prev

Al-Anfal

next

1 : 8

يَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡأَنفَالِۖ قُلِ ٱلۡأَنفَالُ لِلَّهِ وَٱلرَّسُولِۖ فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَصۡلِحُواْ ذَاتَ بَيۡنِكُمۡۖ وَأَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Masahaba Zako wanakuuliza, ewe Nabii, kuhusu ngawira siku ya Badr: utawagawia vipi? Waambie, «Jambo lake limeachiwa Allah Mtukufu na Mtume Wake» Mtume ndiye mwenye kusimamia ugawaji wake kwa amri ya Mola wake. Basi jikingeni na mateso ya Allah Mtukufu wala msithubutu kumuasi, na muache kubishana na kuteta kwa sababu ya mali, na mzitengeneze hali zenu, na mjilazimishe utiifu kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake iwapo nyinyi ni Waumini, kwani Imani inapelekea kumtii Allah Mtukufu na Mtume Wake. info
التفاسير: |

2 : 8

إِنَّمَا ٱلۡمُؤۡمِنُونَ ٱلَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ ٱللَّهُ وَجِلَتۡ قُلُوبُهُمۡ وَإِذَا تُلِيَتۡ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُهُۥ زَادَتۡهُمۡ إِيمَٰنٗا وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ

Hakika wenye kumuamini Allah Mtukufu kikweli ni wale ambao akitajwa Allah Mtukufu nyoyo zao zinaingiwa na kicho, wasomewapo aya za Allah Mtukufu zinawazidishia Imani pamoja na Imani waliyo nayo kwa kuyazingatia maana yake na kwa Mola wao wanategemea: hawamtaraji isipokuwa Yeye na hawamuogopi isipokuwa Yeye. info
التفاسير: |

3 : 8

ٱلَّذِينَ يُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَٰهُمۡ يُنفِقُونَ

Wale ambao wanaendelea kutekeleza Swala zilizofaradhiwa kwa nyakati zake, na katika kile tulichowaruzuku wanatoa kwenye yale tuliyowaamrisha. info
التفاسير: |

4 : 8

أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ حَقّٗاۚ لَّهُمۡ دَرَجَٰتٌ عِندَ رَبِّهِمۡ وَمَغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ

Hawa wanaofanya matendo haya ndio wenye kuyaamini kikweli, nje na ndani, yale Aliyowateremshia Allah Mtukufu, watakuwa na daraja za juu mbele ya Allah Mtukufu, msamaha wa dhambi zao na riziki nzuri ambayo ni Pepo. info
التفاسير: |

5 : 8

كَمَآ أَخۡرَجَكَ رَبُّكَ مِنۢ بَيۡتِكَ بِٱلۡحَقِّ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ لَكَٰرِهُونَ

Na kama mlivyotafautiana juu ya ugawaji wa ngawira, na Allah Mtukufu Akauondoa kwenu na Akauweka kwa Allah Mtukufu na Mtume Wake, sala na salamu zimuendee, hivyo ndivyo Mola wako Alivyokuamrisha utoke Madina uende kupambana na msafara wa Makureshi kwa wahyi aliyokujia nao Jibrili, pamoja na kuwa kundi miongoni mwa Waumini walichukia kutoka. info
التفاسير: |

6 : 8

يُجَٰدِلُونَكَ فِي ٱلۡحَقِّ بَعۡدَ مَا تَبَيَّنَ كَأَنَّمَا يُسَاقُونَ إِلَى ٱلۡمَوۡتِ وَهُمۡ يَنظُرُونَ

Likawa linabishana na wewe, ewe Nabii, kundi hilo la Waumini kuhusu kupigana baada ya kuonekana wazi kwamba hilo ni lenye kutokea, wakawa kana kwamba wao wanaongozwa kupelekwa kwenye kifo na hali wakikitazama waziwazi. info
التفاسير: |

7 : 8

وَإِذۡ يَعِدُكُمُ ٱللَّهُ إِحۡدَى ٱلطَّآئِفَتَيۡنِ أَنَّهَا لَكُمۡ وَتَوَدُّونَ أَنَّ غَيۡرَ ذَاتِ ٱلشَّوۡكَةِ تَكُونُ لَكُمۡ وَيُرِيدُ ٱللَّهُ أَن يُحِقَّ ٱلۡحَقَّ بِكَلِمَٰتِهِۦ وَيَقۡطَعَ دَابِرَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Na kumbukeni, enyi wenye kujadili, ahadi ya Allah Mtukufu kwenu kuwa mtapata ushindi juu ya moja ya mapote mawili: msafara na bidhaa unazozibeba au jeshi la maadui, mpigane nalo na mlishinde. Na nyinyi mnapenda kupata ushindi juu ya msafara badala ya kupigana. Na Allah Mtukufu Anataka kuuthibitisha Uislamu na kuukuza kwa kuwaamuru nyinyi kupigana na makafiri na kuwamaliza makafiri kwa kuwaangamiza. info
التفاسير: |

8 : 8

لِيُحِقَّ ٱلۡحَقَّ وَيُبۡطِلَ ٱلۡبَٰطِلَ وَلَوۡ كَرِهَ ٱلۡمُجۡرِمُونَ

Ili Allah Mtukufu Aupe nguvu Uislamu na watu wake na auondoe ushirikina na watu wake ingawa washirikina watalichukia hilo. info
التفاسير: |
prev

Al-Anfal

next
:
0:00 0:00