prev

Al-Qasas

next

1 : 28

طسٓمٓ

Ṭā, Sīn, Mīm. (Yametangulia maelezo kuhusu herufi ziliokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al- Baqarah). info
التفاسير: |

2 : 28

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Hizi ni aya za Qur’ani niliyokuteremshia, ewe Mtume, yenye kufafanua kila kile ambacho waja wanakihitajia katika ulimwengu wao na Akhera yao. info
التفاسير: |

3 : 28

نَتۡلُواْ عَلَيۡكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرۡعَوۡنَ بِٱلۡحَقِّ لِقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ

Tunakusimulia wewe habari ya Mûsã na Firáwn kwa ukweli (ili wazingatie wale) watu wanaoiamini hii Qur’ani na wakubali kwamba inatoka kwa Allah Mtukufu na wafanye matendo yanayoambatana na uongofu wake. info
التفاسير: |

4 : 28

إِنَّ فِرۡعَوۡنَ عَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَجَعَلَ أَهۡلَهَا شِيَعٗا يَسۡتَضۡعِفُ طَآئِفَةٗ مِّنۡهُمۡ يُذَبِّحُ أَبۡنَآءَهُمۡ وَيَسۡتَحۡيِۦ نِسَآءَهُمۡۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلۡمُفۡسِدِينَ

Hakika Firáwn alifanya kiburi na akapita mipaka katika nchi, akawafanya watu wake kuwa ni makundi tafauti tafauti, akawa analinyongesha kundi moja ya hayo, nalo ni lile la Wana wa Isrãîl, akawa anawaua watoto wao wa kiume na anawabakisha wanawake wao kwa kutumika na kudharauliwa, Hakika yeye alikuwa ni miongoni mwa waharibifu katika ardhi. info
التفاسير: |

5 : 28

وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَنَجۡعَلَهُمۡ أَئِمَّةٗ وَنَجۡعَلَهُمُ ٱلۡوَٰرِثِينَ

Na tunataka kuwaneemesha wale ambao Firáwn aliwafanya wanyonge nchini, tuwafanye ni viongozi katika wema na ni wenye kuulingania, na tuwafanye wao wairithi nchi baada ya kuangamia Firáwn na watu wake. info
التفاسير: |
prev

Al-Qasas

next
:
0:00 0:00