Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany * - Indice Traduzioni

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Traduzione dei significati Sura: Al-Qâri‘ah   Versetto:

Surat Al-Qari'ah

ٱلۡقَارِعَةُ
Inayo gonga!
AL-QAARIA'H, Inayo gonga, ni Kiyama, ambacho kinaanza kwa mpulizo wa mwanzo wa barugumu, na kinaishia itapo katwa hukumu baina ya watu.
Esegesi in lingua araba:
مَا ٱلۡقَارِعَةُ
Nini Inayo gonga?
Kitu gani kilicho cha ajabu zaidi katika ukuu wake, na khatari zake na kitisho chake!
Esegesi in lingua araba:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ
Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?
Na kitu gani kitacho kujuulisha hali ya AL-QAARIA'H katika kitisho chake juu ya nafsi za watu?
Esegesi in lingua araba:
يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ
Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;
Siku hiyo watu watakuwa kama vipepeo kwa wingi na kuhangaika kulia na kushoto, madhaifu na wanyonge!
Esegesi in lingua araba:
وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ
Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!
Na milima itakuwa kama sufi iliyo tiwa rangi na kuchambuliwa kwa kutapanyika vipande mbali mbali na kupeperuka katika anga huku na huku.
Esegesi in lingua araba:
فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ
Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,
Ama yule ambaye mizani yake itakuwa nzito, mema yake yakapindukia kuliko maovu yake,
Esegesi in lingua araba:
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ
Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.
Basi huyo atakuwa na maisha yatayo mridhisha mwenyewe, na nafsi yake itue.
Esegesi in lingua araba:
وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ
Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,
Na ama ambaye mizani yake itakuwa nyepesi, na maovu yake yakazidi kuliko mema yake,
Esegesi in lingua araba:
فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٞ
Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!
Basi makaazi yake yatakuwa Jahannamu.
Esegesi in lingua araba:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ
Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?
Na nini cha kukujuulisha ni nini Hawiya?
Esegesi in lingua araba:
نَارٌ حَامِيَةُۢ
Ni Moto mkali!
Moto ulio mkali, hapana moto unao fikilia ukali wake, hata ukichochewa vipi na kutiwa kuni gani!
Esegesi in lingua araba:
 
Traduzione dei significati Sura: Al-Qâri‘ah
Indice delle Sure Numero di pagina
 
Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany - Indice Traduzioni

Traduzione dei significati del Nobile Corano in swahili di Ali Muhsin Albirwany

Chiudi