Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - Përmbajtja e përkthimeve

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Përkthimi i kuptimeve Surja: Suretu El Kamer   Ajeti:

Surat Qamar

ٱقۡتَرَبَتِ ٱلسَّاعَةُ وَٱنشَقَّ ٱلۡقَمَرُ
Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!
Kiyama kimekaribia na mwezi utapasuka hapana hivi wala hivi.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَإِن يَرَوۡاْ ءَايَةٗ يُعۡرِضُواْ وَيَقُولُواْ سِحۡرٞ مُّسۡتَمِرّٞ
Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.
Na makafiri wakiona Ishara, yaani muujiza mkubwa, wao hupuuza wakaacha kuuamini. Bali husema: Huu ni uchawi wa daima unaendelea!
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَكَذَّبُواْ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡۚ وَكُلُّ أَمۡرٖ مُّسۡتَقِرّٞ
Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.
Na wamewakanusha Mitume na wakafuata yaliyo zainishwa na matamanio yao. Na kila jambo huishia mwisho wake linapo tulia na kuthibiti.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ جَآءَهُم مِّنَ ٱلۡأَنۢبَآءِ مَا فِيهِ مُزۡدَجَرٌ
Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.
Na ninaapa kuwa zimewajia makafiri khabari za mataifa yaliyo tangulia zenye ukweli wa uumbaji ambazo zina mikemeo ya kutosha.
Tefsiret në gjuhën arabe:
حِكۡمَةُۢ بَٰلِغَةٞۖ فَمَا تُغۡنِ ٱلنُّذُرُ
Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!
Haya yaliyo wajia ni hikima kubwa na lengo la kufikia mbali. Lakini maonyo yataleta faida gani kwa wanao zipinga hikima hizo?
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَتَوَلَّ عَنۡهُمۡۘ يَوۡمَ يَدۡعُ ٱلدَّاعِ إِلَىٰ شَيۡءٖ نُّكُرٍ
Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha; .
Ewe Muhammad! Waachilie mbali hawa makafiri, nawe ngojea siku atapoita mwitaji wa Mwenyezi Mungu kuitia jambo ambalo nafsi inalichukia mno!
Tefsiret në gjuhën arabe:
خُشَّعًا أَبۡصَٰرُهُمۡ يَخۡرُجُونَ مِنَ ٱلۡأَجۡدَاثِ كَأَنَّهُمۡ جَرَادٞ مُّنتَشِرٞ
Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika!
Macho yao yatainamia chini kwa wingi wa kitisho, wakitoka makaburini kama kwamba ni nzige walio tawanyika, kwa wingi wao na mbio zao.
Tefsiret në gjuhën arabe:
مُّهۡطِعِينَ إِلَى ٱلدَّاعِۖ يَقُولُ ٱلۡكَٰفِرُونَ هَٰذَا يَوۡمٌ عَسِرٞ
Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.
Wakimkimbilia huyo mwitaji, wakimtazama kwa unyonge na unyenekevu, macho yao yanamwangalia yeye tu. Makafiri watasema Siku ya Kiyama: Hii leo ni siku nzito, siku ya shida!
Tefsiret në gjuhën arabe:
۞ كَذَّبَتۡ قَبۡلَهُمۡ قَوۡمُ نُوحٖ فَكَذَّبُواْ عَبۡدَنَا وَقَالُواْ مَجۡنُونٞ وَٱزۡدُجِرَ
Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.
Kabla ya makafiri wa Makka walikwisha kanusha kaumu ya Nuhu. Walimkadhibisha Nuhu, mja wetu na Mtume wetu, wakamsingizia kuwa ana wazimu. Wakaingiza baina yake na kufikisha kwake Ujumbe kila namna ya maudhi na vitisho.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَدَعَا رَبَّهُۥٓ أَنِّي مَغۡلُوبٞ فَٱنتَصِرۡ
Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!
Nuhu akamwomba Mola wake Mlezi akisema: Hakika mimi nimeshindwa na hawa watu wangu, basi wapatilize hawa kwa ajili yangu!
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَفَتَحۡنَآ أَبۡوَٰبَ ٱلسَّمَآءِ بِمَآءٖ مُّنۡهَمِرٖ
Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.
Basi tukaifungua milango ya mbingu ikamimina maji yasiyo katika;
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَفَجَّرۡنَا ٱلۡأَرۡضَ عُيُونٗا فَٱلۡتَقَى ٱلۡمَآءُ عَلَىٰٓ أَمۡرٖ قَدۡ قُدِرَ
Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.
Na tukaipasua ardhi kwa chemchem zikitibuka maji. Yakakutana maji ya mbinguni na maji ya ardhi kuwahiliki, kama alivyo kadiria Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَحَمَلۡنَٰهُ عَلَىٰ ذَاتِ أَلۡوَٰحٖ وَدُسُرٖ
Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.
Tukampakia Nuhu katika jahazi la mbao zinazo fungwa pamoja kwa kamba, kama mtepe.
Tefsiret në gjuhën arabe:
تَجۡرِي بِأَعۡيُنِنَا جَزَآءٗ لِّمَن كَانَ كُفِرَ
Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.
Likawa linakwenda baharini chini ya hifadhi yetu, kuwa ni malipo kwa Nuhu ambaye watu wake waliendelea kuukanya wito wake.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَد تَّرَكۡنَٰهَآ ءَايَةٗ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?
Na tumeliacha hilo tukio na kuzamishwa makafiri na kuokolewa Waumini liwe ni mawaidha, lakini yupo mwenye kuwaidhika?
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.
Jee, vipi ilikuwa adhabu yangu na onyo langu kwa wakhalifu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?
Ninaapa, tumeifanya Qur'ani iwe sahali kukumbukwa na kutoa mawaidha. Lakini je, yupo wa kuwaidhika?
Tefsiret në gjuhën arabe:
كَذَّبَتۡ عَادٞ فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Kina A'di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
Kina A'di walimkadhibisha Mtume wao Hudi. Je, hali gani adhabu yangu na onyo langu lilikuwa kwa wendao kinyume!
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ رِيحٗا صَرۡصَرٗا فِي يَوۡمِ نَحۡسٖ مُّسۡتَمِرّٖ
Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,
Sisi kwa yakini tuliwapatiliza kwa upepo ubaridi unao vuma, katika siku ya ukorofi wa daima,
Tefsiret në gjuhën arabe:
تَنزِعُ ٱلنَّاسَ كَأَنَّهُمۡ أَعۡجَازُ نَخۡلٖ مُّنقَعِرٖ
Ukiwang'oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng'olewa.
Ukiwang'oa watu na kuwatupa nao wamekufa, kama vinavyo ng'olewa vigogo vya mitende na mizizi yake.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?
Hali gani adhabu yangu na onyo langu lilikuwa kwa walio kwenda kinyume!
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani nyepesi kufahamika; lakini yupo anaye kumbuka?
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya sahali Qur'ani kwa ajili ya mawaidha na mazingatio, basi je, yupo wa kuwaidhika?
Tefsiret në gjuhën arabe:
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ بِٱلنُّذُرِ
Thamudi waliwakanusha Waonyaji.
Thamudi walikadhibisha maonyo ya Nabii wao, Saleh.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَقَالُوٓاْ أَبَشَرٗا مِّنَّا وَٰحِدٗا نَّتَّبِعُهُۥٓ إِنَّآ إِذٗا لَّفِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٍ
Wakasema: Ati tumfuate binaadamu mmoja katika sisi? Basi hivyo sisi tutakuwa katika upotofu na kichaa!
Wakasema: Hivyo aje mtu tu katika sisi, watu wa kawaida, asiye na watu, nasi tumfuate? Tukimfuata huyo basi bila ya shaka sisi tutakuwa mbali mno na haki, na tutakuwa tuna wazimu basi.
Tefsiret në gjuhën arabe:
أَءُلۡقِيَ ٱلذِّكۡرُ عَلَيۡهِ مِنۢ بَيۡنِنَا بَلۡ هُوَ كَذَّابٌ أَشِرٞ
Ni yeye tu aliye teremshiwa huo ukumbusho kati yetu sote? Bali huyu ni mwongo mwenye kiburi!
Uteremshiwe wahyi kwake yeye katika sisi na hali wapo wanao stahiki zaidi? Bali huyo kazikdi katika uwongo, mwenye kukanya neema.
Tefsiret në gjuhën arabe:
سَيَعۡلَمُونَ غَدٗا مَّنِ ٱلۡكَذَّابُ ٱلۡأَشِرُ
Kesho watajua ni nani huyo mwongo mwenye kiburi.
Karibu watakuja jua siku itapo wateremkia adhabu ni nani mwongo anaye ikanya neema. Wao au Saleh, Mtume wao?
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّا مُرۡسِلُواْ ٱلنَّاقَةِ فِتۡنَةٗ لَّهُمۡ فَٱرۡتَقِبۡهُمۡ وَٱصۡطَبِرۡ
Hakika Sisi tutawapelekea ngamia jike ili kuwajaribu, basi watazame tu na ustahamili.
Hakika Sisi tunampelekea Mtume wetu Saleh ngamia mke, awe ni mtihani wao. Basi wangojee, na uwatazame watafanya nini. Na subiri, uvumilie maudhi yao mpaka itapo kuja amri ya Mwenyezi Mungu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَنَبِّئۡهُمۡ أَنَّ ٱلۡمَآءَ قِسۡمَةُۢ بَيۡنَهُمۡۖ كُلُّ شِرۡبٖ مُّحۡتَضَرٞ
Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao; kila sehemu ya maji itahudhuriwa na aliye khusika.
Na waambie kwamba maji yatagawanywa baina yao na ngamia. Kila mmoja wao atakuwa na zamu yake aje kunywa katika siku yake.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَنَادَوۡاْ صَاحِبَهُمۡ فَتَعَاطَىٰ فَعَقَرَ
Basi wakamwita mtu wao akaja akamchinja.
Wakamwita mtu wao mmoja akapania kumchinja yule ngamia, akamchinja.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَكَيۡفَ كَانَ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu!
Basi vipi ilikuwa adhabu yangu na onyo langu kwa hao wakhalifu walio kwenda kinyume na amri.
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ صَيۡحَةٗ وَٰحِدَةٗ فَكَانُواْ كَهَشِيمِ ٱلۡمُحۡتَظِرِ
Hakika Sisi tuliwapelekea ukelele mmoja tu, wakawa kama mabuwa ya kujengea uwa.
Sisi tuliwapatiliza kwa ukelele mmoja tu, wakawa kama miti mikavu anayo ikusanya yeyote atakaye kujengea boma la uwa wake.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur'ani iwe nyepesi kwa kukumbuka, lakini yupo akumbukaye?
Na bila ya shaka Sisi tumeisahilisha Qur'ani iwe nyepesi kwa ajili ya mawaidha na kuzingatia. Lakini je, yupo wa kuwaidhika?
Tefsiret në gjuhën arabe:
كَذَّبَتۡ قَوۡمُ لُوطِۭ بِٱلنُّذُرِ
Kaumu Lut'i nao waliwakadhibisha Waonyaji.
Kaumu Lut'i nao walikadhibisha maonyo ya Mtume wao.
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّآ أَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ حَاصِبًا إِلَّآ ءَالَ لُوطٖۖ نَّجَّيۡنَٰهُم بِسَحَرٖ
Hakika Sisi tukawapelekea kimbunga cha vijiwe, isipo kuwa wafuasi wa Lut'i. Hao tuliwaokoa karibu na alfajiri.
Hakika Sisi tuliwapelekea upepo mkali wa kuwatupia changarawe. Isipo kuwa watu wa Lut'i walio amini. Hao tuliwaokoa na adhabu hii mwisho wa usiku.
Tefsiret në gjuhën arabe:
نِّعۡمَةٗ مِّنۡ عِندِنَاۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَن شَكَرَ
Kwa neema inayo toka kwetu. Hivyo ndivyo tumlipavyo anaye shukuru.
Kwa kuwapa neema iliyo toka kwetu. Neema kama hizo kubwa kubwa ndivyo tunavyo walipa wenye kuishukuru neema yetu kwa imani yao na ut'iifu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ أَنذَرَهُم بَطۡشَتَنَا فَتَمَارَوۡاْ بِٱلنُّذُرِ
Na hakika yeye aliwaonya adhabu yetu; lakini wao waliyatilia shaka hayo maonyo.
Na hakika Lut'i aliwahadharisha watu wake vipi mshiko wetu ulivyo mkali, wakatilia shaka maonyo yake kwa kuwa wanamwona mwongo.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ رَٰوَدُوهُ عَن ضَيۡفِهِۦ فَطَمَسۡنَآ أَعۡيُنَهُمۡ فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ
Na walimtaka awape wageni wake. Tukayapofua macho yao, na tukawaambia: Onjeni basi adhabu na maonyo yangu!
Wakamtaka awape wageni wake wawatende fiili yao, tukayafuta macho yao kuwa ni malipo kwa hilo walilo litaka. Basi waambie kwa kuwakejeli: Igugumieni adhabu yangu, na maonyo yangu!
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ صَبَّحَهُم بُكۡرَةً عَذَابٞ مُّسۡتَقِرّٞ
Na iliwafikia wakati wa asubuhi adhabu yangu ya kuendelea.
Na asubuhi mapema ikawashitua adhabu ya kuthibiti milele.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَذُوقُواْ عَذَابِي وَنُذُرِ
Basi onjeni adhabu na maonyo yangu!<
Wakaambiwa: Igugumieni adhabu yangu na maonyo yangu!
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ يَسَّرۡنَا ٱلۡقُرۡءَانَ لِلذِّكۡرِ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na hakika tumeisahilisha Qur'ani kuikumbuka. Lakini yupo anaye kumbuka?
Na hakika tumeifanya Qur'ani ni sahali kwa ajili ya mawaidha na mazingatio. Je! Yupo anaye waidhika?
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ جَآءَ ءَالَ فِرۡعَوۡنَ ٱلنُّذُرُ
Na Waonyaji waliwafikia watu wa Firauni.
Na watu wa Firauni yaliwajia maonyo ya mfululizo.
Tefsiret në gjuhën arabe:
كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كُلِّهَا فَأَخَذۡنَٰهُمۡ أَخۡذَ عَزِيزٖ مُّقۡتَدِرٍ
Walizikadhibisha Ishara zetu zote, nasi tukawashika kama anavyo shika Mwenye nguvu Mwenye uweza.
Walikadhibisha Ishara zetu na miujiza yetu waliyo kuja nayo Mitume wetu. Tukawaangamiza kwa maangamizo ya nguvu yasiyo shindika, ya uwezo mkubwa.
Tefsiret në gjuhën arabe:
أَكُفَّارُكُمۡ خَيۡرٞ مِّنۡ أُوْلَٰٓئِكُمۡ أَمۡ لَكُم بَرَآءَةٞ فِي ٱلزُّبُرِ
Je! Makafiri wenu ni bora kuliko hao, au yameandikwa vitabuni kuwa nyinyi hamtiwi makosani?
Ati nyinyi, makafiri, mna nguvu zaidi kuliko hao wa kaumu zilizo tangulia ambao wameangamizwa? Au nyinyi mmetolewa makosani kwa ilivyo teremka katika Vitabu vya mbinguni?
Tefsiret në gjuhën arabe:
أَمۡ يَقُولُونَ نَحۡنُ جَمِيعٞ مُّنتَصِرٞ
Au ndio wanasema: Sisi ni wengi tutashinda tu.
Bali ati wanasema hawa makafiri: Sisi ni kikundi kilicho ungana chenye nguvu juu ya maadui wake, hakishindwi.
Tefsiret në gjuhën arabe:
سَيُهۡزَمُ ٱلۡجَمۡعُ وَيُوَلُّونَ ٱلدُّبُرَ
Wingi wao huu utashindwa, na wao watasukumwa nyuma.
Kikundi hicho kitashindwa, na watakimbia mbio wakifurushwa.
Tefsiret në gjuhën arabe:
بَلِ ٱلسَّاعَةُ مَوۡعِدُهُمۡ وَٱلسَّاعَةُ أَدۡهَىٰ وَأَمَرُّ
Bali Saa ya Kiyama ndio miadi yao, na Saa hiyo ni nzito zaidi na chungu zaidi.
Bali Kiyama ndio miadi ya adhabu yao. Na Kiyama ni kizito zaidi, na kichungu zaidi.
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّ ٱلۡمُجۡرِمِينَ فِي ضَلَٰلٖ وَسُعُرٖ
Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu.
Hakika wakosefu kutokana na hawa na hao watakuwa katika hilaki na Jahannamu inayo waka moto.
Tefsiret në gjuhën arabe:
يَوۡمَ يُسۡحَبُونَ فِي ٱلنَّارِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمۡ ذُوقُواْ مَسَّ سَقَرَ
Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!
Siku watapo bururwa kifudifudi katika Moto wakiambiwa: Hilikini kwa machungu ya Jahannamu na joto lake!
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّا كُلَّ شَيۡءٍ خَلَقۡنَٰهُ بِقَدَرٖ
Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo.
Hakika Sisi tumeumba kila kitu. Tumeviumba kwa kukadiria inavyo hitajia hikima.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَمَآ أَمۡرُنَآ إِلَّا وَٰحِدَةٞ كَلَمۡحِۭ بِٱلۡبَصَرِ
Na amri yetu haikuwa ila ni moja tu, kama kupepesa jicho.
Na haikuwa amri yetu tukitaka kitu ila neno moja tu, nalo ni kusema: "Kuwa", nacho huwa, papo hapo kama kupepesa kwa jicho.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَآ أَشۡيَاعَكُمۡ فَهَلۡ مِن مُّدَّكِرٖ
Na bila ya shaka tumekwisha waangamiza wenzenu. Lakini yupo anaye kumbuka?
Na bila ya shaka Sisi tumekwisha waangamiza wengine walio fanana nanyi katika ukafiri. Je! Yupo aliye waidihika?
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَكُلُّ شَيۡءٖ فَعَلُوهُ فِي ٱلزُّبُرِ
Na kila jambo walilo lifanya limo vitabuni.
Na kila kitu walicho kifanya duniani kimeandikwa katika madaftari, kimeambatishwa nao.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَكُلُّ صَغِيرٖ وَكَبِيرٖ مُّسۡتَطَرٌ
Na kila kidogo na kikubwa kimeandikwa.
Na kila dogo na kubwa katika vitendo limeandikwa. Hakipotei kitu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّ ٱلۡمُتَّقِينَ فِي جَنَّٰتٖ وَنَهَرٖ
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na mito.
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani yenye shani kuu, na mito ya namna mbali mbali.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فِي مَقۡعَدِ صِدۡقٍ عِندَ مَلِيكٖ مُّقۡتَدِرِۭ
Katika makalio ya haki kwa Mfalme Mwenye uweza.
Katika baraza ya Haki, hakuna porojo huko wala madhambi, kwa Mwenyewe Mfalme Mtukufu wa uweza
Tefsiret në gjuhën arabe:
 
Përkthimi i kuptimeve Surja: Suretu El Kamer
Përmbajtja e sureve Numri i faqes
 
Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - Përmbajtja e përkthimeve

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

Mbyll