prev

As-Saff

next

1 : 61

سَبَّحَ لِلَّهِ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Vimemtakasa Allah Mtukufu na kila kisichonasibiana na Yeye vyote vilivyoko mbinguni na vilivyoko ardhini, na Yeye ni Mshindi Ambaye hakuna mwenye kushindana naye, Mwingi wa hekima katika maneno Yake na vitendo Vyake. info
التفاسير: |

2 : 61

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لِمَ تَقُولُونَ مَا لَا تَفۡعَلُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo! Kwa nini mnatoa ahadi au mnasema maneno bila kuyatekeleza? Haya ni makaripio kwa ambaye matendo yake yanaenda kinyume na maneno yake. info
التفاسير: |

3 : 61

كَبُرَ مَقۡتًا عِندَ ٱللَّهِ أَن تَقُولُواْ مَا لَا تَفۡعَلُونَ

Ni machukivu makubwa sana kutoka kwa Allah Mtukufu kwenu nyinyi mnaposema kwa ndimi zenu maneno msiyoyafanya. info
التفاسير: |

4 : 61

إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلَّذِينَ يُقَٰتِلُونَ فِي سَبِيلِهِۦ صَفّٗا كَأَنَّهُم بُنۡيَٰنٞ مَّرۡصُوصٞ

Hakika Allah Mtukufu Anawapenda wale wanaopigana katika njia Yake wakiwa wamejipanga kana kwamba ni jengo lililopangika na kuimarika kwa namna ya kutoweza adui kupenya kwenye jengo hilo. Katika aya hii pana maelezo ya ubora wa jihadi na wenye kupigana jihadi, kwa kuwa Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kila upungufu, Anawapenda waja Wake Waumini wanapojipanga kupambana na maadui wa Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

5 : 61

وَإِذۡ قَالَ مُوسَىٰ لِقَوۡمِهِۦ يَٰقَوۡمِ لِمَ تُؤۡذُونَنِي وَقَد تَّعۡلَمُونَ أَنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡۖ فَلَمَّا زَاغُوٓاْ أَزَاغَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُمۡۚ وَٱللَّهُ لَا يَهۡدِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡفَٰسِقِينَ

Na kumbuka na uwakumbushe watu wako, (ewe Mtume), pindi aliposema Nabii wa Allah Mtukufu. Mûsã, amani imshukie, akiwaambia watu wake, «Kwa nini mnaniudhi kwa maneno na vitendo, na hali nyinyi mnajua kuwa mimi ni Mjumbe wa Allah Mtukufu kwenu?» Basi walipopotoka na kuwa kando na haki pamoja na kuwa wanaijua na wakaendelea juu ya hilo, Allah Mtukufu Aliziepusha nyoyo zao wasiukubali uongofu, ikiwa ni mateso kwao kwa sababu ya upotevu wao waliojichagulia wenyewe. Na Allah Mtukufu Hawaongozi watu wenye kutoka nje ya utiifu na njia ya haki. info
التفاسير: |
prev

As-Saff

next
:
0:00 0:00