क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस * - अनुवादों की सूची


अर्थों का अनुवाद आयत: (32) सूरा: सूरा अल्-आराफ़
قُلۡ مَنۡ حَرَّمَ زِينَةَ ٱللَّهِ ٱلَّتِيٓ أَخۡرَجَ لِعِبَادِهِۦ وَٱلطَّيِّبَٰتِ مِنَ ٱلرِّزۡقِۚ قُلۡ هِيَ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا خَالِصَةٗ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ ٱلۡأٓيَٰتِ لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ
Sema, ewe Mtume, uwaambie hao wajinga miongoni mwa washirikina, «Ni nani aliyewaharamishia vazi zuri ambalo Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Amelifanya kuwa ni pambo kwenu? Na ni nani Aiyewaharamishia kujistarehesha kwa chakula kizuri cha halali kilichoruzukiwa na Mwenyezi Mungu?» Sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, «Kwa hakika vile alivyoviruhusu Mwenyezi mungu, miongoni mwa mavazi na vitu vizuri miongoni mwa vyakula na vinywaji, ni haki kwa walioamini pamoja na wengineo katika maisha ya ulimwenguni, na ni haki kwa walioamini peke yao Siku ya Kiyama. Maelezo kama hayo ni mafundisho ambayo Mwenyezi Mungu Anayaelezea kwa watu wenye kuyajua mambo wanayoelezwa na kuyaelewa wanayofafanuliwa.
अरबी तफ़सीरें:
 
अर्थों का अनुवाद आयत: (32) सूरा: सूरा अल्-आराफ़
सूरों की सूची पृष्ठ संख्या
 
क़ुरआन के अर्थों का अनुवाद - स्वाहीली अनुवाद - अब्दुल्लाह मुहम्मद तथा नासिर ख़मीस - अनुवादों की सूची

पवित्र क़ुरआन के अर्थों का सवाहिली अनुवाद, अनुवादक : डॉ. अब्दुल्लाह मुहम्मद अबू बक्र तथा शैख़ नासिर ख़मीस

बंद करें