قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس

next

Al-Buruj

prev

1 : 85

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلۡبُرُوجِ

Allah Mtukufu Anaapa kwa mbingu zenye njia za kupitia jua na mwezi. info
التفاسير: |

2 : 85

وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡمَوۡعُودِ

Na kwa Siku ya Kiyama ambayo Amewaahidi viumbe kuwa Atawakusanya. info
التفاسير: |

3 : 85

وَشَاهِدٖ وَمَشۡهُودٖ

Na kwa shahidi, mwenye kutoa ushahidi, na mwenye kutolewa ushahidi juu yake. «Allah Mtukufu Huapa kwa Anachokitaka, Lakini kiumbe hafai kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu, Kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu ni ushirikina». info
التفاسير: |

4 : 85

قُتِلَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأُخۡدُودِ

Wamelaaniwa waliochimba shimo kubwa ili kuwatesa Waumini. info
التفاسير: |

5 : 85

ٱلنَّارِ ذَاتِ ٱلۡوَقُودِ

Wakawasha moto mkubwa wenye kuni nyingi. info
التفاسير: |

6 : 85

إِذۡ هُمۡ عَلَيۡهَا قُعُودٞ

Wakawa wamekaa kwenye kingo za shimo hilo. info
التفاسير: |

7 : 85

وَهُمۡ عَلَىٰ مَا يَفۡعَلُونَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ شُهُودٞ

Wakishuhudia vitendo vya mateso na adhabu wanavyowafanyia Waumini. info
التفاسير: |

8 : 85

وَمَا نَقَمُواْ مِنۡهُمۡ إِلَّآ أَن يُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ

Na hawakuwatesa mateso hayo isipokuwa wenye kuteswa walikuwa wanamuamini Allah Mtukufu Mshindi Asiyeshindwa, Mhimidiwa wa maneno Yake, Vitendo Vyake na sifa Zake. info
التفاسير: |

9 : 85

ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ

Mwenye ufalme wa mbingu na ardhi Ambaye, kutakasika na sifa za upungufu ni kwake, Anashuhudia kila kitu, hakuna kinachofichika kwake. info
التفاسير: |

10 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ فَتَنُواْ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ وَٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ ثُمَّ لَمۡ يَتُوبُواْ فَلَهُمۡ عَذَابُ جَهَنَّمَ وَلَهُمۡ عَذَابُ ٱلۡحَرِيقِ

Hakika, wale waliowachoma kwa moto Waumini, wa kike na wa kiume, ili kuwazuia watu na dini ya Allah Mtukufu, kisha hawakutubu, watapata, Siku ya Akhera, adhabu ya Jahanamu na watapata adhabu kali yenye kuchoma. info
التفاسير: |

11 : 85

إِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَهُمۡ جَنَّٰتٞ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُۚ ذَٰلِكَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡكَبِيرُ

Hakika wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya amali njema, watapata Pepo ambayo chini ya majumba yake ya kifahari inapita mito, Huko ni kufaulu kukubwa. info
التفاسير: |

12 : 85

إِنَّ بَطۡشَ رَبِّكَ لَشَدِيدٌ

Hakika malipo ya Mola wako kwa maadui Zake na mateso Yake juu yao ni mazito. info
التفاسير: |

13 : 85

إِنَّهُۥ هُوَ يُبۡدِئُ وَيُعِيدُ

Hakika yeye ndiye Mwenye kuanzisha kuumba na kisha kurudisha. info
التفاسير: |

14 : 85

وَهُوَ ٱلۡغَفُورُ ٱلۡوَدُودُ

Na ndiye Mwingi wa kusamehe kwa wenye kutubia, Mwingi wa mapenzi kwa wanaojikurubisha kwake. info
التفاسير: |

15 : 85

ذُو ٱلۡعَرۡشِ ٱلۡمَجِيدُ

Mwenye Arshi tukufu. info
التفاسير: |

16 : 85

فَعَّالٞ لِّمَا يُرِيدُ

Mfanya Alitakalo, hakuna kitu Anachotaka kiwe kisiwe. info
التفاسير: |

17 : 85

هَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ ٱلۡجُنُودِ

Je, (ewe Mtume), imekufikia habari ya makundi yaliyokufuru na kukanusha Mitume walioletewa? info
التفاسير: |

18 : 85

فِرۡعَوۡنَ وَثَمُودَ

Kundi la firauni na Thamūd, na misiba na adhabu iliyowashukia? Hawakuzingatia kwa habari hiyo. info
التفاسير: |

19 : 85

بَلِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ فِي تَكۡذِيبٖ

Bali waliokufuru wanaendelea katika kukanusha kwao, kama walivyokuwa waliokuja kabla yao. info
التفاسير: |

20 : 85

وَٱللَّهُ مِن وَرَآئِهِم مُّحِيطُۢ

Na Allah Mtukufu Amewazunguka kwa Ujuzi na uwezo Wake, hakuna chenye kufichika Kwake kuhusu wao na vitendo vyao. Hii Qur’ani siyo kama wanavyodai wenye kukanusha katika washirikina kuwa ni mashairi na uchawi. info
التفاسير: |

21 : 85

بَلۡ هُوَ قُرۡءَانٞ مَّجِيدٞ

Bali hii ni Qur’ani iliyo tukufu. info
التفاسير: |

22 : 85

فِي لَوۡحٖ مَّحۡفُوظِۭ

Iko kwenye Ubao Uliohifadhiwa, haufikiwi na haubadilishwi wala kupotoshwa. info
التفاسير: |
next

Al-Buruj

prev
:
0:00 0:00