prev

Ad-Dukhan

next

1 : 44

حمٓ

Hā, Mĩm” Yametangulia maelezo kuhusu herufu zilizokatwa na kutengwa mwazo wa sura ya Al- Baqarah. info
التفاسير: |

2 : 44

وَٱلۡكِتَٰبِ ٱلۡمُبِينِ

Ameapa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwa Qur’ani iliyo wazi kimatamshi na kimaana. info
التفاسير: |

3 : 44

إِنَّآ أَنزَلۡنَٰهُ فِي لَيۡلَةٖ مُّبَٰرَكَةٍۚ إِنَّا كُنَّا مُنذِرِينَ

Hakika tuliiteremsha katika Usiku wa Cheo uliobarikiwa wenye kheri nyingi, nao unapatikana katika mwezi wa Ramadhani. Sisi ni wenye kuonya watu kwa kile kinachowanufaisha na kuwadhuru, nako ni kule kupeleka Mitume na kuteremsha Vitabu, ili hoja ya Allah Mtukufu iwasimamie waja Wake. info
التفاسير: |

4 : 44

فِيهَا يُفۡرَقُ كُلُّ أَمۡرٍ حَكِيمٍ

Katika usiku huo linaamuliwa na kupambanuliwa, kutoka kwenye Ubao Uliohifadhiwa na kuletewa waandishi kati ya Malaika, kila jambo lililokadiriwa la muda wa kuishi na riziki katika mwaka huo, na mambo mengine yatakayokuwa, na kukadiriwa na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, mpaka mwisho wa mwaka, hayabadilishwi wala hayageuzwi. info
التفاسير: |

5 : 44

أَمۡرٗا مِّنۡ عِندِنَآۚ إِنَّا كُنَّا مُرۡسِلِينَ

Mambo haya yaliyopangwa kimadhubuti ni amri inayotoka kwetu, kwani yote yanayokuwa na Anayokadiria Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na wahyi Anaouleta, vyote hivyo vinatokana na amri Yake na idhini Yake na ujuzi Wake. Hakika sisi tumetuma Mitume, Muhammad na waliokuwa kabla yake, kwa watu. info
التفاسير: |

6 : 44

رَحۡمَةٗ مِّن رَّبِّكَۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ

Hilo likiwa ni rehema kutoka kwa Mola wako, ewe Mtume, kuwafikia wale wenye kutumiwa. Hakika Yeye ni Msikizi, Anasikia sauti zote, ni Mjuzi wa mambo yote ya waja Wake yaliyojitokeza nje na yanayofichika. info
التفاسير: |

7 : 44

رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ

Muumba mbingu na ardhi na vitu vyote vilivyoko baina ya hivyo viwili. Iwapo nyinyi mna yakini na hilo, basi jueni kuwa Mola wa viumbe Ndiye Mola wa kweli, info
التفاسير: |

8 : 44

لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ

hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Peke Yake, Asiye na mshirika, Anayehuisha na kufisha, Mola wenu na Mola wa baba zenu wa mwanzo, basi muabuduni Yeye, na sio waungu wenu ambao hawawezi kudhuru wala kunufaisha. info
التفاسير: |

9 : 44

بَلۡ هُمۡ فِي شَكّٖ يَلۡعَبُونَ

Bali hawa washirikina wanaifanyia shaka haki; wao wanastarehe na kucheza na hawaiamini. info
التفاسير: |

10 : 44

فَٱرۡتَقِبۡ يَوۡمَ تَأۡتِي ٱلسَّمَآءُ بِدُخَانٖ مُّبِينٖ

Basi ngojea, ewe Mtume, uwaone hawa washirikina siku ambayo mbingu itakuja na moshi wa wazi info
التفاسير: |

11 : 44

يَغۡشَى ٱلنَّاسَۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٞ

Utakaowafunika watu, na hapo waambiwe, «Hii ni adhabu yenye uchungu na yenye kuumiza». info
التفاسير: |

12 : 44

رَّبَّنَا ٱكۡشِفۡ عَنَّا ٱلۡعَذَابَ إِنَّا مُؤۡمِنُونَ

Kisha waseme wakiomba iondolewe na iepushwe nao, Mola wetu! Tuepushie adhabu, kwani ukituepushia sisi ni wenye kukuamini.” (Na hilo lilifanyika na hawakuamini kama walivyoahidi). info
التفاسير: |

13 : 44

أَنَّىٰ لَهُمُ ٱلذِّكۡرَىٰ وَقَدۡ جَآءَهُمۡ رَسُولٞ مُّبِينٞ

Vipi watakuwa ni wenye kukumbuka na kuwaidhika baada ya kuteremkiwa na adhabu, na hali wamejiwa na Mtume mwenye kufafanua, naye ni Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). info
التفاسير: |

14 : 44

ثُمَّ تَوَلَّوۡاْ عَنۡهُ وَقَالُواْ مُعَلَّمٞ مَّجۡنُونٌ

kisha wakaenda kinyume naye na wakasema kwamba alifundishwa na binadamu au makuhani au mashetani, na kwamba yeye ni mwendawazimu na si Mtume? info
التفاسير: |

15 : 44

إِنَّا كَاشِفُواْ ٱلۡعَذَابِ قَلِيلًاۚ إِنَّكُمۡ عَآئِدُونَ

Hakika tutawaondolea nyinyi adhabu kidogo, kisha mtaona mnavyorudia yale ambayo mlikuwa mkiyafanya ya ukafiri, upotevu na ukanushaji, na kwa hakika sisi tutawaadhibu kwa hayo. info
التفاسير: |

16 : 44

يَوۡمَ نَبۡطِشُ ٱلۡبَطۡشَةَ ٱلۡكُبۡرَىٰٓ إِنَّا مُنتَقِمُونَ

Siku tutakayowaadhibu makafiri wote adhabu kubwa kabisa Siku ya Kiyama, nayo ni Siku ya kuwatesa kwa kulipiza. info
التفاسير: |

17 : 44

۞ وَلَقَدۡ فَتَنَّا قَبۡلَهُمۡ قَوۡمَ فِرۡعَوۡنَ وَجَآءَهُمۡ رَسُولٞ كَرِيمٌ

Hakika tushawafanyia mtihani na kuwajaribu watu wa Fir’awn kabla ya hawa washirikina, na aliwajia Mtume mtukufu, naye ni Mûsã, amani imshukie, wakamkanusha na wakaangamia. Basi hivi ndivyo tutakavyowafanya maadui zako, ewe Mtume, wasipoamini. info
التفاسير: |

18 : 44

أَنۡ أَدُّوٓاْ إِلَيَّ عِبَادَ ٱللَّهِۖ إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ

Na Mûsã aliwaambia, «Nipeni waja wa Allah Mtukufu kati ya Wana wa Isrãîl, na waachieni pamoja nami, wapate kumuabudu Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Mimi, kwenu nyinyi, ni mjumbe muaminifu katika wahyi Wake na ujumbe Wake». info
التفاسير: |
prev

Ad-Dukhan

next
:
0:00 0:00