prev

An-Naba

next

1 : 78

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ

Ni kuhusu kitu gani baadhi ya makafiri wa kikureishi wanaulizana? info
التفاسير: |

2 : 78

عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ

Wanaulizana kuhusu habari iliyo na uzito mkubwa kabisa. info
التفاسير: |

3 : 78

ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ

Nayo ni Qur’ani tukufu inayotoa habari za kufufuliwa ambako makafiri wa kikureishi wana shaka nako na wanakukanusha. info
التفاسير: |

4 : 78

كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

Mambo sivyo kama wanavyodhania hawa washirikina. Hapo watajua hawa washirikina upeo wa kukanusha kwao na kitawadhihirikia waziwazi kile Atakachowatenda Allah Mtukufu Siku ya Kiyama. info
التفاسير: |

5 : 78

ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ

Kisha litadhihiri kwao jambo hilo na utadhihiri ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), kuhusu Qur’ani na kufufuliwa. Huu ni utisho na makemeo kwao. info
التفاسير: |

6 : 78

أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا

Kwani hatukuwatandazia ardhi kama tandiko? info
التفاسير: |

7 : 78

وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا

Na Tukawafanyia majabali kuwa ni vigingi, ili isitikisike? info
التفاسير: |

8 : 78

وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا

Na Tukawaumba aina mbali mbali, za kike na kiume? info
التفاسير: |

9 : 78

وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا

Na Tukafanya usingizi wenu ni mapumziko kwa viwiliwili vyenu: ndani yake mnatulia na kupumzika? info
التفاسير: |

10 : 78

وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا

Na Tukaufanya usiku kuwa ni vazi, unawavisha giza lake na kuwafunika, kama nguo inavyomsitiri mwenye kuivaa? info
التفاسير: |

11 : 78

وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا

Na Tukaufanya mchana ni kipindi cha kutafuta maisha, mnatawanyika humo kwa ajili ya maisha yenu na mnatembea humo kwa ajili ya maslahi yenu? info
التفاسير: |

12 : 78

وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا

Na Tukajenga juu yenu mbingu saba, madhubuti jengo lake, lilioumbwa kwa uzuri, halina mapasuko wala nyufa? info
التفاسير: |

13 : 78

وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا

Na Tukalifanya jua kuwa ni taa iwakayo na kung’ara? info
التفاسير: |

14 : 78

وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا

Na Tukateremsha kutoka kwenye mawingu yanyeshayo maji yamiminikayo kwa wingi? info
التفاسير: |

15 : 78

لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا

Ili Tutoe kwa maji hayo nafaka inayoliwa na watu? info
التفاسير: |

16 : 78

وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا

Na nyasi zinazoliwa na wanyama na miti iliyosongamana kwa kutawanyika matawi yake? info
التفاسير: |

17 : 78

إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا

Hakika Siku ya Uamuzi kati ya viumbe, nayo ni Siku ya Kiyama, imekuwa ni wakati na ahadi iliyowekewa muda maalumu kwa watu wa mwanzo na wa mwisho. info
التفاسير: |

18 : 78

يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا

Siku ambayo litapulizwa baragumu na hapo mtakuja makundi kwa makundi. info
التفاسير: |

19 : 78

وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا

Na zikafunguliwa mbingu zikawa ni zenye milango mingi kwa ajili ya kuteremka Malaika. info
التفاسير: |

20 : 78

وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا

Na yakalipuliwa majabali baada ya kuwa yamekita, yakawa ni kama hakukua na kitu. info
التفاسير: |

21 : 78

إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا

Hakika Jahanamu, Siku Hiyo, itawalinda wenye ukafiri ambao Moto huo umeandaliwa wao. info
التفاسير: |

22 : 78

لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابٗا

Kwa makafiri ndio marejeo. info
التفاسير: |

23 : 78

لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا

Watabakia humo muda mrefu ufuatanao, usiokoma, yani milele. info
التفاسير: |

24 : 78

لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا

Hawatakula humo chochote kitakachozima joto la moto. Wala kinywaji kitakachowaondolea kiu yao. info
التفاسير: |

25 : 78

إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا

Isipokuwa maji moto na usaha wa watu wa motoni. info
التفاسير: |

26 : 78

جَزَآءٗ وِفَاقًا

Watakuwa wanalipwa kwa hilo malipo ya sawa yanayolingana na vitendo vyao walivyovitenda duniani. info
التفاسير: |

27 : 78

إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا

Hakika wao walikuwa hawaiyogopi Siku ya Hesabu, na kwa hivyo hawakujitayarisha nayo kwa kufanya matendo ya kuwafaa. info
التفاسير: |

28 : 78

وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا

Na waliyakanusha waziwazi yaliyoletwa na Mitume. info
التفاسير: |

29 : 78

وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا

Na kila kitu Tulikijua na Tukakiandika katika Ubao uliohifadhiwa (Al-Lawḥ Al-Maḥfūḍ). info
التفاسير: |

30 : 78

فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا

Basi Onjeni, (enyi makafiri) hayo, yakiwa ni malipo ya vitendo vyenu, Hatutawazidishia isipokuwa adhabu juu ya adhabu yenu. info
التفاسير: |
prev

An-Naba

next
:
0:00 0:00