prev

Al-Jathiyah

next

1 : 45

حمٓ

Hā, mīm Yametangulia maelezo kuhusu herufi zilizokatwa na kutengwa katika mwanzo wa sura ya Al-Baqarah. info
التفاسير: |

2 : 45

تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ

Hii Qur’ani imeteremshwa kutoka kwa Allah Mtukufu, Aliye Mshindi katika kuwatesa maadui Zake, Mwingi wa hekima katika uendeshaji wa mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير: |

3 : 45

إِنَّ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ

Hakika kwenye mbingu saba na ardhi ambapo humo viumbe vinatoka, na vilivyomo baina ya hivyo viwili miongoni mwa viumbe wa jinsi tofauti na aina mbalimbali, kuna dalili na hoja kwa wenye kuziamini. info
التفاسير: |

4 : 45

وَفِي خَلۡقِكُمۡ وَمَا يَبُثُّ مِن دَآبَّةٍ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يُوقِنُونَ

Na katika kuwaumba nyinyi, enyi watu, na uumbaji wa vilivyotapakaa ardhini miongoni mwa vinavyotambaa juu yake, kuna hoja na dalili kwa watu wenye imani ya yakini juu ya Allah Mtukufu na Sheria Yake. info
التفاسير: |

5 : 45

وَٱخۡتِلَٰفِ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ وَمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مِن رِّزۡقٖ فَأَحۡيَا بِهِ ٱلۡأَرۡضَ بَعۡدَ مَوۡتِهَا وَتَصۡرِيفِ ٱلرِّيَٰحِ ءَايَٰتٞ لِّقَوۡمٖ يَعۡقِلُونَ

Na katika kupishana usiku na mchana na kufuatana, na katika kuwaletea mvua anayoiteremsha Allah Mtukufu kutoka mawinguni, Akaihuisha kwayo ardhi baada ukavu wake, ikasheheni mimea na mazao, na katika kuwaletea upepo kutoka sehemu zote, na kuufanya uwe kwa maslahi yenu, kuna dalili na hoja kwa watu wanaoelewa kuhusu Allah Mtukufu, hoja Zake na dalili Zake. info
التفاسير: |

6 : 45

تِلۡكَ ءَايَٰتُ ٱللَّهِ نَتۡلُوهَا عَلَيۡكَ بِٱلۡحَقِّۖ فَبِأَيِّ حَدِيثِۭ بَعۡدَ ٱللَّهِ وَءَايَٰتِهِۦ يُؤۡمِنُونَ

Aya hizi na hoja hizi tunakusomea wewe, Mtume, kwa haki. Basi ni mazungumzo gani baada ya Allah Mtukufu na dalili Zake kuwa Yeye Ndiye Mola wa kweli Peke Yake, Hana mshirika, watayaamini na kuyakubali na kuyatumia? info
التفاسير: |

7 : 45

وَيۡلٞ لِّكُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٖ

Maangamivu makubwa yatampata kila mrongo sana mwenye dhambi nyingi. info
التفاسير: |

8 : 45

يَسۡمَعُ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ثُمَّ يُصِرُّ مُسۡتَكۡبِرٗا كَأَن لَّمۡ يَسۡمَعۡهَاۖ فَبَشِّرۡهُ بِعَذَابٍ أَلِيمٖ

Anayezisikia aya za kitabu cha Allah Mtukufu akisomewa kisha akaendelea kwenye ukanushaji wake kwa kujiona ni mkubwa zaidi wa kutoweza kumfuata Allah Mtukufu na Mtume wake, kana kwamba hakusikia alichosomewa miongoni mwa aya za Allah Mtukufu. Basi mbashirie, ewe Mtume, huyo mrongo mwenye dhambi nyingi: adhabu yenye uchungu inayoumiza ndani ya Moto wa Jahanamu Siku ya Kiyama. info
التفاسير: |

9 : 45

وَإِذَا عَلِمَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا شَيۡـًٔا ٱتَّخَذَهَا هُزُوًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مُّهِينٞ

Na huyu mrongo mwingi wa dhambi anapojua kitu katika aya zetu anazifanyia shere na mzaha. Hao watakuwa na adhabu itakayowadhalilisha na kuwatia kwenye hizaya Siku ya Kiyama, ikiwa ni malipo ya kuicheza shere kwao Qur’ani. info
التفاسير: |

10 : 45

مِّن وَرَآئِهِمۡ جَهَنَّمُۖ وَلَا يُغۡنِي عَنۡهُم مَّا كَسَبُواْ شَيۡـٔٗا وَلَا مَا ٱتَّخَذُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ أَوۡلِيَآءَۖ وَلَهُمۡ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Basi mbele ya hao wenye kuzifanyia shere aya za Allah Mtukufu patakuwa na moto wa Jahanamu. Na hakitawafaa kitu chochote walichokichuma cha mali na watoto wala waungu wao waliowaabudu badala ya Allah Mtukufu. Na watakuwa na adhabu kubwa yenye uchungu. info
التفاسير: |

11 : 45

هَٰذَا هُدٗىۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِمۡ لَهُمۡ عَذَابٞ مِّن رِّجۡزٍ أَلِيمٌ

Hii Qur’ani tuliyoiteremsha kwako, ewe Mtume, ni uongofu wenye kuondoa upotevu, ni dalili ya haki na inamuongoza kwenye njia iliyonyooka atakayeifuata na akaifanyia kazi. Na wale waliozikataa aya zilizomo ndani ya Qur’ani zenye kutolea dalili Ukweli na wasiziamini, watakuwa na adhabu miongoni mwa adhabu kali zaidi Siku ya Kiyama, yenye uchungu na kuumiza. info
التفاسير: |

12 : 45

۞ ٱللَّهُ ٱلَّذِي سَخَّرَ لَكُمُ ٱلۡبَحۡرَ لِتَجۡرِيَ ٱلۡفُلۡكُ فِيهِ بِأَمۡرِهِۦ وَلِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ

Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kutukuka, Ndiye Aliyewadhalilishia bahari, ili majahazi yatembee juu yake kwa amri Yake, na ili mtafute kheri Zake kwa biashara mbalimbali na shughuli za kiuchumi, na kwamba nyinyi mpate kumshukuru Mola menu kwa kuwadhalilishia hayo, na hivyo basi mumuabudu Yeye Peke Yake na mumtii Yeye katika yale Anayowaamrisha na kuwakataza. info
التفاسير: |

13 : 45

وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ جَمِيعٗا مِّنۡهُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَتَفَكَّرُونَ

Na Akawadhalilishia kila kilichoko mbinguni miongoni mwa jua, mwezi na nyota, na kila kilicho ardhini miongoni mwa wanyama, miti, majahazi na visivyokuwa hivyo kwa ajili ya maslahi yenu. Neema zote hizi ni vipaji alivyowaneemesha navyo Allah Mtukufu Peke Yake na fadhila inayotoka Kwake Aliyowafadhili nayo. Basi Yeye Peke Yake muabuduni, na msimfanye yoyote kuwa ni mshirika Wake. Hakika katika vitu Alivyowadhalilishia Allah Mtukufu kuna alama na dalili juu ya upweke wa Allah Mtukufu kwa watu wenye kuzitia akilini aya za Allah Mtukufu, hoja Zake na dalili Zake, wakazizingatia. info
التفاسير: |
prev

Al-Jathiyah

next
:
0:00 0:00