prev

At-Tariq

next

1 : 86

وَٱلسَّمَآءِ وَٱلطَّارِقِ

Allah Mtukufu Anaapa kwa mbingu na nyota yenye kuchomoza usiku. info
التفاسير: |

2 : 86

وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا ٱلطَّارِقُ

Na ni lipi lilokujulisha ni ukubwa gani wa nyota hiyo? info
التفاسير: |

3 : 86

ٱلنَّجۡمُ ٱلثَّاقِبُ

Hiyo ni nyota ing’arayo na kumeremeta. info
التفاسير: |

4 : 86

إِن كُلُّ نَفۡسٖ لَّمَّا عَلَيۡهَا حَافِظٞ

Hakuna nafsi yoyote isipokuwa imepelekewa Malaika mwenye kusajili amali zake ili ihesabiwe Siku ya Kiyama. info
التفاسير: |

5 : 86

فَلۡيَنظُرِ ٱلۡإِنسَٰنُ مِمَّ خُلِقَ

Basi aangalie binadamu mwenye kukanusha kufufuliwa ameumbwa kwa kitu gani? «Ili ajue kuwa kurudisha umbo lake mara ya pili si vigumu kama kuumbwa mara ya kwanza». info
التفاسير: |

6 : 86

خُلِقَ مِن مَّآءٖ دَافِقٖ

Aliumbwa kwa manii yenye kupenya ndani ya kizazi kwa haraka. info
التفاسير: |

7 : 86

يَخۡرُجُ مِنۢ بَيۡنِ ٱلصُّلۡبِ وَٱلتَّرَآئِبِ

Yatokayo kwenye mgongo wa mwanaume na kifua cha mwanamke. info
التفاسير: |

8 : 86

إِنَّهُۥ عَلَىٰ رَجۡعِهِۦ لَقَادِرٞ

Hakika yule Aliyemuumba binadamu kwa maji haya ni muweza wa kumrudisha kwenye uhai baada ya kufa. info
التفاسير: |

9 : 86

يَوۡمَ تُبۡلَى ٱلسَّرَآئِرُ

Siku zitakapofunuliwa siri ziliofichwa na nafsi, na kutofautishwa jema na baya. info
التفاسير: |

10 : 86

فَمَا لَهُۥ مِن قُوَّةٖ وَلَا نَاصِرٖ

Binadamu hatakuwa na nguvu ya kuitetea nafsi yake, wala hatakuwa na mtetezi wa kumuepushia adhabu ya Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

11 : 86

وَٱلسَّمَآءِ ذَاتِ ٱلرَّجۡعِ

Na Anaapa kwa mbingu yenye mvua ya mara kwa mara. info
التفاسير: |

12 : 86

وَٱلۡأَرۡضِ ذَاتِ ٱلصَّدۡعِ

Na ardhi yenye pasuko za kufanya mimea ichipuke. info
التفاسير: |

13 : 86

إِنَّهُۥ لَقَوۡلٞ فَصۡلٞ

Hakika Qur’ani ni neno lenye kupambanua baina ya haki na batili. info
التفاسير: |

14 : 86

وَمَا هُوَ بِٱلۡهَزۡلِ

Na wala si upuuzi. Haifai kiumbe kuapa kwa asiyekuwa Allah Mtukufu. Akifanya hivyo atakuwa amemshirikisha Allah Mtukufu. info
التفاسير: |

15 : 86

إِنَّهُمۡ يَكِيدُونَ كَيۡدٗا

Hakika wenye kumkanusha Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na Qur’ani, wanafanya vitimbi na mipango ili kuipinga haki na kuitilia nguvu batili. info
التفاسير: |

16 : 86

وَأَكِيدُ كَيۡدٗا

Na Mimi nafanya vitimbi kuidhihirisha haki ingawa makafiri wanachukia. info
التفاسير: |

17 : 86

فَمَهِّلِ ٱلۡكَٰفِرِينَ أَمۡهِلۡهُمۡ رُوَيۡدَۢا

Usiwe na haraka nao, (ewe Mtume), kutaka wateremshiwe adhabu. Wape muhula uwangojee muda mchache wala usiwafanyie haraka, utaona adhabu itakayowafikia, mateso na maangamivu. info
التفاسير: |
prev

At-Tariq

next
:
0:00 0:00