prev

Al-Ma'arij

next

1 : 70

سَأَلَ سَآئِلُۢ بِعَذَابٖ وَاقِعٖ

Mmoja miongoni mwa washrikina amejiombea yeye na watu wake washukiwe na adhabu, adhabu ambayo ni yenye kuwapata siku ya kiama. info
التفاسير: |

2 : 70

لِّلۡكَٰفِرِينَ لَيۡسَ لَهُۥ دَافِعٞ

Bila shaka ni yenye kuwapata makafiri Siku ya kiyama, na hakuna mwenye kuizuia. info
التفاسير: |

3 : 70

مِّنَ ٱللَّهِ ذِي ٱلۡمَعَارِجِ

Hakuna mzuiaji yoyote wa kuizuia hiyo adhabu isipokuwa Allah Mtukufu, (Mwenye kuwa juu na mwenye utukufu na haiba). info
التفاسير: |

4 : 70

تَعۡرُجُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَٱلرُّوحُ إِلَيۡهِ فِي يَوۡمٖ كَانَ مِقۡدَارُهُۥ خَمۡسِينَ أَلۡفَ سَنَةٖ

Malaika na Jibrili wanapanda kuenda Kwake, (Aliyetukuka), kwa siku moja ambayo ni sawa na miaka elfu hamsini katika miaka ya duniani, nayo kwa aliyeamini ni kama muda wa Swala moja ya faradhi. info
التفاسير: |

5 : 70

فَٱصۡبِرۡ صَبۡرٗا جَمِيلًا

Basi vumilia, (ewe Mtume), kule kufanya kwao shere na kutaka kwao wafikiwe na adhabu kwa haraka, uvumilivu usiokuwa na shaka, wala kumshtakia asiyekuwa Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

6 : 70

إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدٗا

Kwa kweli makafiri wanaiona adhabu kuwa iko mbali na wanaona kuwa si yenye kutokea. info
التفاسير: |

7 : 70

وَنَرَىٰهُ قَرِيبٗا

Na sisi tunaiona ni yenye kutokea kwa kipindi cha karibu bila shaka. info
التفاسير: |

8 : 70

يَوۡمَ تَكُونُ ٱلسَّمَآءُ كَٱلۡمُهۡلِ

Siku ambayo mbingu itayayuka iwe kama rojo la mafuta. info
التفاسير: |

9 : 70

وَتَكُونُ ٱلۡجِبَالُ كَٱلۡعِهۡنِ

Na majabali yawe ni kama sufi iliyochanganywa na iliyoshanuliwa na kupeperushwa na upepo. info
التفاسير: |

10 : 70

وَلَا يَسۡـَٔلُ حَمِيمٌ حَمِيمٗا

Wala mtu hatamuuliza jamaa yake wa karibu kuhusu jambo lake, kwani kila mmoja atashughulishwa na nafsi yake. info
التفاسير: |
prev

Al-Ma'arij

next
:
0:00 0:00