அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு- அலி முஃசின் bபிர்வானி * - மொழிபெயர்ப்பு அட்டவணை

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

மொழிபெயர்ப்பு அத்தியாயம்: ஸூரா அல்இன்ஷிகாக்   வசனம்:

Surat Al-Inshiqaq

إِذَا ٱلسَّمَآءُ ٱنشَقَّتۡ
Itapo chanika mbingu!
Mbingu itapo chanika, ikaamrishwa iondoke,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza!
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi na ikamt'ii, na ndio maelekeo yake isikie na kut'ii,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَإِذَا ٱلۡأَرۡضُ مُدَّتۡ
Na ardhi itakapo tanuliwa!
Na ardhi ikazidi upana wake kwa kulazwa milima na kuondolewa kifusi chake,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَأَلۡقَتۡ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتۡ
Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu!
Na ardhi ikatoa nje maiti na khazina ziliyo kuwamo ndani yake, na ikaachana navyo vyote hivyo,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَأَذِنَتۡ لِرَبِّهَا وَحُقَّتۡ
Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza!
Na ikamwelekea Mola wake Mlezi kwa kuzidi kutanuka kwake na kutoa vilio kuwemo ndani yake na kuachana navyo, na hayo ni haki yake kuwa. Yakitokea yote hayo yaliyo tangulia kusimuliwa basi kila mtu atapata malipo ya vitendo vyake.
அரபு விரிவுரைகள்:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلۡإِنسَٰنُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدۡحٗا فَمُلَٰقِيهِ
Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.
Ewe mtu! Hakika wewe unafanya juhudi katika vitendo vyako vikufikishie lengo lako. Basi utakuja kukutana na Mola wako Mlezi kwa a'mali yako, naye atakulipa kwayo.
அரபு விரிவுரைகள்:
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ
Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia!
Ama mwenye kupewa daftari la vitendo vyake kwa mkono wake wa kulia
அரபு விரிவுரைகள்:
فَسَوۡفَ يُحَاسَبُ حِسَابٗا يَسِيرٗا
Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi!
Basi atahisabiwa kwa hisabu nyepesi,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورٗا
Na arudi kwa ahali zake na furaha.
Na atarejea kwa jamaa zake Waumini naye furahani.
அரபு விரிவுரைகள்:
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ وَرَآءَ ظَهۡرِهِۦ
Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,
Ama mwenye kupewa daftari lake kwa mkono wa kushoto wake nyuma ya mgongo wake kwa kudharauliwa shani yake,
அரபு விரிவுரைகள்:
فَسَوۡفَ يَدۡعُواْ ثُبُورٗا
Basi huyo ataomba kuteketea.
Huyo atatamani ajiue,
அரபு விரிவுரைகள்:
وَيَصۡلَىٰ سَعِيرًا
Na ataingia Motoni.
Na ataingia Motoni aungulie mbali!
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّهُۥ كَانَ فِيٓ أَهۡلِهِۦ مَسۡرُورًا
Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.
Kwani huyo hakika duniani alikuwa furahani kati ya jamaa zake akitanaamu na pumbao alilo kuwa nalo hata akapuuza a'mali ya kuitenda kwa mustakabali wake.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِنَّهُۥ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ
Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.
Hakika huyo alidhani kuwa kabisa hatorejea kwa Mwenyezi Mungu akamhisabu.
அரபு விரிவுரைகள்:
بَلَىٰٓۚ إِنَّ رَبَّهُۥ كَانَ بِهِۦ بَصِيرٗا
Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!
Bali atarejea, na atahisabiwa! Kwani Mola wake Mlezi alikuwa anamwona vyema yeye na vitendo vyake.
அரபு விரிவுரைகள்:
فَلَآ أُقۡسِمُ بِٱلشَّفَقِ
Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,
Basi naapa kiapo cha mkazo kwa wekundu wa mbingu baada ya kuchwa jua!
அரபு விரிவுரைகள்:
وَٱلَّيۡلِ وَمَا وَسَقَ
Na kwa usiku na unavyo vikusanya,
Na kwa usiku na unavyo vikusanya vyote katika giza lake, wanaadamu, wanyama na vyenginevyo!
அரபு விரிவுரைகள்:
وَٱلۡقَمَرِ إِذَا ٱتَّسَقَ
Na kwa mwezi unapo pevuka,
Na mwezi unapo kamilika kupevuka na kutimia nuru yake,
அரபு விரிவுரைகள்:
لَتَرۡكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٖ
Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!
Hapana shaka yoyote mtakutana na hali baada ya hali, baadhi yake zina shida zaidi kuliko nyenginezo, za kufa na kufufuliwa na vitisho vya Kiyama.
அரபு விரிவுரைகள்:
فَمَا لَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ
Basi wana nini hawaamini?
Wana nini hawa makafiri yanayo wazuia wasimuamini Mwenyezi Mungu na kufufuliwa baada ya kuwekwa wazi dalili zake zote za kuwajibika kwake?
அரபு விரிவுரைகள்:
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيۡهِمُ ٱلۡقُرۡءَانُ لَا يَسۡجُدُونَۤ۩
Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?
Na pindi wakizisikia Aya za Qur'ani hawasujudu wakanyenyekea?
அரபு விரிவுரைகள்:
بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ يُكَذِّبُونَ
Bali walio kufuru wanakanusha tu.
Bali watu hawa, kwa ukafiri wao, wanakanusha kwa inadi na kutakabari kuikataa Haki!
அரபு விரிவுரைகள்:
وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِمَا يُوعُونَ
Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.
Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua kabisa hayo wanayo yadhamiria katika nyoyo zao.
அரபு விரிவுரைகள்:
فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ
Basi wabashirie adhabu chungu!
Basi wabashirie, kwa kejeli, kuwa watapata adhabu ya kutia uchungu.
அரபு விரிவுரைகள்:
إِلَّا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ أَجۡرٌ غَيۡرُ مَمۡنُونِۭ
Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.
Lakini walio amini na wakatenda mema watapata, kutoka kwa Mwenyezi Mungu, ujira usio wakatikia na wala usio kuwa na hisabu juu yao.
அரபு விரிவுரைகள்:
 
மொழிபெயர்ப்பு அத்தியாயம்: ஸூரா அல்இன்ஷிகாக்
அத்தியாயங்களின் அட்டவணை பக்க எண்
 
அல்குர்ஆன் மொழிபெயர்ப்பு - சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு- அலி முஃசின் bபிர்வானி - மொழிபெயர்ப்பு அட்டவணை

புனித அல் குர்ஆனுக்கான சுவாஹிலி மொழிபெயர்ப்பு- அலி முஃசின் பிர்வானி மூலம் மொழிபெயர்க்கப்பட்டது

மூடுக