prev

Al-Mumtahanah

next

1 : 60

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَّخِذُواْ عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمۡ أَوۡلِيَآءَ تُلۡقُونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَقَدۡ كَفَرُواْ بِمَا جَآءَكُم مِّنَ ٱلۡحَقِّ يُخۡرِجُونَ ٱلرَّسُولَ وَإِيَّاكُمۡ أَن تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ رَبِّكُمۡ إِن كُنتُمۡ خَرَجۡتُمۡ جِهَٰدٗا فِي سَبِيلِي وَٱبۡتِغَآءَ مَرۡضَاتِيۚ تُسِرُّونَ إِلَيۡهِم بِٱلۡمَوَدَّةِ وَأَنَا۠ أَعۡلَمُ بِمَآ أَخۡفَيۡتُمۡ وَمَآ أَعۡلَنتُمۡۚ وَمَن يَفۡعَلۡهُ مِنكُمۡ فَقَدۡ ضَلَّ سَوَآءَ ٱلسَّبِيلِ

Enyi mliomuamini (Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo)! Msiwachukue maadui wangu na maadui wenu mkawafanya ni marafiki halisi na vipenzi, mkawa mnaamiliana nao kwa upendo na mkawapasha habari za Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na Waislamu wengine, na hali wao wameikanusha haki iliyowajia ya kumuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na Qur’ani iliyoteremshwa kwake. Wanamtoa Mtume na wanawatoa nyinyi, (enyi Waumini), kutoka Makkah kwa kuwa nyinyi mnamuamini Allah Mtukufu Mola wenu na mnampwekesha. Mkiwa nyinyi, (enyi Waumini), mmehama katika hali ya jihadi katika njia yangu kwa kutafuta radhi yangu kwenu, basi msifanye urafiki na maadui wangu na maadui wenu. Mnawaambia kwa siri kuwa mnawapenda, na mimi ninayajua mnayoyaficha na mnayoyadhihirisha. Na yoyote anayefanya hivyo miongoni mwenu, ashakosea njia ya haki na usawa na amepotea. info
التفاسير: |

2 : 60

إِن يَثۡقَفُوكُمۡ يَكُونُواْ لَكُمۡ أَعۡدَآءٗ وَيَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ وَأَلۡسِنَتَهُم بِٱلسُّوٓءِ وَوَدُّواْ لَوۡ تَكۡفُرُونَ

Wakipata nafasi hao mnaowapenda kwa siri watawapiga vita na watanyoosha mikono yao kwenu, wawaue na wawateke, na pia ndimi zao, wawatukane na wawatusi, na walitamani, kwa hali yoyote, lau mngekanusha kama wao. info
التفاسير: |

3 : 60

لَن تَنفَعَكُمۡ أَرۡحَامُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُمۡۚ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ يَفۡصِلُ بَيۡنَكُمۡۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ

Hawatawanufaisha jamaa zenu wa karibu wala watoto wenu kitu chochote mnapofanya urafiki na wakanushaji kwa ajili yao. Siku ya Kiyama Allah Mtukufu Atawatenganisha nyinyi na wao, Awatie Peponi wanaomtii na Awatie Motoni wanaomuasi. Na Allah Mtukufu Anayaona mnayoyafanya, hakuna chochote kinachofichika Kwake cha maneno yenu na matendo yenu. info
التفاسير: |

4 : 60

قَدۡ كَانَتۡ لَكُمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ فِيٓ إِبۡرَٰهِيمَ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ إِذۡ قَالُواْ لِقَوۡمِهِمۡ إِنَّا بُرَءَٰٓؤُاْ مِنكُمۡ وَمِمَّا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ كَفَرۡنَا بِكُمۡ وَبَدَا بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكُمُ ٱلۡعَدَٰوَةُ وَٱلۡبَغۡضَآءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَحۡدَهُۥٓ إِلَّا قَوۡلَ إِبۡرَٰهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسۡتَغۡفِرَنَّ لَكَ وَمَآ أَمۡلِكُ لَكَ مِنَ ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖۖ رَّبَّنَا عَلَيۡكَ تَوَكَّلۡنَا وَإِلَيۡكَ أَنَبۡنَا وَإِلَيۡكَ ٱلۡمَصِيرُ

Kwa hakika mlikuwa na kiigizo kizuri, (enyi Waumini), kwa Ibrãhîm na wale waliokuwa pamoja naye waliposema kuwaambia wakanushaji Allah Mtukufu, «Sisi tumejiepusha na nyinyi na vile mnavyoviabudu kinyume na Allah Mtukufu. Tumewakanusha nyinyi na tumeukataa ukafiri mlionao, na umejitokeza nje uadui na machukivu ya milele baina yetu sisi na nyinyi madamu bado mko kwenye ukanushaji wenu, mpaka mmuamini Allah Mtukufu Peke Yake.» Lakini haliingii kwenye kuigiza tendo la Ibrãhîm la kumuombea msamaha baba yake, kwa kuwa hilo lilitokea kabla ya Ibrãhîm kudhihirikiwa kuwa baba yake ni adui wa Allah Mtukufu, na alipodhihirikiwa kuwa yeye ni adui wa Allah Mtukufu alijiepusha naye. Mola wetu! Kwako wewe tumetegemea, na kwako wewe tumerejea kwa kutubia, na kwako wewe ndiko marejeo Siku ya Kiyama. info
التفاسير: |

5 : 60

رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ وَٱغۡفِرۡ لَنَا رَبَّنَآۖ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Mola wetu! Usitufanye ni mtihani wenye kuwanufaisha waliokukanusha, kwa kutuadhibu au kuwapa nguvu makafiri juu yetu, wakatufitini kwa kutuepusha na Dini yetu, au wakawa na nguvu juu yetu wakafitinika kwa hilo, na hapo waseme, «Lau hawa wangekua kwenye haki isingewapata adhabu hii,» na hapo wakazidisha ukafiri. Na utustirie dhambi zetu kwa kutusamehe, ewe Mola wetu! Hakika wewe ni Mshindi Asiyekuwa na mwenye kushindana Naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na matendo Yake. info
التفاسير: |
prev

Al-Mumtahanah

next
:
0:00 0:00