Check out the new design

Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani. * - Tərcumənin mündəricatı

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Mənaların tərcüməsi Surə: əl-Vaqiə   Ayə:

Al-Waqi'ah

إِذَا وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Litakapo tukia hilo Tukio . [1]
[1] Kitakapo tukia Kiyama
Ərəbcə təfsirlər:
لَيۡسَ لِوَقۡعَتِهَا كَاذِبَةٌ
Hapana cha kukanusha kutukia kwake. [2]
[2] Haitotokea nafsi yoyote ya kukadhibisha.
Ərəbcə təfsirlər:
خَافِضَةٞ رَّافِعَةٌ
Literemshalo linyanyualo! [3]
[3] Kiyama hicho kitawateremsha chini walio waovu, na kitawanyanyua juu walio wema.
Ərəbcə təfsirlər:
إِذَا رُجَّتِ ٱلۡأَرۡضُ رَجّٗا
Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso! [4]
[4] Ardhi itakapo tikiswa, na ikatetemeshwa kwa nguvu.
Ərəbcə təfsirlər:
وَبُسَّتِ ٱلۡجِبَالُ بَسّٗا
Na milima itapo sagwasagwa! [5]
[5] Na milima ikavurugwa teketeke,
Ərəbcə təfsirlər:
فَكَانَتۡ هَبَآءٗ مُّنۢبَثّٗا
Iwe mavumbi yanayo peperushwa! [6]
[6] Ikawa vumbi la kupeperushwa, Aya hizi tukufu zinaeleza hadi gani vitakuwa vitisho vitavyo uteremkia ulimwengu kitapo fika Kiyama. Na katika vitisho hivyo ni hayo masaibu ya dunia yatakayo athiri ardhi na mat'abaka yake. Kwani hii ardhi tunayo ishi juu ya mgongo wake si yenye kutulia na kukaa sawa kwa utimilivu. Kwani hiyo imeundwa kwa mat'abaka ya majabali yaliyo ingiliana ovyo. Huenda baadhi yao yakateremka yakaachana na mengineyo yaliyo jirani nayo. Na huwa hiyo inayo itwa kupasuka kwa mat'abaka ya ardhi, Geological cleavage kama inavyo tokea katika maeneo kadhaa wa kadhaa. Mpasuko huu ulikuwa na ungali kuwa ndio asili ya chini kabisa ya zilzala, mitetemeko, mikubwa kwa kuathirika na nguvu za kudidimiza na kuvuta zinazo fuatana na mat'abaka ya ardhi yanapo vunjika. Basi mizani ya utulivu ya nguvu hizi inapo geuka kwa kuathirika na mambo mengineyo ya nje huenda zikafunguka nguvu za mtikiso mkubwa ndio ikatokea mitetemeko na mitikisiko ya ardhi, ambayo hubomoa kila kitu kiliopo juu ya ardhi karibu na ilipo anzia hiyo zilzala. Na hapo tena hutokea uharibifu mkubwa mno. Na hayo maelezo ya kisayansi hayageuzi kitu, wala hayako mbali na nadhari ya kidini. Kwani hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu huenda akajaalia sababu za maumbile za kawaida zikajumuika kwa njia tusiyo izoea sisi ili zikiingiliana kwa njia ya kutisha ndio sababu ya kuharibika dunia. Hapo maelezo ya kisayansi yanafuatana na Aya zenye kuonya kwa vitisho hivyo vikuu. Na yote hayo yanatokana kwa Mwenyezi Mungu. Na hutokea kwa idhini yake Mwenyezi Mungu kutimiza hukumu yake katika dunia yetu.
Ərəbcə təfsirlər:
وَكُنتُمۡ أَزۡوَٰجٗا ثَلَٰثَةٗ
Na nyinyi mtakuwa namna tatu: . [7]
[7] Na mkawa nyote siku hiyo namna tatu kwa mujibu wa vitendo vyenu;
Ərəbcə təfsirlər:
فَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَيۡمَنَةِ
Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani? [8]
[8] Basi watu wa mkono wa kulia, watu wa cheo kilio bora, utukufu ulioje huo wa hali yao!
Ərəbcə təfsirlər:
وَأَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ مَآ أَصۡحَٰبُ ٱلۡمَشۡـَٔمَةِ
Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni? [9]
[9] Na watu wa kushotoni, hao ni watu wa cheo duni, uovu ulioje wa hali yao!
Ərəbcə təfsirlər:
وَٱلسَّٰبِقُونَ ٱلسَّٰبِقُونَ
Na wa mbele watakuwa mbele. [10]
[10] Na walio tangulia mbele katika mambo ya kheri duniani ndio watakuwa mbele katika vyeo vya Akhera.
Ərəbcə təfsirlər:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Hao ndio watakao karibishwa [11]
[11] Hao ndio walio karibishwa mbele kwa Mwenyezi Mungu. Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.
Ərəbcə təfsirlər:
فِي جَنَّٰتِ ٱلنَّعِيمِ
Katika Bustani zenye neema. [12]
[12] Mola wao Mlezi atawatia katika Bustani zenye neema.
Ərəbcə təfsirlər:
ثُلَّةٞ مِّنَ ٱلۡأَوَّلِينَ
Fungu kubwa katika wa mwanzo, [13]
[13] Hawa walio karibishwa mbele ni kundi la wengi katika mataifa yaliyo tangulia na Manabii wao,
Ərəbcə təfsirlər:
وَقَلِيلٞ مِّنَ ٱلۡأٓخِرِينَ
Na wachache katika wa mwisho. [14]
[14] Na wachache katika umma wa Muhammad ukiwalinganisha na hao.
Ərəbcə təfsirlər:
عَلَىٰ سُرُرٖ مَّوۡضُونَةٖ
Watakuwa juu ya viti vya fakhari vilivyo tonewa. [15]
[15] Juu ya viti au vitanda vilivyo nakishiwa kwa nakshi za vito vya thamani,
Ərəbcə təfsirlər:
مُّتَّكِـِٔينَ عَلَيۡهَا مُتَقَٰبِلِينَ
Wakiviegemea wakielekeana. [16]
[16] wakivitegemea kwa raha na utulivu huku wakielekezana nyuso kwa ziada ya mahaba.
Ərəbcə təfsirlər:
 
Mənaların tərcüməsi Surə: əl-Vaqiə
Surələrin mündəricatı Səhifənin rəqəmi
 
Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani. - Tərcumənin mündəricatı

Tərcümə edən: Əli Muhsin əl-Bərvani.

Bağlamaq