Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Fassarar Ma'anoni Sura: Suratu Al'najm   Aya:

Surat An-Najm

وَٱلنَّجۡمِ إِذَا هَوَىٰ
Naapa kwa nyota inapo tua!
Ninaapa kwa nyota inapo tua kwa kuchwa, ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Tafsiran larabci:
مَا ضَلَّ صَاحِبُكُمۡ وَمَا غَوَىٰ
Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
ya kwamba Muhammad hakuiacha Njia iliyo sawa ya kufuata Haki, na wala hakupata kuitakidi upotovu.
Tafsiran larabci:
وَمَا يَنطِقُ عَنِ ٱلۡهَوَىٰٓ
Wala hatamki kwa matamanio.
Wala halitoki katika anayo yatamka ya Qur'ani kwa mapendo ya nafsi yake.
Tafsiran larabci:
إِنۡ هُوَ إِلَّا وَحۡيٞ يُوحَىٰ
Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; .
Hii Qur'ani anayo itamka si chochote ila ni Wahyi (Ufunuo) ulio toka kwa Mwenyezi Mungu anamfunulia yeye.
Tafsiran larabci:
عَلَّمَهُۥ شَدِيدُ ٱلۡقُوَىٰ
Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu!
Aliye mfundisha ufunuo huu ni mwenye nguvu nyingi.
Tafsiran larabci:
ذُو مِرَّةٖ فَٱسۡتَوَىٰ
Mwenye kutua, akatulia!
Ambaye ametua akili zake na maoni yake, akasimama sawa sawa katika sura yake;
Tafsiran larabci:
وَهُوَ بِٱلۡأُفُقِ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.
Naye yuko upande wa juu katika mbingu upeo wa macho wa mwenye kuangalia.
Tafsiran larabci:
ثُمَّ دَنَا فَتَدَلَّىٰ
Kisha akakaribia na akateremka.
Kisha Jibrili alimkaribia, na akazidi kukaribia,
Tafsiran larabci:
فَكَانَ قَابَ قَوۡسَيۡنِ أَوۡ أَدۡنَىٰ
Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.
hata akawa ukaribu wake ni kiasi ya mipinde miwili, bali karibu kuliko hivyo.
Tafsiran larabci:
فَأَوۡحَىٰٓ إِلَىٰ عَبۡدِهِۦ مَآ أَوۡحَىٰ
Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.
Jibrili akamfunulia mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, alicho mfunulia, nao ufunuo huo ni jambo lenye shani kubwa na athari ya mbali kabisa.
Tafsiran larabci:
مَا كَذَبَ ٱلۡفُؤَادُ مَا رَأَىٰٓ
Moyo haukusema uwongo uliyo yaona.
Moyo wa Muhammad haukukanya yale macho yake yaliyo yaona.
Tafsiran larabci:
أَفَتُمَٰرُونَهُۥ عَلَىٰ مَا يَرَىٰ
Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?
Hivyo nyinyi mnamkadhibisha Mtume wa Mwenyezi Mungu na mnabishana naye kwa aliyo yaona kwa macho yake?
Tafsiran larabci:
وَلَقَدۡ رَءَاهُ نَزۡلَةً أُخۡرَىٰ
Na akamwona mara nyingine,
Na bila ya shaka Muhammad alimwona Jibrili kwa sura yake mara nyengine,
Tafsiran larabci:
عِندَ سِدۡرَةِ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Penye Mkunazi wa mwisho.
Katika pahala pasipo juulikana ila na Mwenyezi Mungu tu, ambapo amepaita Sidratul muntahaa, "Mkunazi wa Mwisho".
Tafsiran larabci:
عِندَهَا جَنَّةُ ٱلۡمَأۡوَىٰٓ
Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.
Na akasimulia kuwa hapo ndio ipo Jannatul Ma-awa, Bustani inayo kaliwa.
Tafsiran larabci:
إِذۡ يَغۡشَى ٱلسِّدۡرَةَ مَا يَغۡشَىٰ
Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.
Vikafunikwa na kuzibwa, kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu, visio weza kuelezwa.
Tafsiran larabci:
مَا زَاغَ ٱلۡبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ
Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
Jicho la Muhammad halikubabaika kwa aliyo yaona, na wala hakukiuka mpaka ya aliyo amrishwa kwa kuona kwake huko.
Tafsiran larabci:
لَقَدۡ رَأَىٰ مِنۡ ءَايَٰتِ رَبِّهِ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ
Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.
Hakika ameona mengi katika Ishara za Mwenyezi Mungu na maajabu yake makubwa makubwa.
Tafsiran larabci:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱللَّٰتَ وَٱلۡعُزَّىٰ
Je! Mmemuona Lata na Uzza?
Je! Mmeyajua hayo, na mkayafikiri ya kina Lata na Uzza?
Tafsiran larabci:
وَمَنَوٰةَ ٱلثَّالِثَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ
Na Manaat, mwingine wa tatu?
Na Manata, huyo mwengine wa tatu, mlio wafanya kuwa ni miungu wa kuwaabudu?
Tafsiran larabci:
أَلَكُمُ ٱلذَّكَرُ وَلَهُ ٱلۡأُنثَىٰ
Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na wanawake?
Mkagawa, nyinyi muwe na watoto wa kiume, na mkamfanyia Mwenyezi Mungu awe na watoto wa kike!
Tafsiran larabci:
تِلۡكَ إِذٗا قِسۡمَةٞ ضِيزَىٰٓ
Huo ni mgawanyo wa dhulma!
Huo basi ni ugawaji wa dhulma, mnamgawia Mwenyezi Mungu kile mnacho kichukia nyinyi wenyewe!
Tafsiran larabci:
إِنۡ هِيَ إِلَّآ أَسۡمَآءٞ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّ وَمَا تَهۡوَى ٱلۡأَنفُسُۖ وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ ٱلۡهُدَىٰٓ
Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka kwa Mola wao Mlezi.
Hayo masanamu yenu si chochote ila ni majina tu yasiyo na maana yoyote ya kiungu. Mmeyatunga nyinyi na baba zenu kwa kufuata pumbao lenu la upotovu. Mwenyezi Mungu hakuteremsha nayo hoja yoyote ya kusadikisha huo uzushi wenu mnao wadaia. Na hawa hawafuati ila ni dhana tu, na kipendacho nyoyo zao zilio potoka na kuacha maumbile yaliyo sawa. Na hakika yalikwisha wajia kutoka kwa Mola wao Mlezi yenye uwongofu, laiti wangeli ufuata huo!
Tafsiran larabci:
أَمۡ لِلۡإِنسَٰنِ مَا تَمَنَّىٰ
Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?
Mwanaadamu hapati kila anacho kitamani, ya kupata uombezi wa haya masanamu au mengineyo anayo yatamani kwa nafsi yake.
Tafsiran larabci:
فَلِلَّهِ ٱلۡأٓخِرَةُ وَٱلۡأُولَىٰ
Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
Kwani mambo yote, ya duniani na Akhera, ni ya Mwenyezi Mungu peke yake.
Tafsiran larabci:
۞ وَكَم مِّن مَّلَكٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ لَا تُغۡنِي شَفَٰعَتُهُمۡ شَيۡـًٔا إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ أَن يَأۡذَنَ ٱللَّهُ لِمَن يَشَآءُ وَيَرۡضَىٰٓ
Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na kumridhia.
Na malaika wengi wa mbinguni, juu ya ubora wa vyeo vyao, haufai kitu uombezi wao isipo kuwa baada ya kupewa idhini huyo mwombezi na Mwenyewe Mtukufu, na kumridhia huyo mwenye kuombewa.
Tafsiran larabci:
إِنَّ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ لَيُسَمُّونَ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ تَسۡمِيَةَ ٱلۡأُنثَىٰ
Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
Hakika hao wasio iamini Akhera ndio bila ya shaka wanao sema kuwa Malaika ni wanawake. Wanasema: Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu!
Tafsiran larabci:
وَمَا لَهُم بِهِۦ مِنۡ عِلۡمٍۖ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا ٱلظَّنَّۖ وَإِنَّ ٱلظَّنَّ لَا يُغۡنِي مِنَ ٱلۡحَقِّ شَيۡـٔٗا
Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.
Na kwa kauli hii hawana ujuzi wowote. Hawafuati kitu ila dhana zao tu zilio potoka, na dhana haifai kitu mbele ya haki.
Tafsiran larabci:
فَأَعۡرِضۡ عَن مَّن تَوَلَّىٰ عَن ذِكۡرِنَا وَلَمۡ يُرِدۡ إِلَّا ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا
Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu, na wala hataki ila maisha ya dunia.
Basi jitenge nao hao makafiri walio ipuuza Qur'ani na ikawa hamu yao si chochote ila uhai wa duniani tu, wakiyakataa yenye maslaha nao.
Tafsiran larabci:
ذَٰلِكَ مَبۡلَغُهُم مِّنَ ٱلۡعِلۡمِۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ وَهُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱهۡتَدَىٰ
Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuongoka.
Hayo wanayo yafuata katika itikadi zao, na vitendo vyao ndio ukomo walio yafikilia katika ilimu. Hakika Mola wako Mlezi anamjua vyema anaye shikilia upotovu, na anamjua vyema aliye elekea kupokea uwongofu.
Tafsiran larabci:
وَلِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ لِيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَسَٰٓـُٔواْ بِمَا عَمِلُواْ وَيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ بِٱلۡحُسۡنَى
Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda mema awalipe mema.
Na ni vya Mwenyezi Mungu pekee vyote viliomo katika mbingu na ardhi, kwa kuviumba na kuvidabiri, ili awalipe walio potea wenye kufanya viovu vitendo vyao, na awalipe walio hidika watu wema kwa malipo yaliyo mema.
Tafsiran larabci:
ٱلَّذِينَ يَجۡتَنِبُونَ كَبَٰٓئِرَ ٱلۡإِثۡمِ وَٱلۡفَوَٰحِشَ إِلَّا ٱللَّمَمَۚ إِنَّ رَبَّكَ وَٰسِعُ ٱلۡمَغۡفِرَةِۚ هُوَ أَعۡلَمُ بِكُمۡ إِذۡ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَإِذۡ أَنتُمۡ أَجِنَّةٞ فِي بُطُونِ أُمَّهَٰتِكُمۡۖ فَلَا تُزَكُّوٓاْ أَنفُسَكُمۡۖ هُوَ أَعۡلَمُ بِمَنِ ٱتَّقَىٰٓ
Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua sana mwenye kujikinga na maovu.
Wema hao ndio wale wanao jitenga na madhambi yenye adhabu kubwa kubwa, na yanayo chukiza mno. Lakini Mwenyezi Mungu husamehe dhambi ndogo ndogo. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkuu wa kughufiria, naye anajua vyema hali zenu. Kwani Yeye ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, na mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu katika hali zenu mbali mbali za kukua na kugeuka. Basi msikae mkijisifu nafsi zenu kuwa mmesafika kwa kujigamba na kujifakhari. Na Yeye ndiye Mjuzi mkubwa kabisa wa kila mwenye kumcha na akajisafisha nafsi yake kweli kweli kwa uchamngu wake.
Tafsiran larabci:
أَفَرَءَيۡتَ ٱلَّذِي تَوَلَّىٰ
Je! Umemwona yule aliye geuka?
Je! Umezingatia ukamwona anaye puuza kuifuata Haki,
Tafsiran larabci:
وَأَعۡطَىٰ قَلِيلٗا وَأَكۡدَىٰٓ
Na akatoa kidogo, kisha akajizuia?
Na akatoa kidogo katika mali, na khalafu akakata kabisa kutoa?
Tafsiran larabci:
أَعِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡغَيۡبِ فَهُوَ يَرَىٰٓ
Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona?
Je! Huyo anayo ilimu ya kujua mambo ya ghaibu, basi kwa hivyo ndio anayajua yanayo mpelekea kuiacha kuifuata Haki, na akafanya ubakhili wa mali?
Tafsiran larabci:
أَمۡ لَمۡ يُنَبَّأۡ بِمَا فِي صُحُفِ مُوسَىٰ
Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?
Kwani huyo hakuambiwa yaliomo katika Vitabu vya Musa
Tafsiran larabci:
وَإِبۡرَٰهِيمَ ٱلَّذِي وَفَّىٰٓ
Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi?
Na Ibrahim, aliye fika ukomo wa kutimiza aliyo agana na Mwenyezi Mungu,
Tafsiran larabci:
أَلَّا تَزِرُ وَازِرَةٞ وِزۡرَ أُخۡرَىٰ
Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi madhambi ya mwengine?
Ya kwamba hapana mtu ataye mbebea dhambi mwenginewe?
Tafsiran larabci:
وَأَن لَّيۡسَ لِلۡإِنسَٰنِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?
Na kwamba mtu hapati ila malipo ya vitendo vyake mwenyewe.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّ سَعۡيَهُۥ سَوۡفَ يُرَىٰ
Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?
Na kwamba vitendo vyake vitakuja tangazwa, na ataviona Siku ya Kiyama, iwe ni kumtukuza mtenda mema, na kumkebehi mtenda maovu.
Tafsiran larabci:
ثُمَّ يُجۡزَىٰهُ ٱلۡجَزَآءَ ٱلۡأَوۡفَىٰ
Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.
Kisha kila mtu atalipwa malipo anayo stahiki.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّ إِلَىٰ رَبِّكَ ٱلۡمُنتَهَىٰ
Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.
Na kwamba kwa hakika ni kwa Mola wako Mlezi, wala si kwa mwenginewe, ndio miadi ya kurejea.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَضۡحَكَ وَأَبۡكَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.
Na Yeye peke yake ni Mwenye uweza wa kuufanya uso uonyeshe furaha au maudhiko, na pia ni Mwenye kuziumba sababu za starehe na dhiki.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَمَاتَ وَأَحۡيَا
Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha.
Na hakika ni Yeye, ndiye Mwenye kuondoa uhai, na kuuleta.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّهُۥ خَلَقَ ٱلزَّوۡجَيۡنِ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
Na Yeye ndiye aliye umba vitu kwa jozi, yaani dume na jike, binaadamu na wanyama,
Tafsiran larabci:
مِن نُّطۡفَةٍ إِذَا تُمۡنَىٰ
Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.
Kutokana na manii yanayo miminwa. Makusudio ya Aya hii tukufu ni kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Yeye ameumba waume na wake katika wanaadamu na wanyama wote kutokana na tone ya manii ambayo humo humo mna ume na uke. Na juu ya udogo wake na udhaifu wake ndio chemchem ya uhai. Umuujiza wa Qur'ani unadhihirika katika Aya hii tukufu ukikumbuka kuwa ulimwengu ulikuwa haujui mpaka hivi karibu kuwa katika maji ya mwanamume ndio zimo mbegu "sperms" na katika maji ya mwanamke mna vijiyai "ova", ndio vikikutana vijidudu vya manii ya mwanamume na vijiyai vya mwanamke vikawa kitu kimoja ndio hiyo huwa mimba. Ukweli huu ulitajwa na Qur'ani kabla ya kuvumbuliwa na ilimu za Sayansi.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّ عَلَيۡهِ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُخۡرَىٰ
Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.
Na juu yake Yeye ndio kufufua baada ya kifo.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّهُۥ هُوَ أَغۡنَىٰ وَأَقۡنَىٰ
Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha.
Na Yeye ndiye anaye toa kinacho tosheleza, na akaridhisha kwa kinacho kinaisha na cha kuweka akiba.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّهُۥ هُوَ رَبُّ ٱلشِّعۡرَىٰ
Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya Shii'ra.
Na hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa hii nyota kubwa inayo itwa Shii'ra (Sirius, Dog Star). Makusudio hapa ni Nyota hiyo inayo itwa Ash-shi'ra Alyamaaniya, au wanavyo ita Wazungu Sirius au Dog Star. Nyota hii inang'ara kwa nguvu zaidi kuliko nyota zote ziliomo katika kikundi cha nyota kinacho itwa Alkalbu l-akbar, kwa Kizungu Canis Major au Greater Dog. Nyota hiyo ndiyo inayo zagaa sana mbinguni, na huonekana kusini ya mstari wa kati wa mbinguni kiasi ya daraja 18. Na kwa jina hilo la Nyota ya Mbwa ikijuulikana hata miaka elfu tatu ilio pita. Katika mabaki ya michoro ya Mafirauni wa Misri imeashiriwa pia. Mwenyezi Mungu ameitaja khasa kwa kuwa Waarabu walikuwa wakiiabudu hapo kale, na pia Wamisri wa zamani, kwani kutokea kwake upande wa mashariki katikati ya mwezi wa Julai kabla ya kuchomoza jua kulikuwa kunawafikiana na wakati wa mafuriko ya Misri ya kati, yaani katika tukio muhimu kabisa katika ulimwengu huo wa kale. Na tukio hili huenda ndilo lilio fanya kuanzisha kuwekea kiwango urefu wa mwaka katika dunia nzima. Kwani kudhihiri Nyota ya Shiira kabla ya kuchomoza jua hakutokei ila mara moja tu katika mwaka. Basi huu ndio mwanzo wa mwaka mpya.
Tafsiran larabci:
وَأَنَّهُۥٓ أَهۡلَكَ عَادًا ٱلۡأُولَىٰ
Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza,
Na Yeye ndiye aliye wateketeza kina A'di wa mwanzo, kaumu ya Nabii Hudi. Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.
Tafsiran larabci:
وَثَمُودَاْ فَمَآ أَبۡقَىٰ
Na Thamudi hakuwabakisha,
Na akawateketeza Thamudi, kaumu ya Nabii Saleh. Hakuwabakisha.
Tafsiran larabci:
وَقَوۡمَ نُوحٖ مِّن قَبۡلُۖ إِنَّهُمۡ كَانُواْ هُمۡ أَظۡلَمَ وَأَطۡغَىٰ
Na kabla yao kaumu ya Nuhu. Na hao hakika walikuwa ni madhaalimu zaidi, na waovu zaidi;
Na aliwaangamiza kaumu ya Nuhu kabla ya kuwaangamiza A'di na Thamudi. Hakika hao walikuwa wamekithiri kudhulumu, na wamezidi kwa uasi kuliko A'di na Thamudi.
Tafsiran larabci:
وَٱلۡمُؤۡتَفِكَةَ أَهۡوَىٰ
Na miji iliyo pinduliwa, ni Yeye aliye ipindua.
Na miji ya kaumu Lut'i iliyo pinduliwa juu chini, ni Yeye Mwenyezi Mungu ndiye aliye ipindua.
Tafsiran larabci:
فَغَشَّىٰهَا مَا غَشَّىٰ
Vikaifunika vilivyo funika.
Akaizunguka kwa kuiadhibu kama alivyo izunguka.
Tafsiran larabci:
فَبِأَيِّ ءَالَآءِ رَبِّكَ تَتَمَارَىٰ
Basi neema gani ya Mola wako Mlezi unayo ifanyia shaka?
Basi katika neema za Mola wako Mlezi una shaka nayo ipi?
Tafsiran larabci:
هَٰذَا نَذِيرٞ مِّنَ ٱلنُّذُرِ ٱلۡأُولَىٰٓ
Hili ni Onyo katika maonyo yale yale ya zamani.
Hii Qur'ani ni onyo katika jinsi ya yale yale maonyo ya kale waliyo onywa kwayo watu walio tangulia.
Tafsiran larabci:
أَزِفَتِ ٱلۡأٓزِفَةُ
Kiyama kimekaribia!
Kiyama kimekaribia;
Tafsiran larabci:
لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ كَاشِفَةٌ
Hapana wa kukifichua isipo kuwa Mwenyezi Mungu.
Na wala hapana wa kuujuulisha wakati kitapo tokea ila mwenyewe Mwenyezi Mungu.
Tafsiran larabci:
أَفَمِنۡ هَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ تَعۡجَبُونَ
Je! Mnayastaajabia maneno haya?
Hivyo nyinyi mnapinga kila la kweli? Na mnaistaajabia kwa kuikaataa hii Qur'ani?
Tafsiran larabci:
وَتَضۡحَكُونَ وَلَا تَبۡكُونَ
Na mnacheka, wala hamlii?
Na mnacheka kwa kejeli na maskhaara, wala hamlii kama wafanyavyo wenye yakini,
Tafsiran larabci:
وَأَنتُمۡ سَٰمِدُونَ
Nanyi mmeghafilika?
Nanyi mmo katika pumbao na kutakabari?
Tafsiran larabci:
فَٱسۡجُدُواْۤ لِلَّهِۤ وَٱعۡبُدُواْ۩
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu, na mumuabudu.
Basi msujudieni Mwenyezi Mungu aliye iteremsha Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu wote, na muabuduni Yeye tu peke yake Mwenye kutukuka kwa utukufu wake.
Tafsiran larabci:
 
Fassarar Ma'anoni Sura: Suratu Al'najm
Teburin Jerin Sunayen Surori Lambar shafi
 
Fassarar Ma'anonin Alqura'ni - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - Teburin Bayani kan wasu Fassarori

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

Rufewa