クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany * - 対訳の目次

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

対訳 章: ヌーフ章   節:

Surat Nuh

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوۡمِهِۦٓ أَنۡ أَنذِرۡ قَوۡمَكَ مِن قَبۡلِ أَن يَأۡتِيَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ
Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu.
Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake, na tukamwambia: Waonye watu wako kabla haijawajia adhabu yenye machungu makali.
アラビア語 クルアーン注釈:
قَالَ يَٰقَوۡمِ إِنِّي لَكُمۡ نَذِيرٞ مُّبِينٌ
Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu!
Nuh'u akasema: Enyi watu wangu! Hakika mimi ni mwonyaji kwenu, nina risala kutoka kwa Mola wenu Mlezi kwa lugha mnayo ijua,
アラビア語 クルアーン注釈:
أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱتَّقُوهُ وَأَطِيعُونِ
Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii.
Ya kwamba mumt'ii Mwenyezi Mungu, na mumnyenyekee katika kutimiza waajibu zote; na mwogopeni Yeye kwa kuacha mnayo katazwa, na nit'iini mimi katika ninayo kunasihini.
アラビア語 クルアーン注釈:
يَغۡفِرۡ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمۡ وَيُؤَخِّرۡكُمۡ إِلَىٰٓ أَجَلٖ مُّسَمًّىۚ إِنَّ أَجَلَ ٱللَّهِ إِذَا جَآءَ لَا يُؤَخَّرُۚ لَوۡ كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!
Ndipo Mwenyezi Mungu atapo kusameheni madhambi yenu, na atakupeni umri mrefu mpaka ifike ajali iliyo wekwa mwisho wa umri wenu. Hakika mauti yakija hayaakhirishwi kabisa! Lau kuwa mngeli jua majuto mtakayo kuwa nayo utapo kwisha muda wenu mngeli amini.
アラビア語 クルアーン注釈:
قَالَ رَبِّ إِنِّي دَعَوۡتُ قَوۡمِي لَيۡلٗا وَنَهَارٗا
Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana!
Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu waamini usiku na mchana bila ya kuchoka,
アラビア語 クルアーン注釈:
فَلَمۡ يَزِدۡهُمۡ دُعَآءِيٓ إِلَّا فِرَارٗا
Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.
Hawakuzidishwa na wito wangu ila kuukimbia ut'iifu wako.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَإِنِّي كُلَّمَا دَعَوۡتُهُمۡ لِتَغۡفِرَ لَهُمۡ جَعَلُوٓاْ أَصَٰبِعَهُمۡ فِيٓ ءَاذَانِهِمۡ وَٱسۡتَغۡشَوۡاْ ثِيَابَهُمۡ وَأَصَرُّواْ وَٱسۡتَكۡبَرُواْ ٱسۡتِكۡبَارٗا
Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!
Na mimi kila nikiwataka wakuamini Wewe upate kuwasamehe, hubandika vidole vyao kwenye masikio yao ili wasisikie wito wangu, na hujifunika kwa maguo yao ili wasiuone uso wangu! Na wakasimama kidete juu ya ukafiri wao, na wakatakabari kutakabari kukubwa mno!
アラビア語 クルアーン注釈:
ثُمَّ إِنِّي دَعَوۡتُهُمۡ جِهَارٗا
Tena niliwaita kwa uwazi!
Kisha nikawaita waje kwako kwa sauti ya juu,
アラビア語 クルアーン注釈:
ثُمَّ إِنِّيٓ أَعۡلَنتُ لَهُمۡ وَأَسۡرَرۡتُ لَهُمۡ إِسۡرَارٗا
Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri.
kisha nikaudhihirisha wito kwa namna moja, na nikawaita kisirisiri kwa namna nyengine, ili nijaribu kila njia.
アラビア語 クルアーン注釈:
فَقُلۡتُ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ إِنَّهُۥ كَانَ غَفَّارٗا
Nikasema: Ombeni msamaha kwa Mola wenu Mlezi; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe.
Nikawambia watu wangu: Takeni kwa Mola wenu Mlezi maghfira kwa kufru zenu na maasi yenu. Kwani Yeye bado ni Mwingi wa kusamehe madhambi ya mwenye kurejea kwake.
アラビア語 クルアーン注釈:
يُرۡسِلِ ٱلسَّمَآءَ عَلَيۡكُم مِّدۡرَارٗا
Atakuleteeni mvua inyeshe mfululizo.
Atakuleteeni mawingu yatakayo miminika mvua kwa wingi,
アラビア語 クルアーン注釈:
وَيُمۡدِدۡكُم بِأَمۡوَٰلٖ وَبَنِينَ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ جَنَّٰتٖ وَيَجۡعَل لَّكُمۡ أَنۡهَٰرٗا
Na atakupeni mali na wana, na atakupeni mabustani na atakufanyieni mito.
Na atakupeni mali na wana, na hayo ndiyo mapambo ya dunia, na atakupeni mashamba mtayo starehea kwa uzuri wake na matunda yake, na atakujaalieni mito ya kunyweshea mazao yenu na mifugo yenu.
アラビア語 クルアーン注釈:
مَّا لَكُمۡ لَا تَرۡجُونَ لِلَّهِ وَقَارٗا
Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?
Mna nini nyinyi hata hamumtukuzi Mwenyezi Mungu kama anavyo stahiki kutukuzwa, ili mtaraji akukirimuni kwa kukuokoeni na adhabu,
アラビア語 クルアーン注釈:
وَقَدۡ خَلَقَكُمۡ أَطۡوَارًا
Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?
Na hali Yeye ndiye aliye kuumbeni kwa madaraja, tangu tone ya manii, kisha pande la damu, kisha pande la nyama, kisha mafupa na nyama?
アラビア語 クルアーン注釈:
أَلَمۡ تَرَوۡاْ كَيۡفَ خَلَقَ ٱللَّهُ سَبۡعَ سَمَٰوَٰتٖ طِبَاقٗا
Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?
Kwani huoni vipi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba, moja juu ya moja,
アラビア語 クルアーン注釈:
وَجَعَلَ ٱلۡقَمَرَ فِيهِنَّ نُورٗا وَجَعَلَ ٱلشَّمۡسَ سِرَاجٗا
Na akaufanya mwezi ndani yake uwe nuru, na akalifanya jua kuwa taa?
Na akaufanya mwezi katika mbingu hizo unatoa nuru, na akalifanya jua ni taa ambayo kwayo watu wa duniani ndio wanaona kwa mwangaza wake yote wanayo hitajia kuyaona?
アラビア語 クルアーン注釈:
وَٱللَّهُ أَنۢبَتَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ نَبَاتٗا
Na Mwenyezi Mungu amekuotesheni katika ardhi kama mimea.
Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, akakuotesheni kama miema kwa njia ya ajabu,
アラビア語 クルアーン注釈:
ثُمَّ يُعِيدُكُمۡ فِيهَا وَيُخۡرِجُكُمۡ إِخۡرَاجٗا
Kisha atakurudsheni humo na atakutoeni tena.
Na Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na ardhi, akakuotesheni kama miema kwa njia ya ajabu, kisha baada ya kufa atakurejesheni huko huko kwenye ardhi, na tena atakutoeni huko kwa hakika hapana hivi wala hivi.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَٱللَّهُ جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ بِسَاطٗا
Na Mwenyezi Mungu amekukunjulieni ardhi kama busati.
Na Mwenyezi Mungu ameifanya ardhi iliyo kunjuliwa ili mpate kwenda humo katika njia zenye wasaa.
アラビア語 クルアーン注釈:
لِّتَسۡلُكُواْ مِنۡهَا سُبُلٗا فِجَاجٗا
Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.
Na Mwenyezi Mungu ameifanya ardhi iliyo kunjuliwa ili mpate kwenda humo katika njia zenye wasaa.
アラビア語 クルアーン注釈:
قَالَ نُوحٞ رَّبِّ إِنَّهُمۡ عَصَوۡنِي وَٱتَّبَعُواْ مَن لَّمۡ يَزِدۡهُ مَالُهُۥ وَوَلَدُهُۥٓ إِلَّا خَسَارٗا
Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika hao wameniasi, na wamemfuata yule ambaye mali yake na wanawe hawakumzidishia ila khasara.
Alisema Nuh'u: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikatalia mimi niliyo waamrisha ya kuamini na kutaka msamaha, na wakawafuata madhaifu miongoni mwao ambao mali yao na watoto wao hawawazidishii ila khasara tupu katika Akhera.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَمَكَرُواْ مَكۡرٗا كُبَّارٗا
Na wakapanga vitimbi vikubwa.
Na vitimbi vya hao wenye mali mengi, na wana wengi, kwa wanyonge wanao wafuata ni vitimbi vilivyo fika ukomo kwa ukubwa.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَقَالُواْ لَا تَذَرُنَّ ءَالِهَتَكُمۡ وَلَا تَذَرُنَّ وَدّٗا وَلَا سُوَاعٗا وَلَا يَغُوثَ وَيَعُوقَ وَنَسۡرٗا
Na wakasema: Msiwaache miungu yenu, wala msimwache Wadda wala Suwaa' wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra.
Na wao wakiwaambia: Msiache kuiabudu miungu yenu, wala msimwache Wadda, wala Suwaa' , wala Yaghutha, wala Yau'qa, wala Nasra. Na hawa walikuwa miungu ya masanamu iliyo chongwa kwa sura ya wanyama namna mbali mbali.
アラビア語 クルアーン注釈:
وَقَدۡ أَضَلُّواْ كَثِيرٗاۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا ضَلَٰلٗا
Na hao walikwisha wapoteza wengi, wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
Na miungu hii iliwapoteza watu wengi. Na wala huwazidishii wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa ukafiri na inda, ili kuzidi kubaidika na Haki.
アラビア語 クルアーン注釈:
مِّمَّا خَطِيٓـَٰٔتِهِمۡ أُغۡرِقُواْ فَأُدۡخِلُواْ نَارٗا فَلَمۡ يَجِدُواْ لَهُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ أَنصَارٗا
Basi kwa ajili ya makosa yao waligharikishwa wakaingizwa Motoni, wala hawakuwapata wa kuwanusuru badala ya Mwenyezi Mungu.
Kwa sababu ya madhambi yao wakazamishwa kwa tofani, na baada ya kuangamizwa kwao wakatiwa Motoni kwenye moto mkali wa kuwaka na kuteketeza, na wala wasipate yeyote baada ya kumkosa Mwenyezi Mungu, wa kuwanusuru na kuwakinga na adhabu!
アラビア語 クルアーン注釈:
وَقَالَ نُوحٞ رَّبِّ لَا تَذَرۡ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ مِنَ ٱلۡكَٰفِرِينَ دَيَّارًا
Na Nuh'u akasema: Mola wangu Mlezi! Usimwache juu ya ardhi mkaazi wake yeyote katika makafiri!
Na Nuh'u akasema baada ya kukata tamaa nao watu wake: Mola wangu Mlezi! Usimwache yeyote katika hao wanao kukataa Wewe akabaki akizunguka juu ya ardhi!
アラビア語 クルアーン注釈:
إِنَّكَ إِن تَذَرۡهُمۡ يُضِلُّواْ عِبَادَكَ وَلَا يَلِدُوٓاْ إِلَّا فَاجِرٗا كَفَّارٗا
Hakika ukiwaacha watawapoteza waja wako, wala wao hawatazaa ila waovu makafiri.
Ewe Mola wangu Mlezi! Ukiwaacha hao bila ya kuwateketeza na kuwang'oa watawatia waja wako katika upotovu, na wao hawatozaa ila wenye kupotoka vile vile wakaiacha haki, na wakakithiri kukukanya na kukuasi.
アラビア語 クルアーン注釈:
رَّبِّ ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِمَن دَخَلَ بَيۡتِيَ مُؤۡمِنٗا وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۖ وَلَا تَزِدِ ٱلظَّٰلِمِينَ إِلَّا تَبَارَۢا
Mola wangu Mlezi! Nighufirie mimi na wazazi wangu, na kila aliye ingia nyumbani mwangu kuwa ni mwenye kuamini, na Waumini wote wanaume, na Waumini wanawake. Na wala usiwazidishie walio dhulumu ila kupotea.
Mola wangu Mlezi! Nisamehe mimi na wazazi wangu ambao ndio walio kuwa ni sababu ya kuzaliwa mimi, na kila mwenye kuingia nyumbani kwangu kwa kukuamini Wewe, na uwasamehe Waumini wote wanaume na wanawake. Na usiwazidishie makafiri ila kuwaangamiza.
アラビア語 クルアーン注釈:
 
対訳 章: ヌーフ章
章名の目次 ページ番号
 
クルアーンの対訳 - スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany - 対訳の目次

クルアーン・スワヒリ語対訳 - Ali Muhsen Alberwany

閉じる