prev

Al-Qari'ah

next

1 : 101

ٱلۡقَارِعَةُ

Kiyama chenye kugonga nyoyo za watu kwa vitisho vyake. info
التفاسير: |

2 : 101

مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Ni kitu gani hicho chenye kugonga? info
التفاسير: |

3 : 101

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡقَارِعَةُ

Na ni kipi kilichokujulisha ni kipi hicho chenye kugonga? info
التفاسير: |

4 : 101

يَوۡمَ يَكُونُ ٱلنَّاسُ كَٱلۡفَرَاشِ ٱلۡمَبۡثُوثِ

Siku hiyo watu watakuwa, kwa wingi wao, kugawanyika kwao na kuzunguka kwao, ni kama panzi walioenea. Nao ni wale wanaojitupa motoni. info
التفاسير: |

5 : 101

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ ٱلۡمَنفُوشِ

Na majabali yatakuwa ni kama pamba yenye rangi tofauti inayochambuliwa kwa mkono ikawa kama vumbi jembamba na ikamalizika. info
التفاسير: |

6 : 101

فَأَمَّا مَن ثَقُلَتۡ مَوَٰزِينُهُۥ

Basi mwenye kuwa mizani za mema yake ni nzito, zikashinda mabaya yake. info
التفاسير: |

7 : 101

فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ

Atakua kwenye maisha ya kuridhika Peponi. info
التفاسير: |

8 : 101

وَأَمَّا مَنۡ خَفَّتۡ مَوَٰزِينُهُۥ

Ama mwenye kuwa mizani za mema yake ni nyepesi na mizani za maovu yake ni nzito. info
التفاسير: |

9 : 101

فَأُمُّهُۥ هَاوِيَةٞ

Makazi yake yatakuwa ni Moto wa Jahanamu. info
التفاسير: |

10 : 101

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا هِيَهۡ

Ni kipi kilichokujulisha, (ewe Mtume), ni ipi hii Jahanamu inayoitwa «Hāwiyah»? info
التفاسير: |

11 : 101

نَارٌ حَامِيَةُۢ

Ni Moto unaowaka sana kutokana na vinavyochomwa ndani yake. info
التفاسير: |
prev

Al-Qari'ah

next
:
0:00 0:00