye kuwapa watu mawaidha ya kuwanufaisha,
અરબી તફસીરો:
عُذۡرًا أَوۡ نُذۡرًا
Kwa kuudhuru au kuonya,
Ili iwe ni udhuru kwao na onyo wasiwe na hoja,
અરબી તફસીરો:
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَوَٰقِعٞ
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka yatakuwa!
Hakika haya mliyo ahidiwa ya kuja Kiyama kwa yakini yatatimia tu bila ya shaka yoyote.
અરબી તફસીરો:
فَإِذَا ٱلنُّجُومُ طُمِسَتۡ
Wakati nyota zitakapo futwa,
Basi nyota zitapo ondolewa kabisa,
અરબી તફસીરો:
وَإِذَا ٱلسَّمَآءُ فُرِجَتۡ
Na mbingu zitakapo pasuliwa,
Na mbingu zitapo pasuka,
અરબી તફસીરો:
وَإِذَا ٱلۡجِبَالُ نُسِفَتۡ
Na milima itakapo peperushwa,
Na milima ikavurugwa na ikapeperushiwa mbali na upepo,
અરબી તફસીરો:
وَإِذَا ٱلرُّسُلُ أُقِّتَتۡ
Na Mitume watakapo wekewa wakati wao,
Na Mitume wakawekewa wakati maalumu wahudhurie kwa ajili ya kuwatolea ushahidi kaumu zao.
અરબી તફસીરો:
لِأَيِّ يَوۡمٍ أُجِّلَتۡ
Kwa siku gani hiyo wamewekewa muda huo?
Kwa ajili ya siku gani yametayarishwa mambo haya makubwa makubwa?
અરબી તફસીરો:
لِيَوۡمِ ٱلۡفَصۡلِ
Kwa siku ya kupambanua!
Kwa ajili ya siku watakapo pambanuliwa baina ya viumbe.
અરબી તફસીરો:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ
Na nini kitakacho kujuulisha siku ya kupambanua ni nini?
Na nini cha kukujuvya ina nini hiyo siku ya kupambanua?
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao, siku hiyo hao wanao kanusha!
Ni maangamio ya milele siku hiyo kwa hao wanao kadhibisha walio waahidi Mitume!
અરબી તફસીરો:
أَلَمۡ نُهۡلِكِ ٱلۡأَوَّلِينَ
Kwani hatukuwaangamiza walio tangulia?
Kwani hatukuwaangamiza mataifa ya zamani yaliyo kadhibisha,
અરબી તફસીરો:
ثُمَّ نُتۡبِعُهُمُ ٱلۡأٓخِرِينَ
Kisha tukawafuatilizia walio fuatia?
Na kisha tukawafuatilizia hao wenginewe tukawateketeza hali kadhaalika,
અરબી તફસીરો:
كَذَٰلِكَ نَفۡعَلُ بِٱلۡمُجۡرِمِينَ
Ndio kama hivi tuwatendavyo wakosefu!
Kwa madhambi waliyo yafanya na walivyo mkataa Mwenyezi Mungu?
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Siku hiyo ni siku ya kuteketezwa walio kadhibisha, kama tulivyo waahidi.
અરબી તફસીરો:
أَلَمۡ نَخۡلُقكُّم مِّن مَّآءٖ مَّهِينٖ
Kwani hatukukuumbeni kwa maji ya kudharauliwa?
Kwani hatukukuumbeni kutokana na maji yaliyo dhalili, nayo ni manii,
અરબી તફસીરો:
فَجَعَلۡنَٰهُ فِي قَرَارٖ مَّكِينٍ
Kisha tukayaweka mahali pa utulivu madhubuti?
Na tukayaweka maji haya katika pahala patulivu,
અરબી તફસીરો:
إِلَىٰ قَدَرٖ مَّعۡلُومٖ
Mpaka muda maalumu?
Mpaka kutimilia kuumbwa kwake na kutengenezwa kwake kwa muda anao ujua Mwenyezi Mungu.
અરબી તફસીરો:
فَقَدَرۡنَا فَنِعۡمَ ٱلۡقَٰدِرُونَ
Tukakadiria na Sisi ni wabora wa kukadiria.
Nasi tukaweka vipimo katika kuumbwa kwake, na kutengenezwa kwake, na kutoka kwake. Basi wabora wa kupima na kukadiria ni Sisi.
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Ole wao hao wanao kadhibisha neema za kuumba na kukadiria.
અરબી તફસીરો:
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ كِفَاتًا
Kwani hatukuifanya ardhi yenye kukusanya
Kwani hatukuifanya ardhi kuwa imekusanya juu ya mgongo wake
અરબી તફસીરો:
أَحۡيَآءٗ وَأَمۡوَٰتٗا
Walio hai na maiti?
Viumbe vilivyo hai visio hisabika, na vilio kufa visio kadirika,
અરબી તફસીરો:
وَجَعَلۡنَا فِيهَا رَوَٰسِيَ شَٰمِخَٰتٖ وَأَسۡقَيۡنَٰكُم مَّآءٗ فُرَاتٗا
Na ndani yake tukaweka milima mirefu yenye kuthibiti, na tunakunywesheni maji matamu?
Na tukaweka milima iliyo thibiti imara mirefu, na tukakunywesheni maji matamu?
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo hao wanao kadhibisha neema hizi!
અરબી તફસીરો:
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ مَا كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Nendeni kwenye adhabu mliyo kuwa mkiikanusha!
Siku ya kupambanua wataambiwa makafiri: Nendeni huko Motoni mliko kuwa mkikukanusha.
અરબી તફસીરો:
ٱنطَلِقُوٓاْ إِلَىٰ ظِلّٖ ذِي ثَلَٰثِ شُعَبٖ
Nendeni kwenye kivuli chenye mapande matatu!
Nendeni kwenye joto la moshi wa Jahannamu ulio gawika kwa ukubwa wake mapande matatu.
અરબી તફસીરો:
لَّا ظَلِيلٖ وَلَا يُغۡنِي مِنَ ٱللَّهَبِ
Hakikingi moto, wala hakiwaepushi na mwako.
Hapana cha kujikinga na joto la siku hiyo, wala kivuli hicho hakipunguzi joto la mwako hata kidogo.
અરબી તફસીરો:
إِنَّهَا تَرۡمِي بِشَرَرٖ كَٱلۡقَصۡرِ
Hakika Moto huo unatoa macheche kama majumba!
Moto huo hutupa macheche yenye ukubwa kama majumba,
અરબી તફસીરો:
كَأَنَّهُۥ جِمَٰلَتٞ صُفۡرٞ
Kama kwamba ni ngamia wa rangi ya manjano!
Au utaona hayo macheche kama ngamia weusi wenye kuingia rangi ya manjano.
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanao kanusha kwamba hizi ndizo sifa za Moto.
અરબી તફસીરો:
هَٰذَا يَوۡمُ لَا يَنطِقُونَ
Hii ni siku ambayo hawatatamka kitu,
Haya uliyo simuliwa yatatokea katika siku ambayo hawatatamka kitu cha kuwanufaisha,
અરબી તફસીરો:
وَلَا يُؤۡذَنُ لَهُمۡ فَيَعۡتَذِرُونَ
Wala hawataruhusiwa kutoa udhuru.
Wala hawatakuwa na idhini ya kutamka, wala hawatatoa udhuru, kwani hawana udhuru.
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha siku hii.
અરબી તફસીરો:
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِۖ جَمَعۡنَٰكُمۡ وَٱلۡأَوَّلِينَ
Hii ndiyo siku ya kupambanua. Tumekukusanyeni nyinyi na walio tangulia.
Hii ndiyo siku ya kufafanua baina ya mwenye ukweli, na mwenye uwongo, kwa kuwa kila mmoja atalipwa kwa mujibu wa anavyo stahiki. Enyi mnao mkadhibisha Muhammad! Tumekujaalieni nyinyi na walio kutangulieni walio kadhibisha mfano wenu,
અરબી તફસીરો:
فَإِن كَانَ لَكُمۡ كَيۡدٞ فَكِيدُونِ
kiwa mnayo hila, nifanyieni hila Mimi!
Kama mnayo hila ya kujikinga na adhabu basi fanyeni hila hiyo. Basi njooni muepukane na adhabu yangu.
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao walio kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha ahadi ya Mwenyezi Mungu.
અરબી તફસીરો:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي ظِلَٰلٖ وَعُيُونٖ
Hakika wachamngu watakuwa katika vivuli na chemchem,
Hakika wachamngu wenye kujikinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu watakuwa katika kivuli kikubwa, na chemchem zinazo miminika,
અરબી તફસીરો:
وَفَوَٰكِهَ مِمَّا يَشۡتَهُونَ
Na matunda wanayo yapenda,
Na matunda wanayo yaonea ladha, na wanayo yapenda,
અરબી તફસીરો:
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
Wataambiwa kwa kuamkiwa na kukirimiwa: Kuleni na mnywe chakula na vinywaji kwa starehe kwa sababu ya vitendo vyema mlivyo kuwa mkivitenda duniani.
અરબી તફસીરો:
إِنَّا كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Hakika ndio kama hivyo tunavyo walipa watendao mema.
Hakika Sisi huwalipa mfano wa malipo hayo matukufu watu wema.
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanayo ikadhibisha Pepo.
અરબી તફસીરો:
كُلُواْ وَتَمَتَّعُواْ قَلِيلًا إِنَّكُم مُّجۡرِمُونَ
Kuleni na mjifurahishe kidogo tu. Hakika nyinyi ni wakosefu!
Na makafiri wataambiwa: Kuleni na mjistareheshe kwa starehe isiyo baki muda mrefu, kwani hakika nyinyi ni wakosefu kwa kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu.
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku hiyo wanao ikadhibisha neema.
અરબી તફસીરો:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱرۡكَعُواْ لَا يَرۡكَعُونَ
Na wakiambiwa: Inameni! Hawainami.
Na wakiambiwa: Swalini kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na mnyenyekeeni Yeye, hawanyenyekei wala hawaswali; bali hushikilia kiburi chao!
અરબી તફસીરો:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo hao wanao kanusha!
Wataangamia siku wanao kadhibisha amri za Mwenyezi Mungu na makatazo yake.
અરબી તફસીરો:
فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَهُۥ يُؤۡمِنُونَ
Basi maneno gani baada ya haya watayaamini?
Basi maneno gani hawa watayaamini ikiwa hawaiamini Qur'ani, na hali hii ni muujiza ulio toka mbinguni?
અરબી તફસીરો:
 
શબ્દોનું ભાષાંતર સૂરહ: અલ્ મુર્સલાત
સૂરહ માટે અનુક્રમણિકા પેજ નંબર
 
કુરઆન મજીદના શબ્દોનું ભાષાંતર - સ્વાહિલી ભાષાતર - અલી મોહસીન અલ્ બરવાની - ભાષાંતરોની અનુક્રમણિકા

સ્વાહિલી ભાષામાં કુરઆન મજીદનું ભાષાતર, ભાષાતર કરનારનું નામ મોહસીન અલ્ બરવાની

બંધ કરો