Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Surah: Surah Al-Wāqi'ah   Ayah:

Surat Al-Waqi'ah

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Litakapo tukia hilo Tukio .
Kitakapo tukia Kiyama
Tafsir berbahasa Arab:
لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ
Hapana cha kukanusha kutukia kwake.
Haitotokea nafsi yoyote ya kukadhibisha.
Tafsir berbahasa Arab:
خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ
Literemshalo linyanyualo!
Kiyama hicho kitawateremsha chini walio waovu, na kitawanyanyua juu walio wema.
Tafsir berbahasa Arab:
إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا
Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso!
Ardhi itakapo tikiswa, na ikatetemeshwa kwa nguvu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا
Na milima itapo sagwasagwa!
Na milima ikavurugwa teketeke,
Tafsir berbahasa Arab:
فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا
Iwe mavumbi yanayo peperushwa!
Ikawa vumbi la kupeperushwa, Aya hizi tukufu zinaeleza hadi gani vitakuwa vitisho vitavyo uteremkia ulimwengu kitapo fika Kiyama. Na katika vitisho hivyo ni hayo masaibu ya dunia yatakayo athiri ardhi na mat'abaka yake. Kwani hii ardhi tunayo ishi juu ya mgongo wake si yenye kutulia na kukaa sawa kwa utimilivu. Kwani hiyo imeundwa kwa mat'abaka ya majabali yaliyo ingiliana ovyo. Huenda baadhi yao yakateremka yakaachana na mengineyo yaliyo jirani nayo. Na huwa hiyo inayo itwa kupasuka kwa mat'abaka ya ardhi, Geological cleavage kama inavyo tokea katika maeneo kadhaa wa kadhaa. Mpasuko huu ulikuwa na ungali kuwa ndio asili ya chini kabisa ya zilzala, mitetemeko, mikubwa kwa kuathirika na nguvu za kudidimiza na kuvuta zinazo fuatana na mat'abaka ya ardhi yanapo vunjika. Basi mizani ya utulivu ya nguvu hizi inapo geuka kwa kuathirika na mambo mengineyo ya nje huenda zikafunguka nguvu za mtikiso mkubwa ndio ikatokea mitetemeko na mitikisiko ya ardhi, ambayo hubomoa kila kitu kiliopo juu ya ardhi karibu na ilipo anzia hiyo zilzala. Na hapo tena hutokea uharibifu mkubwa mno. Na hayo maelezo ya kisayansi hayageuzi kitu, wala hayako mbali na nadhari ya kidini. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huenda akajaalia sababu za maumbile za kawaida zikajumuika kwa njia tusiyo izoea sisi ili zikiingiliana kwa njia ya kutisha ndio sababu ya kuharibika dunia. Hapo maelezo ya kisayansi yanafuatana na Aya zenye kuonya kwa vitisho hivyo vikuu. Na yote hayo yanatokana kwa Mwenyezi Mungu. Na hutokea kwa idhini yake Mwenyezi Mungu kutimiza hukumu yake katika dunia yetu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ
Na nyinyi mtakuwa namna tatu: .
Na mkawa nyote siku hiyo namna tatu kwa mujibu wa vitendo vyenu;
Tafsir berbahasa Arab:
فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
Basi watu wa mkono wa kulia, watu wa cheo kilio bora, utukufu ulioje huo wa hali yao!
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
Na watu wa kushotoni, hao ni watu wa cheo duni, uovu ulioje wa hali yao!
Tafsir berbahasa Arab:
وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ
Na wa mbele watakuwa mbele.
Na walio tangulia mbele katika mambo ya kheri duniani ndio watakuwa mbele katika vyeo vya Akhera.
Tafsir berbahasa Arab:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Hao ndio watakao karibishwa
Hao ndio walio karibishwa mbele kwa Mwenyezi Mungu. Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.
Tafsir berbahasa Arab:
فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Katika Bustani zenye neema.
Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.
Tafsir berbahasa Arab:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Fungu kubwa katika wa mwanzo,
Hawa walio karibishwa mbele ni kundi la wengi katika mataifa yaliyo tangulia na Manabii wao,
Tafsir berbahasa Arab:
وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
Na wachache katika wa mwisho.
Na wachache katika umma wa Muhammad ukiwalinganisha na hao.
Tafsir berbahasa Arab:
عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ
Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.
Juu ya viti au vitanda vilivyo nakishiwa kwa nakshi za vito vya thamani,
Tafsir berbahasa Arab:
مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ
Wakiviegemea wakielekeana.
wakivitegemea kwa raha na utulivu huku wakielekezana nyuso kwa ziada ya mahaba.
Tafsir berbahasa Arab:
يَطُوفُ عَلَيۡهِمۡ وِلۡدَٰنٞ مُّخَلَّدُونَ
Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,
Wakiwazungukia kwa kuwakhudumia vijana watakao baki milele hivyo hivyo,
Tafsir berbahasa Arab:
بِأَكۡوَابٖ وَأَبَارِيقَ وَكَأۡسٖ مِّن مَّعِينٖ
Kwa vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.
Nao wamechukua vikombe na mabirika yaliyo jaa vinywaji vya Peponi, na bilauri zenye mvinyo kutoka chemchem zinazo miminika,
Tafsir berbahasa Arab:
لَّا يُصَدَّعُونَ عَنۡهَا وَلَا يُنزِفُونَ
Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.
Vinywaji hivyo haviwaletei kuumwa kichwa wala kutokwa akili kwa ulevi.
Tafsir berbahasa Arab:
وَفَٰكِهَةٖ مِّمَّا يَتَخَيَّرُونَ
Na matunda wayapendayo,
Na matunda ya kila namna wanayo yapenda na wanayo yaona;
Tafsir berbahasa Arab:
وَلَحۡمِ طَيۡرٖ مِّمَّا يَشۡتَهُونَ
Na nyama za ndege kama wanavyo tamani.
Na nyama za ndege kama zinavyo tamani nafsi zao.
Tafsir berbahasa Arab:
وَحُورٌ عِينٞ
Na Mahurulaini,
Na wanawake wenye macho ya vikombe,
Tafsir berbahasa Arab:
كَأَمۡثَٰلِ ٱللُّؤۡلُوِٕ ٱلۡمَكۡنُونِ
Walio kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.
Kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa katika chaza, kwa usafi wao na urembo wao.
Tafsir berbahasa Arab:
جَزَآءَۢ بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
Watapewa haya kuwa ni malipo kwa mambo mema waliyo kuwa wakiyatenda duniani.
Tafsir berbahasa Arab:
لَا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا تَأۡثِيمًا
Humo hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,
Huko Peponi hawatasikia maneno yasiyo kuwa na maana, wala masimulizi ya kumtia dhambini mwenye kuyasikia.
Tafsir berbahasa Arab:
إِلَّا قِيلٗا سَلَٰمٗا سَلَٰمٗا
Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama.
Ila watalo sikia ni kauli ya wao kwa wao: Tunakusalimuni kwa Salama.
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡيَمِينِ
Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa kuliani?
Na watu wa mkono wa kulia, hapana ajuaye nini malipo ya watu wa kuliani.
Tafsir berbahasa Arab:
فِي سِدۡرٖ مَّخۡضُودٖ
Katika mikunazi isiyo na miba,
Katika miti ya mikunazi iliyo katwa miba yake,
Tafsir berbahasa Arab:
وَطَلۡحٖ مَّنضُودٖ
Na migomba iliyo pangiliwa,
Na migomba iliyo pangika na ndizi zake zimepandana juu ya mikungu,
Tafsir berbahasa Arab:
وَظِلّٖ مَّمۡدُودٖ
Na kivuli kilicho tanda,
Na kivuli kilicho enea wala hakiondoki,
Tafsir berbahasa Arab:
وَمَآءٖ مَّسۡكُوبٖ
Na maji yanayo miminika,
Na maji yanayo miminika karibu yao popote wayatakapo,
Tafsir berbahasa Arab:
وَفَٰكِهَةٖ كَثِيرَةٖ
Na matunda mengi,
Na matunda ya namna nyingi na kabila nyingi yasiyo tindikia wakati wowote,
Tafsir berbahasa Arab:
لَّا مَقۡطُوعَةٖ وَلَا مَمۡنُوعَةٖ
Hayatindikii wala hayakatazwi,
Wala hazuiwiliwi ayatakayo,
Tafsir berbahasa Arab:
وَفُرُشٖ مَّرۡفُوعَةٍ
Na matandiko yaliyo nyanyuliwa.
Na matandiko yaliyo nyanyuliwa ya starehe.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّآ أَنشَأۡنَٰهُنَّ إِنشَآءٗ
Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,
Hakika Sisi tulianza kuwaumba Mahurulaini mwanzo,
Tafsir berbahasa Arab:
فَجَعَلۡنَٰهُنَّ أَبۡكَارًا
Na tutawafanya vijana,
Na tukawafanya kuwa ni vijana,
Tafsir berbahasa Arab:
عُرُبًا أَتۡرَابٗا
Wanapendana na waume zao, hirimu moja.
Wenye kupendwa na waume zao, wenye umri ulio karibiana,
Tafsir berbahasa Arab:
لِّأَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Kwa ajili ya watu wa kuliani.
Wa tayari kwa neema ya watu wa kuliani.
Tafsir berbahasa Arab:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Fungu kubwa katika wa mwanzo,
Watu wa kulia ni wengi katika mataifu yaliyo kwisha tangulia,
Tafsir berbahasa Arab:
وَثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
Na fungu kubwa katika wa mwisho.
Na kikundi kikubwa katika umma wa Muhammad.
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلشِّمَالِ
Na watu wa kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
Na watu wa kushoto, hapana anaye jua nini adhabu ya watu wa kushoto.
Tafsir berbahasa Arab:
فِي سَمُومٖ وَحَمِيمٖ
Katika upepo wa moto, na maji yanayo chemka,
Watakuwa kwenye upepo umoto utakao wazunguka, unao penya katika tundu za mwili, na maji yaliyo chemshwa motoni wayanywe na wamiminiwe vichwani,
Tafsir berbahasa Arab:
وَظِلّٖ مِّن يَحۡمُومٖ
Na kivuli cha moshi mweusi,
Na katika kivuli cha kiza cheusi cha moshi umoto,
Tafsir berbahasa Arab:
لَّا بَارِدٖ وَلَا كَرِيمٍ
Si cha kuburudisha wala kustarehesha.
Hapana ubaridi wa kupunguza joto la hewa, wala huruma ya kuwaletea nafuu wanapo vuta pumzi.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّهُمۡ كَانُواْ قَبۡلَ ذَٰلِكَ مُتۡرَفِينَ
Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya anasa.
Hakika hao kabla ya haya walikuwa wamepita kiasi katika kustarehea neema za duniani, wamepumbaa hawataki kumt'ii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَكَانُواْ يُصِرُّونَ عَلَى ٱلۡحِنثِ ٱلۡعَظِيمِ
Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa,
Na walikuwa wameshikilia daima kufanya dhambi kubwa kabisa, kwani waliapa kwa Mwenyezi Mungu kwamba kabisa Mwenyezi Mungu hatamfufua aliye kufa.
Tafsir berbahasa Arab:
وَكَانُواْ يَقُولُونَ أَئِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?
Na walikuwa wakisema kwa kukanusha kurejea tena: Ati tutafufuliwa baada ya kwisha kufa, na baadhi ya miili yetu ikisha kuwa udongo na mengine mifupa iliyo chakaa? Ati sisi tutarudishwa tuwe hai mara ya pili?
Tafsir berbahasa Arab:
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
Au baba zetu wa zamani?
Ati tutafufuliwa sisi na baba zetu wa zamani walio kwisha kuwa udongo ulio tapanyika na umepotea katika ardhi?
Tafsir berbahasa Arab:
قُلۡ إِنَّ ٱلۡأَوَّلِينَ وَٱلۡأٓخِرِينَ
Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho
Waambie kwa kuwajibu kukanusha kwao: Hakika wa zamani na wa mwisho, ambao nyinyi ni katika jumla ya hao,
Tafsir berbahasa Arab:
لَمَجۡمُوعُونَ إِلَىٰ مِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.
Nyote mtakusanywa katika wakati wa siku malumu, na wala hamtoipita.
Tafsir berbahasa Arab:
ثُمَّ إِنَّكُمۡ أَيُّهَا ٱلضَّآلُّونَ ٱلۡمُكَذِّبُونَ
Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,
Kisha nyinyi, enyi mnao ipinga Njia ya Uwongofu, mnao kanusha kufufuliwa,
Tafsir berbahasa Arab:
لَأٓكِلُونَ مِن شَجَرٖ مِّن زَقُّومٖ
Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
Bila ya shaka mtakula mti wa Zaqqumu katika Jahannamu, na mtayajaza matumbo yenu kwa shida ya njaa.
Tafsir berbahasa Arab:
فَمَالِـُٔونَ مِنۡهَا ٱلۡبُطُونَ
Na kwa mti huo mtajaza matumbo.
Na mtayajaza matumbo yenu kwa shida ya njaa.
Tafsir berbahasa Arab:
فَشَٰرِبُونَ عَلَيۡهِ مِنَ ٱلۡحَمِيمِ
Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.
Mtakunywa juu ya mlicho kila maji yenye kutokota, yasiyo ondoa kiu,
Tafsir berbahasa Arab:
فَشَٰرِبُونَ شُرۡبَ ٱلۡهِيمِ
Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu.
Na mtakunywa kwa wingi na pupa kama anavyo kunywa ngamia mwenye kiu kisicho katika kiu chake kwa maji.
Tafsir berbahasa Arab:
هَٰذَا نُزُلُهُمۡ يَوۡمَ ٱلدِّينِ
Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.
Hayo yaliyo tajwa ya mateso mbali mbali ndio karamu yao waliyo andaliwa kwa siku ya malipo.
Tafsir berbahasa Arab:
نَحۡنُ خَلَقۡنَٰكُمۡ فَلَوۡلَا تُصَدِّقُونَ
Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
Sisi tulianza kukuumbeni mlipo kuwa si chochote, basi hebu hamkiri uweza wetu wa kukurejesheni tena baada ya kukufufueni?
Tafsir berbahasa Arab:
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تُمۡنُونَ
Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?
Hamuangalii manii mnayo itia katika tumbo la uzazi?
Tafsir berbahasa Arab:
ءَأَنتُمۡ تَخۡلُقُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡخَٰلِقُونَ
Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
Ni nyinyi ndio mwenye uweza juu yake na kuilea mpaka ikawa mtu, au ni Sisi ndio twenye makadara hayo?
Tafsir berbahasa Arab:
نَحۡنُ قَدَّرۡنَا بَيۡنَكُمُ ٱلۡمَوۡتَ وَمَا نَحۡنُ بِمَسۡبُوقِينَ
Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
Sisi tumekuhukumieni mauti, na tumeweka wakati makhsuri wa kufa kwenu. Na wala Sisi si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu,
Tafsir berbahasa Arab:
عَلَىٰٓ أَن نُّبَدِّلَ أَمۡثَٰلَكُمۡ وَنُنشِئَكُمۡ فِي مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
Na wala Sisi si wenye kushindwa kukubadilisheni sura zenu, na kuzileta nyengine, na tukakuumbeni katika umbo jengine na sura nyengine msiyo ijua.
Tafsir berbahasa Arab:
وَلَقَدۡ عَلِمۡتُمُ ٱلنَّشۡأَةَ ٱلۡأُولَىٰ فَلَوۡلَا تَذَكَّرُونَ
Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
Bila ya shaka mmekwisha yakinika kuwa Mwenyezi Mungu alikuumbeni mara ya kwanza, basi je, hamkumbuki kwamba Mwenye kuweza hayo ni Mweza zaidi wa kufanya tena.
Tafsir berbahasa Arab:
أَفَرَءَيۡتُم مَّا تَحۡرُثُونَ
Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?
Je! Hamuangalii mbegu mnayo ipanda katika ardhi?
Tafsir berbahasa Arab:
ءَأَنتُمۡ تَزۡرَعُونَهُۥٓ أَمۡ نَحۡنُ ٱلزَّٰرِعُونَ
Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye kuotesha?
Ni nyinyi mnao ifanya imee au ni Sisi peke yetu ndio tunaifanya imee?
Tafsir berbahasa Arab:
لَوۡ نَشَآءُ لَجَعَلۡنَٰهُ حُطَٰمٗا فَظَلۡتُمۡ تَفَكَّهُونَ
Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki mnastaajabu,
Tungeli taka tungeli ifanya mimea hiyo iwe mabua na mapepe yaliyo katika katika kabla haijapevuka, mkawa mkistaajabu tu kwa uovu ulio isibu,
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّا لَمُغۡرَمُونَ
Mkisema: Hakika sisi tumegharimika;
Huku mkisema: Hakika sisi tumepata khasara baada ya juhudi yetu.
Tafsir berbahasa Arab:
بَلۡ نَحۡنُ مَحۡرُومُونَ
Bali sisi tumenyimwa.
Bali sisi hatuna bahati, tumenyimwa riziki.
Tafsir berbahasa Arab:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلۡمَآءَ ٱلَّذِي تَشۡرَبُونَ
Je! Mnayaona maji mnayo yanywa?
Je! Hamyaoni maji matamu mnayo yanywa?
Tafsir berbahasa Arab:
ءَأَنتُمۡ أَنزَلۡتُمُوهُ مِنَ ٱلۡمُزۡنِ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنزِلُونَ
Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni Sisi ndio wenye kuyateremsha?
Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni, au ni Sisi ndio Wenye kuyateremsha kuwa ni rehema juu yenu? Katika Kiarabu limetajwa neno Almuzni. Maana yake ni mawingu yanayo leta mvua. Na kitendo cha kunyesha mvua kinahitajia mambo yaliyo khusiana na hali ya hewa maalumu ambayo mwanaadamu hana mamlaka nayo, au kuyaleta kwa juhudi zake. Kwa mfano zinahitajiwa pepo zinazo kwenda kwa mkondo zilizo baridi juu ya nyengine zilizo za joto, au hali za kuondoka utulivu katika anga. Na watu wamejaribu kuinyesha mvua kwa mawingu yanayo pita kwa njia ya ufundi, lakini juhudi hizo mpaka sasa ni majaribio, na lilio thibiti katika sayansi ni kufuzu kwa majaribio hayo ni kudogo mno, na hata hivyo kunalazimu ziwepo hali maalumu za maumbile zinazo saidia.
Tafsir berbahasa Arab:
لَوۡ نَشَآءُ جَعَلۡنَٰهُ أُجَاجٗا فَلَوۡلَا تَشۡكُرُونَ
Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona hamshukuru?
Lau tungeli taka tungeli yafanya hayo maji yakawa ya chumvi yasiyo nyweka. Basi mbona hamumshukuru Mwenyezi Mungu aliye yajaalia matamu yenye kunyweka?
Tafsir berbahasa Arab:
أَفَرَءَيۡتُمُ ٱلنَّارَ ٱلَّتِي تُورُونَ
Je! Mnauona moto mnao uwasha?
Je! Hamuuoni moto huo mnao uasha?
Tafsir berbahasa Arab:
ءَأَنتُمۡ أَنشَأۡتُمۡ شَجَرَتَهَآ أَمۡ نَحۡنُ ٱلۡمُنشِـُٔونَ
Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
Ni nyinyi ndio mlio uotesha mti wake, na mkautia ndani ya huo mti moto, au ni Sisi ndio tulio uumbia hivyo, kadhaalika?
Tafsir berbahasa Arab:
نَحۡنُ جَعَلۡنَٰهَا تَذۡكِرَةٗ وَمَتَٰعٗا لِّلۡمُقۡوِينَ
Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko nyikani.
Sisi tumeufanya huu moto uwe ni ukumbusho wa Moto wa Jahannamu mtapo uona, na uwe ni manufaa kwa wasafiri wa msitu na nyika, wakinafiika kwa kupikia chakula chao na kuotea moto wakati wa baridi.
Tafsir berbahasa Arab:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
Basi dumisha kusabihi, kutakasa, kwa kulidhukuru jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema hizi nzuri.
Tafsir berbahasa Arab:
۞ فَلَآ أُقۡسِمُ بِمَوَٰقِعِ ٱلنُّجُومِ
Basi naapa kwa maanguko ya nyota,
Basi ninaapa kweli kwa maangukio ya nyota pale zinapo tua mwisho wa usiku wakati wa Tahajudi, ibada za usiku, na kustaghafiru.
Tafsir berbahasa Arab:
وَإِنَّهُۥ لَقَسَمٞ لَّوۡ تَعۡلَمُونَ عَظِيمٌ
Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti mngeli jua!
Na hakika bila ya shaka hicho ni kiapo kikubwa chenye maana ya kufikia mbali, lau kuwa mnafikiri makusudio yake. Aya mbili hizi zinabainisha hadi ya umuhimu wa kiapo hichi kikubwa. Kwani nyota ni vitu vyenye kutoa mwangaza wenyewe, na nyota ya karibu mno kwetu sisi, nayo ni jua, ni kiasi ya masafa ya miaka 500 ya mwangaza. Na nyota ifuatayo kwa ukaribu iko mbali nasi kwa kiasi cha miaka 4 ya mwangaza takriban. Basi nguvu tunazo zitumia kutokana na jua ndizo zinazo tuwezesha kuishi. Lau kuwa umbali wa jua kutokana na ardhi ni duni ya hivyo au zaidi ya hivyo basi hapana shaka kuwa maisha yangeli kuwa taabu, bali ni muhali. Kadhaalika ukubwa wa nyota unakhitalifiana. Zipo nyota kubwa mno hata ukubwa wake unaweza kukusanya hii ardhi na jua juu ya umbali wao. Vipo vikundi vya nyota vinavyo itwa A'naqiid vinaogelea angani zikivuka Njia ya Maziwa The Milky Way mara kwa mara. Wakati wa kupita kwake zikasadifiana kukutana na kikundi cha jua na zikagongana basi hakika hapo itakuwa ndio maangamizo na kumalizika kwa kweli. Hata ikikaribia nyota moja katika nyota zitokazo kwenye jua basi hayo pia yataleta kuharibika mizani na kupelekea maangamizo na kumalizika ulimwengu. Kwa hivyo basi hakika Ishara za mazingatio na uweza wa Mwenyezi Mungu zinaonekana katika ulimwengu huu alio uumba Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taala na akaupanga.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّهُۥ لَقُرۡءَانٞ كَرِيمٞ
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani Tukufu,
Hakika hii bila ya shaka ni Qur'ani yenye manufaa mengi,
Tafsir berbahasa Arab:
فِي كِتَٰبٖ مَّكۡنُونٖ
Katika Kitabu kilicho hifadhiwa.
Imo katika ubao ulio hifadhiwa Al-lauhu-lmahfudh, usio karibiwa na yeyote ila Malaika walio karibishwa kwa Mwenyezi Mungu. (Kwa watumiaji Computer wanaweza kukisia kuwa hiyo Al-lauhu-lmahfudh ni kama Disk iliyomo ndani ya Computer na haigusi mtu, na Misahafu tunayo iona, na kuisoma, ni kama yapigwayo chapa kutoka hiyo Disk.)
Tafsir berbahasa Arab:
لَّا يَمَسُّهُۥٓ إِلَّا ٱلۡمُطَهَّرُونَ
Hapana akigusaye ila walio takaswa.
Hawaigusi Qur'ani Tukufu ila walio t'ahirika na najisi na hadathi, vitengua udhu;
Tafsir berbahasa Arab:
تَنزِيلٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ni uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
imeteremshwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Tafsir berbahasa Arab:
أَفَبِهَٰذَا ٱلۡحَدِيثِ أَنتُم مُّدۡهِنُونَ
Ni maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
Je! Mnapuuza? Ni Qur'ani hii tukufu ndio nyinyi mnaidharau?
Tafsir berbahasa Arab:
وَتَجۡعَلُونَ رِزۡقَكُمۡ أَنَّكُمۡ تُكَذِّبُونَ
Na badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
Na badala ya kuishukuru riziki yenu ndio mna ikadhibisha?
Tafsir berbahasa Arab:
فَلَوۡلَآ إِذَا بَلَغَتِ ٱلۡحُلۡقُومَ
Yawaje basi itakapo fika roho kwenye koo,
Basi je! Ikifika roho ya mmoja wenu kwenye mapitio ya pumzi,
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَنتُمۡ حِينَئِذٖ تَنظُرُونَ
Na nyinyi wakati huo mnatazama!
Na nyinyi inapo fika roho kwenye koo nanyi mnamwangalia huyo anaye kufa,
Tafsir berbahasa Arab:
وَنَحۡنُ أَقۡرَبُ إِلَيۡهِ مِنكُمۡ وَلَٰكِن لَّا تُبۡصِرُونَ
Na Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
Na Sisi tuko karibu zaidi kwa huyo aliye kabiliwa na mauti na tunaijua zaidi hali yake kuliko nyinyi, lakini nyinyi hamjui hayo wala hamhisi.
Tafsir berbahasa Arab:
فَلَوۡلَآ إِن كُنتُمۡ غَيۡرَ مَدِينِينَ
Na lau kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
Basi je! Ikiwa nyinyi si wenye kunyenyekea kwa Ungu wetu,
Tafsir berbahasa Arab:
تَرۡجِعُونَهَآ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
Mrudishieni roho yake huyo aliye kabiliwa na mauti ikiwa nyinyi mwasema kweli kwamba nyinyi mnazo nguvu na hamshindwi.
Tafsir berbahasa Arab:
فَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُقَرَّبِينَ
Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,
Ama akiwa huyo aliye kabiliwa na mauti ni katika walio tangulia walio karibishwa ,
Tafsir berbahasa Arab:
فَرَوۡحٞ وَرَيۡحَانٞ وَجَنَّتُ نَعِيمٖ
Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
Basi mwisho wake ni raha, na rehema, na riziki njema, na Pepo yenye neema.
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Na akiwa katika watu wa upande wa kulia,
Ama akiwa katika watu wa mkono wa kulia,
Tafsir berbahasa Arab:
فَسَلَٰمٞ لَّكَ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡيَمِينِ
Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande wa kulia.
Basi ataambiwa kwa maamkio na takrima: Unapewa salamu kutokana na watu wa kuliani.
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَمَّآ إِن كَانَ مِنَ ٱلۡمُكَذِّبِينَ ٱلضَّآلِّينَ
Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
Na ama akiwa ni katika wa kushoto, wanao kanusha, walio wapotovu,
Tafsir berbahasa Arab:
فَنُزُلٞ مِّنۡ حَمِيمٖ
Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,
Basi atakirimiwa maji ya moto hadi ya kuchemka,
Tafsir berbahasa Arab:
وَتَصۡلِيَةُ جَحِيمٍ
Na kutiwa Motoni.
Na kubabuliwa na moto wa mwisho wa ukali.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ هَٰذَا لَهُوَ حَقُّ ٱلۡيَقِينِ
Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.
Hakika haya yaliyo tajwa katika Sura hii tukufu bila ya shaka ni kiini cha yakini iliyo thibiti, isiyo ingiliwa na shaka.
Tafsir berbahasa Arab:
فَسَبِّحۡ بِٱسۡمِ رَبِّكَ ٱلۡعَظِيمِ
Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa.
Tanguliza tasbihi kwa kumdhukuru Mola wako Mlezi aliye Mkubwa, kwa kumtakasa na kumshukuru kwa neema zake.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Surah Al-Wāqi'ah
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Terjemahan Makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke Bahasa Sawahili oleh Ali Muhsin Al-Barwani

Tutup