prev

Ibrahim

next

1 : 14

الٓرۚ كِتَٰبٌ أَنزَلۡنَٰهُ إِلَيۡكَ لِتُخۡرِجَ ٱلنَّاسَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذۡنِ رَبِّهِمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Alif, Lãm, Rã.Hii Qur’ani ni kitabu tulichokuletea wahyi ili uwatoe binadamu kutoka kwenye upotevu kuwapeleka kwenye uongofu na mwangaza, kwa idhini ya Mola wao na taufiki Yake kwao, kwenye Uislamu ambao ndio njia ya Allah Mtukufu Mwenye kushinda Anayehimidiwa kwa kila hali. info
التفاسير: |

2 : 14

ٱللَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۗ وَوَيۡلٞ لِّلۡكَٰفِرِينَ مِنۡ عَذَابٖ شَدِيدٍ

Allah Mtukufu Ambaye ni Vyake vilivyoko mbinguni na vya ardhini, kwa kuviumba, kuvimiliki na kuviendesha. Yeye Ndiye Ambaye ni lazima ibada Afanyiwe Yeye Peke Yake. Na wale waliogeuka na wasimuamini Allah Mtukufu na wasiwafuate Mitume Wake watapata maangamivu na adhabu kali Siku ya Kiyama. info
التفاسير: |

3 : 14

ٱلَّذِينَ يَسۡتَحِبُّونَ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَا عَلَى ٱلۡأٓخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَيَبۡغُونَهَا عِوَجًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ضَلَٰلِۭ بَعِيدٖ

Na hawa wenye kugeuka wasimuamini Allah Mtukufu na wasimfuate Mtume Wake ndio wanaochagua maisha ya dunia yenye kutoweka na wanaacha Akhera yenye kusalia, wanawakataza watu kufuata dini ya Allah Mtukufu na wanaitaka iwe ni njia iliyopotoka ili iafikiane na mapendeleo yao. Hao waliosifiwa kwa sifa hizi wamo ndani ya upotevu wa kutoiona haki, wako mbali na njia zote za uongofu. info
التفاسير: |

4 : 14

وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوۡمِهِۦ لِيُبَيِّنَ لَهُمۡۖ فَيُضِلُّ ٱللَّهُ مَن يَشَآءُ وَيَهۡدِي مَن يَشَآءُۚ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na hatukutuma Mitume kabla yako, ewe Nabii, isipokuwa kwa lugha ya watu wake, ili awafafanulie sheria ya Allah Mtukufu, ili Allah Mtukufu Apate kumpoteza Anayemtaka awe kando na uongofu na amuongoze Anayemtaka kwenye ukweli. Na yeye Ndiye Mshindi katika ufalme Wake, ni Mwenye hekima Anayeyaweka mambo mahali pake kulingana na hekima. info
التفاسير: |

5 : 14

وَلَقَدۡ أَرۡسَلۡنَا مُوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ أَنۡ أَخۡرِجۡ قَوۡمَكَ مِنَ ٱلظُّلُمَٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ وَذَكِّرۡهُم بِأَيَّىٰمِ ٱللَّهِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٖ

Na kwa hakika tulimtuma Mûsâ kwa Wana wa Isrâĩl na tukamsaidia kwa miujiza yenye kuonyesha ukweli wake na Tukampa amri awalinganie wao kwenye Imani, ili awatoe kutoka kwenye upotevu awatie kwenye uongofu na awakumbushe neema za Allah Mtukufu na mateso Yake katika wakati wake. Katika kukumbusha huku mambo hayo kuna dalili nyingi kwa kila mvumilivu sana juu ya utiifu wa mwenye kuyaepuka yaliyoharamishwa na Yeye na kuyakubali maandiko Yake, mwenye kushukuru sana, mwenye kusimama kutekeleza haki za Allah Mtukufu na anayemshukuru Allah Mtukufu kwa neema Zake. Aina mbili hizi za watu zimetajwa mahsusi, kwa kuwa wao ndio wanaozingatia hizo dalili na hawaghafiliki nazo. info
التفاسير: |
prev

Ibrahim

next
:
0:00 0:00