Tradução dos significados do Nobre Al-Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis

Número de página:close

34 : 14

وَءَاتَىٰكُم مِّن كُلِّ مَا سَأَلۡتُمُوهُۚ وَإِن تَعُدُّواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ لَا تُحۡصُوهَآۗ إِنَّ ٱلۡإِنسَٰنَ لَظَلُومٞ كَفَّارٞ

Na Akawapa nyinyi kila mlichomuomba. Na mkihesabu ili kujua idadi ya neema za Allah Mtukufu juu yenu, hamtaweza kuzihesabu na kudhibiti idadi yake wala kusimama itakikanavyo kushukuru kwa hizo kwa wingi wake na aina zake. Hakika Binadamu ni mwingi wa kujidhulumu nafsi yake, ni mwingi wa kukanusha neema za Mola wake. info
التفاسير: |

35 : 14

وَإِذۡ قَالَ إِبۡرَٰهِيمُ رَبِّ ٱجۡعَلۡ هَٰذَا ٱلۡبَلَدَ ءَامِنٗا وَٱجۡنُبۡنِي وَبَنِيَّ أَن نَّعۡبُدَ ٱلۡأَصۡنَامَ

Na kumbuka, ewe Mtume, pindi Ibrãhîm aliposema akimuomba Mola Wake, baada ya kumfanyia makao mwanawe wa kiume, Ismã‘îl, pamoja na mamake, Hãjar, kwenye bonde la Makkah, «Ewe Mola ijaalie Makkah ni mji wa amani, awe kila aliye humo yuko kwenye amani, na uniepushe mimi na wanangu na kuabudu masanamu». info
التفاسير: |

36 : 14

رَبِّ إِنَّهُنَّ أَضۡلَلۡنَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلنَّاسِۖ فَمَن تَبِعَنِي فَإِنَّهُۥ مِنِّيۖ وَمَنۡ عَصَانِي فَإِنَّكَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Ewe Mola wangu! Masanamu yamesababisha kuwaepusha watu wengi na njia ya ukweli. Basi mwenye kunifuata mimi katika kumpwekesha Allah Mtukufu, yeye atakuwa kwenye Dini yangu na mwendo wangu, na mwenye kwenda kinyume na mimi, katika mambo ambayo si ya ushirikina, basi wewe ni Mwingi wa kusamehe dhambi za wenye kufanya madhambi, kwa fadhila zako, ni Mwingi wa huruma kwao, unamsamehe unayemtaka miongoni mwao. info
التفاسير: |

37 : 14

رَّبَّنَآ إِنِّيٓ أَسۡكَنتُ مِن ذُرِّيَّتِي بِوَادٍ غَيۡرِ ذِي زَرۡعٍ عِندَ بَيۡتِكَ ٱلۡمُحَرَّمِ رَبَّنَا لِيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ فَٱجۡعَلۡ أَفۡـِٔدَةٗ مِّنَ ٱلنَّاسِ تَهۡوِيٓ إِلَيۡهِمۡ وَٱرۡزُقۡهُم مِّنَ ٱلثَّمَرَٰتِ لَعَلَّهُمۡ يَشۡكُرُونَ

«Ewe Mola wetu! Mimi nimewafanya watoto wangu wakae kwenye bonde lisilo na mimea wala maji, penye ujirani na mji wako mtakatifu. Mola wetu! Mimi nimefanya hilo kwa amri Yako, ili wasimamishe Swala kwa namna yake itakikanayo, basi ifanye mioyo ya baadhi ya viumbe vyako ilemee kwao na ipendelee, na uwape riziki ya kila aina ya matunda wakiwa mahali hapa, ili wakushukuru kwa neema zako.» Allah Mtukufu Akakubali maombi yake. info
التفاسير: |

38 : 14

رَبَّنَآ إِنَّكَ تَعۡلَمُ مَا نُخۡفِي وَمَا نُعۡلِنُۗ وَمَا يَخۡفَىٰ عَلَى ٱللَّهِ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ

«Ewe Mola wetu! Hakika wewe unajua kila tunachokificha na tunachokionyesha. Na hakuna chochote chenye kupotea na kuwa nje ya ujuzi wa Allah Mtukufu miongoni mwa vilivyoko ardhini na mbinguni». info
التفاسير: |

39 : 14

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي وَهَبَ لِي عَلَى ٱلۡكِبَرِ إِسۡمَٰعِيلَ وَإِسۡحَٰقَۚ إِنَّ رَبِّي لَسَمِيعُ ٱلدُّعَآءِ

Ibrâhĩm anamsifu Mola wake na anasema, «Shukrani zote ni za Allah Mtukufu Aliyeniruzuku, pamoja na uzee wangu, wanangu wawili, Ismã‘îl na Isḥãq, baada ya maombi yangu kwani Mola wangu ni mwenye kusikia maombi ya mwenye kumuomba; na mimemuomba na Hakuyapitisha patupu matarajio yangu». info
التفاسير: |

40 : 14

رَبِّ ٱجۡعَلۡنِي مُقِيمَ ٱلصَّلَوٰةِ وَمِن ذُرِّيَّتِيۚ رَبَّنَا وَتَقَبَّلۡ دُعَآءِ

Ewe Mola wangu! Nijaalie ni mwenye kuendelea kutekeleza Swala kwa njia ya ukamilifu zaidi na ujaalie katika kizazi changu wenye kuendelea nayo. Ewe Mola wetu! Na uyakubali maombi yangu na uikubali ibada yangu. info
التفاسير: |

41 : 14

رَبَّنَا ٱغۡفِرۡ لِي وَلِوَٰلِدَيَّ وَلِلۡمُؤۡمِنِينَ يَوۡمَ يَقُومُ ٱلۡحِسَابُ

«Ewe Mola wetu! Nisamehe iwapo yametokea kutoka kwangu mambo ambayo binadamu hawasalimiki nayo, na uwasamehe wazazi wangu wawili (Hapa ni kabla haijamfunukia kwamba baba yake ni adui wa Allah Mtukufu) na uwasamehe Waumini wote Siku ambayo watu watasimama kuhesabiwa na kulipwa» info
التفاسير: |

42 : 14

وَلَا تَحۡسَبَنَّ ٱللَّهَ غَٰفِلًا عَمَّا يَعۡمَلُ ٱلظَّٰلِمُونَۚ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمۡ لِيَوۡمٖ تَشۡخَصُ فِيهِ ٱلۡأَبۡصَٰرُ

Na usidhani, ewe Mtume, kwamba Allah Mtukufu ni mwenye kughafilika na yale wanayoyafanya madhalimu, ya kukukanusha wewe na Mitume wengine na kuwakera Waumini na maasia mengineyo. Kwa kweli, anachelewesha kuwaadhibu mpaka Siku ngumu ambayo macho yao yatakodoka na hayatafumbika kwa kitisho cha yale yanayoyaona. Katika hii pana kumliwaza Mtume Muhammad, rehema na amani zimshukie. info
التفاسير: |
prev

Ibrahim

next
:
0:00 0:00