prev

Fussilat

next

1 : 41

حمٓ

«Ḥā, Mīm» Yameshatangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa mwanzo wa sura ya Al- Baqarah. info
التفاسير: |

2 : 41

تَنزِيلٞ مِّنَ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلرَّحِيمِ

Hii Qur’ani ni Teremsho linalotoka kwa Allah Mtukufu Mwenye kueneza rehema Zake kwa wema na waovu ulimwenguni, Mwenye kuhusisha rehema Zake kwa wema watupu kesho Akhera. Amemteremshia Nabii Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). info
التفاسير: |

3 : 41

كِتَٰبٞ فُصِّلَتۡ ءَايَٰتُهُۥ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا لِّقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Ni Kitabu kilichobainishwa aya zake ubainifu uliotimia, na ikafafanuliwa maana yake na hukumu zake, ikiwa ni Qur’ani ya Kiarabu iliyofanywa nyepesi kuielewa kwa watu wanaoijua lugha ya Kiarabu. info
التفاسير: |

4 : 41

بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا فَأَعۡرَضَ أَكۡثَرُهُمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ

Hali ya kuwa ni yenye kubashiri malipo ya haraka na ya baadaye kwa anayeiamini na akafanya matendo yanayolingana nayo, na ni yenye kuonya adhabu ya haraka na ya badaye kwa anayeikanusha. Hivyo basi wengi wa watu waliipa mgongo wakawa hawaisikii kusikia kwa kukubali na kuitikia. info
التفاسير: |

5 : 41

وَقَالُواْ قُلُوبُنَا فِيٓ أَكِنَّةٖ مِّمَّا تَدۡعُونَآ إِلَيۡهِ وَفِيٓ ءَاذَانِنَا وَقۡرٞ وَمِنۢ بَيۡنِنَا وَبَيۡنِكَ حِجَابٞ فَٱعۡمَلۡ إِنَّنَا عَٰمِلُونَ

Na wamesema hawa wenye kukataa na kumkanusha (Nabii Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), «Nyoyo zetu zina vifuniko vyenye kutuzuiya kuelewa unayotuambia, na masikio yetu yana uziwi hatusikii, na baina yetu sisi na wewe, (ewe Muhammad), pana pazia linalotuzuia kuitika mwito wako. Basi fanya matendo kulingana na dini yako, kama ambavyo sisi tunavyofanya kulingana na dini yetu». info
التفاسير: |

6 : 41

قُلۡ إِنَّمَآ أَنَا۠ بَشَرٞ مِّثۡلُكُمۡ يُوحَىٰٓ إِلَيَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَٱسۡتَقِيمُوٓاْ إِلَيۡهِ وَٱسۡتَغۡفِرُوهُۗ وَوَيۡلٞ لِّلۡمُشۡرِكِينَ

Waambie, (ewe Mtume), «Hakika yangu mimi ni binadamu kama nyinyi, Allah Mtukufu Ananiletea wahyi kwamba Mola wenu Anayestahiki kuabudiwa ni Mola Mmoja Asiyekuwa na mshirika. Basi fuateni njia yenye kufikisha Kwake na mtake msamaha Wake.» Maangamivu na mateso yatawapata washirikina walioabudu masanamu, yasiyonufaisha wala kudhuru, badala ya kumuabudu Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

7 : 41

ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَهُم بِٱلۡأٓخِرَةِ هُمۡ كَٰفِرُونَ

Wale wasiojisafisha nafsi zao kwa kumpwekesha Mola wao na kumtakasa, na wasiotoa Zaka kuwapa wanaostahiki, basi hao hawamtakasii Muumba wala hawanufaishi viumbe; na wao hawaamini Ufufuzi wala Pepo na Moto. info
التفاسير: |

8 : 41

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونٖ

Hakika ya wale wanaomuamini Allah Mtukufu, Mtume Wake na Kitabu Chake na wakafanya matendo mema, hali ya kumtakasia Allah Mtukufu katika matendo hayo, watapata malipo makubwa yasiyokatika wala kuzuiliwa. info
التفاسير: |

9 : 41

۞ قُلۡ أَئِنَّكُمۡ لَتَكۡفُرُونَ بِٱلَّذِي خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ فِي يَوۡمَيۡنِ وَتَجۡعَلُونَ لَهُۥٓ أَندَادٗاۚ ذَٰلِكَ رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Sema, (ewe Mtume), uwaambie washirikina kwa kuwakaripia na kulionea ajabu tendo lao, hivi nyinyi mnamkanusha Allah Mtukufu Aliyeumba ardhi kwa siku mbili, mnamfanya kuwa Ana washirika na wanaofanana Naye mkawa mnawaabudu pamoja Naye? Muumbaji Huyo Ndiye Mola wa viumbe wote. info
التفاسير: |

10 : 41

وَجَعَلَ فِيهَا رَوَٰسِيَ مِن فَوۡقِهَا وَبَٰرَكَ فِيهَا وَقَدَّرَ فِيهَآ أَقۡوَٰتَهَا فِيٓ أَرۡبَعَةِ أَيَّامٖ سَوَآءٗ لِّلسَّآئِلِينَ

Na Akajaalia (Mwenye kutakasika) katika ardhi majabali yaliyojikita juu yake, Akaibariki kwa kuifanya iwe na kheri nyingi kwa watu wake, Akakadiria humo riziki za chakula kwa watu wake na yale yanayowafaa maishani kwa kipindi cha Siku nne: Siku mbili Aliumba ndani yake ardhi na Siku mbili Aliweka katika ardhi majabali yaliyojikita na Akakadiria katika Siku mbili hizo riziki zake zikiwa sawa kwa wenye kuuliza, yaani kwa mwenye kutaka kuliuliza hilo apate kulijua. info
التفاسير: |

11 : 41

ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰٓ إِلَى ٱلسَّمَآءِ وَهِيَ دُخَانٞ فَقَالَ لَهَا وَلِلۡأَرۡضِ ٱئۡتِيَا طَوۡعًا أَوۡ كَرۡهٗا قَالَتَآ أَتَيۡنَا طَآئِعِينَ

Kisha akaikusudia mbingu «akawa juu ya arshi yake», na ilikuwa moshi hapo kabla «yani mbingu», Akasema kuiambia mbingu na ardhi, «Fuateni amri yangu kwa hiari au kwa nguvu!» Nazo zikasema, «Tumekuja tukiwa watiifu kwako. Hatuna matakwa kinyume cha matakwa yako». info
التفاسير: |
prev

Fussilat

next
:
0:00 0:00