Check out the new design

Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani. * - Tərcumənin mündəricatı

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Mənaların tərcüməsi Surə: əl-Mutaffifin   Ayə:

Al-Mutaffifin

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ
Ole wao hao wapunjao! [1]
[1] Wataangamia wanao punja,
Ərəbcə təfsirlər:
ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ
Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe. [2]
[2] Ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi,
Ərəbcə təfsirlər:
وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ
Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza. [3]
[3] Na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!
Ərəbcə təfsirlər:
أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ
Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa . [4]
[4] Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa,
Ərəbcə təfsirlər:
لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ
Katika Siku iliyo kuu! [5]
[5] Katika siku ya vitisho vikuu?
Ərəbcə təfsirlər:
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote? [6]
[6] Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?
Ərəbcə təfsirlər:
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin. [7]
[7] Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa! Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.
Ərəbcə təfsirlər:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ
Unajua nini Sijjin? [8]
[8] Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?
Ərəbcə təfsirlər:
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Kitabu kilicho andikwa. [9]
[9] Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.
Ərəbcə təfsirlər:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha! [10]
[10] Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.
Ərəbcə təfsirlər:
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo. [11]
[11] Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.
Ərəbcə təfsirlər:
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ
Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi. [12]
[12] Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.
Ərəbcə təfsirlər:
إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale! [13]
[13] Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!
Ərəbcə təfsirlər:
كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma. [14]
[14] Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.
Ərəbcə təfsirlər:
كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi. [15]
[15] Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.
Ərəbcə təfsirlər:
ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ
Kisha wataingia Motoni! [16]
[16] Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.
Ərəbcə təfsirlər:
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha. [17]
[17] Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!
Ərəbcə təfsirlər:
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin. [18]
[18] Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.
Ərəbcə təfsirlər:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin? [19]
[19] Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?
Ərəbcə təfsirlər:
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Kitabu kilicho andikwa. [20]
[20] Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake,
Ərəbcə təfsirlər:
يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Wanakishuhudia walio karibishwa. [21]
[21] Wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.
Ərəbcə təfsirlər:
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema. [22]
[22] Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi,
Ərəbcə təfsirlər:
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia. [23]
[23] Juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.
Ərəbcə təfsirlər:
تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema, [24]
[24] Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.
Ərəbcə təfsirlər:
يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ
Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri, [25]
[25] Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa;
Ərəbcə təfsirlər:
خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana. [26]
[26] Kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.
Ərəbcə təfsirlər:
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ
Na mchanganyiko wake ni Tasniim, [27]
[27] Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi,
Ərəbcə təfsirlər:
عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa. [28]
[28] Nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.
Ərəbcə təfsirlər:
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini. [29]
[29] Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.
Ərəbcə təfsirlər:
وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ
Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana. [30]
[30] Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.
Ərəbcə təfsirlər:
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ
Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi. [31]
[31] Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.
Ərəbcə təfsirlər:
وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea. [32]
[32] Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad.
Ərəbcə təfsirlər:
وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao. [33]
[33] Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.
Ərəbcə təfsirlər:
فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri, [34]
[34] Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.
Ərəbcə təfsirlər:
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia. [35]
[35] Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.
Ərəbcə təfsirlər:
هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda? [36]
[36] Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?
Ərəbcə təfsirlər:
 
Mənaların tərcüməsi Surə: əl-Mutaffifin
Surələrin mündəricatı Səhifənin rəqəmi
 
Qurani Kərimin mənaca tərcüməsi - Səvahili dilinə tərcümə - Əli Muhsin əl-Bərvani. - Tərcumənin mündəricatı

Tərcümə edən: Əli Muhsin əl-Bərvani.

Bağlamaq