next

Al-Humazah

prev

1 : 104

وَيۡلٞ لِّكُلِّ هُمَزَةٖ لُّمَزَةٍ

Shari na maangamivu yatampata kila mwenye kusengenya watu na kuwatia doa na kuwatusi. info
التفاسير: |

2 : 104

ٱلَّذِي جَمَعَ مَالٗا وَعَدَّدَهُۥ

Ambaye hamu yake ni kukusanya mali na kuihesabu. info
التفاسير: |

3 : 104

يَحۡسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخۡلَدَهُۥ

Akidhani kuwa mali yake ambayo ameikusanya itampa dhamana ya kuishi milele duniani na kukwepa kuhesabiwa akhera. info
التفاسير: |

4 : 104

كَلَّاۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِي ٱلۡحُطَمَةِ

Anavyodhania sivyo. Atatiwa ndani ya Moto ambao huvunjavunja kila kinachotiwa humo. info
التفاسير: |

5 : 104

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلۡحُطَمَةُ

Na nikipi kilichokujulisha (ewe Mtume), kua ni upi huo Moto unaovunjavunja? info
التفاسير: |

6 : 104

نَارُ ٱللَّهِ ٱلۡمُوقَدَةُ

Huo ni Moto wa Allah Mtukufu uliowashwa. info
التفاسير: |

7 : 104

ٱلَّتِي تَطَّلِعُ عَلَى ٱلۡأَفۡـِٔدَةِ

Ambao kwa ukali wake hupenyeza miilini na kufika kwenye nyoyo. info
التفاسير: |

8 : 104

إِنَّهَا عَلَيۡهِم مُّؤۡصَدَةٞ

Hakika moto huo ni wenye kufungwa na kutiwa minyororo huku watu hao wa motoni wakiwa ndani yake. info
التفاسير: |

9 : 104

فِي عَمَدٖ مُّمَدَّدَةِۭ

Minyororo hiyo ni yenye kufungwa kwenye nguzo ndefu. info
التفاسير: |
next

Al-Humazah

prev
:
0:00 0:00