Check out the new design

Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani. * - Tərcumənin mündəricatı

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Mənaların tərcüməsi Surə: əl-Ənbiya   Ayə:
لَا يَسۡمَعُونَ حَسِيسَهَاۖ وَهُمۡ فِي مَا ٱشۡتَهَتۡ أَنفُسُهُمۡ خَٰلِدُونَ
Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale zinayo yatamani nafsi zao. [102]
[102] Hawatasikia sauti ya Moto wake unavyo vuma. Nao huko watapata kila ambacho nafsi inatamani, daima milele.
Ərəbcə təfsirlər:
لَا يَحۡزُنُهُمُ ٱلۡفَزَعُ ٱلۡأَكۡبَرُ وَتَتَلَقَّىٰهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ هَٰذَا يَوۡمُكُمُ ٱلَّذِي كُنتُمۡ تُوعَدُونَ
Hicho Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. Na Malaika watawapokea (kwa kuwaambia): Hii ndiyo Siku yenu mliyo kuwa mkiahidiwa!. [103]
[103] Hawato huzunishwa na Kitisho Kikubwa kinacho wafazaisha makafiri. Na Malaika watawapokea kwa kuwapongeza kwa kusema: Hii ndiyo Siku yenu ya neema aliyo kuahidini Mola wenu Mlezi!
Ərəbcə təfsirlər:
يَوۡمَ نَطۡوِي ٱلسَّمَآءَ كَطَيِّ ٱلسِّجِلِّ لِلۡكُتُبِۚ كَمَا بَدَأۡنَآ أَوَّلَ خَلۡقٖ نُّعِيدُهُۥۚ وَعۡدًا عَلَيۡنَآۚ إِنَّا كُنَّا فَٰعِلِينَ
Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni watendao. [104]
[104] Siku tutapo zikunja mbingu kama zinavyo kunjwa karatasi katika kitabu. Na tutawarejeza viumbe kwa ajili ya hisabu na malipo. Wala hatushindwi kuwarejeza, kwani tuliwaumba mara ya kwanza. Na kama tulivyo waanza tutawarejeza. Ahadi yetu kwa hayo ni ahadi ya kweli. Daima Sisi tunatenda tunayo yaahidi.
Ərəbcə təfsirlər:
وَلَقَدۡ كَتَبۡنَا فِي ٱلزَّبُورِ مِنۢ بَعۡدِ ٱلذِّكۡرِ أَنَّ ٱلۡأَرۡضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ ٱلصَّٰلِحُونَ
Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema. [105]
[105] Na tulikwisha andika katika Zaburi - nacho ni Kitabu cha Daud baada ya Taurati - kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema wapate kuitengeza, na kusahilisha njia za maisha bora humo. ("Bali wenye upole watairithi nchi"..Zaburi 37.11 "Wenye haki watairithi nchi, nao watakaa humo milele".. Zaburi 37.29)
Ərəbcə təfsirlər:
إِنَّ فِي هَٰذَا لَبَلَٰغٗا لِّقَوۡمٍ عَٰبِدِينَ
Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada. [106]
[106] Hakika katika haya tuliyo yataja, khabari za Manabii pamoja na kaumu zao, na khabari za Pepo na Moto, yanatosha kuwakumbusha na kuwafanya wazingatie watu walio tayari kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee na hawasalitiki na mapambo ya dunia.
Ərəbcə təfsirlər:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا رَحۡمَةٗ لِّلۡعَٰلَمِينَ
Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote. [107]
[107] Na hatukukutuma, ewe Nabii, ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
Ərəbcə təfsirlər:
قُلۡ إِنَّمَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ أَنَّمَآ إِلَٰهُكُمۡ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞۖ فَهَلۡ أَنتُم مُّسۡلِمُونَ
Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu. Je! Mmesilimu?. [108]
[108] Ewe Nabii! Sema: Hakika kiini cha Wahyi aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni kwamba hakika nyinyi hamna Mungu isipo kuwa Yeye. Na yote yaliyo bakia niliyo funuliwa yanafuata asili hii. Ikiwa mambo ni hivyo, basi inakuwajibikieni mjisalimishe na mnyenyekee kwa Mwenyezi Mungu peke yake.
Ərəbcə təfsirlər:
فَإِن تَوَلَّوۡاْ فَقُلۡ ءَاذَنتُكُمۡ عَلَىٰ سَوَآءٖۖ وَإِنۡ أَدۡرِيٓ أَقَرِيبٌ أَم بَعِيدٞ مَّا تُوعَدُونَ
Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au mbali hayo mliyo ahidiwa. [109]
[109] Wakito ujali wito wako, basi waambie: Nimekufunzeni yote aliyo niamrisha Mola wangu Mlezi; na kwa hivyo tumekuwa sawa kwa kuyajua hayo. Wala mimi sijui hayo ya kufufuliwa na kuhisabiwa mliyo ahidiwa, yatakuwa karibu au mbali.
Ərəbcə təfsirlər:
إِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلۡجَهۡرَ مِنَ ٱلۡقَوۡلِ وَيَعۡلَمُ مَا تَكۡتُمُونَ
Hakika Yeye anajua kauli ya dhaahiri na anajua myafichayo. [110]
[110] Hakika Mwenyezi Mungu anayajua yote yasemwayo, mnayo yadhihirisha na mnayo yaficha.
Ərəbcə təfsirlər:
وَإِنۡ أَدۡرِي لَعَلَّهُۥ فِتۡنَةٞ لَّكُمۡ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ
Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka muda kidogo. [111]
[111] Na sijui pengine huko kupewa muhula na kuakhirishiwa adhabu nyinyi ndio Mwenyezi Mungu anakufanyieni mtihani tu, na kukustarehesheni kwa ladha za maisha mpaka alipo kadiria Mwenyezi Mungu kukuhisabieni kwa hikima yake.
Ərəbcə təfsirlər:
قَٰلَ رَبِّ ٱحۡكُم بِٱلۡحَقِّۗ وَرَبُّنَا ٱلرَّحۡمَٰنُ ٱلۡمُسۡتَعَانُ عَلَىٰ مَا تَصِفُونَ
Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayo yazua;. [112]
[112] Ewe Nabii! Sema: Ewe Mola Mlezi! Tuhukumu baina yangu na hawa nilio wafikishia Wahyi kwa uadilifu ili wasiwe sawa Waumini na makafiri. Na Mola wetu Mlezi Mwenye kuneemesha kwa neema kubwa, Mwenye kustahiki kuhimidiwa na kushukuriwa, ndiye wa kutakiwa msaada kuvunja uzushi mnao zua, enyi makafiri.
Ərəbcə təfsirlər:
 
Mənaların tərcüməsi Surə: əl-Ənbiya
Surələrin mündəricatı Səhifənin rəqəmi
 
Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani. - Tərcumənin mündəricatı

Tərcümə edən: Əli Muhsin əl-Bərvani.

Bağlamaq