prev

Al-Muzzammil

next

1 : 73

يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡمُزَّمِّلُ

Ewe uliojifunika nguo zako! info
التفاسير: |

2 : 73

قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلٗا

Inuka uswali kipindi cha usiku isipokuwa sehemu chache yake. info
التفاسير: |

3 : 73

نِّصۡفَهُۥٓ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلًا

Inuka kwa muda wa nusu ya usiku au chini ya hapo kidogo mpaka ufikie theluthi. info
التفاسير: |

4 : 73

أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلًا

Au ongeza zaidi ya nusu mpaka ufikie theluthi mbili. Na usome Qur’ani kwa utaratibu na utulivu, uzipangilie vizuri herufi zake na vituo vyake. info
التفاسير: |

5 : 73

إِنَّا سَنُلۡقِي عَلَيۡكَ قَوۡلٗا ثَقِيلًا

Hakika tutakuteremshia, (ewe Nabii), Qur’ani tukufu inayokusanya maamrisho na makatazo na hukumu za kisheria. info
التفاسير: |

6 : 73

إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِيَ أَشَدُّ وَطۡـٔٗا وَأَقۡوَمُ قِيلًا

Hakika ibada unayofanya ndani ya usiku ina athari kubwa zaidi moyoni, na maneno yanabainika zaidi, kwa kuwa moyo uko mtupu hauna bughudha za kilimwengu. info
التفاسير: |

7 : 73

إِنَّ لَكَ فِي ٱلنَّهَارِ سَبۡحٗا طَوِيلٗا

Hakika wewe katika kipindi cha mchana una wakati wa kuzunguka na kushughulika katika mambo yenye maslahi nawe, na kufanya harakati nyingi kwa majukumu ya utume, basi wakati wa usiku ipe nafasi nafsi yako kumuabudu Mola wako. info
التفاسير: |

8 : 73

وَٱذۡكُرِ ٱسۡمَ رَبِّكَ وَتَبَتَّلۡ إِلَيۡهِ تَبۡتِيلٗا

Na ulitaje, (ewe Nabii), jina la Mola wako, umuombe kwalo na ujitundike Kwake kikamilifu katika ibada yako na ujitegemeze Kwake. info
التفاسير: |

9 : 73

رَّبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَٱتَّخِذۡهُ وَكِيلٗا

Yeye Ndiye Mmiliki wa Mashariki na Magharibi. Hakuna muabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Basi mtegemee na umuachie Yeye mambo yako. info
التفاسير: |

10 : 73

وَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَٱهۡجُرۡهُمۡ هَجۡرٗا جَمِيلٗا

Na uvumilie kwa yale ambayo washirikina wanayasema kuhusu wewe na kuhusu Dini yako. Na uende kinyume na wao katika maneno yao ya ubatilifu pamoja na kuwapuuza na kuacha kuwarudishia. info
التفاسير: |

11 : 73

وَذَرۡنِي وَٱلۡمُكَذِّبِينَ أُوْلِي ٱلنَّعۡمَةِ وَمَهِّلۡهُمۡ قَلِيلًا

Na uniache mimi, (ewe Mtume), na hawa wakanushaji wa aya zangu, wenye starehe na kubobea kwenye ulimwengu, na uwape mhula wa muda mchache kwa kucheleweshewa adhabu mpaka muda wa wao kuadhibiwa ufike. info
التفاسير: |

12 : 73

إِنَّ لَدَيۡنَآ أَنكَالٗا وَجَحِيمٗا

Kwa hakika wao watapata kwetu huko Akhera pingu nzito na Moto wenye kuwaka ambao watachomwa nao. info
التفاسير: |

13 : 73

وَطَعَامٗا ذَا غُصَّةٖ وَعَذَابًا أَلِيمٗا

Na watapata chakula cha kuchukiza chenye kusakama kooni kisicho na ladha, na adhabu inayoumiza. info
التفاسير: |

14 : 73

يَوۡمَ تَرۡجُفُ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ وَكَانَتِ ٱلۡجِبَالُ كَثِيبٗا مَّهِيلًا

Siku itakapotikisika na kusukikasukika ardhi na majabali mpaka majabali yawe mlima wa mchanga wenye kutiririka na kupeperuka, baada ya kuwa kwenye hali ya ugumu na ukavu. info
التفاسير: |

15 : 73

إِنَّآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡكُمۡ رَسُولٗا شَٰهِدًا عَلَيۡكُمۡ كَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ رَسُولٗا

Hakika sisi tumemtuma kwenu nyinyi, (watu wa Makkah), Muhammad kuwa ni Mtume, mwenye kutoa ushahidi wa ukafiri na uasi unaotokana nanyi, kama vile tulivyomtuma Mûsã kuwa Mtume kwenda kwa Fir’awn aliyepita kiasi katika uasi. info
التفاسير: |

16 : 73

فَعَصَىٰ فِرۡعَوۡنُ ٱلرَّسُولَ فَأَخَذۡنَٰهُ أَخۡذٗا وَبِيلٗا

Basi Fir’awn akamkanusha Mûsã na asiukubali utume wake, na akakataa amri yake, tukamuangamiza maangamivu makali. Hapa pana onyo la kumuasi Mtume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kwa kuogopea isije ikamfika mwenye kuasi mfano wa kile kilichomfika Fir‘awn na watu wake. info
التفاسير: |

17 : 73

فَكَيۡفَ تَتَّقُونَ إِن كَفَرۡتُمۡ يَوۡمٗا يَجۡعَلُ ٱلۡوِلۡدَٰنَ شِيبًا

Vipi mtajikinga nafsi zenu, mkikufuru, na adhabu ya Siku ya Kiyama ambayo huwafanya watoto wadogo watokwe na mvi kwa ukubwa wa janga lake na unguliko lake? info
التفاسير: |

18 : 73

ٱلسَّمَآءُ مُنفَطِرُۢ بِهِۦۚ كَانَ وَعۡدُهُۥ مَفۡعُولًا

Mbingu zitapasuka Siku hiyo, kwa ukubwa wa janga lake, hakika ahadi ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ya kuwa Siku hiyo itakuja ni yenye kutimia bila shaka. info
التفاسير: |

19 : 73

إِنَّ هَٰذِهِۦ تَذۡكِرَةٞۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلًا

Hakika hizi aya ambazo ndani yake kuna kukhofisha na ukemeaji ni mawaidha na mazingatio kwa watu. Basi mwenye kutaka kuwaidhika na kunufaika nazo, na achukue utiifu na uchamungu kuwa ni njia ya kumfikisha kwenye radhi za Mola wake Aliyemuumba na kumlea. info
التفاسير: |
prev

Al-Muzzammil

next
:
0:00 0:00