பக்க எண்:close

5 : 49

وَلَوۡ أَنَّهُمۡ صَبَرُواْ حَتَّىٰ تَخۡرُجَ إِلَيۡهِمۡ لَكَانَ خَيۡرٗا لَّهُمۡۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ

Na lau wangesubiri mpaka ukawatokea ingekua bora zaidi kwao mbele ya Allah Mtukufu, kwa kuwa Allah Mtukufu Amewaamrisha kukuheshimu. Na Allah Mtukufu ni Mwingi wa msamaha kwa yale yaliyotokea kwao ya madhambi na utovu wa adabu kwa kutojua kwao, ni Mwingi wa rehema kwao kwa kutowaharakishia mateso. info
التفاسير: |

6 : 49

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِن جَآءَكُمۡ فَاسِقُۢ بِنَبَإٖ فَتَبَيَّنُوٓاْ أَن تُصِيبُواْ قَوۡمَۢا بِجَهَٰلَةٖ فَتُصۡبِحُواْ عَلَىٰ مَا فَعَلۡتُمۡ نَٰدِمِينَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, Akiwajia mtu aliyetoka nje ya maadili ya Dini na habari yoyote, ihakikisheni habari yake kabla ya kuiamini na kuisambaza mpaka mjue usahihi wake, kwa kuchelea msijekuwatuhumu watu wasio na hatia kwa kosa lenu mkaja kujuta kwa hilo. info
التفاسير: |

7 : 49

وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ فِيكُمۡ رَسُولَ ٱللَّهِۚ لَوۡ يُطِيعُكُمۡ فِي كَثِيرٖ مِّنَ ٱلۡأَمۡرِ لَعَنِتُّمۡ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ حَبَّبَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡإِيمَٰنَ وَزَيَّنَهُۥ فِي قُلُوبِكُمۡ وَكَرَّهَ إِلَيۡكُمُ ٱلۡكُفۡرَ وَٱلۡفُسُوقَ وَٱلۡعِصۡيَانَۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلرَّٰشِدُونَ

Na mjue kuwa baina yenu yupo Mtume wa Allah Mtukufu, kuweni na adabu naye, kwani yeye anayajua zaidi mambo yanayowafaa kuliko nyinyi, anawatakia kheri, na nyinyi huenda mkajitakia shari na madhara ambayo Mtume hawakubalii, na lau yeye angewafuata nyinyi katika mengi mnayoyachagua, hilo lingepelekea muingie kwenye usumbufu. Lakini Allah Mtukufu Amewafanya muipende Imani na Akaifanya ipambike ndani ya nyoyo zenu ndipo mkaamini, na Amewafanya mchukie kumkanusha Allah Mtukufu, na kutoka nje ya twaa Yake na kumuasi. Hao waliosifika kwa sifa hizi ndio waongofu wenye kufuata njia ya haki. info
التفاسير: |

8 : 49

فَضۡلٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَنِعۡمَةٗۚ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ

Kheri hii walioipata ni fadhila kutoka kwa Allah Mtukufu juu yao na ni neema. Na Allah Mtukufu Anamjua vizuri anayezishukuru neema Zake, ni Mwingi wa hekima katika kuendesha mambo ya viumbe Vyake. info
التفاسير: |

9 : 49

وَإِن طَآئِفَتَانِ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ٱقۡتَتَلُواْ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَاۖ فَإِنۢ بَغَتۡ إِحۡدَىٰهُمَا عَلَى ٱلۡأُخۡرَىٰ فَقَٰتِلُواْ ٱلَّتِي تَبۡغِي حَتَّىٰ تَفِيٓءَ إِلَىٰٓ أَمۡرِ ٱللَّهِۚ فَإِن فَآءَتۡ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَهُمَا بِٱلۡعَدۡلِ وَأَقۡسِطُوٓاْۖ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُقۡسِطِينَ

Na makundi mawili ya Waumini yakipigana, fanyeni upatanishi, baina yao kwa kuyaita yakubali kuamuliwa na Kitabu cha Allah Mtukufu na (Sunnah) za Mtume Wake, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na kuridhika na uamuzi wa hivyo viwili. Iwapo kundi mojawapo ya yale mawili litalifanyia uadui kundi lingine na litakataa kukubali mwito huo wa upatanishi, basi lipigeni vita mpaka lirudi kwenye uamuzi wa Allah Mtukufu na Mtume Wake, na likirudi fanyeni upatanishi baina ya hayo mawili kwa haki, na mfanyeni uadilifu katika uamuzi wenu kwa kutotoka nje ya hukumu ya wenyezi Mungu na hukumu ya Mtume Wake katika uamuzi wenu. Hakika Allah Mtukufu Anawapenda waadilifu katika uamuzi wao, wanaohukumu baina ya viumbe Vyake kwa haki. (Katika aya hii pana kuthibitisha sifa ya mapenzi kwa Allah Mtukufu kihakika, kama inavyonasibiana na utukufu Wake Aliyetakasika na kila sifa ya upungufu). info
التفاسير: |

10 : 49

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ إِخۡوَةٞ فَأَصۡلِحُواْ بَيۡنَ أَخَوَيۡكُمۡۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ لَعَلَّكُمۡ تُرۡحَمُونَ

Hakika Waumini ni ndugu katika Dini, basi fanyeni upatanishi baina ya ndugu zenu wawili wakipigana. Na mwogopeni Allah Mtukufu katika mambo yenu yote, kwa kutarajia mrehemewe. info
التفاسير: |

11 : 49

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا يَسۡخَرۡ قَوۡمٞ مِّن قَوۡمٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُونُواْ خَيۡرٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا نِسَآءٞ مِّن نِّسَآءٍ عَسَىٰٓ أَن يَكُنَّ خَيۡرٗا مِّنۡهُنَّۖ وَلَا تَلۡمِزُوٓاْ أَنفُسَكُمۡ وَلَا تَنَابَزُواْ بِٱلۡأَلۡقَٰبِۖ بِئۡسَ ٱلِٱسۡمُ ٱلۡفُسُوقُ بَعۡدَ ٱلۡإِيمَٰنِۚ وَمَن لَّمۡ يَتُبۡ فَأُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na mkafuata Sheria Zake kivitendo, wasitoke wanaume Waumini wakawacheza shere wanaume Waumini wengine, huenda akawa yule anayechezwa shere katika wao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere, na wasitoke wanawake Waumini wakawacheza shere wanawake Waumini wengine, kwani huenda yule anayechezwa shere miongoni mwao ni bora kuliko wale wenye kucheza shere. Wala msitiane dowa nyinyi kwa nyinyi, wala msiitane majina ambayo yanachukiwa na wenye kuitwa nayo, kwani ubaya wa sifa na jina ni utokaji nje wa maadili ya Dini, nao ni kucheza shere kwa njia ya dharau, kuaibisha kwa maneno au ishara na kupeana majina mabaya, baada ya kuwa mmeingia kwenye Uislamu na mmeufahamu. Na Asiyetubia na huku kuchezeana shere, kutiana dowa, na kuitana majina mabaya na utokaji nje wa maadili ya Dini, basi hao ndio watu waliozidhulumu nafsi zao kwa kuyatenda mambo haya yaliyokatazwa. info
التفاسير: |
prev

AlHujurat

next
:
0:00 0:00