prev

Al-Insan

next

1 : 76

هَلۡ أَتَىٰ عَلَى ٱلۡإِنسَٰنِ حِينٞ مِّنَ ٱلدَّهۡرِ لَمۡ يَكُن شَيۡـٔٗا مَّذۡكُورًا

Kishampitia binadamu kipindi kirefu cha wakati kabla hajapulizwa roho ambapo hakuwa ni kitu kinachotajika wala haijulikani athari yake. info
التفاسير: |

2 : 76

إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٖ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا

Sisi tumemuumba binadamu kutokana na tone la manii la mchanganyiko wa maji ya mwanaume na maji ya mwanamke, ili tumtahini kwa kumuamrisha mambo ya kisheria baadaye, hivyo basi tumemfanya ni mwenye masikio ya kusikia na macho ya kuonea, apate kuzisikia aya na kuziona dalili. info
التفاسير: |

3 : 76

إِنَّا هَدَيۡنَٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرٗا وَإِمَّا كَفُورًا

Sisi tumembainishia na kumfahamisha njia ya uongofu na upotevu na wema na ubaya, ili awe ima ni mwenye kuamini na kushukuru. Au awe ni mwenye kukanusha na kukataa. info
التفاسير: |

4 : 76

إِنَّآ أَعۡتَدۡنَا لِلۡكَٰفِرِينَ سَلَٰسِلَاْ وَأَغۡلَٰلٗا وَسَعِيرًا

Sisi Tumewaandalia wakanushaji pingu za chuma za kuifunga miguu yao, na minyororo ya kufungiwa mikono yao hadi shingo zao, na moto ambao watachomwa nao. info
التفاسير: |

5 : 76

إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ يَشۡرَبُونَ مِن كَأۡسٖ كَانَ مِزَاجُهَا كَافُورًا

Hakika watu wa utiifu na ukweli wa Imani wanaotekeleza haki za Allah Mtukufu, watakunywa, Siku ya Kiyama, kutoka kwenye kikombe ambacho ndani yake mna Pombe iliyochanganywa na aina bora kabisa ya harufu nzuri, nayo ni maji ya kafuri. info
التفاسير: |
prev

Al-Insan

next
:
0:00 0:00