prev

Al-Bayyinah

next

1 : 98

لَمۡ يَكُنِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ مُنفَكِّينَ حَتَّىٰ تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡبَيِّنَةُ

Haikua kwa wenye kukufuru miongoni mwa mayahudi na manaswara na washirikina ni wenye kuacha ukafiri wao isipokua mpaka iwajie alama walioahidiwa katika vitabu vilivyopita, yani walikua wanadai kua wakiona hiyo alama wataamini, lakini wakageuka isipokua wachache. info
التفاسير: |

2 : 98

رَسُولٞ مِّنَ ٱللَّهِ يَتۡلُواْ صُحُفٗا مُّطَهَّرَةٗ

Na alama hiyo ni Mtume wa Allah Mtukufu, Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), mwenye kuwasomea Qur’ani iliyomo kwenye kurasa zilizo safi. info
التفاسير: |

3 : 98

فِيهَا كُتُبٞ قَيِّمَةٞ

Ndani ya kurasa hizo mna habari za kweli na amri za uadilifu zenye kuongoza kwenye haki na kwenye njia iliyonyooka. info
التفاسير: |

4 : 98

وَمَا تَفَرَّقَ ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡكِتَٰبَ إِلَّا مِنۢ بَعۡدِ مَا جَآءَتۡهُمُ ٱلۡبَيِّنَةُ

Na hawakutofautiana wale waliopewa Kitabu, miongoni mwa Mayahudi na manaswara, juu ya kuwa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ni Mtume wa kweli, kwa sifa zake walizokua wakiziona katika vitabu vyao, isipokuwa baada ya kuwathibitikia kuwa yeye ndiye Nabii waliyeahidiwa katika Taurati na Injili. Walikuwa wanakubali, kwa umoja wao, kuwa unabii wake ni wa kweli. Lakini alipopewa utume walimkanusha na wakatofautiana. info
التفاسير: |

5 : 98

وَمَآ أُمِرُوٓاْ إِلَّا لِيَعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ حُنَفَآءَ وَيُقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَيُؤۡتُواْ ٱلزَّكَوٰةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ ٱلۡقَيِّمَةِ

Na hawakuamrishwa katika sheria zote zilizopita isipokuwa wameamrishwa wamuabudu Allah Mtukufu Peke Yake, wakikusudia kwa ibada zao kupata Radhi Zake, na kuepuka ushirikina na kuelekea kwenye Imani, wasimamishe Swala na watoe Zaka. Kufanya hayo ndio Dini iliyonyooka, nayo ni Uislamu. info
التفاسير: |
prev

Al-Bayyinah

next
:
0:00 0:00