prev

Ash-Shura

next

1 : 42

حمٓ

Ḥā, Mīm. info
التفاسير: |

2 : 42

عٓسٓقٓ

‛Ayn, Sīn, Qāf Yametangulia maelezo juu ya herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al-Baqarah . info
التفاسير: |

3 : 42

كَذَٰلِكَ يُوحِيٓ إِلَيۡكَ وَإِلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Kama Alivyokuteremshia Allah Mtukufu, ewe Nabii, hii Qur’ani, Aliteremsha Vitabu na Kurasa kwa Manabii kabla yako. Na Yeye Ndiye Mshindi katika kutesa Kwake, Ndiye Mwenye hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. info
التفاسير: |

4 : 42

لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡعَظِيمُ

Ni vya Allah Mtukufu Peke Yake vilivyoko mbinguni na ardhini, na Yeye Ndiye wa juu kwa cheo Chake na utendeshaji nguvu Wake, Aliye Mkuu Ambaye Ana ukubwa na utukufu. info
التفاسير: |

5 : 42

تَكَادُ ٱلسَّمَٰوَٰتُ يَتَفَطَّرۡنَ مِن فَوۡقِهِنَّۚ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمۡدِ رَبِّهِمۡ وَيَسۡتَغۡفِرُونَ لِمَن فِي ٱلۡأَرۡضِۗ أَلَآ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Zinakaribia mbingu kupasuka pasuka, kila moja juu ya ile inayoifuata, kutokana na ukubwa wa Allah Mtukufu Mwingi wa rehema na haiba Yake, Mwingi wa fadhila na utukufu, na hali Malaika wanamtakasia shukrani Mola wao na kumtakasa na kila sifa ambayo hanasibiani nayo, na wanamuomba Mola wao msamaha wa dhambi za waliyoko ardhini miongoni mwa wale wanaomuamini. Jueni mtanabahi kwamba Allah Mtukufu Ndiye mwingi wa kusamehe dhambi za waja Wake Waumini, na Ndiye Mwenye kuwarehemu. info
التفاسير: |

6 : 42

وَٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَ ٱللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيۡهِمۡ وَمَآ أَنتَ عَلَيۡهِم بِوَكِيلٖ

Na wale waliowafanya wasiokuwa Allah Mtukufu kuwa ni waungu badala Yake wakawategemea na kuwaabudu, basi Allah Mtukufu Anavidhibiti vitendo vyao, ili Awalipe kwavyo Siku ya Kiyama. Na wewe hukuwakilishwa kuvidhibiti vitendo vyao. Hakika yako wewe ni muonyaji tu, hivyo basi ni juu yako kufikisha na ni juu yetu kuhesabu. info
التفاسير: |

7 : 42

وَكَذَٰلِكَ أَوۡحَيۡنَآ إِلَيۡكَ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّتُنذِرَ أُمَّ ٱلۡقُرَىٰ وَمَنۡ حَوۡلَهَا وَتُنذِرَ يَوۡمَ ٱلۡجَمۡعِ لَا رَيۡبَ فِيهِۚ فَرِيقٞ فِي ٱلۡجَنَّةِ وَفَرِيقٞ فِي ٱلسَّعِيرِ

Na kama tulivyowapelekea wahyi Manabii kabla yako, tulikuletea wahyi wa Qur’ani kwa lugha ya Kiarabu, ili uwaonye watu wa (Makkah) na watu wote wengine pembezoni mwake(1), na uwaonye na siku ya Mkusanyiko, nayo ni Siku ya Kiyama, ambayo kuja kwake hakuna shaka, ambapo watu Siku hiyo watakuwa mapote mawili: pote moja litakuwa Peponi, nalo ni lile la waliomuamini Allah Mtukufu na wakayafuata yale aliyokuja nayo Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na pote lingine litakuwa Motoni, nalo ni lile la waliomkanusha Allah Mtukufu na wakaenda kinyume na yale aliyokuja nayo Mtume Wake, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). info
التفاسير: |

8 : 42

وَلَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ لَجَعَلَهُمۡ أُمَّةٗ وَٰحِدَةٗ وَلَٰكِن يُدۡخِلُ مَن يَشَآءُ فِي رَحۡمَتِهِۦۚ وَٱلظَّٰلِمُونَ مَا لَهُم مِّن وَلِيّٖ وَلَا نَصِيرٍ

Na lau angetaka Allah Mtukufu Kuwakusanya viumbe Wake kwenye uongofu na kuwafanya wawe kwenye mila moja iliyoongoka angefanya 1 Kwa kuwa Makkah ni kituo cha ardhi Umm al Q mtukufu kuliko miji yote, ndio ikawa miji yote imeizunguka Makkah na iko pembezoni mwake. U za ardhi pia umithibiti kwenye hadithi za Mtume(s kufasiri aya hii: 42:7. hivyo, lakini Yeye Anataka kuwatia kwenye rehema Yake Anaowataka miongoni mwa waja Wake. Na wale wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kufanya ushirikina, basi hao hawatakuwa na yoyote wa kumtegemea atakayesimamia mambo yao Siku ya Kiyama, wala msaidizi atakayewanusuru kutokana na adhabu ya Allah Mtukufu Aliyetukuka. info
التفاسير: |

9 : 42

أَمِ ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِهِۦٓ أَوۡلِيَآءَۖ فَٱللَّهُ هُوَ ٱلۡوَلِيُّ وَهُوَ يُحۡيِ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Bali hawa washirikina waliwafanya wasiokuwa Allah Mtukufu kuwa wategemewa, wakawa wanawategemea. Allah Mtukufu Peke Yake Ndiye Mwenye kutegemewa, mja anamtegemea kwa kumuabudu na kumtii, na Yeye Anawasimamia waja Wake Waumini kwa kuwatoa kwenye giza kuwatia kwenye mwangaza, na kwa kuwasaidia katika mambo yao yote. Na Yeye Anahuisha waliokufa wakati wa kufufuliwa, na Yeye kwa kila jambo ni Muweza, hakuna chochote kinachomshinda. info
التفاسير: |

10 : 42

وَمَا ٱخۡتَلَفۡتُمۡ فِيهِ مِن شَيۡءٖ فَحُكۡمُهُۥٓ إِلَى ٱللَّهِۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُ رَبِّي عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ

Na kitu chochote kile mnachotafautiana kwacho, enyi watu, miongoni mwa mambo ya dini yenu, basi hukumu irudishwe kwa Allah Mtukufu katika Kitabu Chake na (Sunnah) ya Mtume Wake, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Huyo Ndiye Allah Mtukufu, Mola wangu na Mola wenu, Kwake Yeye nimetegemea katika mambo yangu, na Kwake Yeye ninarejea katika hali zangu zote. info
التفاسير: |
prev

Ash-Shura

next
:
0:00 0:00